Waandishi wa Bongo na mikutano ya kimataifa
Aiseee Michuzi...
Nipo hapa Johannesburg niki-cover mkutano uitwao SECOND AFRICA WATER WEEK ambao unahudhuriwa na wajumbe kama 1,700 hivi kutoka sehemu mbalimbali za Africa na duniani kwa ujumla.
Watani wa jadi (Kenya) imetuma waandishi 21, Uganda 14, Rwanda 7 Burundi 8, Nigeria 11, Ghana 6, Zambia 8, Malawi 8, Botswana 9, na Swaziland na Lesotho wapo 6 kila nchi. Press Gallery hapa Callegher Conference Centre ni wengi ajabu.
Cha kushangangaza, Bongo ni mimi pekee mwandishi nipo hapa. Hivi ni kwanini Bongo tupo nyuma vile katika kuandika habari nje ya mipaka yetu, na hasa zile zinazohusu maendeleo ya watu?
Je tunauweza uandishi wa ki-utandawazi?
Nipo hapa Johannesburg niki-cover mkutano uitwao SECOND AFRICA WATER WEEK ambao unahudhuriwa na wajumbe kama 1,700 hivi kutoka sehemu mbalimbali za Africa na duniani kwa ujumla.
Watani wa jadi (Kenya) imetuma waandishi 21, Uganda 14, Rwanda 7 Burundi 8, Nigeria 11, Ghana 6, Zambia 8, Malawi 8, Botswana 9, na Swaziland na Lesotho wapo 6 kila nchi. Press Gallery hapa Callegher Conference Centre ni wengi ajabu.
Cha kushangangaza, Bongo ni mimi pekee mwandishi nipo hapa. Hivi ni kwanini Bongo tupo nyuma vile katika kuandika habari nje ya mipaka yetu, na hasa zile zinazohusu maendeleo ya watu?
Je tunauweza uandishi wa ki-utandawazi?
Nawasilisha.
DEO MUSHI,
JOHANNESBURG,
Bw. Mushi nakutakia kila la heti huko Jo'burg ila naomba kuuliza.
ReplyDeleteNini hasa maana ya neno 'aisee'?
kwanza hongera ze kaka!!then tufahamishe kama na wewe umetumwa na tz au binafsi..na taarifa ulizipataje...na ulijitahidi kiasi gani kuwapa news on time wenzako ili waweze kuhudhuria..maana usiishie kulaumu tuuu...tupe mfano nani ulimwita akakataa kwenda...mi huwa cpend maulalamishi bila vitendo bwana!!ni ayo tu
ReplyDeleteBy Graduate Engineer Emmanuel-
Mdau Graduate Engieer Emanuel asante sana. Bwana Mushi hongera sana kwa kupata newz mapema za kwenda huko J'berg lakini tatizo lako ni moja ungetumia blog ya Michuzi kueleza wadau wenzako kuwa kuna mkutano kama huo na sio kulaumu pili uwezo waandishi wengi wa bongo ni wanakipato kidogo na wamiliki ni wagumu unategemea wafikaje huko? au kuna sponsorship?
ReplyDeleteWenzako wakizipata hizo 'trip' za nje wanaziita vekesheni na wanakula maisha kwenda mbele kivyaovyao.
ReplyDeleteKama una huruma na wenzako si ungekataa kwenda peke yako? Sitashangaa hata nikisikia ulitoa rushwa ili upachikwe huko au kuna mkono wa fisadi katika safari yako.
Kaka Deo hongera kwa kuwa wa kwanza darasani, Teh Teh Teh!!!!!1
ReplyDeleteUkirudi naomba uninunulie tarumbeta la kuishangilia Simba mwenzio sauti huwa inakauka.
Unaposema "Kenya imetuma waandishi 21" unamaana gani? Acha lawama, wataarifu wenzako unapopata habari za mikutano maalum na kama kuna vyanzo vya mkwanja wa nauli na Malazi kwa waioweza kufandhiliwa na vyombo vyao mapema!
ReplyDeleteAISEE NI KI-CHAGGA, DEO ULITAKA KuTUAMBIA kuwa UKO NJE TU, KWANI WEWE ULIPATAJE HIZO HABARI ZA KUWA KUNA KAMKUTANO KAMA AKO, SI UNGE WABONYEZA WENZAKO NA WEWE PIA NI MCHOYO. WATANZANIA NDIVYO TULIVYO, KWANI KUNA VITU VINGAPI VYA BURE VYA KIMATAIFA KAMA SHULE WANAKULA WAKUBWA PEKEE YAO
ReplyDeleteDeo...umetumwa na dailynews, Media Fund au MCT? au kaka Asa Mwambene alikutonya kuhusu hiyo safari? mmmmm! hata the home of great newspaper wameshindwa kutuma hata correspondent mmoja jamani? wamlipe stori ikitoka?.....nge nge nge'..Tafakari!
