Habari za kazi kaka michuzi,
Naomba niwekee hii kitu kwenye blog ya jamii au nisaidie wewe mwenyewe kama unaweza Mimi nina tatizo.
Bwana wangu ambaye nimeishi nae kama miaka 9 sasa na tuna watoto 2 hajaniowa japo tulipanga tungeowana tulikuwa tunaubishano wa dini. Nakuta sms za wasichana kwenye simu yake, huwa nasoma kwa kuiba kwani hataki nishike simu yakeNa simu nyingine sasa hivi kwaweka pin code siwezi kufungua.
Na kuna msichana anampigia simu karibu kila siku nikichungulia lazima jina lake liwepo na ni huyo naonaga sms za mapezi. Nishawahi kufua nguo zake nikakuta condom kwenye shati lake nilipo mpa akasema umeitolea nini nikamwambia nilikuwa nafua basi.
Je nifanyeje najua kabisa mr. wangu ananisaliti? Au nisisome sms maana ndio kila nikisoma zinaniumiza sana, wakati mwingine nasema ngoja nisisome ili nisiumie najikuta nimesoma nashindwa kuvumilia.
Siwezi kuandika mengi kwa ufupi ni hayo naomba ushauri nifanyeje tafadhali napungua uzito kila siku kwa mawazo.
Mdau PN
Pole sana dada. Kwanza naweza kusema mapenzi ni kupenda na kupendwa, ukiona hupendwi wakati unapenda unakuwa mtumwa wa mapenzi. Sasa wewe kwa ufupi ni mtumwa wa mapenzi unapenda usipopendwa, kwa sababu hakupendi tena huyo, na anajua unampenda ndio maana anafanya anavyotaka,na kwa kuwa mshazaa basi ndio anajua huna pa kwenda na watoto hao.
ReplyDeleteSasa cha muhimu na wewe kuanzia sasa hivi anza kutazama maisha yako, panga jinsi gani utaondokana nae kwa kuweka mikakati ya maisha yako ya baadae. Hakikisha unakuwa strong kwa sababu hapo unaachana na mtu unaempenda. Weka maisha yako sawa ukishakuwa na kazi yako na sehemu yako ya kukaa ukaweza kujua unafanya nini, beba watoto na kilicho chako toka mbio bila kuaga halafu uone atafanya nini kama haja analia na huku kapiga magoti na ukimrudia basi wewe umerogwa, kumbuka kama wewe unajali watoto je yeye anajali hilo?
Hajali lolote kama angekuwa anajali asingefanya hayo. WAKE NOW BEFORE ITS TOO LATE.
Vitamu kula na wenzio, acha roho mbaya hiyo..! Hakuna chapeke yako, wako akiwa kwako tu, akitoka nje siwako, gawana na wenzako!
ReplyDeleteUjumbe: Wanaume wako kama panya kila siku hutafuta shimo jipya!
Jinyonge ufee kabisa kwani penzi linaua
ReplyDeletePole sana dadaa. Kosa si kosa, kosa kurudia kosa. Nakushauri uzungumze nae juu ya ahadi yake ya kukuoa. Kama hatokuambia maneno yenye maana ya kukuoa haraka iwezekanayo ondoka hapo ulipo ili kuepuka uchafu mnaofanya kwani ni kumuasi Muumba wako. Usikate tamaa katika huruma za Mungu kwani yeye ndiye mpaji. Kuhusu watoto hao ni watoto wako, ondoka nao, kama huwezi kuishi mwenyewe rudi kwa wazazi au ndugu zako wa karibu watakusitiri.
ReplyDeleteKumbuka kuna maradhi mengi, ukikuletea ukimwi utasemaje? ulikuwa unasubiri uolewe?
Tatu, hata kama angekuwa amekuoa, hiyo tabia ya kuzini bado ni hatari kwenu.
Najua ni mapenzi ni suala zito lakini dada yangu rejea kwa Mungu wako na angalia maisha yako na ya watoto wako.
nautiakas huo ndo ushauri gani?Dada yangu sikiliza penzi ni upofu ila uvumilivu mwingine hauna mpango.huyo jamaa muonjesha ladha ya dawa yake mwenyewe.Tafuta kaboyfriend ka pembeni nawe anza kujilia vyako,wala usifiche.Akiuliza mwambie ndio karne mpya hii mambo ya open relationship haya,Tena mwenzio mchezo anaujua haswaa.wewe endelea huko na mimi naendele huku.
