Bwana michuzi kwa niaba ya Watanzania wenzangu naomba niwakilishe hizi picha mbili kuonesha Jinsi gani BOXI linavyopigika huku UK. Na pia kuwaelewesha wenzetu wa Tanzania kuacha kufanya fujo na misaada wanayopelekewa kwani hapa inaonesha ni jinsi gani tunavyopigika kuitafuta hiyo shilingi ya kusaidia Nyumbani
Ahsante
wako mdau wa UK
MACOMPUTER



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Acha FIX zako weweee..

    Box la ma-Mtoni ni la kiheshima bwana.. Full ma-Mashine, ma-Robbot na vitendea kazi vya usalama wa hali ya juu.

    Usipime kabisa na hizo taswira zako ulizozitoa kwenye internet kuonyesha ufanyaji kazi wa Africa kusini.

    Shika adabu zako ww Mla vumbi unayetengeneza Story fake.

    New Yorker.

    ReplyDelete
  2. We new yorker vipi!!??, soma hata mabango katika jengo utaona ni UK na sio South Africa,box ni box tu ili mradi mkono uende kinywani,Kazi zote halali ni za heshima, elimika ndugu.

    Mdau
    Trondheim.
    Norway

    ReplyDelete
  3. he hee ngoja waamke leo nitacheka sana manake kuna watu humu ndani ni jamii ya joti

    ReplyDelete
  4. Anony wa kwanza mbona unakuwa mkali kwa mwenzio aliyetoa "siri"! Kazi ni kazi bola mkono uende kinywani. Lakini duu washikaji hizo picha nilidhani ni wale watu waliokuwa wakijirusha nje wakati majengo ya WTO yalipokuwa yakiungua mwaka 1991! Poleni sana!!

    ReplyDelete
  5. Acha zako wewe kusaidia nyumbani kwa vijipaundi alfualfu? We tunaza wazee wa kizungu kaa kimya. Mtu aliepiga shule ya maana bingo anapata kazi na mshiko wa maana.

    ReplyDelete
  6. New Yorker, mtoe makosa mwenzako lakini hakuna sababu ya kumtukana na kumvunjia heshima.
    Ndugu Michuzi, comments kama hizi zinataka kuwa censored.

    ReplyDelete
  7. kwani umelazimishwa kukaa huko si urudi nyumbani? Na tumekwambia tunahitaji hivyo vihela vyako? kama unapigika kivyakovyako!

    ReplyDelete
  8. anachangamsha genge huyo mlatope vumbi lina afadhali town zake anazozijua ni 2 tu NAIROBI AND DARESALAAM

    ReplyDelete
  9. HUO NI ULIMBUKENI KWA WEWE ULIEWEKA HII POST
    KAA UKIJUA BO HALILIPI SIKU HIZI
    MTU ANAYEOSHA VIZEE NDIO ANAKULA HELA YA MAANA KWA SAA HADI POUND15 MASAA 40 KWA WEEK JUMLA POUND600 HAYA KWA MWEZI POUND 2400=4,500,000/=
    UKITOA KODI INABAKI KAMA 3,000,000 MATUMIZI KWA MWEZI KWA MIE NAJINYIMA INABAKI 2,000,000 KWA NINI NISIJISIFIE KIMA WEWE...!KWA MSHAHARA HUO BONGO NANI AKUPE KUNGUNI WEWE...

    NDIO MAANA BONGO SIRUDI MPAKA NIJILIPUE NA KULA MAKARATASI NDIO NTARUDI...
    BAKINI HUKO HUKO TUACHENI NA MBINGUNI KWETU HUKU

    ReplyDelete
  10. mna vifafa

    unajisifia utumwa??nyambafu

    kufa kivyenu nani kakuomba izo senti zako?

    ReplyDelete
  11. Wajameni wacheni utoto!wakubwa nyie aka!

