Mdau Issa Kessu amekula nondozzz adimu ya Arts in European culinary Management inayotambulika na Manchester Metropolitan University UK na International Hotel Management Institute Switizerland. Kwa sasa anakuwa ni Executive chef mdogo kuliko wote Tanzania kuwa HACCP certified, yaania amefuzu kufungua na kuongoza Five Star hotel popote duniani. Mwezi Juni mwaka huu alichaguliwa kama Mmatumbi pekee kuhudhuria moja ya matamasha makubwa duniani ya sanaa lijulikanalo kama ART BASEL ambalo hufanyika kila mwaka ktk jiji la Basel, Switzerland. Katika fani ya misosi Chef Issa aliwafunga magoli ya kisigino pale alipofanikiwa kufanya production ktk VIP fine dining restaurant ambayo kila alieingia alitakiwa awe na kima cha chini angalau kiasi cha dola za kimarekani millioni 50 ktk akaunti. Yaani waliokula hapo ni wenye nazo has na sio chenji. Hakika nikitu cha kujivunia sana kama Mtanzania. Pichani juu na chini ni wakati wa mafunzo yake hayo.
Mdau Issa akipiga 'pepa' la mwisho
Chef Issa akila nondozzzz yake
Chef Issa akiwa na wala nondozzz wenzie




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. hongera kaka Inshaallah elimu uliyopata iwe ni ufunguo wa uelewa kwa wale ambao wanadharau fani hii yetu ya hotel management.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Issa kwa mafanikio hayo. Uendelee kuchagiza wengine na uwe mfano bora zaidi na zaidi!

    ReplyDelete
  3. saafi saaana. angalau wabongo tumeanza kuthamini fani nyingine na sio kushikilia udaktari au uanasheria. natumai mdau atarudi bongo aendeleze fani yake maana position za machef katika mahoteli na migahawa mikubwa zote zimeshikiliwa na wageni. karibu sana nyumbani mkuu ila kama utaweza kuongeza ujuzi na vyakula vya far east na india itakua poa zaidi.

    ReplyDelete
  4. Wasafisha midomo watasema wanachosema, lakini ukweli unabaki palepale kuwa Chef Issa AMEULA...Chefhood ni kazi inayolipa mno, hasa ukiipatia kama Chef Isa...inalipa kokote kule kwani WATU WAKISHATAFUTA HELA (MATAJIRI) WANATAKA KULA VIZURI
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  5. HONGERA SANA MDAU.HAYA NDIO MAMBO WABONGO YA KUJIVUNIA.
    KEEP IT UP MAN,UKO JUU.
    Cha chandu-uk

    ReplyDelete
  6. congratulations to you ........

    ReplyDelete
  7. Hongera sana sana. Hayo ndio mambo mazuri ya kujivunia.

    ReplyDelete
  8. JK UPOOOO!!! Kama unahitaji mtaalamu wa mamsosi huyo hapo. Kaka Isa unajua kupika makande?? Maana raisi wetu mara ghafla ana hamu ya bamia. duvi na ugali. LOL Hongera ndugu

    ReplyDelete
  9. kazi ni kazi kaka.! ukirudi bongo ndani ya miezi 3 utakuwa na usafiri mzuri.wish u all the best!

    ReplyDelete
  10. SAFI SANA BWAMDOGO..HIZI NI FANI AMBAZO VIONGOZI WETU WANAZIDHARAU...WANAZIPIGILIA ZILE FANI ZA KUFANYA MADILI.. HONGERA SANA TENA SANA MHESHIMIWA

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Issa; ninaamini kabisa umefuata moyo wako kusomea huu ujuzi muhimu sana. Watanzania tuige mfano wa Issa fani ziko nyingi sana kuliko Sheria, Udaktari, Uhasibu na IT.

    Mdau,

    Network Engineer (NE)
    Reading, UK

    ReplyDelete
  12. hongera saaaana issa kweli penye nia pana njia kweli nondo yako ni ya uhakika kazi utapata popote duniani lazima watu wale hongera sana
    manka wa canada

    ReplyDelete
  13. SASA AMESOMEA WAPI FAN HIYO, UMEELEZA TU KUWA INATAMBULIKA NA MANCHESTER METROPOLITAN UNIVERSITY NA INTERNATIONAL SCHOOL OF HOTEL MANAGEMENT SWISZERLAND, CHEF HAWEZI KUONGOZA HOTEL KUTOKANA NA MAELEZO YAKO HAPO JUU. HACCP NI HAZARD ANALYSIS AND CRITICAL CONTROL POINT, NI SYSTEM APPLIED TO MONITOR AND CONTROL MICROBIOLOGICAL, PHYSICAL AND PRODUCTION OF ANY FOOD MANUFACTURING PROCESS NA HII ILIANZISHWA NA NASA WAKATI WAKITENGENEZA VYAKULA VYA ASTRONAULT WAKATI WAKIWA SPACE. KILA KIWANDA CHA CHAKULA AU MA-HOTEL WANA UTARATIBU WAO WA KUPIMA SO IT IS NOT ABOUT GREAT EDUCATION ANYBODY CAN DO THAT AND YOU DONT NEED TO GO TO COLLEGE FOR THAT.