ReplyDeleteMimi napinga mdau wa kwanza kwakusema eti uondoke kisilisili.
ReplyDeleteKawaida mtu mliyezanaye watoto sio vizuli kuachana nae bila kuagana.Wewe kutokana na hayo yoote ambayo yanakuonyesha kwamba hakupendi tena!na ameshakua na mahawala wa pembeni,mwambie ukweli mliongeree kwa badae ndo unaweza kuchukua hatua.Lakini kama hujakaa naye mkaliongerea wewe unamakosa.
PIGA BUNDA.
ReplyDeleteKama hujamkuta jamaa juu ya kiuno cha mtu haina maana kwamba anajivinjari ndani na nje ya uwanja wake wa nyumbani.
ReplyDeleteMwongezee manjonjo ya mahaba nyumbani...kina dada wa Tanga wanaelewa. Akishakolea upya ongea naye yanayokusumbua. Kama baada ya yote anakuibia basi unaweza kufanya uamuzi mwingine. Chagua mwenyewe methali ya wahenga: "adui mpende", "kunguru mwoga hukimbiza ubawa wake", "mficha uchi hazai" au "dawa ya moto ni moto".
Hey we dada vip? mwanaume malaya kama huyo bado unangoja nini hapo? kwanza hakupendi full stop! Wangapi wamezaa bwn... hebu jiondokee
ReplyDeleteMimi naomba kwanza atuambie anajishugulisha na nini huyo dada! Maana wanaume majuha wakiona huna la kufanya wananyanyasa sana wanawake! Ndio yale mawazo ya kusema lazima uoe mwanamke aliye na elimu chini yako hili uweze kuendeleza mifumo dume!
ReplyDeleteAmekuheshimu kweli kama anatembea nje na anavaua kondomu!
ReplyDeleteIla watoa ushauri wengine bwana, Mama sikiliza mi ni mwanaume, ni kweli nahisi maumivu unayoyapata, Jamaahuyo pengine anaonekana ni sisi wenye umfumo dume fulani ambao umepitwa na wakati. Kaa chini na mwenzio mweleze kwa upole tena kwaupendo tu kuwa unajua kila kitu kinachoendelea kati yake nahuyo mwanamke. mwambie sio tu unaumia juu ya yeye kutoka nje ya penzi bali juu ya watoto watakavyoteseka endapo mtajikuta mmeambukizana magonjwa ya zinaa. Maana hata wewe hakika kuna wanaume wachwara watakaokuwa wanakusumbua ila hukufanya hivyo kwa kuheshimu uhusiano. Ukiona anakuja juu fanya hivi ila usitimize. mwambie na mimi nitakubali kutoka na wanaume wenzio wanaokuhitaji ila naruria tena usifanye kama utakavyomwambia bali tu ni kutuliza jazba zake maana kama anakupenda kweli ataomba msamaha na wakati huo utumie nafasi hiyo kujieleza na kutoa hisia zako kwake. ataacha. akikataa tafuta ndugu ama rafiki yake anaepatana nae vema wmeleze, ikishindikana na kuonyesha hana mapenzi, Du kuachana sishauri sana ila usikubali tendo [ngono] uone mabadiliko. akiendelea, basi huyo dada naona hakupendi na sio mwenye kujali familia bali ni wale wenzangu na mimi ambao hulala kila kitanda hata kama kina knguni. Pole sana dada ila jaribu ushauri niliokupa. ni hayo tu, [Marik]
ReplyDeletehatma ya kuendelea kukaa na huyo jamaa ni kujitafutia maambukizi ya maradhi ya zinaa(ukimwi nk).
ReplyDeleteHapo ni dhahir kuwa huyo umuitaye mpenzio hana mapenzi juu yako.sababu pekee ya kuendelea kukaa na wewe ni kukutumia kimapenzi na kukugeuza kitendea kazi chake.
