MDAU WA MILIONI SITA ATAPATIKANA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA WADAU KAENI MKAO WA KULA MAANA SPIDI YA HESABU ZA WADAU SI YA KAWAIDA KWA MUJIBU WA TARAKIMU ZINAVYOONESHA HAPO CHINI KULIA KUELEKEA KWENYE MILIONI SITA, NA HAMNA KWIKWI WALA NINI....

NAMNA YA KUJISHINDIA DOLA 1,000 ZITAZOTOLEWA NA VODACOM TANZANIA KUPITIA HUDUMA YAKE BOMBA YA 'THE GRID' NI RAHISI SANA.

UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KWAMBA ENDAPO UTAFUNGUA GLOBU YA JAMII NA KUKUTA TARAKIMU PALE CHINI ZIKIONESHA 6,000,000 BASI UJUE UMEULA.

UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUKOPI UKURASA HUO WENYE TARAKIMU HIZO ZA 6,000,000 NA KUUTUMA KWA EMAIL KWENDA:



NA MUDA SI MREFU UTATANGAZWA MSHINDI NA UTAAMBIWA UTAPATAJE MKWANJA WAKO.


NAMNA YA KUKOPI UKURASA HUO NI AIDHA PIGA PICHA SEHEMU HUSIKA NA KUITUMA AMA BOFYA KIDUDE CHA 'Prt SC Sys Rq' AMA CHA AINA HIYO KINACHOKUWEZESHA KUKOPI UKURASA (KWA WATUNMIAJI WA MAC) , KISHA NENDA KWENYE 'START' AMBAPO UKISHABOFYA TAFUTA 'PAINT' KUPITIA 'ACCESSORIES' NA UKISHABOFYA NENDA KWENYE 'EDIT' AMBAPO UTABOFYA 'PASTE' NA KUKUTA UKURASA ULIOKOPI UNAJAA HAPO. 'SAVE' NA KISHA TUMA KAMA ATTACHEMENT KWENDA EMAIL HIYO.

MASHARTI NI YALE YALE
1. MSHINDI NI MMOJA TU NA MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO GLOBU YA JAMII INAPOPATIKANA RUKSA KUSHIRIKI.
2. UJANJA UNJANJA HAURUHUSIWI NA WALA USIJISUMBUE KWANI JOPO LA WATALAMU LIKO MACHO KUNG'AMUA HILO
3. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO, HAKUNA KUTAKA RUFAA
4. MSHINDI ATAPATIWA MKWANJA WAKE CHAP CHAP NA MARA TU BAADA YA KUTHIBITISHWA KUWA INGIZO LAKE NI LA HALALI.
5. ENDAPO KAMA MSHINDI YUPO DAR ATAELEKEZWA WAPI AJE KUCHUKUA MZIGO WAKE, KAMA YUKO NJE YA DAR ANARUHUSIWA KUTUMA WAKALA KUMCHUKULIA, AMA ATASEMA ATUMIWE VIPI MKWANJA WAKE POPOTE.
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2009

    Kwa speed hii ya wadau, vodacom wakajitoa karibu, maana wadau 1,000,000 watakuwa wanapatikana kwa week, na baadae kwa siku tu. Sijui itakuwaje hapo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2009

    Njomba michupu, mbona chupidi imekuwa kali, kama pungo anakimbia nkuki wa achumani bin chipoku!tayaricha vidola vyako hivyo nakuja kuvichukua njomba!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2009

    Mdau huyo ni mimi----

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2009

    Sasa mi sijaelewa. Mdau wa milioni 6 anahesabiwa kwa kufungua blog au kutuma maoni?

    Nieleweshwe

    ReplyDelete
  5. Mdau, OmanJuly 03, 2009

    Mkuu hamna zawadi kwa mdau wa 6,000,001? yaani juhudi zote nimeambulia patupu!! haina neno, there is always next time!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2009

    Mkuu wa wilaya, haya mambo mazuri sana. mimi ilikuwa kiduchu tu. kwani mwenzako ilikuwa 999999. Heko nyingi kwa aliejinyakulia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2009

    mzee wa nanihii noma,
    nimekosa kiduchu kaka,kweli mwenye bahati habahatishi.ongera zako uliyenyakua kitita hicho.
    carlos

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2009

    duh!!!! nimekuwa mdau wa milioni sita moja kudadadeki bado kidogo tu kaka mithupu ungenipa vidola vyako hivyo.....

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2009

    Hii kweli ni bahati nasibu. Maana counter emeenda, mimi nikapata 599,999 nikiwa kwenye compyuta yangu, na mkewangu pia akiwa kwenye compyuta yake akapata naye 599,999. Tukashangaa hapo tukasema, lazima kutatokea watu wa milioni6 zaidi ya mmoja kutokana na tulichokiona. Sasa tusubiri kusikia watakaudhulimiwa.Maana kutakuwa na wa halali na ofcourse kuna wale wajanja pia. OK LETS WAIT MAJIBU SASA!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2009

    nina matumaini ya kuwa mdau wa millioni 6.
    fatuma.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 03, 2009

    Ona hawa watu, mshindi nimetulia wenyewe wanawahi wahi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 03, 2009

    I was 6000001, so sad. inabidi kuwe na run up wawili yaani just before and just after.

    Nampa hongera mdau huyo ila ntakutumia picha ya 6000001 angalau hata uiweke tu nami nijisikie nilikuwa sooo close.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 03, 2009

    Mdau wa nne nadhani walimu wako wote wa shule wameingia wazimu kwa kujaribu kukuelimisha wewe, hivi kweli kama umesoma post hii yote ungeliweza kuuliza suali kama hilo? pole sana tena sana tu, duhhhh

    ReplyDelete
  14. Michuzi, je wakipatikana wadau zaidi ya mmoja wenye namba hiyo utafanyaje...Mini na rafiki yangu tumepata namba moja ya 5999999 na bahati baya katika kuendelea kujaribu page yangu inasema " wait for http://issamichuzi.blogspot.com" nahisi kwamba mimi ni mshindi sasa sijui nisubiri mpaka lini hii page iffunguke

    ReplyDelete
  15. oya nyie hayo majina vipi mbona yana appear ina maana mnajua majina ya walio shiriki? au chenga la macho mbona langu halipo? au ndo wizi mtupu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...