Mdau Andrew Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa, yuko vekesheni Marekani katika jimbo la New Mexico. Hapa ametembelea Trinity Site, sehemu ambayo bomu la atomiki lilijaribiwa saa 11;29: 45 alfajiri ( 5;29.45am) ,,Mountain War Time, July 16,1945. Baada ya hapo ,bomu liliangushwa Hiroshima na Nagasaki. Hiyo picha moja ni aina ya bomu lilionguka Hiroshima,''[imetengenezwa to scale] Fat Man'',. Bomu liitwalo Fat Man lilianguka Hiroshima,na Little Boy, lilianguka Nagasaki.
Huyo hapo ni mdau Andrew na wenyeji wake wa New Mexico, Mama Lulu Mattson. Hii Trinity Site inafunguliwa kwa umma mara mbili tu kwa mwaka. Leo ni siku mojawapo. Huo mnara ndipo mahali ambapo bomu hilo liliripukia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Huyu ni kweli sio FISADI. Mtoko wake unaonyesha hili live...

    ReplyDelete
  2. kweli Nyerere hakuwa FISADI hata kidogo, angalia hali anayoonekana nayo mwanae!tuna kila sababu ya kumuenzi baba wa Taifa.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli Nyerere alimpenda jirani yake km yeye mwenyewe. Kakaa madarakani karibu miaka 25 lkn angalia watoto wake walivyo simple. Kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Sasa njoo kwa watoto wa mafisadi wa sasa (wale ambao Mwalimu aliwapa elimu bure) - ngazi ya kati tu: director, ministers... - yaani watoto wao wanatoka kifisadi pia.

    Nyerere RIP daima.

    ReplyDelete
  4. Huwezi kuamini kuwa mtoto kazaliwa na kukulia Ikulu huyu. Mwalimu uliwalea watoto wako vizuri sana. Wewe ni mfano wa kuigwa. Very simple.

    ReplyDelete
  5. kuna kuwa simple na smart. Angenyoosha shati, akaava suruali size, au pengine na kuchomekea, angekuwa smart. Huyu yuko 'rafu'. Ni maoni yangu tu

    ReplyDelete
  6. jamaa yupo kienyeji kweli

    ReplyDelete
  7. huyu kakulia butiama au bandari ya salama magogoni?

    ReplyDelete
  8. Huyu ukikutana naye Uswazi huwezi kuamini kuwa alikuwa mtoto wa Mkubwa. Sasa Legacy ya maneno matupu ina faida gani? Looks Tired as landfill.Hizi sifa za Ujamaa ni za ajabu.

    ReplyDelete
  9. Najua mafisadi na watoto wenu mtaponda tu....

    ReplyDelete
  10. Jamani kashindwa hata suti ya mchikichini-ilala bei poa tzs 5000.
    huyu sio smart tu,nadhani yuko butiama analima.

    ReplyDelete
  11. Huyu Blaza ni simple and complex. Kama unaelewa hiyo sentensi ndiyo utamuelewa. Ni bonge la mjeshi wa kurusha madege ya kivita, hapo anaangalia shughuli yake kwa jicho jingine. Tena ni mswalihina wa kivyake. Halafu ni mtoto wa mjini kinoma alikuwa rafiki yake sana Marehemu Ray Abdul na Marehemu Marijani Rajabu walisoma naye kwa hiyo ukishajua hivyo ndiyo utajua unamtazama nani.

    ReplyDelete
  12. duuh mtoto wa nyerere katoka kilugaluga kweli utadhani yupo nkonkilangi.c mchezo.

    ReplyDelete
  13. Mdau wa 12:58 I agree with you, and thank you for your brave insight. Kwa nini uwe mchafu eti tu kwa kuwa ulilelewa uwe simple? Mi nadhani hayo ni mawazo ya kizamani na kasumba za kikoloni tulizoachwa nazo baadhi yetu wabongo. Ni sawa na Mwl. Nyerere alivyokuwa akipinga matumizi ya tv majumbani akidai eti ni luxury, how the hell did he expect his people to be informed??!