    ReplyDelete
  14. UWEZI KUONGOZA HOTELETI KWA SABABU WEWE NI HACCP CERTIFIED.

    NDUGU WANANCHI KUNA MTU HAPO AMEELEZEA VIZURI SANA KUHUSU HACCP NA HISTORIA YAKE.

    LAKINI MKITANA KUJUA ZAIDI KUHUSU HACCP NJOONI HAPA KWENYE OFISI ZETU TIRDO (TANZANIA INDUSTRIA RESEARCH AND DEVELOPMENT ORGANIZATION.)

    TUNAO WATAALAM WENGI TU HAPA AMBAO NI HACCP CERTIFIED.

    NAFIKIKIRI HUYO KIJANA ANGEKUJA HAPA TUMUAJIRI AJIUNGE NA WENZIE NA SIO KUONGOZA HOTELI.

    ReplyDelete
  15. nyinyi hapo juu msijifanye kuichambua nondo ya mwenzenu anajua alichosomea acheni gubu ebo kujifanya mnajua saaana leteni na nyinyi nondo zenu sio msubiri za wenzenu na kuanza kuzichambua kama vile nyie ndo maprofesa kha!

    ReplyDelete
  16. Hongera Garry Coleman kwa kupata nondoz yako.Nasubiri uje utufanyie mambo kemps...

    ReplyDelete
  17. Hongera Issa, mwenye wivu na ajinyonge, endelea na elimu zaidi wala usirudi Bongo, huko uliko utaula maana kazi ya chef majuu inalipa, asikudanganye mtu eti njoo uajiriwe hapa TIRDO kuna watu kibao wenye hiyo HACCP certified ni wengi, hata kama ni wengi je wana degree ya Uchef? Wabongo acheni wivu, nyie kaeni hapo TIRDO na vumbi la Msasani Maandazi road, kuleni maandazi na vitumbua vya mavumbi kutoka maandazi road, na chips kuku za hapo nje barabarani.

    ReplyDelete
  18. Doctor bingwa wa wanawake na doctor bingwa wa watoto ni taaluma mbili lakini ukiwa doctor bingwa wa wanawake na watoto unakua juu zaidi sasa huwezi kua Executive chef bila ya kuwa HACCP certified dogo ameula mdau Tido huna idea yeyote namambo ya hotel nyamaza kinachomfanya issa aqualify ni Art in european culinary management na HACCP ni muhimu sana Mdau USA

    ReplyDelete
  19. Hapo Tido unawataalamu ambao ni HACCP certified lakini sio ma chef na utakuaje HACCP certified bila ya kusoma na ndio maana tunawataalamu wababaishaji tanzania usioongee kitu we mdau wa Tido hatuna machef ambao HACCP wengi wanafanya kazi kwa uzoefu na riski ya usalama wa chakula ktk mahotel Tanzania ni kubwa sana tunaponea kudra za mungu chef Issa oyeeee umefanya mapinduzi makubwa kwa machef Tanzania ktk umri mdogo sana mdau Arusha

    ReplyDelete
  20. Nashukuru sana wadau kwa hongera zenu pamoja na maoni yenu yote ni changamoto ya kwangu mola anijaliapo kurudi home nitajitaidi kugawa ujuzi nilioupata kwa ndugu zangu watanzania kama shukurani kwa wazazi wangu kunisomesha na mungu kunijalia afya na kufaulu kwa kiwango cha hali ya juu mola awabariki chef Issa

    ReplyDelete
  21. Ili uwe executive chef certified unatakiwa ufanye kazi kwa muda kadhaa kama kiogozi pia baada ya masomo ya darasani mwisho mnafanyiwa mashindano pamoja na mtihani wa vitendo inaangaliwa uwezo wako wa kumili jiko, ushirikiano na staff, test ya chakula na time management huwezi faulu kama hujaweza yote hayo chef Issa uko juu ulaya hawabahatishi unatisha General Manager Hotel Zanzibar

    ReplyDelete
  22. MDAU WA TIDO UNAMTIMANYONGO WA AJABU KWELI NABII HAKUBALIKI KWAO NA TANZANIA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA WAGENI NINI TUJIVUNIE IKIWA WAZAWA WALIOJIKOMBOA TUNAPIGA VITA NINGEKUA NA HOTEL NIGEKUPA KAZI YA GENERAL MANAGER CHEF ISSA KWANI KUA EXECUTIVE CHEF SIO MCHEZO WEWE NDIO UTI WA MGONGO WA HOTEL CHEF NI LULU YA HOTEL MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU YOUR THE REAL GENTLE CHEERS!!! MDAU Netherland

