Rais wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) na Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano la Tanzania Mh. Samwel Sitta akila taswirazzzz katika hifadhi ya taifa ya serengeti mchana wa leo wakati wa ziara ya siku moja aliyowaandalia wajumbe wa mkutano huo unaofanyika A-taun ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Zanzibar, Ngorongoro, Manyara, Tarangire pamoja na Mlima Kilimanjaro
Viboko katika bwawa Serengeti
Mh. Sita na wageni wake pia walitembelea Kempinski Bilila Lodge iliyo ndani ya Hifadhi ya Serengeti na ambayo majuzi imetangazwa kuwa hoteli bora kuliko zote Afrika mashariki na kati
wageni waliona wanyama wengi sana leo, hawa ni nyati
Simba akikatisha mbele ya wageni wengi wao wakiwa ni mara ya kwanza kuona wanyama wakiwa maeneo yao ya asili. wengi wao wameamua kubaki na kufaidi vivutio hivyo mara baada ya mkutano huo wa 55 kumalizika Jumanne ijayo, wakati wengine wanaenda kujipanga na kuja kivyao baadaye.
Tembo pia walionekana
Mh. Sitta na wageni wake wakiangalia wanyama









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. fantastic idea, ingawa that means millions of shillings to Tanzanians, naamini inasaidia kufanya promotions ya tourist attractions zetu.

    ReplyDelete
  2. Nanihii hiyo picha ya simba anakatisha umeiramba vizuri kweli, kweli nimekukubali kwa kipaji cha picha! big up anko nanihii.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, picha hizo zimekaa sawa mno. Uwe unazipiga "watermark", ili wazushi wasizifanyie uzushi.

    ReplyDelete
  4. ahsante Hon.Six ze fulanazz bab kubwa inabidi na mithupu apate kama hiyo.

    ReplyDelete
  5. Michuzi ulitoka ndani ya gari kupiga hiyo picha ya simba nini? Nashangaa kwa nini hakukushitukia. Picha zimetulia sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...