    ReplyDelete
  12. Acha ujinga wewe unaye sifia saving ya 2,000,000 ndio Manaa mkirudi mnajirusha mwenzi mmoja then flat, njooni nyumbani tujenge nchi yetu, chinga wanamake zaidi yako au dereva wa daladala

    ReplyDelete
  13. mtoa maoni wa aug 31 0:3:22pm umenifurahisha kweli wewe umeongea cha maanA na nakubaliana na wewe asilima mia moja.BOX halina soko kabisa hapa UK nashangaa watu wananga"nga"nia BOX BOX acha zako wewe.upepo umegeukia kwa kwa VIBIBI huko ndo POUND inaongea maana kwa hesabu ya haraka haraka mimi binafsi nafanya na RESIDENTIAL HOME monthly NAKULA KAMA POUND ELFU MBILI NA MIA TANO after TAX na NATIONAL INSURANCE NUMBER nikingia ukutani nakuta wameniachia kama pound elfu moja na mia tano hadi mia saba.hiyo pesa ukiichenji kwa madafu ya bongo ni kama milioni tatu na ushee.mshahara wa mafisadi huo bongo au mnasemaje WAOSHA VICHWA.sasa unaniambia nirudi BONGO nimesahau nini?huko siji mpaka nipate MAKARATASI.bila hivyo haji mtu huko msije mkanibakisha bure huko.Naingia Night Shift ntarudi badae wadau.Kaka MICHUZI upo hapo na WAOSHA VICHWA WENGINE?!!! MDAU U.K...

    ReplyDelete
  14. Hii kazi ya kusafisha madirisha na majengo inalipa sana. Kazi yoyote yenye element ya 'kufakufa' hulipa , zingine za 'kufakufa' ni kupiga welding mabomba ya gesi na mafuta chini ya bahari, kuzibua 'sewage system' ya majiji ya London au New York ambako unaweza kukumbwa na mafuriko ya maji machafu ukiwa ndani ya bomba kubwa la sewage system.

    Ahsante kwa kuwapatia wadau wa blogu ya jamii, kazi mbalimbali za halali tufanyazo ughaibuni.

    Mdau
    New York City

    ReplyDelete
  15. Wadau waosha vibibi tunawezakupata taswirazz ukiwa unakichambisha kibibi?? tupostieni hapa tule chabozz,itatuongezea mizuka ya kujoin huko.

    Mpiga Chabo mzoefu Michuzi Globu.

    ReplyDelete
  16. Kazi zinazolipa u.k, ni ya unesi,bus driver,kuzoa taka majumbani mwa watu,{hiyo inalipa hasa,ukianza alfajiri saa tano mchana umeshamaliza kazi}mfagizi wa airport,porter hospitali,kulea vizee,kama una makaratasi somea ualimu{kazi kama hiyo utapata}mshahara mzuri pia. kama mvivu wa kusoma somea angalau teaching assistant{shule zikifungwa na wewe una mapumziko yako}u.k mara kwa mara shule zinafungwa.na nyinginezo nitaziorodhesha baadae.

    ReplyDelete
  17. WEWE NEUYOKA WA KWANZA SAUZI AFRIKA HAKUNA BINGO KAMA KTK TANGAZO HAPO JUU KUNA LOTTO TU KWAHIO USIROPOKE KABLA HUJACHUNGUZA HAPO INAWEZA IKAWA INCHI NYENGINE YEYOTE LAKINI SIO SAUZI

    ReplyDelete
  18. yaani kuna watu very low class sasa ukipata makaratasi ya utumwani ndio nini?watu bongo wana kazi zao za maana wanakuja holiday uk,america dunia ya sasa sio ya mwaka 47 wewe unajisifia kufanya kazi za care tatizo uk ni nchi yenye watu wa kila class wapumbavu wasio na elimu wengine walikuja huku kwa miguu hata ndege hawakupanda sasa unajisifia unapata pound 2000 kazi yenyewe care kweli tutafika kweli?!!! watu wa uk acheni kuropoka wenzenu America wametulia na ndio life iko kule sio nyie vijumba kama tundu la ndege,maisha low quality,wajinga wengi mwanaume na akili zake hawezi kufanya care akajisifia.kufanya kazi za care kama una elimu yako ni kukosa confidence kwani kazi ughaibuni niliko mimi ziko sio lazima care.

    ReplyDelete
  19. Japo sijafika Ukerewe lakini kwa ufahamu wangu Bradford ni moja ya sehemu za Ukerewe. Mdau unayedai hii ni Afrika Kusini nahisi unabahatisha. Ingekuwa jengo linasomeka Mpumalanga ningeweza kuamini kwa urahisi zaidi mawazo yako.