    ReplyDelete
  23. Chef Issa mi nina diploma ya chuo cha hotel botswana please ukirudi home mi naomba tu nisome log book yako maana ninaimani itakua na recipe zakufa mtu huwezi graduate bila kutengeneza logbook inayocover overall course learning outcomes kaka unatisha rudi home utupe mautaalamu nakutamani sana chef wangu karibu home kaka.
    chef Kempiski Dar

    ReplyDelete
  24. TUNABURUZWA SANA NA MACHEF WA KIZUNGU NA WAKENYA HAPA TANZANIA PLEASE PLEASE CHEF ISSA RUDI NYUMBANI TUPUMUE WAZUNGU NASI WATUHESHIMU KAKA UMEJIKOMBOA FANI YA CULINARY HAPA NYUMBANI HATUNA WATAALAMU TUNAJIVUNIA SANA MAFANIKIO YAKO MUNGU AKUBARIKI UWE MPOLE USAIDIE KUELIMISHA NASI TUFIKIE VIWANGO.
    MDAU MOVENPICK DAR

    ReplyDelete
  25. Hahaha duh mtu anakuwa HACCP certified halafu hajaenda shule inakuaje hiyo roho mbaya sio mpaka uuwe hata kurudisha nyuma maendeeo ya watu ni wivu wa ajabu sana huo inabidi ufukuzwe kazi wewe unaajiri certified people ambao hawajaenda shule Tido vipi mnachekesha sana tumesoma sana tunashindwa kurudi kujenga taifa kwajili ya majungu yasio na msingi nyumbani mdogo wangu chef Issa Hongera sana mimi Daktari bingwa wa meno Mmatumbi SPAIN

    ReplyDelete
  26. Congratulations mume wangu I am proud of you

    ReplyDelete
  27. Hongera Issa umewini na ukweli unabaki palepale watu watasema ni kawaida ya waafrika badala ya hongera wao wanaona wivu kama huyo mdau anaesema haoni sababu ya wee kwenda kusoma europe me nadhani hajui anachosema kabisa kwani hakuna asiejua kuwa tz na europe haiwezi kuwa sawa kwa upande wa elimu na nadhani hajui kuwa hakuna mtu anaweza kusoma chuo huko bila kuwa colyfied so sijui jamaa hata yeye alisoma chuo gani? any way maoni kwa watanzania............TUSIIGE TU MAVAZI KWA WAZUNGU ILA HATA TABIA YAO PIA NI VIZURI KUIGA TUMPE HONGERA MTANZANIA MWENZETU NA SIO WIVU WAKIJINGA ILA WIVU WA MAENDELEO...pole bro Isaa yupo juuuuuuuuuuuuuuuuuu

    Mdau London

    ReplyDelete
  28. we jamaa wa tido mshamba sana unatakiwa usome uelewe chef issa kasomea European culinary management ndio inayomfanya aweze kuongoza hotel kokote duniani na HACCP ni sehemu ya elimu aliyopata sio sababu ya kua executive chef pia uzoefu na taaluma aliyonayo ndio anapata heshima hiyo ya kua executive chef mdau tido unalo limekuganda na utajiju Mdau PARIS

    ReplyDelete
  29. Great job Chef Issa what an accomplishment.This is one of the rare degrees Tanzanians take abroad,I'm tired of wahamiaji kuchukua kazi muhimu na nyeti kama hizi Tanzania.Once again Congratulation..You did it.
    Mdau Houston.

    ReplyDelete
  30. Issa mdogo wangu hongera sana, hata siamini ni wewe mdogo wangu, kweli alipangalo mungu hakuna awezaye pangua.

    mdogo wangu nakukumbuka sana enzi tukiwa wote moevnpick Royal Palm,tukiwa night unanitengenezea chakula.
    mkeo na mwanao / wanao hawajambo? wasalimie sana.

    tuwasiliane
    Sis Jacque.

    ReplyDelete
  31. Sina la kusema ila kukupa hongera sana Issa. Umeiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika fani hii inayojengeka na kusifika sana. Wafaransa wanawania kuwa wanafani hii wa kwanza duniani. Fikiria na wewe unaiingiza Tanzania katika mashindano haya. Nani ajuaye? Tanzania itajikuta iko juu zaidi kuliko Kilimaniaro. Nakukaribisha Norway nikupeleke wakuhoji katika utangazaji wao. Nitafurahi ukipata fursa ya kimpikia Mfalme wao na ma vikining wengine. Hongera mno. Ninajivunia kuwa nimetoka nchi moja na wewe. Unanifanya nitembee bimenyoosha mgongo na shingo hapa baridini.
    Mimi ni dada wa nchi moja na wewe,
    Chiku Ali
    Bergen, Norway

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...