Ukiwa kama mwanamke,una haki ya kuthaminiwa,kuheshimiwana kutambuliwa.haya yote huyapati kwa huyo jamaa.
Kuacha kutazama message sio suluhisho hapa.unatakiwa ujitafutie ukombozi wa maana hapa.
Ujikomboe kutokana na udhalilishaji,uonevu na ukandamizaji unaofanyiwa.
Na pengine kuondokana na mdhalilishaji huyu ndio mwanzo wa kuonyesha kuwa una nia ya kujiletea ukombozi.
Hapa ndiyo umuhimu wa kuelimisha wanawake katika jamii unapokuwa muhimu. Kama ungekuwa independent, namaanisha ungekuwa umesoma na umeajiriwa au umejiajiri, kwanza asingekuletea mchezo na pili ungeweza kuondoka ukiwa na uwezo wa kujitunza mwenyewe, kuwatunza watoto wako na kuwasomesha watoto wako bila hata kumtegemea yeye. Ingawa hukusema kama una uwezo au hauna uwezo wa kujitegemea, ninaweza kukusoma kutokana na maelezo yako kwamba huna elimu ya juu na hauna kazi yeyote. Unaonekana unamuogopa sana huyo mwanaume, yeye ndiyo anayefanya makosa, lakini wewe ndiyo unayetetemeka, wapi na wapi? hakuheshimu huyo. Kusanya virago vyako uende kwenu, cha kuhakikisha ni kwamba huyo mwanaume wako akusomeshee watoto wako, kwani kama huo mzunguko utaendelea wa kutokuwa na elimu ya juu, minyanyaso ya namna hii itaendelea. Ondoka humo ndani, rudi kwenu au anza kuchoma mikate ya kumimina uuze, ili ujitegemee
ReplyDeleteahsante
Mshazini weeee, na wanaharamu mmeleta duniani sasa unalalamika... kwani hukujua kwamba mnachofanya ni kinyume na maadili/dini...UA hujui hekima ya Ngono nje ya ndoa kuitwa ZINAA??
ReplyDeleteMungu anasema Wazinifu kwa wazinifu na wasio wazinifi kwa wasio wazinifu.
Akili kumkichwa hapo..
Michuzi usibanie, nimetumia lugha hiyo makusudi ili wazinifu waelewe.
Ramadhani inakuja Mjomba misupu, ado ado na picha za ajabu ajabu kama hiyo hapo juu...
Dada,
ReplyDeleteMiaka 9 na watoto 2 ni zaidi ya NDOA YA KWENYE KARATASI. Mpe mmume wako mapenzi yote, onyesha kumjali hata kama umechoka, kuwa mbunifu zaidi ya alivyokukuta miaka 9 iliyopita, usimsakame sana hata kama hamjafanikiwa kiuchumi unavyoota, kuwa mshauri wake mkuu, jaribu wakati wote mle chakula pamoja, yaani kwa ufupi 'mlee'. Uongee na mumeo kwa taratibu na kwa namna isiyoudhi, yaani mumeo asikie raha ufunguapo kinywa chako iwe ushauri, mahaba au ma-stori.
Bwana mzee, acha kuhangaika na wengine, kuwa mvumilivu maana nimeshamwambia mkeo nini afanye ili 'ujisikie raha kuwahi nyumbani' . Maana uyapatayo nyumba ndogo tayari nimemfahamisha na mkeo akufanyie-tena zaidi.
Mungu awabariki.
Mdau
KUNGWI KUBWA LAO
NENDA KAPIME VIRUSI, UNAWEZA KUKUTA UNAPUNGUA UZITO KWA KUATHIRIKA TAYARI....