    Nyerere alikuwa mtu mzuri lakini vitu vingine ni too much hyped out and too ideological about him! Come on now, wake up people!!

    Survivor D - UK

    ReplyDelete
  14. Habari za siku mzee michuzi..Labda tu niwaeleze wandau kuna TAFAUTI KUBWA KATI YA KUWA SIMPLE NA SHAGHALABAGALA SASA UNAWEZA VAA SHATI SIZE YAKO NA VIATU SIZE YAKO NA NGUO ZIKAPASIWA VIZURI HAIJALISHA NI MTUMBA AMA NI NGUO YA BEI YA GHALI NA UKAONEKANA KAWAIDA TU...MAANA NAONA HAPA WATU WAMEPISHANA KWENYE USIMPLE NA UFALUFALU...ASANTE SANA

    ReplyDelete
  15. Kweli huyu mtoto wa Nyerere amekaa kinja njaa sana, yaani kweli Baba raisi miaka yote hiyo si angejimiksi at least kama Makongoro?

    ReplyDelete
  16. Huu unaitwa uzembe wa mavazi na kutojipenda hakuna jengine lolote....

    ReplyDelete
  17. Direct from Butiama to US,Duh!!

    This is NOT what we call SIMPLE,rather;is SHABBY!! jamani lol!!

    ReplyDelete
  18. NYERERE ALIKUWA MTU WA WATU NA ALIKUWA MKWELI NDANI YA ROHO YAKE, WHAT HE WAS SAYING HE MEANT THEM, NIKUPE MFANO MMOJA AU MIWILI, WA KWANZA ROSEMARY NYERERE NI MTOTO WA KIKE AMBAYE ALIKUWA AKIMPENDA SANA NA ALIKUWA NA BADO NI MWENYE AKILI SANA, BAADA YA KUMALIZA KOROGWE GIRLS ALIPATA NAFASI YA KUSOMEA UDAKTARI MUHIMBILI IKATOKEA AKAFELI MITIHANI BASI MKUU WA CHUO AKAMPIGIA SIMU MWALIMU(NYERERE) KUMUUELEZA KUWA ROSE AMEFELI SASA AFANYAJE? NYERERE VERY SIMPLE AKAMUULIZE KWANI WENGINE WAKIFELI KWA KIWANGO HICHO INAKUWAJE? AKAJIBU TUNAWAKATISHA MASOMO, WATU WALIOPITIA VYUO WANAJUWA HII TERM DISCO, NYERERE AKASEMA BASI NA HUYO NI HIVYO HIVYO, ROSE AKAPIGWA CHINI NA AKAENDA MZUMBE KUFANYA ACCOUNTANCY AKAMALIZA NA KAZI HAKUPATA ALIJITAFUTIA MWENYEWE TU, KAMA SIKOSEI HUYU ANDREW ALISOMEA MAZENGO BASI ALIKUWA ANAPATA SPECIAL TREATMENT TOKA KWA WALIMU BASI SIKU MOJA NYERERE AKAENDA MAZENGO AKAKUTA ANAFANYIWA HIVYO NYERERE AKASEMA MARUFUKU KUMPA SPECIAL TREATMENT, APEWE HUDUMA KAMA WATOTO WENGINE, NYERERE ALIKUWA TOFAUTI NA VIONGOZI WENGINE WOTE SI TANZANIA TU, AU AFRICA BALI DUNIANI ALITAKA USAWA KWA WOTE NA MAENDELEO KWA WOTE, MIMI KWA MAONI YANGU NAHISI HATA WATOTO WAKE HAWAKUMUELEWA NDO MAANA WENGI WAO HAWAJAFANYA VIZURI MAISHANI WALIKUWA NA KINYONGO KWA CHA KWA NINI BABA AMECHUKUWA MSIMAMO HUO JUU YA WATOTO WAKE, LAKINI NATUMAINI SASA WANAELEWA NYERERE ALIKUWA NA MAANA GANI KAMA KIONGOZI WA NCHI CHANGA NA MASIKINI. TOFAUTI NA SASA WATOTO WA VIGOGO WOTE WAKO JUU KATIKA NYANJA ZOTE NI WAO TU KATIKA NAFASI KUBWA KUBWA ZA MAKAZI HII SI KWELI KUWA WANA-AKILI KUPITA WENGINE NI UPENDELEO WA MAKUSUDI KWA KUTUMIA NAFASI ZA WEZEE WAO. NI KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LAKINI KAMA KIONGOZI LAZIMA UONYESHE MFANO HUWEZI KUKEMEA MAOVU KAMA WEWE MWENYEWE HUONYESHI MFANO, HAYA NI YALE YA AKINA KABILA, BABA KAFA UNACHUKUWA MADARAKA, YA OMARI BONGO, BABA KUFA MTOTO ANACHUKWA CHEO CHAKE NA MIFANO MINGI TU, NA TANZANIA SASA IMEZIDI HASA SEHEMU ZA KAZI NAFASI ZOTE ZIMESHIKWA NA WATOTO WA MTANDAO.