    ReplyDelete
  20. Ha ha ha ha..so interesting. kuna watu humu wana vipaji vya kuchekesha...mimi naona wangeongea na Kanumba wawekwe ktk filamu flan flan...zitauzika...

    ReplyDelete
  21. nawasikitikia ndugu za hawa jamaa, yani kutuma vijisenti kwao basi anaona taabu, i think ni ulimbukeni... kama ni shida hivyo rudini nyumbani washamba nyie, ooh mradi mnaishi nje, chumba kimoja mnalala kwa zamu ili muweze ku survive...poleni mwe, kwani mlitumwa mwende huko, bana... ufanye kazi, acha kulalamika kama kweli mwanaume

    ReplyDelete
  22. Hivi mnafikiri nyumbani maisha ni magumu kiasi hicho kama Mungu alikujalia elimu kiasi fulani na kazi?? Mnacho angalia ni "figure" za mshahara lakini bei za mahitaji UK hamziangalii kabisa.

    Mfano ukichukulia kama unasoma chuo ada zenyewe za vyuo ziko juu sana. Utasave kitu gani kama kweli unataka kusoma shule ya maana?

    ReplyDelete
  23. Hivi nyie mnaolinganisha mishahara ya bongo na ya uk mmerukwa na akili au tusemeje mnaposahau kuwa bei za vitu na matumizi kwa ujumla kati ya bongo na uk ni vitu viwili tofauti.UK MATUMIZI YAKO JUU KUIZIDI BONGO SO OFCOURSE MISHAHARA HAIWEZI KULINGANA LKN JE HICHO UNACHOKI-SAVE HUKO UK UNAWEZA KUNUNUA NINI?AMBACHO NA MWENYE MSHAHARA BONGO AKI-SAVE HATOWEZA KUKINUNUA?TV,SIMU,MIWANI,VIATU??HIO HELA UNAYOOITA KUBWA KWA HUKO UK KWAKO ULIPO HUPATI HATA TV KALI BWANA BADO HUNA KITU KAPUKU TU TULIA.NI SAWA SAWA NA USEME UNAPIGA BOKSI ZIMBABWE KWA MWEZI UNA-MAKE BILIONI 7 WAKATI UNANUNUA KAMBA ZA VIATU TU KWA PESA HIO.UNGENAMBIA KUWA KILA MSHAHARA WAKO UNAWEZA KUNUNUA NYUMBA HAPO ULIPO NINGEKUSOMA

    ReplyDelete
  24. swali: hivi hawa wana bima? viuno hivyo jamani....

