JK akizungumza na mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa dar es Salaam akitokea Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha mika mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Africa Inland church Tanzania zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Kirumba jijini Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mbona giza???? JK u can't tell something is wrong?

    ReplyDelete
  2. hiki ni kipindi cha mgao wa umeme huko home

    ReplyDelete
  3. Jamani humu ndani mimi naomba niulize. Hivi hawa jamaa---Mkuu wa Mkoa (DAR)-Mkuu wa Majeshi-(CDF, Mkuu wa Polisi (IGP), na viongozi wengine kama makakmu wa raisi na wengine huwa hawana kazi ya kufanya hadi kila raisi anaposafiri wanakwenda kumuaga, anaporudi wanakwenda kumpokea--je kuna kitu ambacho mimi sielewi, hii ndio protocal inavyokwenda? kuna tulikuwa tunaongelea hii kitu weekend--yeye akawa anafikiri kuwa hawa jamaa utendaji wao wa kazi unautata ndio maana inabidi waende kumkumbusha jamaa kwa, "tupo." Mafuta wanayotumia kwenda na kurudi airport, na misafara yao ni usumbufu kwetu sisi inaotubidi tukae kwenye foleni kusubiri wapite...........je ni wengine humu ndani manoona hili tatizo.

    ReplyDelete
  4. Viongozi wetu wanaona giza kitu cha kawaida tu, jamani kazi ipo!!

    JK, sasa hapo sijua anongea nini na Lukuvi, rais unapokelewa gizani. Uoni kwamba ni tatizo kubwa hilo.

    ReplyDelete
  5. Hawa viongozi sio kwamba hawana kazi. Kazi zipo nyingi, tatizo ni vision hakuna.

    Logistics zote za kukusanya viongozi kwenda airport kumuaga au kumpokea rais kwa kweli ni waste of time, other resources na usumbufu mkubwa kwa wananchi ambao wanatumia barabara kwa sababu inabidi wakae kwenye foleni na kusimamisha shughuli zao.

    Kuna mambo mengi zaidi ya kufanya kuliko viongozi kupoteza muda kwenye jambo kama ili.

    Wakati umefika kuacha na utamaduni huu.

    ReplyDelete
  6. HAWA HUACHIWA JUKUMU LA KUWADHIBITI WAPINZANI HIVYO KILA ANAPOONDOKA HUWAKABIDHI JUKUMU HILO EAPOTI NA ANPORUDI WAO HUMPA RIPOTI HAPOHAPO MAHALI WALIPOKABIDHIANA, MMEMSAHAU GEWE! hiyo ndiyo demokrasia simnajua viongozi wengi wa ccm ni wanajeshi wastaafu.

    ReplyDelete
  7. HAWA JAMAA WANAENDA KUHAKIKISHA KUNA USALAMA WA MIZIGO YA BWANA MKUBWA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT, WANAIMARISHA USALAMA.

    ReplyDelete
  8. hapo kikwete anasema yaani bado tu, mzigo haujafika kwenye mkanda, mkuu wa mkoa anajibu ah! bosi usihofu kuna vijana wangu wakazi nimewaweka wanakagua kuona kama kila kitu kiko sawa.

    ReplyDelete
  9. i love that idea kwa aloitoa its something to consider and a waste of resourses.rais anaondoka msafara anarudi kupokelewa watu lukuki na msafara.good point ma bro

    ReplyDelete
  10. Jamani lazima mkumbuke kuwa Raisi sio mtu. Raisi ni taasisi (institution). Hao viongozi kwenda anapoondoka na kurudi ni Itifaki (Protocol). Raisi hasafiri peke yake ni taasisi nzima.

    ReplyDelete
  11. Mimi nadhani hao viongozi wanaokwenda kumpokea rais hawajui hata kwa nini wanashika nyadhifa walizo nazo achalia mbali kutokua na kazi!Wao wamejijazia nafasi walizopewa tu.Maana haya ni mambo ya ki-ROBOT.Very sickning!!!

    ReplyDelete
  12. sawa raisi ni taasisi. na giza je?ni nini? au protocol yake ni hipi?

    ReplyDelete
  13. Hii ndio staili yetu bwana, wee acha kwenda kumsindikiza/kumpokea mkuu uone kama kibarua chako kitakaa! Kazi nzurii.. asikwambie mtu hata kama kwa kujikombakomba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...