    ReplyDelete
  19. hii ni ithibati tosha kwamba yule mwalimu lengo lake lilikuwa kutunyamazisha na kisha kututawala watz kwa fimbo ya umaskini!!
    hivi kwe kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi tanzania mwanawe anaweza kuonekana lofa kiasi hiki?
    huu kama si ulofa wa kutupwa ni kitu gani?
    hata hao wachina na warusi walioutangaza ujamaa si malofa kama huyu jamaa.
    kisha eti kuna watanzania wanajitokeza kama kumsifu BABA YAO WA TAIFA!!
    nashindwa kushangaa.
    huu ndio ufisadi uliopindukia mipaka.
    si ajabu ikawa elimu ya lazima katika tanzania ya karne ya ishirini ni ile tu ya kufuta ujinga wa kusoma na kuandika.
    tungeweza kufanya nini sisi katika dunia hii?
    kilimo kikawa duni.
    viwanda kimoja baada ya kingine kikafa.
    majumba yaliyotaifishwa yakaangamia.
    matokeo yake tukala unga wa kuoza wa njano na sukari tope.
    na si kama hatukuwa na pato, ila lilitumia kuzineemesha nchi jirani kupigania uhuru.
    ni ekspiriensi inayotisha sana.
    mheshimiwa yule alikuwa fisadi kuliko hata hawa mafisadi wa sasa.
    angalieni alivyokifisidi hata kizazi chake mwenyewe, huwezi kuamini!!
    Mdau, Leicester

    ReplyDelete
  20. HHHHHeee! hii ni kiboko jamani, sio ishu ya ufisadi hapa, walau ulingane nastatus yako! hata mie 2 wamkulima sijawa ivyo!

    labda hawabebeki jamani! mbona nilisikia baba yao alikuw mjanja na mwenye akili sana.

    masikini cjui hawa watoto wake wana nini!!!!

    kweli c lazima wa nyoka awe nyoka. nasema sio lazima, kwa nafasi ya baba yao hata wangekuwaje lazima wangeingia kwenye system na jina la baba yao lingewika daima na watu wangelikubali tu.

    wana matatizo watoto wa taifa nawaambia. sio ufisadi wala nini...

    ReplyDelete
  21. Kuvaa ni kustiri mwili wala si kujionyesha. Andrew kastiri mwili. Basi inatosha. Kuvaa kujionyesha ni mawazo ya Kiafrika yasiyo na maana. Weusi - wale Afrika au Marekani au Karibiani - hutumia hela nyingi sana kuvaa ili waonekane. Na maongezi yao ni fulani anakula nini na anavaaje. Lkn angalia watu walioendelea km Wazungu, Wajapan... hawatumii muda wao kwenye mambo km haya. Wanavaa kujisitiri na wala si kuonyeshana nani anavaa nini.

    Wandugu, twende mbele. Tubadilike. Kuvaa ni kujistiri. Basi. Pinda (PM) naye katukumbusha.