    ReplyDelete
  25. PETER NALITOLELASeptember 01, 2009

    UKWELI KUHUSU NANI BORA UKELEWE NA BONGO....! KUTOKA KWA EXPART

    MIMI NILIKAA CANADA NIKAPIGA BOX NIMEMALIZA MPAKA MASTERS NIKO HAPA BONGO NINAPATA MSHAHARA MILLION 1 MAISHA HAPA BONGO KWA KWELI NI MAGUMU SIYO KAMA ZAMANI NIKIWA HUKO CANADA NILIWEZA KUSOMA NA KULIPA ADA NA BILL ZINGINE NIKABAKI NA WALLAU DOLLAR 600-700 KWA MWEZI. SASA NIPO HAPA ARUSHA NYUMBA NALIPA SHS.LAKI300 KWA MWEZI MKOPO WA GARI NAKATWA LAKI 1 NDUGU WANANISUBILI NIWASOMESHE. ADA WATOTO 2 NI MIL 2 KWA MWAKA MAMAA HANA KAZI NI KULA KULALA. KILA MWISHO WA MWEZI NABAKI NA SHS. ELFU 50 TU MAFUTA BADO NGUO BADO BIA BADO NA MAHITAJI MENGI NAJUTA KURUDI BONGO MNANICHANGANYA KABISA NA HIZI KASHFA NINGEKUWA NA MAKARATASI CANADA NA HII MASTERS YANGU NINGEKUWA MBALI HUKU, TUNA SHIDA NYINGI KUANZIA MATIBABU, SHULE HAKUNA MIKOPO YA UHAKIKA BARABARA MBOVU UMEME MGAO MAJI SHIDA AJARI KILA CORNER UJAMBAZI KILA KUKICHA SASA JAMANI KUNA KULINGANISHA KWELI MAISHA NA ULAYA/MAREKANI HAPA AMA NI KUPOTEZEANA MUDA? KABLA YA KUBISHA NA KULINGANISHA MAISHA WAPI BORA JAMANI NENDENI MKAJIONEE MSISUBIRI HIZI PICHA. SWALI LA KIZUSHI MPIGA DEBE WA UKELEWE NI SAWA NA MPIGA DEBE BONGO? DACTARI BONGO NI SAWA NA DAKTARI UKELEWE? PROFESA BONGO NI SAWA NA PROFESA UKELEWE? HOUSE BOY BONGO NI SAWA NA HOUSE BOY UKELEWE? DEREVA WA BASI BONGO NI SAWA NA DEREVA WA BASI UKELEWE? MWANAFUNZI BONGO NI SAWA NA MWANAFUNZI UKELEWE? MAJIBU UTAKUTA UKELEWE NI BOMBA ZAIDI LAKINI SASA KAMA UNAJARIBU KUZUNGUMZIA NANI ANAMAISHA BORA KATI YA KINJEKITILE NGOMABLEMWIRU AMA MICHUZI ISSA NA MPIGA BOX UKELEWE SI AJABU KINJE NA MICHUZI WANAMAISHA MAZURI. SASA NAWAACHIA MTIHANI KAZI KWENU KUTAFAKARI NA UKWELI NDIYO HUO NIMEWAPA KWA KIFUPI UKELEWE TAMBALALE MOST OF PEOPLE HERE MAISHA NI MAGUMU LABDA MPAKA UMWIBIYE MWAJILI WAKO AMA UMUDHULUMU MTU NDIYO MAISHA YANAKUWA WALAU MAZURI. WENZETU HUKO UKELEWE WANALIPWA KWA SAA SASA KAMA UNASHIDA SANA YA PESA UNAPIGIKA KINOMA. KUMBUKA MPIGA BOX HAPA BONGO UNALIPWA KWA KUPAKUA BEHEWA NYING SIYO KWA SAA. ASILIMIA KUBWA YA WAFANYA KAZI HAPA WAKIPATA MAGONJWA MAKUBWA KAMA HEART ATTACK WANAISHIA KUFA KWA SABABU MATIBABU YETU NI FINYU HATUNA VIFAA VIZURI VYA KUTIBU MAGONJWA MENGI KAMA HYPERTENSION, OPEN HEART SURGERY, HATA ANGIOPLAST. KUPATA CT SCAN, EKG TU INAKUWA TAABU LAKINI MFANO USA HIVI VYOTE NI WORK IN CASE. SASA KAMA UNAFANYA MFANO BANK, SIGARA, TIGO ,VODA UKIPIGWA NA HEART ATTACK UNAHELA KWELI YA KWENDA INDIA KUFANYIWA OPEN HEART SURGERY AMA ANGIO? SASA JAMANI HIZI HELA ZA KUNYWA BIA NA KUCHUKUA MADEMU SIYO ZA KUPIGIA KELELE UNAPO COMPARE MAISHA BORA SIYO KUWA NA HOUSE GIRL SIYO KUNYWA SANA BIA SIYO KUFANYA KAZI NUSU SIKU NI PAMOJA NA MATIBABU I MEAN AFYA,COMMUNICATION, USAFIRI I MEAN BARABARA NZURI, NA UMEME SIYO KUKAA GIZANI KISA MAJI HAYATOSHI. KUWA NA UHURU WA KUONGEA SIYO KUTUPWA JERA KWA KUSEMA KIKWETE HATUFAI, SIYO KUUA ZERUZERU KISA WANA UGONJWA WA NGOZI, SIYO KUCHOMA WAZEE KISA MACHO MEKUNDU. HAYA NDIYO MAMBO MUHIMU YA KULINGANISHA WAPI BORA. HAYA YOTE YAKITEKELEZWA SI AJABU WENGI WATAPENDA KURUDI NYUMBANI NA KUPIGA BOX HUMU HUMU BONGO. LAKINI KAMA NITALIPWA KWA KUPAKUA IDADI NGAPI YA BEHEWA HAFADHALI NIKAE NAPAKUA BEHEWA HAPA HUKU NIKIPEWA INSUARANCE NA KULIPWA KWA SAA NILIYOPAKUA HILO BEHEWA, PIA NISIWE NA WASIWASI WA KULOGWA KISA NIMESOMA NA NINA MIAKA MIDOGO KULIKO BOSS WANGU. ASANTENI SANA..

