
MDAU WA MILIONI SITA ATAPATIKANA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA WADAU KAENI MKAO WA KULA MAANA SPIDI YA HESABU ZA WADAU SI YA KAWAIDA KWA MUJIBU WA TARAKIMU ZINAVYOONESHA HAPO CHINI KULIA KUELEKEA KWENYE MILIONI SITA, NA HAMNA KWIKWI WALA NINI....
NAMNA YA KUJISHINDIA DOLA 1,000 ZITAZOTOLEWA NA VODACOM TANZANIA KUPITIA HUDUMA YAKE BOMBA YA 'THE GRID' NI RAHISI SANA.
UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KWAMBA ENDAPO UTAFUNGUA GLOBU YA JAMII NA KUKUTA TARAKIMU PALE CHINI ZIKIONESHA 6,000,000 BASI UJUE UMEULA.
UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUKOPI UKURASA HUO WENYE TARAKIMU HIZO ZA 6,000,000 NA KUUTUMA KWA EMAIL KWENDA:
NA MUDA SI MREFU UTATANGAZWA MSHINDI NA UTAAMBIWA UTAPATAJE MKWANJA WAKO.
NAMNA YA KUKOPI UKURASA HUO NI AIDHA PIGA PICHA SEHEMU HUSIKA NA KUITUMA AMA BOFYA KIDUDE CHA 'Prt SC Sys Rq' AMA CHA AINA HIYO KINACHOKUWEZESHA KUKOPI UKURASA (KWA WATUNMIAJI WA MAC) , KISHA NENDA KWENYE 'START' AMBAPO UKISHABOFYA TAFUTA 'PAINT' KUPITIA 'ACCESSORIES' NA UKISHABOFYA NENDA KWENYE 'EDIT' AMBAPO UTABOFYA 'PASTE' NA KUKUTA UKURASA ULIOKOPI UNAJAA HAPO. 'SAVE' NA KISHA TUMA KAMA ATTACHEMENT KWENDA EMAIL HIYO.
MASHARTI NI YALE YALE
1. MSHINDI NI MMOJA TU NA MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO GLOBU YA JAMII INAPOPATIKANA RUKSA KUSHIRIKI.
2. UJANJA UNJANJA HAURUHUSIWI NA WALA USIJISUMBUE KWANI JOPO LA WATALAMU LIKO MACHO KUNG'AMUA HILO
3. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO, HAKUNA KUTAKA RUFAA
4. MSHINDI ATAPATIWA MKWANJA WAKE CHAP CHAP NA MARA TU BAADA YA KUTHIBITISHWA KUWA INGIZO LAKE NI LA HALALI.
1. MSHINDI NI MMOJA TU NA MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO GLOBU YA JAMII INAPOPATIKANA RUKSA KUSHIRIKI.
2. UJANJA UNJANJA HAURUHUSIWI NA WALA USIJISUMBUE KWANI JOPO LA WATALAMU LIKO MACHO KUNG'AMUA HILO
3. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO, HAKUNA KUTAKA RUFAA
4. MSHINDI ATAPATIWA MKWANJA WAKE CHAP CHAP NA MARA TU BAADA YA KUTHIBITISHWA KUWA INGIZO LAKE NI LA HALALI.
5. ENDAPO KAMA MSHINDI YUPO DAR ATAELEKEZWA WAPI AJE KUCHUKUA MZIGO WAKE, KAMA YUKO NJE YA DAR ANARUHUSIWA KUTUMA WAKALA KUMCHUKULIA, AMA ATASEMA ATUMIWE VIPI MKWANJA WAKE POPOTE.
-MICHUZI
-MICHUZI


Kwa speed hii ya wadau, vodacom wakajitoa karibu, maana wadau 1,000,000 watakuwa wanapatikana kwa week, na baadae kwa siku tu. Sijui itakuwaje hapo.
ReplyDeleteNjomba michupu, mbona chupidi imekuwa kali, kama pungo anakimbia nkuki wa achumani bin chipoku!tayaricha vidola vyako hivyo nakuja kuvichukua njomba!
ReplyDeleteMdau huyo ni mimi----
ReplyDeleteSasa mi sijaelewa. Mdau wa milioni 6 anahesabiwa kwa kufungua blog au kutuma maoni?
ReplyDeleteNieleweshwe
Mkuu hamna zawadi kwa mdau wa 6,000,001? yaani juhudi zote nimeambulia patupu!! haina neno, there is always next time!
ReplyDeleteMkuu wa wilaya, haya mambo mazuri sana. mimi ilikuwa kiduchu tu. kwani mwenzako ilikuwa 999999. Heko nyingi kwa aliejinyakulia.
ReplyDeletemzee wa nanihii noma,
ReplyDeletenimekosa kiduchu kaka,kweli mwenye bahati habahatishi.ongera zako uliyenyakua kitita hicho.
carlos
duh!!!! nimekuwa mdau wa milioni sita moja kudadadeki bado kidogo tu kaka mithupu ungenipa vidola vyako hivyo.....
ReplyDeleteHii kweli ni bahati nasibu. Maana counter emeenda, mimi nikapata 599,999 nikiwa kwenye compyuta yangu, na mkewangu pia akiwa kwenye compyuta yake akapata naye 599,999. Tukashangaa hapo tukasema, lazima kutatokea watu wa milioni6 zaidi ya mmoja kutokana na tulichokiona. Sasa tusubiri kusikia watakaudhulimiwa.Maana kutakuwa na wa halali na ofcourse kuna wale wajanja pia. OK LETS WAIT MAJIBU SASA!
ReplyDeletenina matumaini ya kuwa mdau wa millioni 6.
ReplyDeletefatuma.
Ona hawa watu, mshindi nimetulia wenyewe wanawahi wahi.
ReplyDeleteI was 6000001, so sad. inabidi kuwe na run up wawili yaani just before and just after.
ReplyDeleteNampa hongera mdau huyo ila ntakutumia picha ya 6000001 angalau hata uiweke tu nami nijisikie nilikuwa sooo close.
Mdau wa nne nadhani walimu wako wote wa shule wameingia wazimu kwa kujaribu kukuelimisha wewe, hivi kweli kama umesoma post hii yote ungeliweza kuuliza suali kama hilo? pole sana tena sana tu, duhhhh
ReplyDeleteMichuzi, je wakipatikana wadau zaidi ya mmoja wenye namba hiyo utafanyaje...Mini na rafiki yangu tumepata namba moja ya 5999999 na bahati baya katika kuendelea kujaribu page yangu inasema " wait for http://issamichuzi.blogspot.com" nahisi kwamba mimi ni mshindi sasa sijui nisubiri mpaka lini hii page iffunguke
ReplyDeleteoya nyie hayo majina vipi mbona yana appear ina maana mnajua majina ya walio shiriki? au chenga la macho mbona langu halipo? au ndo wizi mtupu?
ReplyDelete