JK akifunua kitambaa kuweka jiwe la Msingi kuzindua mradi wa Maji Mjini Manyoni leo mchana kushoto liyevaa t-shirt ya Bluu ni mfadhili mkuu wa mradi huo Padre Timothy Coday wa Shirika la Damu Azizi ya Yesu la Kanisa Katoliki na Kulia ni Mbunge wa Manyoni ambaye pia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa John Chiligati.
JK akimpongeza Padre Timothy Coday wa Shirika la Damu Azizi ya Yesu la Kanisa Katoliki muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo la Mtoo, mjini Manyoni,mkoani Singida leo mchana.Padre Coday ni mfadhili mkuu wa mradi huo kwa kushirikiana na Halmashauri wa Mji wa Manyoni.Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Ole Kone na kulia nia katibu Mkuu wizara ya Maji Christopher Sayi.

Padre Timothy Coday wa Shirika la Kanisa Katoliki la Damu Azizi ya Yesu akimwonesha JK pampu katika kituo cha maji alichokizindua katika mji wa Manyoni,Mkoani Singida leo mchana. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kwenye hilo jiwe la msingi naona JK nae kawa Dk au hiyo abbrev. MH. DK. jakaya kikweke inamaana gani?

    ReplyDelete
  2. Hongereni Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na wananchi katika kupambana na matatizo yao ya msingi ya kila siku. Pia Naona Kikwete Kawejka uapndeni suti zake na kuvaa vazi linalopendeza, Asante Mama Salama kwa kumpamba. na Pamba hiyo ya Kitanzania. Mdau Abdul Omari

    ReplyDelete
  3. Shati la Mr. Presidaa ni kali!

    ReplyDelete
  4. Hongera Kanisa Katoliki, moyo wenu wa kujitolea kwa ajili ya watu wote bila ubaguzi, ni wa kuigwa, HONGERENI SANA, JK UMEPENDEZA!!

    ReplyDelete
  5. hilo shati siyo vazi la kitanzania hilo ni vszi lenye asili ya kusini mwa afrika nafikiri linatoka swaziland kutokana na prints zinafanana na za kizulu na kiswati.

    ReplyDelete
  6. Haya angalieni kazi za wamisionari za maendeleo ya watu na sio kupiga blaa blaa majukwaani ambazo hazina maendeleo. Dini yoyote ni lazima imkomboe binadamu kiroho na kimwili. hongera sana padre Coday

    ReplyDelete
  7. Kanisa katoliki siku zote linajihusisha na maendeleo ya kweli katika nchi hii. huduma za maji, hospitali, wazee na watoto wasiojiweza pamoja na mashule kibao. hongereni sana huo ndio unabii wa kweli.

    ReplyDelete
  8. nchi yetu inanufaika sana na misaada ya kidini,maana bila misaada ya kidini wengine tusingejua maji shule hata dispensary.mfano tu mkoa wa singida serikali huwa inautelekeza ila kuna hawa wasweden ,wadenish mungu awazidishie huwa wanasaidia sana kijijini kwetu wamejenga shule,hospital wanamatrekta wanasaidia watu kulima,wameleta mashine ya kusaga na kukoboa mahindi na vitu mbali mbali ambavyo kwa kweli wanahitaji kushukuliwa.

    ReplyDelete
  9. manyoni ziko mbili mashariki na magharibi,wabunge hawa wote wamefanana na hawana chembe hata moja ya ufisadi wanastahili pongezi.

    ReplyDelete
  10. Vyombo vya kidini, NGO's na wanaharakai wanaojitolea ndio wamekuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo ya kweli ktk jamii yetu ya watu maskini lakini serikali yao inabaki kula pesa za walipa kodi na kutanua na GX V8 zenye gharama za milioni 200 moja..

    Ushindi wa kishindo kweli umeingiliwa mwaka huu.

    ReplyDelete
  11. Bwana mkubwa hajaenda vekesheni Marekani muda mrefu kweli. Kranchi imekausha nauli nini lol

    ReplyDelete
  12. SHATI LA MHESH. RAIS KIKWETE LINAFANANA NA SHATI LA PAROKO WETU WA KANISA LA MAGOMENI LANGO LA JIJI PADRE BENO. K. MANGENGO MICHAEL. HONGERA MAMA SALMA KWA KUMPEZESHA MMEO MZEE MRISHO KIKWETE

    ReplyDelete
  13. Kutokana na juhudi zake za kutatua mgogoro kati ya Kibaki na Odinga, Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya kilimpatia "honorary" digrii ya "doctorate"!

    ReplyDelete
  14. Waziri Mkulo alisema wawe wanalipa kodi hawa jamaa wa dini... swali je huo mradi wamelipa kodi kuleta hivyo vifaa???

    ReplyDelete
  15. mnaona kuwa tuna mavazi mwanana bongo! kwa nini jk asiifanye hiyo suti kuwa 'trade mark' yake? vazi la kitanzania sio lazima kila kitu kiwe cha kitanzania bali ni ubunifu wa kukuza kitu chako kwa kuchukua kutoka huku na kule. akikubali kuifanya 'trade mark' (kwa maana hata akitembelea obama atakuwa ameivaa) basi tutaikuza na kuiita 'kikwete suit' na hivyo angaa takuwa ameacha kitu cha kukumbukwa katika historia ya utawala wake!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...