stendi kuu ya mabasi Mbabane
Kaka Michuzi,
Basi bwana baada ya mambo ya Reed Dance kuwasisimua wana blog leo jioni nilikuwa kwenye viunga vya mji wa Mbabane ambao ni makao makuu ya nchi ya Swaziland. Yaani Ofisi zote za Serikali zipo hapa pamoja na maduka makubwa ya nguo na vyakula yapo katika eneo hili.
Eneo lipo juu zaidi toka usawa wa bahari, ni la milimani ukilinganisha na kitogoji cha Lobambo eneo la Ludzidzin ambako Reed Dance hufanyikaga katika Palace (jumba la mfalme) la Mama yake King Msawti III.
Mji wa Mbapane upo juu kama unatokea eneo la Ezulwini, yaliyopo makazi ya King Mswati, na hali ya hewa yake huwa ya baridi sana, kwa haraka haraka unaweza kufananisha na eneo la Mbeya kwa wale waliofika Mbeya wanaweza kupata picha kamili.
Aidha, nchi hii ina wakaazi wanaokadiriwa kufikia milioni 1.2 na eneo lake kama moja za wilaya hapo Bongo! picha hizi zinawasilisha taswira ya mji wa Mbabane, na hapa ni city centre yao, hakuna tena kama hapa.
Naomba kuwasilisha...
Mdau wa muda wa Swaziland
baadhi ya vikwangua anga na milima kwa mbali

mojawapo ya barabara kuu za Mbabane
shopping mall la nguvu kama mlimani city yetu

vipanya kama kawa




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Sawa sawa mdau, kumbe tulikuwa pamoja kwenye Reed Dance juzi lol! Mswati ni noma. Vipi mbona hujabandika taswira za tukio?????

    Amani iwe nawe.

    ReplyDelete
  2. mdau big up kwa picha.
    sasa mi nauliza vipi upatikanaji wa totoz hapo?? mademu wa hapo ukitaka kumtokea ukajinyooshe inakuwaje, ni shughuli pevu au nao wanatoa tu bila hiana?? hebu nipe nyeti mzee manake ndo najipanga kubajeti trip ya huko. wale watoto matiti wazi bado hawajanitoka kichwani kaka!! nipe data inakuwaje??

    ReplyDelete
  3. wananifurahisha sana watu wa huko swazi, yaani wanatunza vizuri vitabu vyao, mfano mfalme wao anafungua kimoja kimoja kila mwaka tena vipya na original toka kwenye plastic zake naturally anapasua mwenyewe.
    sio second hand vilivyo tolewa cover, waswahili wanasema kipya kinyemi.
    wewe mdau wafaidi vipyaaa, ntakuja huko tuachie huko na sisi ati vipya mambo ya twasira.

    ReplyDelete
  4. Makao makuu yanaonekana kama upo mkoani Singida! Naona infrastructure yao wala haijatulia, Naona Dar ipo mbali sana makao makuu hayafikii hata jiji la Mwanza!

    ReplyDelete
  5. Manzini kidogo pakubwa na pazuri kuliko mbabane japo ndo capital

    ReplyDelete
  6. hizi picha zina fanana na kampala Uganda

    ReplyDelete
  7. Mji huu ni mzuri sana sana na mimi natamani kuishi kwa King Muswati,imagine hiyo idadi inazidi wilaya za Dar na umepangiliwa mbaya na unaonekana kuwa msafi kinoma tu,na vipanya vyao havionekani vichakavu kama vyetu..kutu etc.

    Jamani tutafika?? asante mdau umenikumbusha mwaka 2006 nilienda kikazi nilitamani nisirudi bongo kwetuu.

    ReplyDelete
  8. Bosi tunaomba utuongezee zile picha za dansi....achana na hizi za magorofa

    ReplyDelete
  9. Kumbe wanajua kuvaa nguo pia...!!
    Mi nlidhani uchi uchi ndo maisha yao ya kila siku >>

    ReplyDelete
  10. Kama wewe ni mtu wa kujichanganya ......Mambo yote yapo Manzini...............hapo hakuna ishu..........

    ReplyDelete
  11. Kama kuna mdau wa Man Zini tupe taswira. Kuna mdau ametoa ulinganifu.
    E bwana huo mji vipi, mbona sioni mifuko ya Marlboro mitaani?

    ReplyDelete
  12. Bongo watu hugombea kuwahi seat ya mbele kwenye daladala hali ni tofauti kwa Swaziland...seat ya mbele huwa ndiyo ya mwisho kukaliwa na abiria.

    ReplyDelete
  13. Afrika is Afrika tu.

    ReplyDelete
  14. Kwa watu ni Kwa watu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...