
ile viro iliyopigwa bustani ya mnazi mmoja gaden ya jijini dar inaendelea kuwepo, ambapo walipa kodi wanaishia kuona kwa nje tu sehemu hii ya kupumzikia. redio mbao zinajulisha kwamba bustani hii inapigwa viro kwa kile ambacho mababa wa jiji wanasema ati wadau si waangalifu ukiifungua hiyo viro wanaweza kuitumia ndivyo sivyo. ila kuona kwa macho na kukaa nje ruksa. bongo tambarare...
i
Halafu huwezi amini kwamba jiji kama la Dar hakuna sehemu yakupumzikia zaidi ya pale Posta ya zamani!! Viongozi wa jiji wanakumbuka kujenga majumba tu lakini "open space" kwa ajili kupumzika watu hakuna!! Angalau wenzetu Zanzibar wanayo sehemu nzuri tu ya kupumzikia. Angali na haya "majiji" mengine, Mbeya, Mwanza, Tanga na Arusha, kulikoni??
ReplyDeletemhh ukiona hivyo keshauziwa mtu hapo!
ReplyDeleteukoloni
ReplyDelete""Bustan ya mnazi mmoja Gaden"" yapendeza, lakini si inatakiwa wakae watu jamani!
ReplyDeleteKama ni botanic garden inaweza kufanywa na jiji kama kitega uchumi. Watu waka wanaaingia kwa kwa kulipia. Ukawa na bei za matourists na za wenyeji. Hii itasaidia Bustani kujiendeleza yenyewe bila kutegemea pesa za kodi za walala hoi.Hiyo sehemu nakumbuka zamani za miaka ya 80ilikuwa wazi na iliharibika sana. Sina uhakuka kama kunakutoa chochote maana siku nyingi sijafika hapo.
ReplyDeleteIringa ipo pale posta tena kuna hata viti vya kukaa na miti mingi.
ReplyDeletehapa marekani pia bustani kama hizo zipo sema wanaweka walinzi maalum wa bustani...kwani wasifanye hivyo????keli bongo noma....cashmoneymore.
ReplyDeleteTatizo sio city tatizo ni wananchi wenyewe wachafu mno wakiruhusiwa hapo watalala hapo hapo watakunya hapohapo watakojoa pia basi balaa tu weka viro tu waione kwa nje safi sana mpka watakapo starabika
ReplyDelete