    ReplyDelete
  22. Wabongo, bwana! Ukiwasaidia baadae wanakuona fala. Nyerere katupa elimu ya bure, watoto wa wakulima nao tukafika mjini na hata nje kubeba box, sasa hivi tunamwona fala.

    Haya, mafisadi wa sasa wanatu-EPA, tu-Richmond etc tunalalamika. Sasa sijui uwafanyie nini binadamu? Ama kweli tenda wema nenda zako, usingoje shukurani..

    ReplyDelete
  23. hongera sana mdau wa leicester hapo juu mi naungana nawewe kwa asilimia mia moja. Watu inabidi tuamke na kukemea vikali ufisadi aliotufanyia nyerere siwezi kusaha njaa tuliokuwanayo enzi zake tunakimbizana na magari ya neshno miling na kujiandikisha kwenye matawi ya ccm kwa ajili ya kupata chakula tena unapangiwa sukari kilo lazima na unga wa yanga kilo mbili ukikutwa na colgate basi wewe ni mlnguzi halafu mnakaa mnamsifu fisadi yule.kwahiyo watanzania mnapenda kuwa maskini sio? ukweli ni kwamba hakuna yeyote anaeupenda kila mtu anapenda vitu vizuri ,maendeleo, elim na maisha bora. unless kama hali hairuhusu.Angalia Sokoine alivyomkolimba kisa alikua anataka kuleta maendeleo, angalia leo watanzania tulivyonyuma kielim tunashindwa hata na watani wetu wakenya yote sababu ni yeye. Tuamke na tujifunze kutoka kwa wenzetu wanaoishi duniani sio sisi tunaosukuma siku. michuzi huu ni mtazamo tu na kila mtu anademokrasia ya kutoa mawazo usinibanie.

    ReplyDelete
  24. Nakubaliana na baadhi ya wadau, unaweza ukavaa simple lakini bado ukawa very smart.
    Mfano mzuri ni mwalimu mwenyewe,alikuwa anavaa simple lakini always very smart.
    Mshikaji hapa anadhani bado Frelimo wapo msituni wakipigania uhuru.
    Siafiki maoni ya mdau wa Leicester,
    Tunajua nyie ndio walewale...

    ReplyDelete
  25. yani mdau wa leicester na hapa juu yangu mmenena mie nalia na elimu sana tuu yani kweli inaeleweka fika elimu ni ufunguo wa maisha lakini baba yule alibana sana hiyo elimu ya bure ni ipi? ile ya shule ya msingi au??? kutwa kumsifia tuu kwa mazuri yappi? barabara ovyoo mgao wa umeme ndo umepamba moto maji nayo mgao mgao machafu afya duniiiiii maviwanda yamekufa yamebakia kutaifishwa manake walipewa watu ambao hawana ujuzi wa elimu wakaviua ndiyo ni baba wa taifa masikini angalia kiinglish cha wabongo ni cha kuunga unga tuuu yote hii ni kwa ajili ya kile kidingi angewaacha tu wakoloni wakae kama south chekini kulivyo bomba uchumi uko juu uspime kabisa simfagilii hata kidogo yeye ndo chanzo cha ufisadi watu walikuwa na mali zao akawafilisi sasa ndo wanalipiza paka akiondoka panya utawala. michuzi wa jina ujumbe huu ufike

    ReplyDelete
  26. NAKUBALIANA NA MAONI YA WADAU WENGI HAPA JAMVINI. NYERERE BWANA HAKUWA FISADI NA WATOTO WAKE WOTE VERY SIMPLE, ILA WALE AMBAO SI WATOTO WAKE, NI NDUGU TU KAMA WA WATOTO WADOGO ZAKE NDIO WANAOTAMBA NA KUTUMIA JINA KWA NGUVU, ILI KUPATA KAZI NA KADHALIKA. MUNGU AWABARIKI WATOTO WA HUYU BABA WA TAIFA, YAANI WOOTE ANGALIA HAPA ANDREW, UKIMWONA ROSE, ANNA, MAGIGE, MADARAKA, MAKONGORO, WOTE WAKO SIMPLE TU.
    TUNATAKIWA KUMUENZI MILELE.