ReplyDeleteDeo Mushi kila la heri huko, lakini chunga watoto wa kizulu, hawakopeshi. Ningefurahi ungetuletea picha ya maeneo ya Soweto kwani sijawhi kuona mambo yalivyo huko. wanasema ni kama kambi ya fisi Tandale!!!!!!!!!!
ReplyDeleteTatizo gego kaka!! kama gego halipandi ni bora kujifanya kama hawana taarifa tu. taarifa wanazo sana sema gego ishu wanaogopa kukanumba!!! gego kwake michuzi!!! halafu we kaka ni kama huwa nakupatagapataga kule kwenye ile forum ya wanajamii.
ReplyDeleteKaka yangu usikonde!
ReplyDeleteWaandishi wetu (sio wote) naona wako busy sana kuandika mambo ya kifisadi na mambo mengine mbali mbali ambayo kwa kusema ukweli hayatuhusu na wala hayachangii maendeleo ya nchi yetu. Kuna mdau mwengine hapo juu ameseam kwamba ilibidi uwashtue wenzao, aaahh! Mtu lazima ufanye utafiti mwenyewe, hio ndio kazi uandishi. Usingojee kuambiwa dili liko sehemu gani. Ndio maana mpaka leo tuko nyuma hatuna initiative yoyote, kazi ya kuongea tu! Kila kheri kaka!
Mushi anauliza as if hajui mazingira ya kazi yake. Hivi kuna freelance journalist anaweza kuingia gharama ya kwenda bondeni ku-cover mkutano wakati hana uhakika wa soko la news atakayoiandika?
ReplyDeleteKama mwandishi hajatumwa na media houses ama serikali (kupitia magazeti ya serikali), dont expect mtu aende ku-cover mkutano kwa gharama zake mwenyewe.
Michuzi kila siku yuko vekesheni na hatujawahi kumsikia akiuliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu. Lengo ni kutaka kuwadhalilisha waandishi wenzako ama? Kama hawana uwezo wa kujilipia unataka waanze ufisadi? Watu kama nyinyi ndiyo mnachangia baadhi ya waandishi wapate tamaa ya kupokea hela za mafisadi na kuanza kupika habari za kufikirika ili kuwasafisha mafisadi na kuwapaka wengine matope ili wote waonekane ni wachafu mbele ya jamii.
Wewe umesema nchi nyingine ZIMETUMA, sasa ukituuliza sisi unataka tukujibu nini? Waandishi wa Tanzania wanategemea watumwe na media houses zao. Swali lako hukutakiwa kulielekeza kwa waandishi bali kwa Wahariri Wakuu ama Owners wa Media houses. Kuwauliza waandisha wa habari ni kuwaonea pia huwezi kupata jibu.
Hata kama waandishi wangekuwa wana information kwamba kuna mkutano kama huo, hawawezi kwenda wenyewe. Si ajabu wako wengine ambao walikuwa na taarifa na waliomba kwa wahariri wakuu ama owners wa media houses na wakanyimwa funds kwa kuwa maamuzi ya ku-cover mikutano ama matukio yanatofautiana uzito kulingana na mtazamo wa Media House ama Owner wake. Ulishawahi kuona Mtanzani, Rai na dada zake wameandika news ya kumkandia Rostam Azziz? Ama ulishaona magazeti ya IPP yakimkandia Mengi?
Nawashangaa hawa waanishi wakitanzania wanaotegemewa kupeanwa assignments na editors wao/vyombo vya habari.
ReplyDeleteMimi ni mkenya, na majuzi nilikuwa na Deo Mushi huko Denmark na ndiye aliyenionyesha website hii ua Michusi.
Waandishi wanapaswa kujenga network na mashirika mbalimbali kwa ajili ya kupata sponsorships na sio kukaa tuu fwaaa.
Wengi ya waandishi walioenda South Africa lutoka Kenya najua wamegharamiwa na mashirika kama UNEP.WaterAid, Un Habitat na baadhi ya NGOs.
Hata Deo Mushi najua kalipiwa na shirika moja la kimataifa lililopo Kenya na sio mhariri au media yake.
Kifupi waandishi wa habari wa TZ mmelala. Munahitaji kiboko matakoni muaamke na kujua namna ya kufanya kazi. Ukimtegemea mmiliki/mhariri utakufa maskini.