Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imesema kwamba fainali ya kumsaka nyota wa Bongo Star Search itafanyika Oktoba 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wa shindano hilo ambalo linalenga kuibua vipaji vya muziki miongoni mwa vijana hapa nchini.Meneja Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna alisema Vodacom imetenga zawadi mbalimbali kwa washindi.
“Katika fainali hiyo tumetenga zawadi mbalimbali kwa washindi, zawadi hizo zimeganyika katika mafungu mbalimbali kutegemeana na nafasi ya mshindi,” alisema.
Alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni 25, mshindi wa pili shilingi milioni tano na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha shilingi milioni tatu.
Mshindi wa nne hadi wa kumi,kila mmoja atapata shilingi 400,000, alisema
Alisema Vodacom inaamini kwamba zawadi hizo zitatumika kama chachu ya kuendeleza vipaji vya wasanii husika na hivyo kusaidia katika kutimiza malengo ya baadaye ya wasanii hao.
Aliwapongeza wasanii wote walioshiriki BSS ambao walitoka katika kila kona ya nchi yetu. “Kwa dhati pia nawapongeza waliofanikiwa kuingia fainali, ninaomba wajiamini ili waweze kuonyesha na kudhihirisha vipaji vyao kwa Watanzania,”
Aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano hilo.
“Nawapongeza waandaaji kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwamba Vodacom Tanzania tuko pamoja nao.
Hongereni sana BSS,hiyo zawadi ya mshindi ni safi sana maana inaonyesha BSS imeongeza kiwango.
ReplyDeleteIla jamani hamuoni kuna gape kubwa sana ya zawadi kati ya mshindi wa kwanza na wa pili yaani from 25 to 5?
Mbona kuna tofauti kubwa sana ya zawadi ya mshindi wa kwanza na wa pili?that is not fair wametumia vigezo gani kupanga hizo zawadi?
ReplyDeleteMdau
shindano linaonekana ni la kitapeli kujaza matumbo ya wachache,gap la zawadi haliingii akilini kabisa ni kwanini basi mtu asisign contract apewe ushindi milioni 15 wachukue waandaaji 10 wampe yeye na bado anafaida
ReplyDeleterank zangu 1.25m 2.20m 3.15m 4.10m 5.5m
Ili kuweka ushindani wa dhati na msisimko jamani!
ReplyDeleteNawapongeza sana wadhamini Vodacom na waandaaji wa shindano hili Benchmark Production. na Kilimanjaro maana linainua vipaji vya wahusika. Ila jamani mbona nyanja nyingine za sanaa mnazisahau? Kila ukisikia udhamini na mashindano na zawadi nono ni katika kuimba tu.Tanzania kuna sanaa nyingi kuna wahunzi,kuna wafinyanzi,kuna wasusi wa aina na vitu mbalimbali,kuna wanachoraji,kuna wachongaji,kuna watengenezaji batiki,kunawashonaji,kunawatengeneza mapambo na vyombo,kuna wanaotengeneza vifaa kutokana na vitu vilivyotumika (recycle),kuna wafumaji,kuna wapishi (chefs),kuna wapigapicha n.k hebu jaribuni kuwaangalia na hawa ili kukuza vipaji vyao na pia dunia ya leo ina soko kubwa la ufundi wao.
ReplyDeleteHuyu Mama hayo macho... duu!! Niko hoi!!!
ReplyDeleteYule PITA MSECHU mbona simuoni hapo?
ReplyDeleteAu ndo kaenda Kwao Kigoma kuonana na KALUM***ILA ili arekebishe mambo?
Poa mwanangu kweli bwana usisahau utamaduni wetu
Wengine wanajisumbua Mshindi akusha andaliwa ni huyo Mtoto wa kipare ambaye nyumba yao kakodisha Ritha.
ReplyDeletekaka Michuzi cant you waona wahusika before siku ya shindano ili waweze kurekebisha huo mfumo wa kiwango cha zawadi?as naona hakuna uwiano kati ya mtu wa kwanza na wa pili kama vipi washushe kiwango wa kwanza awe mil 20 wa pili kumi na kuendelea...huwezi kumpa wa kwanza nyumba wa pili walet haileti sense hata kidogo
ReplyDeletehiyo zawadi zao haziko proportional kabisa.milioni 25 kwa mshindi wa kwanza na milioni 5 kwa wa pili?mbona gap inakuwa kubwa sana hapo??halafu badala ya kumpa hela zote hizo mshindi wa kwanza kwa nini asipate contract ya kurekodi album kwa MJ ya mwaka mmoja angalau?ili kipaji chake kiendelee kukua?kwa sababu wamekua wakiimba nyimbo za watu tuu sasa itakuwa changamoto yake mshindi atunge zake angalau 3 mpaka 6 ya jujiintroduce kwa washabiki wa mziki wa kitz.
ReplyDeletehabrir mimi naona hakuna hata kidogo uiano wa zawadi kuna gap kubwa sana kati ya mshindi wa kwanza hadi wa tatu jaribuni kupanga upya kabisa
ReplyDeleteMadam Rita, nxt yr naomba mashindano yawe ya kiwango cha juu, coz wadhamini wanakusuport sana lkn matunda hayalidhishi. Mdau yeyote anaeangalia Project Fame anajua mimi nazungumza nini, mshindi wa PF ambao wapo kiwango cha juu kushinda BSS ni KSh 5M na BSS Tsh 25M lkn BSS bado kabisa, washiriki wengi uwezo wao wa kuimba ni mdogo mno...madam fund ipo ya kutosha, tunahitahita star wa kweli na si longolongo.
ReplyDeleteninaomba waongeze zawadi kwa mshindi wa 2 mpaka wa 10 tafadhali, ili wasijisikie vibaya
ReplyDeletenapendekeza wa kwanza apewe 20mill,wa pili 10m, wa tatu 3 mill ,wa nne 2mill na 5 mill 1 mill
6-10 laki 5 kila mmoja ndio italeta msisimko zaidi
otherwise mnawademorolise washiriki walio chini ya 5 bora