    ReplyDelete
  26. jamani hii kazi inalipa sana!mimi nilifanya miaka zaidi ya mitano.naklumbuka nilivokua nasomea haya madude instructor wangu alikua mtashaa gali la faya linawapaishaa angani afu unashuka kune kamba ww na mwalimu anakupa assistenci.tulivo fika chini jama akawa anashanga eti kaifanya hio kazi miaka nenda rudi ilaaa alikua hajapata wanafunzi wa kiswaili i mean negger.kazi inalipa saanaa tu maana hio ni risk maana ukidondokaa lazima kinyesi kitapakaee mtaa mzima.ni hayo tu kwa leo.cheti nnacho hadi mitaa 70m angani na dunda tu

    ReplyDelete
  27. mie yangu macho, unasave kisha vile vile unakopa ili ujalizie Ada ya shule, ukimaliza unajisifu umesave ni sawa na milioni siju kadhaa za bongo, kama kweli una save kasome University ya Serikali ya UK nione kama unasave ila usije kunikopa.

    ReplyDelete
  28. first world = third world? duuk kweli kuna watu wabishi.mimi nitakubali siku nitakaposikia serikali ya bongo imetoa msaada kwa serikali ya UK

    ReplyDelete
  29. Anayesema vitu bongo bei rahisi namshauri aende pale mlimani city akafanye shopping woolworth,mr.price, akanunue lcd tv au tube light na housing yake pale game, au vyombo vya ndani shoprite au akanunue gari used imported japanese kwenye yard zenu,au kanunue wese pale BP,Oryx na Total uone habari yake. unanunua gari GX100 ya 1997 kwa tsh.11mil si uchizi huo halafu unasema eti bongo vitu bei rahisi kaulizie Toyota Harrier used ya 2004 kama mfanyakazi wa kawaida utaigusa ukimudu najinyonga, labda uwe mwizi aka mjanja!vinginevyo ni simulizi tu na mshahara wako wa laki 800,0000/= kwa mwezi. Kima cha chini bongo ni wa ngapi wanaoweza kufanya shopping pale mlimani city mara 10 tu kwa mwaka ya vyombo vya ndani na nguo kama hawajaishia kununua mikate tu shoprite..Anyway sorry Tanzanian kama nimemtusi mtu lakini ukweli life ya bongo ni tafu sana ni basi tu kwkuw ni home

    ReplyDelete
  30. nalitolela ameongea ukweli kina kinje na michuzi ni kama kina Larry King na will smith huku marekani? Kikwete ni kama Obama? Dudu baya ni kama 50 cents? lady jaydee ni kama Alisha Keys. Mengi ni kama Bill Gates? mpiga box bongo ni kama mpiga box USA? bank manager bongo ni kama bank manager UK? doctor bongo ni kama Doctor USA? passport ya bongo ni kama passport ya USA? Bongo inatoa green card/lottery? sasa nyie mnaotukana na kulinganisha maisha ya ulaya na bongo fanyeni utafiti kwa njia hizo nilizotoa. Siyo kuwa MBUMBUMBU KUFANANISHA WATOTO WA KIKWETE NA WALE WA MASAI WANAOISHI POLINI UKITEGEMEA WATOTO WA MASAI WA POLINI WANAMAISHA BORA KULIKO WA KIKWETE! AMA OYSTERBAY DAR NA SINGIDA USWEKENI! SASA MWISHO MTASEMA OBAMA ANAMAISHA MAGUMU NA HA SAVE HELA KAMA KIKWETE HAFADHALI ANGECHUKUA URAIA WA KENYA NA KUWA RAIS WA KENYA. FIKIRIA KABLA YA KUROPOKA. SI HAFADHALI HAO WANAOSHA VIYOO WANATUMA NYUMBANI KWAO NA KUSAIDIA NDUGU SI AJABU HATA WEWE ULIYE POST HII PICHA KWA MICHUZI UMETOKA KUMWOMBA AKUTUMIE SHATI NA CHUPI, ULITAKA WAUZE PIPI, KARANGA, MACHUNGWA, AMA KUPIGA KIWI BONGO?

