Chef Issa akila nondozzzz yake
Chef Issa akila nondozzzz yake
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Chef Issa akila nondozzzz yake Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hongera kaka Inshaallah elimu uliyopata iwe ni ufunguo wa uelewa kwa wale ambao wanadharau fani hii yetu ya hotel management.
ReplyDeleteHongera sana Issa kwa mafanikio hayo. Uendelee kuchagiza wengine na uwe mfano bora zaidi na zaidi!
ReplyDeletesaafi saaana. angalau wabongo tumeanza kuthamini fani nyingine na sio kushikilia udaktari au uanasheria. natumai mdau atarudi bongo aendeleze fani yake maana position za machef katika mahoteli na migahawa mikubwa zote zimeshikiliwa na wageni. karibu sana nyumbani mkuu ila kama utaweza kuongeza ujuzi na vyakula vya far east na india itakua poa zaidi.
ReplyDeleteWasafisha midomo watasema wanachosema, lakini ukweli unabaki palepale kuwa Chef Issa AMEULA...Chefhood ni kazi inayolipa mno, hasa ukiipatia kama Chef Isa...inalipa kokote kule kwani WATU WAKISHATAFUTA HELA (MATAJIRI) WANATAKA KULA VIZURI
ReplyDeleteMdau
Japan
HONGERA SANA MDAU.HAYA NDIO MAMBO WABONGO YA KUJIVUNIA.
ReplyDeleteKEEP IT UP MAN,UKO JUU.
Cha chandu-uk
congratulations to you ........
ReplyDeleteHongera sana sana. Hayo ndio mambo mazuri ya kujivunia.
ReplyDeleteJK UPOOOO!!! Kama unahitaji mtaalamu wa mamsosi huyo hapo. Kaka Isa unajua kupika makande?? Maana raisi wetu mara ghafla ana hamu ya bamia. duvi na ugali. LOL Hongera ndugu
ReplyDeletekazi ni kazi kaka.! ukirudi bongo ndani ya miezi 3 utakuwa na usafiri mzuri.wish u all the best!
ReplyDeleteSAFI SANA BWAMDOGO..HIZI NI FANI AMBAZO VIONGOZI WETU WANAZIDHARAU...WANAZIPIGILIA ZILE FANI ZA KUFANYA MADILI.. HONGERA SANA TENA SANA MHESHIMIWA
ReplyDeleteHongera sana Issa; ninaamini kabisa umefuata moyo wako kusomea huu ujuzi muhimu sana. Watanzania tuige mfano wa Issa fani ziko nyingi sana kuliko Sheria, Udaktari, Uhasibu na IT.
ReplyDeleteMdau,
Network Engineer (NE)
Reading, UK
hongera saaaana issa kweli penye nia pana njia kweli nondo yako ni ya uhakika kazi utapata popote duniani lazima watu wale hongera sana
ReplyDeletemanka wa canada
SASA AMESOMEA WAPI FAN HIYO, UMEELEZA TU KUWA INATAMBULIKA NA MANCHESTER METROPOLITAN UNIVERSITY NA INTERNATIONAL SCHOOL OF HOTEL MANAGEMENT SWISZERLAND, CHEF HAWEZI KUONGOZA HOTEL KUTOKANA NA MAELEZO YAKO HAPO JUU. HACCP NI HAZARD ANALYSIS AND CRITICAL CONTROL POINT, NI SYSTEM APPLIED TO MONITOR AND CONTROL MICROBIOLOGICAL, PHYSICAL AND PRODUCTION OF ANY FOOD MANUFACTURING PROCESS NA HII ILIANZISHWA NA NASA WAKATI WAKITENGENEZA VYAKULA VYA ASTRONAULT WAKATI WAKIWA SPACE. KILA KIWANDA CHA CHAKULA AU MA-HOTEL WANA UTARATIBU WAO WA KUPIMA SO IT IS NOT ABOUT GREAT EDUCATION ANYBODY CAN DO THAT AND YOU DONT NEED TO GO TO COLLEGE FOR THAT.
ReplyDeleteUWEZI KUONGOZA HOTELETI KWA SABABU WEWE NI HACCP CERTIFIED.