ReplyDeleteGIVE HIM ULTIMATUM, MWAMIE AACHE MCHEZO WAKE LA UNATIA TIMU, KWANI KAMBA HUKATIKIA PABOVU UTAKUFA NA UKIMWI KWANI KONDOMU TUNAVAAGA SIKU YA KWANZA, YA PILI, YA TATU NA YA NNE TUNSEMA SI TUMESHAZOEANA YA NINI TENA KULA PIPI NDANI YA PLASTIKI HUWAGA SI TAMU EBU NYAMA KWA NYAMA BASI TUNAJARIBISHA NA UTAMU UKIKOLEA HATUACHI HATA UKIWA MKALI KIASI GANI. SO BE VIGILANT AND ALERTED OTHERWISE YOU GONNA GO WITH WATER, YOU WHAT IS HIV, NO PANACEA UNTIL NOW, JUST VIJIDAWA VYA KUKUONGEZEA MUDA UKIJITAHIDI SANA 5 YEARS THEN BYE BYE, SO SISTER BE SERIOUS KWA HUYO MKWARE OTHERWISE CHICKEN OUT SONNER NO LATER. HUYO NI MME WAKO KUTOKANA NA SHERIA ZA TANZANIA OMBA TALAKA MIGAWANE MALI SAWA 50/50 NA UANZE MBELE.
ReplyDeleteNi hivi,Unajua mara nyingi wanaume walio wengi wakikubaliwa na msichna mmoja na akapendwa sana na huyo, anapenda kujaribu kwingine kuona kama anapendwa pia, na akipata matatizo huko kwingine atakumbuka kule alikotoka,na akikuta kule alikotoka pameharibika pia hujuta na harudii tena kosa hilo. sasa mamaa jaribu kuongea na Mtu aliye kwenye ndoa atakupa maelezo mengi ya maana zaidi.ila ninamfahamu huyu mmeo ni mtu wa pombe pia ukatae usikatae, mwambie aache pombe zake.
ReplyDeleteDada pole sana!
ReplyDeleteMimi naungana na KUNGWI KUBWA LAO Anon Tue Aug11, 01:03:00 kwamba jukumu la kurekebisha mambo hapo nyumbani liko kwako. Mumeo huyo hakubadilika tabia hivi hivi...kuna kamchango kutoka kwako, pengine you have taken things for granted.
Unachotakiwa kufanya sasa ni kusahau kwamba kuna wanaomwandikia sms za mapenzi na kwamba anatembea nje na halafu umpe mapenzi kuliko ambayo anaweza kupata huko nje. Mfanye aone kwamba kuja nyumbani ni sawa na kwenda peponi... mwanaume kutembea nje ni kwamba anatafuta mahali pa kupunguzia stress za nyumbani...
Kazi kwako dada...fungulia mapenzi kuliko zamani.
Nakutakia mafanikio!
Dada zangu. hii mada ya mwenzeno inasikitisha. mie mtoto wa kiume nachokiana hapa ni kama ifuatavyo.
ReplyDeleteHuyu dada alimpenda sana huyu mpenzi wake isipokuwa hakuzingatia mambo muhimu kabla ya kuzaa na huyu jamaa. Inaonekana wazi kwa dada alikuwa na 70%upendo kwa jamaa; ila jamaa 30% upendo ndio sababu anamtesa binti. Jitahidi unapoingia kwenye mapenzi siku hizi usiingie kichwa kichwa kwa miguu yote. Mpe mwenzio mitihani ya kutosha kupima upendo wake ni sawa na Asilimia ngapi? na unakaribia na asilimia ulizonazo wewe kwake. Inaelekea dada aliamuwa kubeba mimba kuzaa na jamaa akifikiria jamaa anakuwa committed kwake na anaongeza mapenzi kisa amemzalia watoto. Angalieni sana ili swala. Wa kina dada siku hizi wanapenda sana Ndoa ila wanakosea kubeba mimba bila kujua anayezaa naye anaupendo kiasi gani na baada ya mtoto ataendelea kuwa na upendo ule ule au la; Wanawake mpende mtu jinsi alivyo usiangalie mali wala pesa utaenjoy life. Ila ukimpenda kisa anapenda au mali ukaforce kubeba mimba ili uolewe na jamaa awecommitted,inakuwa Vice versa kama hana true luv hata akikuoa bado anaendelea na tabia zile zile.
