Leo tarehe 27/09/2009 umetimia mwaka mmoja tangu alipotutoka mpendwa mama yetu FELISTA NYANGETA. Unakumbukwa sana na Mumeo Mwl. Cyril Arsen Matai, mama yako mzazi Bibi Busimba, watoto wako Peter, Felician, George, Arsen, Specioza, Joyce, Regina, Eugenia na David. Vile vile wajukuu zako wapenzi: Angel, Michael, Stella, Pius, Evaline, Emil, Elsa, Elna, Ally, Said, Zainab, Veronica, John, Andrew, Geofrey, Zephania, Stanslaus na Kelvin pamoja na ndugu na jamaa wote.
Ucheshi, upendo na ukarimu wako daima tutaukumbuka. Tulikupenda sana lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi. Kimwili haupo nasi lakini tunaamini kwamba kiroho upo pamoja nasi.
Mungu akupe Pumziko la Milele, AMINA.
Ibada za kumbukumbu ya Mama Felista zitafanyika katika Kanisa la Mt. Gasper Mbezi Beach Dar es Salaam tarehe 27/09/2009 saa tatu asubuhi na katika Kanisa la South Cathedral Beijing China saa nne na nusu asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...