spika wa bunge la jamhuri ya muungano mh. samwel sitta akionesha uzi mpya wa Simba SC baada ya kuuzindua katika Simba Day uwanja wa Uhuru jijini dar wikiendi ilopita. Mh. Sitta hafichi mapenzi yake kwa klabu hiyo ya msimbazi na swali la kizushi ni kwa nini viongozi wengine hawaigi mfano huu wa kuweka hadharani uyanga ama usimba wao?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Wanyamwezi wote Simba wachache sana Yanga.

    ReplyDelete
  2. Hata Wanyamwezi wanaoishi Morogoro na Zanzibar kama vile Ng'atingwa Padre E. Dimoso wote Simba!, kweli Simba ni Wanya-Mwezi!

    ReplyDelete
  3. ni kwa shauri hao viongozi wangine wanaona sifa wakishabikia manu, barca, bwawala maini, chelisea nk. na ni kwamba hawana mapenzi na simba yanga wala costo yunioni, hata cosmo au paniafrika.

    Au pangine sio washabiki wa kweli wa simba wala yanga huenda wao Ni walikuwa washabiki wa Mecco, tukuyu staz, rtc kigoma, rtc shinyanga, pulizna ambazo zote ni marehemu na sasa ivi hawana timu ya kushabikia

    ReplyDelete
  4. - je kuna ukweli wowote yanayosemwa hapa kuwa wanyamwezi wangi ni washabiki wa 'Simba'?..

    - Mbeya, Mwanza na Unguja ni ngome ya Yanga..

    ReplyDelete
  5. Viongozi mashuhuri wanazi wa Simba Na YANGA ni kama ifuatavyo.

    SIMBA.
    John Samuel Malecela
    Edward lowassa
    Fredirick Sumaye
    Edward Sokoine
    Salim Ahmed Salim
    Samuel Sitta
    Professor Kapuya
    Rashid Mfaume Kawawa

    YANGA.
    Julius Nyerere
    Ali Hassan Mwinyi
    Jakaya Kikwete
    Abeid Amman Karume

    ReplyDelete
  6. duh! kwenu unyanyembe hakuna timu? Glory hunting brigade? Yanga na Simba ni timu za wazaramo na wandengereko. Pia na wakavirondo waliozaliwa dar-es-salaam wanaweza kuwa Simba au Yanga. Wakavirondo waliozaliwa Bariadi, Mara, Igungo, Rujewa, Kantalamba, Chamwino, Same nk; support your local team, its the best way to improve competition in our game.

    Mdau, maji chumvi tangu asili

    ReplyDelete
  7. ameshaharibu kwenye siasa amekimbilia kujionyesha huku kutufanya tusahau.
    wewe mtu msafi gani,kama kuna usafi utakubali ukae nyumba ya dola elfu7 kwa mwezi??
    $7000x12=98,000/year!!!
    kwa nini husingetafuta ya dola2000 pale bongo ni nyumba safi tu!
    $98,000 kwa pango tu! isingewasaidia wakazi wako maskini wa kutupwa wa ulambo??

    ReplyDelete
  8. Hongera sana mzee sitta tunakusubiri uje kufungua tawi hapa Washington DC.

    ReplyDelete
  9. Mdau,Maji Chumvi tangu asili, Mr Umechemsha Simba na Yanga ni timu tu lakini si za makabila uliyoyataja na pia mimi naona Unakaa nyagwa. Tabora kuna Timu kama umewahi kusikia Mirambo lakini matatizo ni Tabora kiuchumi ndio tatizo si kwamba hakuna timu nakuonea uruma sana unaonekana mgeni au baba alihamishiwa Dar ndio ulizaliwa. Kwa kifupi wanyamwezi wengi Simba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...