    ReplyDelete
  27. hapo mnatathmini yeye alivyo na si nguo alizovaa, hizo nguo hazina kasoro yoyote na hata nikivaa mimi au avae mzungu ataonekanaq yupo ok na amependeza, lkn pia huyo si kijana wa miaka yenu wengi mnaotoa comments hapo ni 20's or 30's. ukitafakari utanielewa

    ReplyDelete
  28. Sitamjadili Bwana Andrew, ingawa angejitahidi zaidi. Nadhani sehemu kama hiyo siyo ya suti kama mdamu mmoja alivyosema lakini nadhani angevaa jeans tu na t-shirt. Naaamini ni mtu makini na mwenye akili, lakini kama wajamaa wengine, nguo siyo kitu.

    Mbona wadau hamjajadili kuhusu hao 'fat man' na 'little man' na kukaa kumkandia baba wa watu ambaye alitutumikia kwa moyo wote?

    Michuzi, with all due respect, nina tatizo moja, na nadhani kwa kusema hivi hautatoa comment zangu. Watu wakimshutumu Mwalimu comment zao hauna tatizo la kuzitoa (wengine inatuuma kuona watu wanakosa shukrani na heshima kwake), lakini ukisema kitu direct kuhusu raisi wa sasa unabana. Mimi siafiki hiyo kabisa.

    ReplyDelete
  29. Maskini ní maskini tu. Ama kweli sasa nimeamini kua Tanzania watu wanaheshimu nguo kabla ya utu wa mtu. Hawaangalii mtu anafanya nini na anastahili heshima gani wanaangalia amevaa nini japo ni fisadi, malaya au mwizi kwa njia nyingine. Huyu jamaa hanuki ndio maana hata huyo mwenyeji wake hajaziba pua. Pili hiyo nguo kujikunja kwake ni sababu ya kukaa kwa muda mrefu. Nyie mnao anza kushambualia mavazi mnafanya hivyo kwasababu kuvaa vizuri mmeanzia uzeeni kubali kataa mna limbuka leo kwa mavazi mwenzenu ni mtu wa majukumu na wala sio soga jifunzeni muelewe. Na hii ni salamu tuu pamoja na wale Polisi mlionisumbua kule Moshi kwasababu nilikua nimevaa kaptula mwishoni mkabaki mdomo wazi. Jifunzeni kuheshimu utu, utu wa mtu ni kitu muhimu sana.

    ReplyDelete
  30. - kweli kuna watu wanaongea 'wasovijua kwa undani'..Yule aloongea kuhusu urafiki wa Andrew na marehemu Ray Abdul - '..buti jiwe, kaa chini, t- - yeye!, adebayo.. anafahamu ya undani. jamaa tangu enzi izo hajui kuvaa, maana alikua mtu wa kombati ama akidaka kaunda za baba wa taifa..naona hajazoea kununua viwalo - lol!..

    ReplyDelete
  31. The GrandPMCOctober 05, 2009

    i dont mean to offend the lad,but he is very,i mean VERY shaby

    ReplyDelete
  32. Anon Mon Oct 05, 04:59:00 PM,

    Asante kwa maoni yako. Naomba nikuulize Ray Abdul -'..buti jiwe, kaa chini, t..yeye!, adebayo..

    Ni nani kwa jina lake la halisi? Alisoma wapi? Aliwahi kufanya kazi wapi? Alikuwa anaishi wapi? na alifahamihana vipi na Braza Andrew?

    Ukitutajia jina maarufu la Braza Andrew au lile alilokuwa akiitwa na Marehemu Mzee wetu (Baba wa Taifa) na ndugu na rafiki zake wa karibu na jina la halisi la Marehemu Ray Abdul utakuwa umeninyamazisha. Vinginevyo!? Achana kabisa na hii issue.

    Mura kaka Andrea, kura bintu mbaka ujoke. Bro komamanga, Rest In Peace, I/we miss you badly.

