anko nanihii anaishi nyumba ya nne kushoto karibu na uchochoro wa tano kulia, mbele kuna duka la mpemba na fundi baiskeli. uliza kwa binti saidi utaelekezwa kwa mangi kisha utapelekewa nyumbani kabisa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. nchi isiokuwa na muongozo utaijua tu.

    ReplyDelete
  2. Nchi yenye viongozi wavivu, waongozwaji wavivu na watendaji wavivu. Ipo wapi mipango miji?, kuna watu wameajiriwa na wanalipwa mshahara wa walipa kodi bila hata kuufanyia kazi. Kwa nini walimtoa magufuli wizara ya ardhi?. Jamaa ni mchapa kazi alitaka kuanza na mipango miji.

    ReplyDelete
  3. nyumba yake ileeeee nimeshaiona!

    ReplyDelete
  4. so?moral of the story?

    ReplyDelete
  5. Yaani kuna mitaa haipitiki Dar hasa ukienda Mtoni kwa Azizi Ali. Hata Ambulance haipitiki. Mkoloni aliipondoka ma mitaa ikafa. Nasikia katika ramani ya mji kuna sehemu ziliwekwa kwa ajili ya watoto kucheza (playgrounds) sehemu hizo zimejengwa nyumba za kushi na Idara ya wmekula pesa. Sehemu amabayo inatakiwa ipite barbara watu wamejenga Fence bila idhini ya serikali na Idara ya Ardhi wanakula pesa. Western countries nyingi zilizoendelea hauruhusiwi kuongeza jengo kwenye ile ramani iliyopitishwa na city. watakuja kuvunja na gharama juu yako. Mitaa inawekwa mmoja wa magari na mwngine wa nyuma ya nyumba kwa ajili ya gari la kuzoa taka. Kinachonishangaza Bongo ni kuwa wengi watu wa jiji waliisha fika Ulaya na wameona jinsi wengine wanavyoendesha miji yao lakini Bongo wanashindwa kuiga utaratibu huo. Nchi nyingi za Ulaya wameendelea kwa sababu ya kubadilishana technolojia na kukopi mambo mazuri waliyofanya wengine. Naomba Kikwete na serikali yake waamke na watoe mikakati ya dhati kurekebisha miji ya Tanzania kama kweli wanjali Watanzania.

    ReplyDelete
  6. ankoo mithupu naomba utubandikie bei ya madafu ijuma tarehe13-11-2009.

    mdauuu kontjeee

    ReplyDelete
  7. Anko nanihii siuliwahi kutuambia Kwamba hapo Kwenye BATI LA KIJANI? ila Anko nanihii Maharufu sana hiyo sehemu hata ukimuuliza KUKU au Mbuzi Anko nanihii anaishi wapi anageuza Shingo tu kwahiyo unafata njia alipogeuza shingo. Pazi.

    Hivyo ndio vituko Uswahilini Mwizi akifukuzwa kumpata ngumu Raha sana.

    ReplyDelete
  8. viongozi wetu wenyewe wanataka kuongozwa,mambo ya address kwetu bado na kama si mwenyeji wa vichochoro utajikuta waingia chumbani kwa mtu.mdau

    ReplyDelete
  9. NA UKISIKIA JOGOO ANAWIKA NDO HAPO HAPO.

    ReplyDelete
  10. ANKO NIMEIMIND SAT NAV YAKO, IMEKAA KIBONGO BONGO KWELI, LOL!!!!

    ReplyDelete
  11. Alafu ucshangae kusikia wengine wana sema hoo mm kwetu geti kali heee

    ReplyDelete
  12. November 11
    Yemen 2 - 1 Tanzania
    Hakuna mtu mwenye video ya matokeo haya ya jana kati ya Yemen na Tanzania?

    ReplyDelete
  13. miundo mbinu ni full kwikwi

    ReplyDelete
  14. tatizo bongo hata hiyo mitaa haina maana kwani nyumba hazina namba wala hakuna mpangilio wowote yaani ni vurugu tupu watanzania tembeeni ulaya na usa mjifunze nini maana ya mitaa yaani mtu unaweza safari sehemu yoyote na kufika nyumba unayokwenda bila kuuliza hata mtu mmoja maana kila nyumba ina namba na kila mtaa una jina na bado kuna maelekezo mengi ya kuksaidia mgeni sio kama bongo yaani haijulikani which is which

    ReplyDelete
  15. bongo kumebadilika kweli!!yaani maendeleo kila sehemu,nyie wabeba mabox mliondoka miaka kumi na zaidi si mnaona maendeleo hayo nyie kaeni huko huko na mabox yenu!!

    ReplyDelete
  16. Wadanganyeni wamarekani kuwa tanzania ina W.M.D waje watungue jiji zima halafu watujengee kama wanavyofanya IRAQ,LOL.

    ReplyDelete
  17. uswazi ile mbaya

    ReplyDelete
  18. Kinachoshangaza zaidi wakati mambo haya yanatokea kwetu technolgia ya computer ilishakuwepo kwanini sasa tumeshindwa kupanga kikamilifu jiji letu.Hii nikiwa na maan kwamba wakati wenzetu wanapanga miji yao karne 15 mpaka 16 hata technologia ilikuwa sio kubwa kama nchi yetu ambayo haina hata karne tangu tupate uhuru.Kazi tunayo,,,,,,!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. Bombi nyumbii wenzangu wa Songea watanielewa.

