Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego ( kushoto) akiwa na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Ahmed Ng’eni , ( kulia) wakipita kuangalia maeneo yaliyokumbwa na mafuriko mjini Kilosa baada ya mto mkondoa kuacha mkondo wake wa maji na kusababisha kusambaa maeneo ya makazi ya wananchi na shule ya msingi ya Mkondoa.
Gari la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , ukipita katika dimbwi kubwa la maji , katika barabara ya kwenda Kitongoji cha Mapangano, Kata ya Kanga, Wilaya ya Mvomero , ambapo msitu wa hifadhi wa asili wa jumuiya ya Wami – Mbiki ambapo wananchi wamevamia na kuweka makazi ya kudumu, kilimo pamoja na wafugaji kuligeuza eneo la malisho ya mifugo

Duka la Dawa muhumimu ambalo linafanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi wa kitongiji cha Mapangano, Kata ya Kanga, Wilaya ya Mvomero. Picha zote na mdau na John Nditi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. huyo dereva au mkuu wa mkoa sidhani kama angepita through hilo dimbwi kama gari ingekuwa yake binafsi

    ReplyDelete
  2. Hao hawajipendi hayo maji yanaonekana madogo lakini hayakawii kulichukua hilo gari....

    ReplyDelete
  3. Dereva achunguzwe kama ana akili timamu....pia duka la madawa hilo nafikiri halina cha ajabu kwani ni la kiwango cha kijiji cha Mapangano

    ReplyDelete
  4. sasa nimejua kwanini wananunua 4WD, hii picha wangeiweka kwenye magazeti afu wakaitumia kujidefend kwa wananchi sababu ya mashangingi, kudadadeki huyu dereve anatakiwa afungwe maisha huwezi kutumbukiza dola laki moja kwenye maji kisa sio zako.

    ReplyDelete
  5. Huyo dereva ana matatizo ya problem, gari cruiser yenye mkonga ndio unaweza ukaipitisha ktk kina kirefu cha maji hata kioo kikazibwa, lakini hilo halina mkonga ukifatilia utakuta liko gereji limeshakunywa maji gari ya million 240 kwa uzembe apimwe akili.

    ReplyDelete
  6. NAWAOMBA WANANCHI WAWE WAVUMILIVU. HAYA MAJI TUNAYAHITAJI SANA KUENDESHEA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME. TUMECHOKA MGAO WA UMEME. KWA UKWELI KABISA NAPENDA INYESHE ZAIDI YA HAPO.

    ReplyDelete
  7. OYAAAAAA TFDA MPO WAPI.....

    ReplyDelete
  8. tatizo siyo dereva yeye si anaambiwa tu na boss wake, unataka apingwe chini vilevile roho haiumi hiyo gari si ya jamhuri likiharibika si litatengenenzwa au kupewa jipya hela ipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...