Mkurugenzi wa Benchmark Production Madame Rita Paulson(katikati)akiongea na waandishi wa habari juu ya kutangaza zawadi kwa washindi wa Bongo Star search(BSS)(kushoto)Brand Manager wa Kilimanjaro George Kavishe(kulia)Meneja Udhamini wa Vodacom Tanzania Emillian Rwejuna.Mashindano haya yatafanyika Diamond Jubilee Jumanne ijayo.
Baadhi ya washiriki walioingia katika kinyanganyiro cha kumpata mshindi wa Bongo Star Search (BSS)wakiwa wanaimba mbele ya waandishi wa habari kuonyesha vipaji vyao kabla ya shindano lao la mwisho litakalofanyika Diamond Jubilee Jumanne ijayo.Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo.

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imesema kwamba fainali ya kumsaka nyota wa Bongo Star Search itafanyika Oktoba 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wa shindano hilo ambalo linalenga kuibua vipaji vya muziki miongoni mwa vijana hapa nchini.Meneja Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna alisema Vodacom imetenga zawadi mbalimbali kwa washindi.

“Katika fainali hiyo tumetenga zawadi mbalimbali kwa washindi, zawadi hizo zimeganyika katika mafungu mbalimbali kutegemeana na nafasi ya mshindi,” alisema.

Alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni 25, mshindi wa pili shilingi milioni tano na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha shilingi milioni tatu.

Mshindi wa nne hadi wa kumi,kila mmoja atapata shilingi 400,000, alisema
Alisema Vodacom inaamini kwamba zawadi hizo zitatumika kama chachu ya kuendeleza vipaji vya wasanii husika na hivyo kusaidia katika kutimiza malengo ya baadaye ya wasanii hao.

Aliwapongeza wasanii wote walioshiriki BSS ambao walitoka katika kila kona ya nchi yetu. “Kwa dhati pia nawapongeza waliofanikiwa kuingia fainali, ninaomba wajiamini ili waweze kuonyesha na kudhihirisha vipaji vyao kwa Watanzania,”

Aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano hilo.
“Nawapongeza waandaaji kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwamba Vodacom Tanzania tuko pamoja nao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongereni sana BSS,hiyo zawadi ya mshindi ni safi sana maana inaonyesha BSS imeongeza kiwango.

    Ila jamani hamuoni kuna gape kubwa sana ya zawadi kati ya mshindi wa kwanza na wa pili yaani from 25 to 5?

    ReplyDelete
  2. Mbona kuna tofauti kubwa sana ya zawadi ya mshindi wa kwanza na wa pili?that is not fair wametumia vigezo gani kupanga hizo zawadi?
    Mdau

    ReplyDelete
  3. shindano linaonekana ni la kitapeli kujaza matumbo ya wachache,gap la zawadi haliingii akilini kabisa ni kwanini basi mtu asisign contract apewe ushindi milioni 15 wachukue waandaaji 10 wampe yeye na bado anafaida

    rank zangu 1.25m 2.20m 3.15m 4.10m 5.5m

    ReplyDelete
  4. Ili kuweka ushindani wa dhati na msisimko jamani!

    ReplyDelete
  5. Nawapongeza sana wadhamini Vodacom na waandaaji wa shindano hili Benchmark Production. na Kilimanjaro maana linainua vipaji vya wahusika. Ila jamani mbona nyanja nyingine za sanaa mnazisahau? Kila ukisikia udhamini na mashindano na zawadi nono ni katika kuimba tu.Tanzania kuna sanaa nyingi kuna wahunzi,kuna wafinyanzi,kuna wasusi wa aina na vitu mbalimbali,kuna wanachoraji,kuna wachongaji,kuna watengenezaji batiki,kunawashonaji,kunawatengeneza mapambo na vyombo,kuna wanaotengeneza vifaa kutokana na vitu vilivyotumika (recycle),kuna wafumaji,kuna wapishi (chefs),kuna wapigapicha n.k hebu jaribuni kuwaangalia na hawa ili kukuza vipaji vyao na pia dunia ya leo ina soko kubwa la ufundi wao.

    ReplyDelete
  6. Huyu Mama hayo macho... duu!! Niko hoi!!!

    ReplyDelete
  7. Yule PITA MSECHU mbona simuoni hapo?

    Au ndo kaenda Kwao Kigoma kuonana na KALUM***ILA ili arekebishe mambo?

    Poa mwanangu kweli bwana usisahau utamaduni wetu

    ReplyDelete
  8. Wengine wanajisumbua Mshindi akusha andaliwa ni huyo Mtoto wa kipare ambaye nyumba yao kakodisha Ritha.

    ReplyDelete
  9. kaka Michuzi cant you waona wahusika before siku ya shindano ili waweze kurekebisha huo mfumo wa kiwango cha zawadi?as naona hakuna uwiano kati ya mtu wa kwanza na wa pili kama vipi washushe kiwango wa kwanza awe mil 20 wa pili kumi na kuendelea...huwezi kumpa wa kwanza nyumba wa pili walet haileti sense hata kidogo

    ReplyDelete
  10. hiyo zawadi zao haziko proportional kabisa.milioni 25 kwa mshindi wa kwanza na milioni 5 kwa wa pili?mbona gap inakuwa kubwa sana hapo??halafu badala ya kumpa hela zote hizo mshindi wa kwanza kwa nini asipate contract ya kurekodi album kwa MJ ya mwaka mmoja angalau?ili kipaji chake kiendelee kukua?kwa sababu wamekua wakiimba nyimbo za watu tuu sasa itakuwa changamoto yake mshindi atunge zake angalau 3 mpaka 6 ya jujiintroduce kwa washabiki wa mziki wa kitz.

    ReplyDelete
  11. habrir mimi naona hakuna hata kidogo uiano wa zawadi kuna gap kubwa sana kati ya mshindi wa kwanza hadi wa tatu jaribuni kupanga upya kabisa

    ReplyDelete
  12. Madam Rita, nxt yr naomba mashindano yawe ya kiwango cha juu, coz wadhamini wanakusuport sana lkn matunda hayalidhishi. Mdau yeyote anaeangalia Project Fame anajua mimi nazungumza nini, mshindi wa PF ambao wapo kiwango cha juu kushinda BSS ni KSh 5M na BSS Tsh 25M lkn BSS bado kabisa, washiriki wengi uwezo wao wa kuimba ni mdogo mno...madam fund ipo ya kutosha, tunahitahita star wa kweli na si longolongo.

    ReplyDelete
  13. ninaomba waongeze zawadi kwa mshindi wa 2 mpaka wa 10 tafadhali, ili wasijisikie vibaya

    napendekeza wa kwanza apewe 20mill,wa pili 10m, wa tatu 3 mill ,wa nne 2mill na 5 mill 1 mill

    6-10 laki 5 kila mmoja ndio italeta msisimko zaidi

    otherwise mnawademorolise washiriki walio chini ya 5 bora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...