    ReplyDelete
  33. hata msemeje jamaa yuko rafu utadhani ametoka segerea lol!!

    ReplyDelete
  34. SWALI LANGU NI,HIVI KWA NINI MUMUHUSISHE UVAAJI WA HUYU KAKA NA BABA YAKE?ANDREW NI K.M ANDREW NA BABA WA TAIFA NI BABA WA TAIFA;SASA K.M YEYE MWENYEWE AMEAMUA KUVAA SIMPLE OR SHABBY(K.M MNAVYOITA) JAMANI SI NI YEYE MWENYEWE?KINAWAKEREKETA NINI?NYIE MNAOMKANDIA JITOKEZENI BASI TUONE JINSI MNAVYOJUA KUVAA VIZURI MAANA ANAYEMSHOOYESHA MWENZIE KIDOLE KAMWE HAPINDISHI KIDOLE AKAJIANGALIA MAPUNGUFU YAKE MWENYEWE;UKUTE NYIE NDIYO MNAORUDIA NGUO WIKI NZIMA KWA KUSEVU MATUMIZI YA SABUNI; KUVAA KWAKE AU MUONEKANO WAKE USIHUSISHWE KABISA NA BABA WA TAIFA,WALA MALEZI KWA HUYU KAKA.WATANZANIA TUACHE MIDOMO NI AIBU.

    ReplyDelete
  35. Aisee anonym wa oct 06,08:07:00 umenikuna kweli na comments zako,na utakuta hao wanaorusha hizi zuga ni wasomi hasa,mtu yuko masomoni nje labda anafanya masters au degree ya kwanza lakini anachokuja rusha humu blogoni utafikiri hakwenda shule hata darasa moja!hivi ni usomi gani huu, usomi siyo wa darasani tu, wa kuvaa joho,umeshika cheti na kujisifu; pia unajumuisha busara na akili ya maisha ndani yake;ni bora yule aliyeishia darasa la saba au ambaye hakusoma kabisa lkn ana akili ya maisha,na muda wake mwingi anautumia kujitafutia riziki au kumtembelea jirani yake mgonjwa hospitali au kufanya mambo ya maendeleo kuliko wasomi wetu wanaokuja kuongea ujinga wa kumponda mtu eti alivyo;hovyo sana

    ReplyDelete
  36. NIMESOMA COMMENT ZENU WOTE HAPO JUU NI UJINGA MTU....KUVAA NYINYI MNAONA NDIYO MAISHA????HUYU JAMAA AKITAKA KUVAA ANAWEZA KUPWEWA ANACHOTAKA SEHEMU YOYOTE DUNIA..SEMA HAWA NI WATU WAMELELEWA NA REALY FATHER...MDAU MONEY.

    ReplyDelete
  37. Kwakifupi huyu jamaa hana uhusiano wa aina yoyote kisheria na baba yake, ni mtu mzima anae faa kujitegemea, kama alichezea umri na kweli kachoka ni kivyake. mbona wako wengi tu watoto wa kishua lakini walichezea shule na nafasi kadhaa wa kadha za kujiokoa kimaisha walizopew, na leo wako mtaani wanasota na baba zao wako hai na wana nafasi kubwa kubwa tu.

    kingine, jamaa kuvaa hivyo ni hulka yake tu labda, kama kaweza kufika ughaibuni inakuwaje iwe shida kununua pamba? mbona wakinga kibao wana hela na wanavaa kandambili wanapokuwa kwenye international trip? mbona hatuwashangai?sometimes ni hulka tu. baba wa taifa kuhusu suala la munonekano wa Andrew hana la kuchangia, kila mtu ataishi maisha aliyojichagulia na atavaa anavyopenda...bila kujali mshiko mfukoni

    ReplyDelete
  38. Nyerere hakuwa shaghalabaghala kama huyo kijana wake anavyoonekana, na yeye kuwa hivyo ni akili zake na mwenendo wake na haina maana kuwa ndio uadilifu wa Nyerere. Nguo utafikiri zimetoka tafunwa na ng'ombe kha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...