ReplyDeleteNDUGU WANANCHI KUNA MTU HAPO AMEELEZEA VIZURI SANA KUHUSU HACCP NA HISTORIA YAKE.
LAKINI MKITANA KUJUA ZAIDI KUHUSU HACCP NJOONI HAPA KWENYE OFISI ZETU TIRDO (TANZANIA INDUSTRIA RESEARCH AND DEVELOPMENT ORGANIZATION.)
TUNAO WATAALAM WENGI TU HAPA AMBAO NI HACCP CERTIFIED.
NAFIKIKIRI HUYO KIJANA ANGEKUJA HAPA TUMUAJIRI AJIUNGE NA WENZIE NA SIO KUONGOZA HOTELI.
nyinyi hapo juu msijifanye kuichambua nondo ya mwenzenu anajua alichosomea acheni gubu ebo kujifanya mnajua saaana leteni na nyinyi nondo zenu sio msubiri za wenzenu na kuanza kuzichambua kama vile nyie ndo maprofesa kha!
ReplyDeleteHongera Garry Coleman kwa kupata nondoz yako.Nasubiri uje utufanyie mambo kemps...
ReplyDeleteHongera Issa, mwenye wivu na ajinyonge, endelea na elimu zaidi wala usirudi Bongo, huko uliko utaula maana kazi ya chef majuu inalipa, asikudanganye mtu eti njoo uajiriwe hapa TIRDO kuna watu kibao wenye hiyo HACCP certified ni wengi, hata kama ni wengi je wana degree ya Uchef? Wabongo acheni wivu, nyie kaeni hapo TIRDO na vumbi la Msasani Maandazi road, kuleni maandazi na vitumbua vya mavumbi kutoka maandazi road, na chips kuku za hapo nje barabarani.
ReplyDeleteDoctor bingwa wa wanawake na doctor bingwa wa watoto ni taaluma mbili lakini ukiwa doctor bingwa wa wanawake na watoto unakua juu zaidi sasa huwezi kua Executive chef bila ya kuwa HACCP certified dogo ameula mdau Tido huna idea yeyote namambo ya hotel nyamaza kinachomfanya issa aqualify ni Art in european culinary management na HACCP ni muhimu sana Mdau USA
ReplyDeleteHapo Tido unawataalamu ambao ni HACCP certified lakini sio ma chef na utakuaje HACCP certified bila ya kusoma na ndio maana tunawataalamu wababaishaji tanzania usioongee kitu we mdau wa Tido hatuna machef ambao HACCP wengi wanafanya kazi kwa uzoefu na riski ya usalama wa chakula ktk mahotel Tanzania ni kubwa sana tunaponea kudra za mungu chef Issa oyeeee umefanya mapinduzi makubwa kwa machef Tanzania ktk umri mdogo sana mdau Arusha
ReplyDeleteNashukuru sana wadau kwa hongera zenu pamoja na maoni yenu yote ni changamoto ya kwangu mola anijaliapo kurudi home nitajitaidi kugawa ujuzi nilioupata kwa ndugu zangu watanzania kama shukurani kwa wazazi wangu kunisomesha na mungu kunijalia afya na kufaulu kwa kiwango cha hali ya juu mola awabariki chef Issa
ReplyDeleteIli uwe executive chef certified unatakiwa ufanye kazi kwa muda kadhaa kama kiogozi pia baada ya masomo ya darasani mwisho mnafanyiwa mashindano pamoja na mtihani wa vitendo inaangaliwa uwezo wako wa kumili jiko, ushirikiano na staff, test ya chakula na time management huwezi faulu kama hujaweza yote hayo chef Issa uko juu ulaya hawabahatishi unatisha General Manager Hotel Zanzibar
ReplyDeleteMDAU WA TIDO UNAMTIMANYONGO WA AJABU KWELI NABII HAKUBALIKI KWAO NA TANZANIA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA WAGENI NINI TUJIVUNIE IKIWA WAZAWA WALIOJIKOMBOA TUNAPIGA VITA NINGEKUA NA HOTEL NIGEKUPA KAZI YA GENERAL MANAGER CHEF ISSA KWANI KUA EXECUTIVE CHEF SIO MCHEZO WEWE NDIO UTI WA MGONGO WA HOTEL CHEF NI LULU YA HOTEL MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU YOUR THE REAL GENTLE CHEERS!!! MDAU Netherland
ReplyDeleteChef Issa mi nina diploma ya chuo cha hotel botswana please ukirudi home mi naomba tu nisome log book yako maana ninaimani itakua na recipe zakufa mtu huwezi graduate bila kutengeneza logbook inayocover overall course learning outcomes kaka unatisha rudi home utupe mautaalamu nakutamani sana chef wangu karibu home kaka.
