Habari za kusikitisha zilizopatikana mapema leo,zinaeleza kuwa mvua kubwa ilionyesha wilayani Same mkoani Kilimanjaro usiku wa kuamkia leo,imesababisha maporomoko ya ardhi na kupelekea maafa ya watu wanaokadiriwa kufika 25 ,taarifa zinaeleza kuwa maporomoko hayo yalizikumba nyumba saba zilizokuwa na watu,ambao walikuwa usingizini,katika kijiji cha Goha,wilayani Same.
Hadi jioni hii inaelezwa kuwa jumla ya maiti 15 zimeshapatikana na miongoni mwao 10 ni za kike na 5 ni wa kiume. Jitihada za kunasua maiti nyingine bado zinaendelea.Kwa habari zaidi baadaye kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. uwi kiru yesu wangu weee,Tina wa new york tumefiwa sisi huku home na mama,pamoja na baba katika mafuriko haya,yesu wangu tina pokea simu yako please..mimi Anita..

    ReplyDelete
  2. ooh my God, this s terrible...
    polen sana mliofikwa na maafa na wengine wa mabondeni na sehemu nyingne hatarishi kuepukana na matatzo
    Kama warning zimetolewa sn kuhusiana na mvua zinazotarajiwa (elnino).

    Mungu awa rehemu wote.

    ReplyDelete
  3. Jamani sasa watu waende wapi??? Sehemu kama Kinodoni maji yanajaa vile vile hata sehemu nyingine sio mabondeni.

    Ni kuwa viongozi wa serikali za mitaa waboreshe miundombinu. Wasimamie ipasavyo.

    Mfano tangu mvua hizi zianze kutangaziwa sijaona badiliko lolote ambalo serikali hasa hawa viongozi wa mitaa wakifanya.

    Mitaro bado imejaa vile vile, hakuna lolote lililofanywa kuhusu usafi na uzibuaji.

    Hakuna mafunzo yoyote yaliyotolewa kuhusiana na majanga ya mafuriko kama ilivyo nchi nyingine wanavyofanya.

    Mfano mzuri Malawi ni nchi pia moja bado changa lakini wanatushinda sie, wao weshaanza kuwafundisha wananchi jinsi ya kukabiliana na majanga ya mvua.

    Naamini hapo ni kuilaumu serikali hakuna wakulaumiwa zaidi ya wao.

    Wao ndio wangetakiwa kutilia mkazo ikiwezekana viongozi wa mitaa wapite wahakikishe kila mitaa yao watu walio katika maeneo hayo wapo katika hali iliyo salama ikiwamo kucheki je nyumba wanazo ishi ni salama kukabiliana na mvua kubwa kama sivyo wawape notice wahame na je kila mtaa mifereji iliyopo inakidhi kupitisha maji mengi? Kama haikidhi wajikusanye hata kushirikiana na wananchi wasafishe mitaro na kuipanua zaidi.

    Hakika hawa viongozi wa serikali yetu ya Tanzania wamekuwa wakilala sana. Wananikinaishaaaaa.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana jamani.

    jana tu nilikua naangalia news nikaona haya maporomoko yametokea huko TN. Nikajiuliza hivi mbona Tanzania sijawahi kuona haya wakati tuna milima sana? kumbe hata sisi udongo wetu ni hivyo hivyo.

    Jamani hiyo comment ya kwanza imenisikitisha sana...haya mambo ya kuzima simu usiku sio mazuri. Hata mimi nilishafiwa walinipigia simu usiku mzima hawanipati simu zote nilikua nimezima. Lakini toka siku hiyo nimelearn my lesson. Simu za usiku wa manane zinashtua sana. na nyingine wala sio za misiba ni za wale wazembe fulani hata uwaeleze vipi tofauti ya masaa ya huku na Tanzania hawasikilizi. Wao watakupigia tu simu saa kumi asubuhi. halafu ukipokea tu utasikia ah kumbe umelala basi nitakutafuta baadaye....heeeee

    Poleni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...