Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Marcio Maximo akiongea na wanahabari jijini Dar leo wakati timu ya taifa Taifa Stars ilipokabidhiwa Bendera ya Taifa tayari kwa safari ya kuelekea Kigali Rwanda kwa mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayochezwa katikati ya wiki hii nchini humo. Shoto ni Naibu mkurugenzi wa Michzo kutoka wizara ya habari, utamaduni na michezo Bwana Charles Matoke na Meneja uhusiano wa Serengeti Breweries Teddy Mapunda kulia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Thedy Mapunda mdogo wangu umenenepa sana, yaani tumeolewa tarehe ,siku moja na mwaka mmoja, 28 June 1997, unakumbuka? wee mdogo kwangu ila umepata kazi nzuri naona umesahau gym! kazana mdogo wangu, umekuwa mkubwa mno!

    ReplyDelete
  2. HIVI NINI SABABU YA KWELI KWELI YA KUMUACHA KASEJA NESHNO TIMU?? MI NAONA KAMA HIZI SOUND ZA MAXIMO KUHUSU UZALENDO NA UREFU NI BULL SH*T. anakwenda safari na kipa anayeumwa tumbo (Dihile) WHAT FOR????!!!! HATA KAMA ANA BIFU NAYE, KASEJA IS THE BEST GOLIKIPA BONGO. Ni Mtazamo tu wadau.

    mdau deslam

    ReplyDelete
  3. na pia nidhamu ni kitu muhimu sana kwenye michezo tatizo mtu akishakuwa almaarufu bichwa hilo dharauu kwa kwenda mbele ndo hivyo sasa mdharau mwiba mguu huota tende! paula abdul naye kaleta nyodo fukuzilia mbali sikio halizidi kichwa
    mdau canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...