heshima yako mkuu wa kaya


kwa heshima na taadhima naomba nikuletee picha hii ili uone vijana wako walivyo makini na kazi!Hizi ni kingo za daraja lileee karibu na tegeta stendi! Vijana wako walikuwa na kazi ya kupaka rangi kwenye vyuma hivi takriban mwezi mmoja hivi na kazi kama unavyoiona wamemaliza!!


Samahani sana mkuu ila naona kama si sahihi kilichotendeka, kwa nini basi wasingenyoosha nyoosha kidogo hivi vyuma halafu wakavipiga rangi? SAWA nakubali sio kazi yao, lakini hapa si kama wamechafua zaidi?
Mkuu nina uchungu na kodi yangu sijui nihame nchi?????!!!!!!!!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ACHA UNOKO WEWE!! TANZANIA TUMEJIZOELEA KILA KITU KUINGIZIA USANII. WEWE UNATAKA KUTIA MCHANGA KITUMBUA CHA WATU HUONI KWAMBA HIYO NI OPOTUNITE YA KESHO ATATAFUTWA MKANDARASI ILI ANYOOSHE ZENI VIPIGWE TENA RANGI. KOMA KABISA NA ROHO YAKO YA KWANINI.

    ReplyDelete
  2. Ufisadi umeota mizizi, na hao ni TANROADS DSM.Kaazi kweli kweli !!
    Mradi wapepata 10% yao, ni kanyaga kanyaga twende, tafuta mradi mwingine wa kula.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli nakuunga mkono na kusapoti (kwa kushngaa) jinsi hiyo kazi ilivyofanyika, nilikuwa sina hakika nimuulize (kwa barabara ya Bagamoyo RODI hata pale Mlalakuwa wamepaka) nani kwani unapaka rangi sehemu gani au ilitolewa fungu la rangi ndio ikawa "paka bila kurekebisha".

    Niliwahi kusikia kunasheria ya anayesababisha hizo kingo au alama za barabarani kuwa katika muonekano tofauti na uliowekwa na TANROD/HALMASHAURI anastahili kutengeneza ni kweli au ni katita ile NCHI ILIYOKO NDANI YA KICHWA CHANGU?
    anyway this is very very my bilavd kantri ninayoipenda hasa kwa vitu vyake vya ....

    ReplyDelete
  4. huyu mdau vipi,
    anauliza kuhama,kwani anasubiri nini?

    ReplyDelete
  5. Mnamwaga pumba tu!kwavile mmekaa mbele ya PC na mshajishibia ugali wenu mnasahau kama kuna kinamama wajawazito hawana damu huko mahospitalini na jinsi tunavyobakishiwa mashimo makubwa makubwa matupu na wanaoyabaka madini yetu bila faida yeyote?kwa generation yetu ya baadae? eti daraja halina rangi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...