    ReplyDelete
  31. NALITOLELA UNATAKA KURUDI CANADA? UMEACHA TOTO LA KIZUNGU HUKO SASA UNATESEKA NA JIMAMA ATM..HAHAHA KULA KULALA...CHUMA UNIPE...SAFI SANA

    ReplyDelete
  32. Mdau wa Tue Sept 1 01:46:oo am umesomea nini, na wafanya kazi katika industry ipi? it seems hujui thamani yako au hujajua wapi pa kufanya kazi. Pay hizo ni za serikali kuu na wao wanaridhika kwa kua kuna vitu vingi wanapata kama subsidies na safari. Ushauri wangu jaribu kunetwork na watu hasa uliowakuta hapa ili wakupe habari kamili na utaweza kuifurahia elimu yako. Its not good kwa mtu wa elimu yako unalalamikia maisha kiasi hicho it seems umeland katika wrong destination. U worth more than that bro, hujajua tu.

    ReplyDelete
  33. Hiyo kazi inapy sana ...good money ...lakini ni kazi inayoua sanaaaana tu hapa USA na wanayoifanya ni waspanish tu....Wabongo wanajipenda saaana tu


    Google tu "window washer rescued" uone makashikashi yake

    ReplyDelete
  34. Mimi nina elimu yangu nilijisomesha mwenyewe u.k,baada ya miaka 10,nikaomba uraia kwani nilipiga mahesabu yangu nikaona bora niendeleze maisha hapahapa,nikaivuta familia yangu pamoja na watoto wangu,atleast wanapata elimu ya bure.Bongo ukitaka mtoto wako awe na elimu bora,kwa kukisia umezaa watoto wawili basi ni milioni 3 kwa mwaka. u.k atleast kuanzia primary na kuendelea wanapata elimu ya bure.matibabu hali kadhalika ingawa utakuwa katika waiting list.

    ReplyDelete
  35. nimechekaaa haki ya nani we mdau wa new york wewe ni funga kazi yani humu ndani kuna watu wanachekesha wadau wenzao kwa point zao acha tu hii blog inatibu msongo wa mawazo jamani kucheka ni dawa BLOG YA JAMII IDUMU!!
    mdau canada

    ReplyDelete
  36. watoto wa porini/shamba hawana 'stress' wala nini, hawana 'obesity' wala 'mental health issues'.

    Hivyo watoto/ wananchi wa porini/ shambani wanafuraha ya moyo kuliko wewe 'mutoto wa mujini'- kila siku stress ya nitapata wapi hela ya daladala/mafuta, kodi ya chumba, hela ya chakula, hela ya 'kuji-show-off, hela ya kwenda kwenye starehe n.k

    Ndo maana Karl Marx alisema kweli watu wameharibiwa na 'utajiri wa pesa(sarafu na noti)' , yaani mabepari wanachukua mali ' madini, ardhi, majengo,viwanda' halafu mnachekelea kupewa sarafu na noti.

    Mdau
    Mtoto wa Shamba

    ReplyDelete
  37. MAisha bongo yako tafu hacheni mchezo nyinyi, sema kwa watu wanakuja uk sasahivi mambo magumu hasikwambie mtu kupata kazi ni ngumu.Watu tunaishi maisha mazuri mtu wanafunzi lakini mwisho wa mwaka P60 inasema pound 23,500 piga maesabu pesa ngapi kwa mwezi, usifananishe bongo na mtoni watu wengi bongo ishahara midogo ila wanaishi kiujanja ujanja tu kuibiana tu ndio maana rushwa imejaa kupita kiasi kila mtu anataka kitu kidogo.
    Kuna wale watu wamekuja uk kusoma na kusomeshwa na pesa kutoka home hawajui chochote kuhusu maisha ya huku watoto wa mama wakimaliza shule wanakimbiria kurudi home kwa kuwa hawajawai kushika pesa ukiwaripa million moja kwao ni nyingi wanaka kwenye nyumba ya baba hawajui chochote kile maisha kuangaika wazee.