Sasa namshauri dada kwani maji yamesha mwagika. Umemvumilia sana miaka 9;We mueleze ukweli unajua yote na huyo binti unayekuta message zake pamoja na mabinti mwengine kwamba inakuumiza na umpe mda kama miezi miwili tu ya kujirekebisha huu unamuonyesha upendo wa kawaida halafu ukiona kipindi cha miezi miwili hajabadilika anaendelae. Basi mwambie live we na yeye basi uende kwenu au utafute mwaminifu mmoja ukaishi naye. Ila usilazimishe akuoe anakuowa kwa kuzidhisha ila ukweli anaendelea na tabia yake. Pole sana
Pole sana dada na hayo matatizo uliyokutana nayo,ni sehemu ya maisha kuna wengine wanapatwa na makubwa kuliko hayo yaliyokupata wewe.Mchango wangu kiushauri ni kuwa kwa kuwa pamoja na hayo yote ambayo huyo Mr. wako amekufanyia kwa mtazamo wangu inaonekana bado unampenda mbali na kuwa umeshazaa naye.Lakini kumbuka dada wahenga walisema "mapenzi ni...." nafikiri umeshawahi kusikia huo msemo.Kama amekuwa mbinafsi kiasi hicho suala la msingi ni kuachana naye,maana huwezi kumlazimisha mtu akupende tena,tafuta maisha yako na nikukumbushe tu kuwa una haki ya kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetu wewe unatambulika kama mke kwani sheria inasema mtu akisha ishi na mwanamke zaidi ya miezi 6 mwanamke anatambulika kisheria kuwa ni mke halali.Akibisha mpeleke mahakamani atleast abanwe na sheria asomeshe watoto na kutunza familia mpaka watakapo fikisha umri wa kujitegemea.Sizani kama litakuwa jambo la busara kutumia sheria kumlazimisha mgawane mali au akutunze ndiyo maana nishauri umbane atunze watoto wake wakati wewe unatafuta maisha yako.Niamini ukijituma na kufanya kazi kwa bidii utatoka tu na utapata mtu atakaye kupenda wewe kama wewe bila kujali elimu yako na kazi yako.Ubarikiwe.
ReplyDeletePole Dadangu.. lakini shukuru pia kuwa mshkaji anakumbuka kuvaa kifanyio/kondom. HALAFU ACHA HUO UTARATIBU WA KUBONYEZABONYEZA SIMU ISIYO YAKO, UTAJITIA MIPRESHA KAMA HIYO BUREEEEEEEE. Na WEWE MSHKAJI HEBU IPENDE FAMILIA YAKO
ReplyDeleteNimependa sana maneno yako MDAU KUNGWI KUBWA LAO.
ReplyDeleteUshauri kama huu ndiyo unaotakiwa siyo kama wale wanaokurupuka tu.
Nimefaidika bna ushauri wake kwani hata mimi nina tatizo kama la huyu mdada.
Haya mambo ya kuchunguza chunguza sms kwenye simu za waume ama wake zenu zitawaletea matatizo sana. ndio maana simu hizo zikaitwa za kiganja, maana yake zinamuhusu muhusika mmoja tu na ndiye mwenye kumiliki. acheni kuingiliana na kuchunguzana mapenzi hayaendi hivyo.
ReplyDeleteNaomba niwaambieni kuwa kuoa ama kuolewa si mwisho wa kupenda.utaendelea kupendwa na wengine ama kupenda wengine ata baada ya kuoa na kuolewa!!! huo ndio ukweli wa binadamu. vinginevyo mkaishi mwezini peke yenu.muhimu hapa ni uaminifu kwenu nyinyi wana ndoa. kuaminiana na kujaliana na kupendana na kuhakikisha vishawishi hivi nilivyovitaja amuvitumikii.lakini mkiendelea kupekenyuapekenyua simu iwe kwa mke ama mume amtadumu katika ndoa.mfahamishe mumeo kuwa unafahamu yote kuhusu maisha yake ya kimapenzi mwambie aache tabia hiyo na kuwa umemsamehe na muanze ukurasa mpya. ila mambo ya simu achana nayo, iwe kwake ama kwako, maana yatawasumbua sana.
