Siku ya saba – Kazi imekamilika. Gerald Hando (shoto), na Madaraka Nyerere kileleleni Uhuru (5,896m).
Madaraka Nyerere akipokea cheti cha kufika Uhuru Peak (5,896m) kutoka kwa Yahoo.

Gerald Hando akipokea cheti cha kufika Uhuru Peak (5,896m) kutoka kwa Yahoo.

Yahoo anamkabidhi Notburga Maskini cheti cha kufika Stella Point (5,745m) baada ya kurudi mjini Moshi kwenye hoteli ya Springlands.

Siku ya nne - Safari ya kutoka kambi ya Shira 2 kuelekea kambi ya Barranco.
Siku ya tano – Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutokea kambi ya Karanga (3,963m).
Siku ya saba – Yahoo (Muongozaji) kushoto, na Gerald Hando wakikagua mandhari juu Mlima Kilimanjaro dakika chache baada ya kufika Uhuru Peak (5,896m). Safari ilianza saa 6 usiku kufika kambi ya Barafu (4,600m) na kukamilika asubuhi kabla ya saa 3:30. Nyuma yao unaonekana Mlima Meru.
Siku ya kwanza – Safari ya kuelekea Big Tree Camp 2,650m). L-R Madaraka Nyerere, Gerald Hando, Notburga Maskini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Duh mlima wetu jamani haukuwa hivi. Sasa hivi tunaelekea pabaya. Miaka ya nyuma kama 90 hivi mimi nikwenda kupanda mlima kulikuwa ni barafu tuu hadi maji ukifungua yanabarafu, now kumekuwa jangwa hivyo??? Hatari......... Huu uchafuzi wa hali ya hewa utaisha lini jamani. Bado tuu kidogo kivutio chetu cha mlima huo kitapotea kwani barafu na baridi ya huko ndiyo ilikuwa inavutia kutokana pia na mazingira mazuri yaliyokuwemo.

    Now nahisi basi kila mmoja ataweza kupanda mlima kwa namnahiyo coz hakuna tena ile hali ya hewa kama ya zamani. Enzi hizo ilikuwa issue kupanda kufikia kilele kwani unaweza ganda wakati mwingine.

    ReplyDelete
  2. Hongera Gerald na wenzako, kikweli unastahili sifa kwani si wote wanaweza kuhimili hiyo hewa huku Mt. Kilimanjaro. UKO JUU. na unahaki ya kujisifia, hapa nasubiri kusikia ukijisifu na Bi B. Hassan akikosa cha kuendeleza kwa kuweka tangazo.
    kuna mahali unaweka photoz za huko juu?
    WELL DONE - find the T-shirt "I HAVE CLIMB MT KILIMANJARO, HAVE YOU!

    ReplyDelete
  3. Hilo bango la kuonyesha highest peak ya afrika linatia aibu wazee. Tumejaaliwa kuwa na kilele kirefu afrika nzima, kuweka bango la maana pia kwikwi daah!!! Watu wanatoka ulaya kila kukicha kuja kukwea mlima wetu.Lakini sijui kama wanatamani hata kupiga picha na hilo bango.Mheshimiwa Balozi peleka haka kaujumbe mezani kwa wazee !!! AIBU hii

    ReplyDelete
  4. Michuzi, Roger MTAGWA kamtandika mtu kwa nok-out tuwekee mambo humu tafadhali.Tanzania jina kubwa sasa baada ya HASHIM THABIT , sasa ROGER MTAGWA!!

    ReplyDelete
  5. Mbona hatumwoni Jaffer Idd Amin Dada the Conquerer of the British Empire? Au alijaribu kupanda na kuishia Moshi mjini? Maana Moshi mjini kwenyewe ni zaidi ya meta 2000 kutoka usawa wa bahari. Sasa kama umetokea Dar kufika Moshi mjini unakuwa tayari umekwisha kata zaidi ya hizo meta 2000 kwa hiyo unaweza kushindwa kuendelea km hizo 2000 zitakuwa zimekuchosha tayari.

    ReplyDelete
  6. madaraka hongera, lakini nina wasi wasi hukuwa na proper high altitude clothing. umevaa jeans kwenye summit ya Kilimanjaro?

    ReplyDelete
  7. Jeans nilivaa siku ya kwanza tu, siku nyingine zote nilivaa nguo stahili.

    ReplyDelete
  8. WABONGO BWANA....UTAJIITAJE YAHOO???

    ReplyDelete
  9. duh! kweli hapa ndo kuna maajabu! mdau anashangaa jamaa kujiita YAHOO wakati ye anaitwa KILO! hahahaaaa! hii kiboko.