    ReplyDelete
  38. Peter Nalitolela, umenena sana. Tatizo hapa kwa Balozi, wadau wengi hawajasoma (jaribu kutoa maoni ya Kiingereza). Tangu Internet access iwe Tsh.500 kwa saa, kila mlala hoi sasa anataka kutoa sumni yake, hata kama haelewi maisha ya nje wala elimu yoyote ya uchumi wa dunia unavyokwenda.

    Kulinganisha peke yake maisha ya nchi ya kimasikini na ya kitajiri, umeshapata "F grade" ya nguvu darasa la biashara au uchumi. Kuishi Bongo au ulaya ni swala binafsi, hauwezi kulinganisha na swala la kiuchumi hapa wala kazi. Nina rafiki wengi tu wamerudi Bongo na wanaishi vizuri hata kama kuna matatizo ya umeme, maji, elimuy na kadhalika. Kuna wengine kama mimi sitarudi Bongo hata ukinilipa dola 20,000 kwa mwezi kwa kuwa pesa peke yake sio muhimu kwangu. Nataka usalama, maji safi na elimu bora kwa watoto wangu. Sio wote tuliokuwa nje tunasafisha madirisha au kubeba maboxi au kusafisha vizee, japo waosha vinywa wengi hapa watapinga mpaka kiama. Wengine tunaishi vizuri tu na ofisi zetu, likizo Miami, London, au Zurich na pensheni nzuri tu inatusubiri tukivuka miaka 60. Kuna wengi pia wanaishi na mishahara midogo lakini wamerizika na maisha yao. Maisha ya ulaya ni magumu lakini kama una elimu nzuri na bahati ya kazi basi utastarehe tu. Kuishi kwa kujua kuwa nitapatiwa matibabu ya hali ya juu nikiumwa peke yake ni sababu kubwa ya kunifanya niishi hapa mpaka kufa. Kaeni na Bongo yenu Tambarare, nasubiri maombi ya misaada kama kawaida kutoka kwa maraisi wenu.

    ReplyDelete
  39. MICHUZI LET ME SAY THIS KAMA MZUNGU AU HATA MIMI MWENYEWE NIKIJA BONGO NA KUWALIPA WATU MFANO TU $ 15 KWA SAA NA BAADA YA MASAA 40 KWA WIKI NAKUPA OVERTIME I MEAN TIME AND HALF WAMCHAMBE KUMTUNZA BIBI KIZEE,KUNA MAMENEJA NA MADAKTARI WANGAPI NA WEWE UNAYESAGIA KUCHAMBA VIBIBI MTAVUNJA MIGUU KUGOMBANIA KUIPATA HIYO KAZI? SI AJABU WENGINE MTAUA VIZERUZERU ILI MUIPATE HIYO KAZI KWA HIYO KAMA KUNA MTU ANAFANYA KAZI NZURI BASI HIYO NI YAKE NA FAMILIA YAKE HAITUSAIDII SISI TULIYEKO 8000 MILES AWAY, KUWEPO KWETU HUKU KUNAKUSAIDIA WEWE MTOAMATUSI INDIRECT TUNATUMA $ NYUMBANI NA SERIKALI NDIYO INAFAIDIKA NA HIZO HELA ZA KIGENI INAWEZA KUKUPA MISHAHARA NA DAWA KUTIBU MALALIA, KIFUA KIKUU NA UKIMWI KWA BAADHI YA WAATHILIKA. HIZO PESA ZA DOUBLE TUNAZOPIGA HUKU NDIYO ZINAWAPA MISAADA MINGI MNAPO OMBA ULAYA/AMA USA KWA BUSH/OBAMA. NI HELA WATU WAMEKATWA TAX, SASA TUSIDHALAULIANE KILA MTU NA SEHEMU YAKE WEWE KAMA UKO POA FINE DON`T WORRY ABOUT OTHERS HAKUNA MTU KAKUOMBA PESA KAMA UNA STRESS MEZA DAWA.