kusema ukweli nakuonea huruma dada, kwanini ulikubali kuzaa watoto kabla hamjaoana,?? maana hapo uhusiano ukivunjika mzigo wa watoto utakuwa wako, sidhani kama huyo bwana atachukua hao watoto, mimi ni mwanammke mwenzako bwana wangu nimeishi nae miaka saba sasa, sina watoto ila tuna tofauti ya kidini, ila mimi naona wanaume wengine wanachukulia suala la dini kama kikwanzo kumbe nia yao hasa ni kukuacha na kupata binti mwengine mdogo amuoe, utakuta ataoa pia dini tofauti, dini sio sababu hata kidogo kama mtu anakupenda maelewano tuu, na mimi huyu bwana wangu akiendelea kuimba hiyo dini, wala sitoganda nina elimu yangu najitegemea sina shida yoyote , nipo njiani kupanga maisha yangu na niko tayari kuishi bila yeye maana naona ananipotezea muda,hivyo usidanganywe na mtu, eti mtu hapo juu anasema umpe mapenzi zaidi mwanamme unamkuta na condoms mfukoni umpe mapenzi zaidi??ya nini akuchoshe looooh achana nae kabla hajakuletea maradhi, hii ni karne ya 21 sio karne ya kuabudu wanaume na kuwabembeleza mungu ana uwezo kuliko mtu mwengine anaweza akakuletea mzuri zaidi kuliko yeye usijiumize dada.achana nae
ReplyDeletejamani kwa kweli inauma, hivi wanawake ni lini tutajikomboa? hivi sisi tuna miili ya chuma na wao wanamiili ya binadamu? ungefanya HAYO WEWE, UNAHAKIKA MPAKA SASA HIVI ANGEKUA NA WEWE???!!! hujachelewa bado kujua ufanye nini inaonyesha unampenda sana na pengine unaogopa kufanya step nyingine hasa kwa kuona watu watasemaje, kwanza yeye kwa uhakika hakupendi, hakuheshimu,hakuthamini, na wala hajali familia yake, sasa naomba ujiulize unafaidika na nini na huyu mtu? kumbuka si ndugu yako mlikutana mkiwa watu wazima, atakapoamua kuachana nawe atakuacha kwa dakika na wala hatafikiria ulivyomvumilia yeye, hivi unajua mwezanko ana deal na wewe kutokana na weakness point yako? naamini unafanya kazi humtegemei kwa kila kitu, hata kama unakipato kidogo kiasi gani haina maana unyanyasike kiasi hicho, jiulize mara kwa mara ingekua wewe je angekua na wewe mpaka LEO HII? jiulize sana je inathamani kweli wewe kunyanyasika kiasi unacho nyanyasika? sheria inasema kukuaa na mtu miaka zaidi ya miwili huyo ni mumeo, kabla hujaamua kuchukua uamuzi wowote ningekushauri ujue sheria itakulinda namna gani hasa kwa kuwa una watoto iliwasihangaike, nenda WAMWA, ukaeleze watakusaidia ushauri mzuri na kukusaidia kimawazo pia ujue utafanyaje, jiulize pia je unastahili kuishi katika hali unayojisikia nayo? kwanini uishi kwa uchungu na kukosa furaha na amani ndani ya nyumba yako mwenyewe? pia naomba nikuulize na ikiwezekana ningependa unijibu, UNATAKA UTOKE HUMO NDANI NA MAJERAHA NA UKIMWI ndio uaamini kumbe ni kweli jamaa alikua hakutendei haki? ukiugua ukimwi watoto wako wataishije ukiwa umekufa? hakuna mtu anahangaika na watoto wa mtu kwa maisha haya ya siku hizi, sasa huoni ni muhimu kuwalinda hao watoto sasa hivi kabla hujawaingiza kwanye kukuosa wewe katika maisha yao ya baadae? kwa nini unagamble na maisha katika ulimwengu huu wa sasa? aliyekushauri ukapime afya yako pia amekushauri vizuri, unawezaje kumpenda mtu ambae alikupenda kwa wakati fulani na sasa hakupendi tena ila anashindwa kukutamkia? usidanganyike kwa siku mbili tatu anazobadilika na kukujali, anafanya hivyo ili azidi kukutumia, utakapoamua la kufanya utakuta hata wale waliokuwa wanakupa offer za drink hawapo tena, mwenye macho haambiwi tazama, unatakiwa kuact now now!! zaidi ya yote muombe sana Mungu akuongoze katika kipindi hiki na mtegemee yeye zaidi na zaidi.
