Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Amani Abeid Karume kwa kutunukiwa nondozzz ya heshima ya Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki Memorial University viwanja vya Karimjee jijini Dar. Maalim Seif na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba walikuwepo kushuhudia tukio hilo ikiwa nji mwendelezo wa kuendeleza muafaka uliofikiwa karibuni huko visiwani ambapo sasa CUF wanamtambua rasmi Mh. Karume kuwa Rais wa Zanzibar
Mkuu wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dk. Salim Ahmed Salim akimtunuku shahada ya Heshima Rais wa Zanzibar, Dk. Abeid Aman Karume wakati wa mahafali ya 7 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam, jana. Chini Dk. Salim Ahmed Salim akimpongeza Mh. Karume kwa kutunukiwa shahada hiyo. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii
Hongera Mheshimiwa... anasema Dk Salim Ahmed Salim baada ya kumtunuku shahada ya heshima Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi Dr Kairuki alishafariki kumbe. That's new... Nilikua sifahamu jamani

    ReplyDelete
  2. Mshanifahamu sasa??? wakimbizi wa CUF ughaibuni mpo?? Watu ndio wamepatana. Safi sana.

    ReplyDelete
  3. Wafuasi halisi wa Nyerere ni Hamad na Karume katika top brass ya uongozi wa nchi hii kwa sasa. Wengine wote wababaishaji tuu. Wasomi hebu jaribuni kutoa dira ya nchi kutoka kwenye mfano huu mahiri ya wazanzibari hawa?

    ReplyDelete
  4. PhD ya kuiba kura hiyo.

    ReplyDelete
  5. mdau wa 06.24,acha choyo,ukimbizi ughaibuni ulikwisha zamani na watu wana vitabu vyekundu kazi kwako wewe unae endelea kuchagua mafisadi huku haupo na kule haupo,CCM Chukua Chapo Maapema,ishi kivyako na wacha watu waishi kivyao,pole sana roho mbaya haijengi,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...