    ReplyDelete
  40. acheni dharau kukaa mamtoni tumependa tikitaka kurudi tutarudi

    ni maisha yetu kwani bongo madirisha hayasafishwi
    bongo hambebi box?mi nakzi yangu zuri tu hapa new york na bongo nakuja kila mara. msiliganishe bongo na mamtoni acheni ujinga tembea ujionee.
    kalagabahoo
    tambarrrraaaarrrrrreeeeee
    sily cow

    ReplyDelete
  41. we mdau wa new york,mbavu sina na tumbo linaniuma naomba uwe unacoments ili tupanue mbavu,asante!!lakini ni kweli kabisa kazi za kufa kufa zinalipa sana kwasababu watu si wanazikwepa?kwa hiyo ukijitosa tu!wewe ni milionea!!!!!!

    ReplyDelete
  42. Nilikuwa bongo last week hivi sasa niko canada,mtu yeyote anayesema maisha bongo ni rahisi ana matatizo ya akili tena sana.bongo vitu ni expensive sana ukichange $100 asubuhi jioni imekwisha na haujafanya lolote la maana.hivi ni vitu nilivyogundua hapo bongo
    Gas ni bei mbaya kuliko huku
    electronics bei mbaya kuliko huku
    Nyumba bei mbaya kuliko huku...hapa namaanisha ukitaka apartment ambayo inafanana kidogo na huku sio zile za manzese.
    huduma za afya bei mbaya.....naweza kuendelea mpaka kesho...sasa huo urahisi uko wapi,nimekutana na jamaa kibao ambao walikuwa huku lakini kwa bahati mbaya makaratasi yalikataa,wenyewe wanakiri kuwa maisha yao yalikuwa bora mara100 huku walipokuwa wanabeba box kuliko kapo bongo....hivi mnajua kuwa kwa kipato changu cha box naweza kuwalipa madaktari 4 hapo bongo kila mwezi....wenye hasira wajibu.....kifo=usingizi? wachezi zenu waosha vinywa msilete hadithi za sungura sizitaki mbichi hizi....

    ReplyDelete
  43. teheteheeee heheeh ehea haaahhahahahaaaaa du comments za leo kaziiiiiii kwelikweli wabebeshwa maboxi leteni comments zaidi nifurahi mie.....

    ReplyDelete
  44. Miji inayoongoza kwa wakazi wake kuwa na 'msongo wa mawazo' aka STRESS Marekani ni Chicago, Los Angels, New York na Cleveland.

    Mfano wakazi wa Chicago, gharama za maisha zipo juu, 11% ya wakazi wake jobless, msongamano wa watu, usafiri wa kinyonga hata ktk Highway toka Chicago Loop mpaka Airport ya O'hare International inachukua kuazia dakika 30 mpaka hata 120, hewa chafu, ukata na nyumba walizojenga zinaporomoka bei. Na usisahau upepo unaopuliza mfululizo Chicago ni wa karibu ya Kimbunga hivyo huwezi kutoka ukasema napunga upepo mwanana ktk eneo lolote la wazi Chicago.

    Mchanganyiko huo hapo juu huwafanya wakazi wa Chicago kuwa na msongo mkubwa wa mawazo na kutoyafurahiya maisha.

    Hivyo usistuke ukiona New Yorker au mkazi wa Chicago, Los Angeles na Cleveland wanapotoa michango ya mawazo ktk hii blogu ya jamii.

    Mdau
    www.forbes.com/america's most stressful cities

    ReplyDelete
  45. Habari Siku njema,

            Je, wewe ni katika haja ya mkopo ?? unaweza kupata matatizo yako kutatua wakati
    kuendesha na yeye, ni Rose Vallarta kutoka Texas, Marekani, kulikuwa na wakati, mimi
    alikuwa anatafuta mkopo kulipia bili yangu, hivyo i kupata mwenyewe katika mikono
    kashfa ya tofauti na i alikuwa ulaghai na Taasisi mbalimbali, Kama siyo kwa
    Sandra ambaye ni rafiki yangu mzuri kuanzisha yangu kwa Mr charrin Obert
    (C.E.O) charrin mkopo kampuni, naye kunisaidia kwa mkopo wa $ 95,000.00.
    bila msongo. Hivyo watu wangu mzuri wa Marekani, unaweza kuwasiliana naye kupitia
    Barua pepe: charrinloanfirm@hotmail.com, na usisahau kumwambia, ambayo
    i kuanzisha wewe Kampuni yake

    Aina Wako,
    Mr charrin Obert

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...