    Ukifika kwenye bomba la maji basi ndio nyumbani kwetu (Bombi Nyumbii).

    Hapo kwenye bomba ndio nyumbani

    Mjusi

    ReplyDelete
  20. Na sio lazima waende ulaya, wangeenda hata hapa karibu kwa wenzetu wa Rwanda waone wanavyofanya kazi kwa kuipenda nchi yao.

    huezi amini nchi imetoka kwenye vita miaka 15 iliyopita. wanachi wanajituma sana kila jumamosi ya mwisho wa mwezi wanafanya community work kila kata ambao huko kwao wanaita mudugudu. na kiongozi wa kata anahakikisha kila raia anashiriki katika huo usafi ndio maana mji wao ni msafi sana katika Afrika Mashariki. na pia wafungwa walioko magerezani pamoja na kuwa wanatumikia kifungo chao lakini pia moja ya adhabu zao ni kushiriki katika kazi za ujenzi wa nchi yao kama kutengeneza barabara za mawe ambazo zinaingia kwenye mitaa mbalimbali, upandaji miti ujenzi wa mashule n.k. kwa kweli vision 2020 watakuwa wamepiga hatua kubwa sana.

    Rwanda huwezi ukaingia na mfuko wa plastiki maana ni marufuku mifuko ya plastik kuonekeana kwenye nchi yao hata ukishuka uwanja wa ndege kama una mfuko wa plastik unaucha hapo hapo uwanjani unapewa mifuko mingine ya karatasi au nguo ubebee vitu vyako. wanajitahidi sana kutunza mazingira yao. lakini kwetu mifuko ya plastiki kila kona mpaka nvua ikinyesa maji yanakosa pa kupita maana mifereji imeziba, chemba za maji zimefuka basi taabu tu uchafu kila kona achilia mbali hiyo mipango miji ni bure na watengenezaji wa mifuko ya plastiki ndio haohao wenye madaraka kwa hiyo hata wakitangaza kupiga vita mifuko ya plastiki Tanzania ni kiini macho.

    Watanzania tubadilike jamani tuipende nchi yetu na kuithamini, tujali mazingira yetu iwe nchi ya amani na mazingira mazuri na upepo mwanana sio upepo wenye hewa chafu.

    ReplyDelete
  21. Anony 11:31AM

    Yaani hiyo ya kufanya community work Jumamosi na tena ya mwisho wa mwezi ikija Bongo, itakuwa balaaaah! Yaani kwanza inabidi bar na club zote zifungwe ndiyo hii sera iweze kufanya kazi. Mmbongo anaamka jmoc na hang over mbaya, harafu anaamkia bar kupata supu na chapati, then makamuzi yanaanza tena mpk usiku wa manane, Bongo raha nyie acheni mchezo. Si mnakumbuka song la Mzee Ngwair, Mitungi,Plant, Mikasi...

    ReplyDelete
  22. Annon wa 01:52:00

    Ni kweli penye nia pana njia kama tunadhamiria. Bila hivyo tutabaki kuwa wa kuongea saaana na kulalamika basi. Watu wakiona uchafu wanalalamikia serikali, manispaa haizoi uchafu, n.k sasa hii serikali ni nani hasa bila sisi wenyewe kuonyesha uzalendo na nchi yetu. utakuta mtu uchafu mpaka mlangoni kwenye nyumba yake bado anataka manispaa ije imsafishie. kwa hali hii kipindupindu kitaisha kweli?

    Kweli Rwanda ikifika J. mosi ya mwisho wa mwezi kuanzia asubuhi maduka, masoko, vilabu, n.k vyote vinafungwa kwa ajili ya usafi mpaka mchana ndio vinafunguliwa. kwa hiyo hata wananchi wamezoea kuwa ndio utaratibu hivyo mwenye manunuzi ya lazima anafanya ijumaa ukizingatia huko hata masoko yanafungwa saa mbili za usiku, sehemu nyingine mpaka saa nne za usiku. Hivyo huwezi kusema umekosa hitaji lako. unajua akili inavyojityuni ndiyo na mwili wako unavyo respond.

    tubadilike jamani.

    ReplyDelete
  23. MIMI NASEMA KILA SIKU KWA MAENDELEO TANZANIA TUKO NYUMBA SIO KAMA HATUTAKI ..LAAA KUNA WATU WACHACHE WANAZUIA MAENDELEO YASIWEPO KWASABABU ZAO BINAFSI. NAKUBALIANA NA MDAU MMOJA ALIYEZUNGUMZIA KUHUSU MAGUFULI..ALIKUWA MCHAPA KAZI KWELI...ANGALIA HATA ALIPO SASA HIVI..KUNA WAZIRI ALIYEPIGA HATUA KAMA YEYE....LABDA WANAOAJILIWA HAWANA VYETI VYA UKWELI...KWANI MIMI SIONI KWANINI WASIWEZE KUIGA MFANO KAMA WENZAO NI VERY SImple

    ReplyDelete
  24. NIMEKUPATA!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...