    ReplyDelete
  10. HONGERA SANA MADARAKA HAYAWI HAYAWI MATOKEO YAKE YAMEKUWA SAFI SANA NA HATA MIMI NIKIJA NYUMBANI NITAJITAHIDI KAMA KUKIWA NA UWEZEKANO NIPANDE MLIMA KILIMANJARO

    ReplyDelete
  11. SIKU ZOTE NYANI HALIONI KUND...U LAKE HUWA ANALIONA LA MWENZIE NDIO HUYO KILO KUMSHANGAA YAHOO,NENDA MIKOA YA PWANI au Kusini KWA WAJOMBA ZANGU WAZARAMO NA MAJINA YA KWETU UTASHANGAA MPAKA UTALIA

    ReplyDelete
  12. Gerald hongera sana sana.

    ur class mate, srss.
    Salma.

    ReplyDelete
  13. Hongera zenu sana jamani kwa kuweza kufikia Afrikas highest point! Mi natamani but nina asthma nahisi haitawezekana, jamani wenye afya zenu pandeni mfaidi. God bless u.

    ReplyDelete
  14. NAMTAFUTA MTU ALIYEJIITA YAHOO SI MUONI NA KILO JEE NI SAWA? JINA NI JINA TU HATA UKIJIITA PAKA NI SAWA TU. UMESAHAU KUWA KUNA AKINA NGURUWE, MBAWALA.

    ReplyDelete
  15. Hongereni sana Madaraka na Hando ni jambo la kufurahisha na kumshukuru Mungu kwa afya zenu njema alizowajalia, ni wangapi wanatamani lakini hawawezi? ni wangapi wana uwezo lakini hawajalifikiria hilo? Take care my boys and God bless you for adoring his creation.

    ReplyDelete
  16. unajua inaleta raha kama ukiona aibu ni vizuri kurekebisha tatizo, wa Tanzania wengi tunalalamika sana na kukana nchi yetu. ushauri kwa ANANYMOUS wa sat 10th 02:07pm, ile dhana ya kujitolea ua kufadhili inaanzia hapa, peleka signpost inayoleta raha pale juu. mbona tumapokea contributions (ili kutopotezana ask Wizara ni bango gani linahitajika ili usisumbuke. all the same THAT IS THE HIGHEST POINT sign mpaka apatkane mwenye hasira ya kubadilisa. SMILE

    ReplyDelete
  17. Notburga hongera sana kwa kupanda mlima wa nyumbani. Yaani kule kukuona kwenye blog ya Uncle DC wa nanihii umenikumbusha mbaaaali sana - enzi zile za "Steno" Shycom.

    ReplyDelete
  18. heee jamen nipeni siri ya kuapnda uo mlima
    ITS MY LIFE DREAM EVER
    nataka kuupanda ila sijui nianzaje si mwajua sie tuliopo makazini?ili nijue kupanda likizo/ruhusa na majira ya kupanda mlima,PIA SANA SANA MAZOEZI gani nichukue?

    nawaonea fahari sana wanaopanda mlima huu

    mnijibu

    ReplyDelete
  19. Ahsanteni kwa maoni yenu na pongezi. Ni kweli kupanda mlima inahitaji kujipanga, ukifanikiwa ni furaha tupu.

    Nilikuwa na ndoto hiyo tangu miaka ya tisini mwanzoni Sasa imetimia namshukuru Mungu, na Madadaraka aliyeanzisha wazo hili. Ni jambo zuri na lina faida sana.

    Kama uko kazini unaweza ukapanga likizo yako ikaangukia tarehe za kupanda mlima kama sehemu ya mapumziko ya likizo yako.

    Madaraka mwasisi wa shughuli hii ni mwalimu mzuri bila shaka atakueleza zaidi tarehe ya kupanda mwakani na mazoezi yanayofaa. Aidha; fungua blog yake http://madarakanyerere.sportsblog

    Agnes nakushukuru kwa kunikumbuka. Nilishtuka marafiki zangu hawasomi blog hii japo wengine walinitumia text massage.

    Ni kweli enzi zetu za Masteno Shycom shines nakukumbuka vizuri sana tulitimiza wajibu wetu pale.

    Je utapanda mlima? Kama utapanda niambie nitarudia tena twende wote.

    Agnes uko wapi sasa? Ni vizuri kupanda mlima kutumia afya tuliyo nayo kabla ya kuchoka sana si unajua miaka ina kwenda juu na nguvu zinapungua?

    Inabidi kuwahi ili tuwe na cha kusimulia kwa vizazi vinavyokuja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...