ReplyDelete...achana naye fasta na ukapime ngoma huyo mwanaume ni changudoa wa kiume ni bora uumie kwa kuachana naye kuliko uje uumie na machungu ya ngoma na penzi lenyewe hufaidi lala mbele aliachika princess diana aliyekuwa na ndoa na watoto juu kwani nini bwana! utapata tu wa kukupa mapenzi ya kweli achana na huyo fisadi wa mapenzi yani limenikeraa hadi basi
ReplyDeletemdau canada
jamani kubwa lao kuna mijanaume mingine ni sugu hadi basi hata ulibebe mgongoni ndo kwanza unacheza makida yani sijui ni hulka? hata uliimbie kuchi kuchi huta hee.... ndo linazidi kuwa kipanga tuu leo anatumia condom vikinogile aah wapi mbona condom zipo na bado watu wanakufa na ngoma? iko siku ataacha hapo sasa!!
ReplyDeletemdau canada
mumeo ni fisadi la kimapenzi,funga virago chukua watoto rudi kwenu.simple as that
ReplyDeleteasa si afadhali wewe mimi alikua haongei na mimi anakula hapo wewe unamwangalia tu wewe kakuachia elfmoja kuanzia asubuhi utaifanyaje elfumoja na haongei na wewe kala chips zake roho kwatu.nilivyoona hivyo ameondoka kazini mimi moto kakuta mesegi mezani tu.kaomba msamaha nimemwambia acha nipumzike,pia leo unaongea na mimi maajabu leo naonekana umeniona wamuhim. niache nitulie.nilikua najishugulisha na saloon.wewe je hayo umekonda je ungekua kama mimi,mimi nilikonda na nilikua na mtoto wa miezi 6 ikatisha tamaa ya kua na mwanaume. ukiona vipi timua wazungu hapo ndio wanatushinda.
ReplyDeleteDada utakofa bure uache watoto wako yatima buure! Kwani wanaume watu wa kawaida? Sisi wamama ndio mara nyingi tunakumbuka hatma ya watoto wetu,huyo anafurahi mfe wote tu.Naelewa saa nyingine inauma kuona unavyopoteza haki za wanao maana jamaa litaleta tu mwingine pindi uondokapo,ila ni vyema kuliko kufa wote kwa KIMWI na kuacha watoto wakihangaika.Ungekuwa na ndoa ningekushauri uvumilie ila hakikisha mnatengana vyumba .
ReplyDeletedada fungasha ondoka,MAPENZI KITU GANI?JIANGALIE WEWE NA WATOTO WAKO,UKIFA HAPO UNADHANI HUYO MALAYA ATAJALI WATOTO WAKO??WATOTO AKO KUTESEKA.KAMA UMEPANGIWA TAOLEWA UTAOLEWA TU,WANGAPI WAMEOLEWA NA WANAUME AMBAO HAWAJAZALISHWA NAO?MAPENZI NI KUPENDANA KWA DHATI NA KUJALIANA,KUBEBA CONDOM SIO NDIO KUITUMIA,ANAWEZA KUWA NA BOX ILA AKATUMIA MOJA,KWENGINE AKAPIGA KAVU.UNAUJUA UTAMU WAKE KAVU...NI UKIMWI.ENDELEA KUKAA HAPO UONE.
ReplyDeleteMimi nashindwa kuelewa hawa wanaume hivi kwanini wakipata vimada wasihamie huko jumla???Hawajihurumii unakuta mtu anaenda kibaruani asubuhi akitoka huko huyoo kwa kimada usiku wa manane ndio anarudi nyumbani sasa kwa nini wasihamie kwa hao vimada jumla hawajihurumii tabu zote hizo za nini???
ReplyDeletetopics za aina hii bwana!!! huwa zinapata comments nyiiiingi!!!
ReplyDeleteweka ki-english kama cha mashaka uone mchezo wake....watu wote wanalala mbele ha ha ha!!