Na Mwandishi wako glob ya jamii Minnesota
Ile timu kabambe inayoundwa na vijana watanzania waishio Minnesota, jana ijumaa katika kusherehekea saba saba 2009 inayo sherehekewa kila mwaka 4th of july,ikicheza kwa ustadi na huku ikitandaza kabumbu la kisasa, iliweza kuibanjua timu ngumu ya kutoka Uganda inayoundwa na Waganda wanaoishio Minnesota.
mechi ilikua kali huku Tanzania ikiishambulia uganda takribani muda wote kipindi cha kwanza cha mchezo,na kama si jitihada za golikipa wa Uganda,Vijana hao Watanzania wangekua na karamu kubwa ya mabao.
ilikua kwenye dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza Frank Lahinana(Ndombolo) aliipatia Tanzania bao la kuongoza baada ya gonga za hapa na pale na hatimae mpira kumfikia mfungaji aliepiga shuti kali la nyavu ndogo huku akimuacha golikipa wa uganda,Robert akigalagala chini asijue la kufanya na huku beki ya Uganda ikibaki ikilaumiana.
mpaka mapumziko vijana Watanzania walikua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Uganda,refa kutoka Cameroun aliimudu mechi ya jana vyilivyo,kunako dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza alimtoa Renes mchezaji kutoka Uganda kwa kadi nyekundu baada ya kupiga ngumi mchezaji David Kinyaiya wa Tanzania beki wa kushoto ambaye alikua anakaba mpaka anawatia fowadi hasira.
kipindi cha pili kilianza taratibu huku Tanzani ikiendelea kutawala mchezo lakini umaliziaji ulikua butu,Kocha Peter wa Tanzania aliifanyia mabadiliko safu ya ushambuliaji ndipo alimtoa Ebra,Kevo na Frank na nafasi zao kuchukuliwa na Robert, Tom na Jerry Katope.
mabadiliko hayo yalionekana kuongeza nguvu na kasi ya ushambuliaji huku mshambuliaji Tuma akiinyanyasa ngome ya Uganda kama anavyotaka,na kunako dakika ya 74 ya mchezo supa sab Robert aliipatia Tanzania bao la 2 kwa kuunganisha krosi ya Tuma kutoka wingi ya kulia,mpira ambao ulianzia kwa beki ya kulia God aliyepanda na mpira na kumtanguliazia tuma aliyekimbia na mpira wingi ya kulia na kufuatwa na mabeki wa Uganda huku wakimsahau mfungaji akiwa peke yake na golikipa wa Uganda.
Tuma aliinua macho na kumwangalia mfungaji na kupiga krosi iliunganishwa na Rob kwa guu lake la kulia na kumuacha kipa akipishana nao.
baada ya bao hilo Kocha wa Uganda Noah alifanya mabadiliko ya kumtoa lyod na kumwingiza Henry mabadiliko hayo yaliongeza ya nguvu kwenye safu ya uganda na ndipo katika dakika ya 97 Kiojozi aliweza kuipatia Uganda bao la kufutia machozi,kwa pasi kutoka kwa Henry.
mpaka dakika 90 Tanzania 2-Uganda 1


na mkifungwa pia mharakishe hapa kutujulisha!!!
ReplyDeletehongera kwa kupata ushindi wabongo lkn mbona kikosi kina wazee wengi vijana wako wapi?
ReplyDeleteHii timu ni watanzania au ya wakenya.Maana naona mnasema watanzania lakini zaidi ya nusu wachezaji 6 wa timu hiyo mnayoita watanzania ni Wakenya.Semeni ukweli siyo Watanzania ni Wakenya na Watanzania wameifunga Uganda.Kenya/Tanzania 2-Uganda 1
ReplyDeleteSamahani wadau,naomba kujua kwanini hawa jamaa(waganda) mnawaita shemeji au wakwe zetu? hua sielewi kama wametuolea dada/watoto zetu au sisi tumeoa kwao?
ReplyDeleteannon 9.30am
ReplyDeletekaribu sana ktk blogu/globu hii ya jamii
muulize mithupu atakutanabaisha vizuri tu yakhe