ReplyDeletechef Kempiski Dar
TUNABURUZWA SANA NA MACHEF WA KIZUNGU NA WAKENYA HAPA TANZANIA PLEASE PLEASE CHEF ISSA RUDI NYUMBANI TUPUMUE WAZUNGU NASI WATUHESHIMU KAKA UMEJIKOMBOA FANI YA CULINARY HAPA NYUMBANI HATUNA WATAALAMU TUNAJIVUNIA SANA MAFANIKIO YAKO MUNGU AKUBARIKI UWE MPOLE USAIDIE KUELIMISHA NASI TUFIKIE VIWANGO.
ReplyDeleteMDAU MOVENPICK DAR
Hahaha duh mtu anakuwa HACCP certified halafu hajaenda shule inakuaje hiyo roho mbaya sio mpaka uuwe hata kurudisha nyuma maendeeo ya watu ni wivu wa ajabu sana huo inabidi ufukuzwe kazi wewe unaajiri certified people ambao hawajaenda shule Tido vipi mnachekesha sana tumesoma sana tunashindwa kurudi kujenga taifa kwajili ya majungu yasio na msingi nyumbani mdogo wangu chef Issa Hongera sana mimi Daktari bingwa wa meno Mmatumbi SPAIN
ReplyDeleteCongratulations mume wangu I am proud of you
ReplyDeleteHongera Issa umewini na ukweli unabaki palepale watu watasema ni kawaida ya waafrika badala ya hongera wao wanaona wivu kama huyo mdau anaesema haoni sababu ya wee kwenda kusoma europe me nadhani hajui anachosema kabisa kwani hakuna asiejua kuwa tz na europe haiwezi kuwa sawa kwa upande wa elimu na nadhani hajui kuwa hakuna mtu anaweza kusoma chuo huko bila kuwa colyfied so sijui jamaa hata yeye alisoma chuo gani? any way maoni kwa watanzania............TUSIIGE TU MAVAZI KWA WAZUNGU ILA HATA TABIA YAO PIA NI VIZURI KUIGA TUMPE HONGERA MTANZANIA MWENZETU NA SIO WIVU WAKIJINGA ILA WIVU WA MAENDELEO...pole bro Isaa yupo juuuuuuuuuuuuuuuuuu
ReplyDeleteMdau London
we jamaa wa tido mshamba sana unatakiwa usome uelewe chef issa kasomea European culinary management ndio inayomfanya aweze kuongoza hotel kokote duniani na HACCP ni sehemu ya elimu aliyopata sio sababu ya kua executive chef pia uzoefu na taaluma aliyonayo ndio anapata heshima hiyo ya kua executive chef mdau tido unalo limekuganda na utajiju Mdau PARIS
ReplyDeleteGreat job Chef Issa what an accomplishment.This is one of the rare degrees Tanzanians take abroad,I'm tired of wahamiaji kuchukua kazi muhimu na nyeti kama hizi Tanzania.Once again Congratulation..You did it.
ReplyDeleteMdau Houston.
Issa mdogo wangu hongera sana, hata siamini ni wewe mdogo wangu, kweli alipangalo mungu hakuna awezaye pangua.
ReplyDeletemdogo wangu nakukumbuka sana enzi tukiwa wote moevnpick Royal Palm,tukiwa night unanitengenezea chakula.
mkeo na mwanao / wanao hawajambo? wasalimie sana.
tuwasiliane
Sis Jacque.
Sina la kusema ila kukupa hongera sana Issa. Umeiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika fani hii inayojengeka na kusifika sana. Wafaransa wanawania kuwa wanafani hii wa kwanza duniani. Fikiria na wewe unaiingiza Tanzania katika mashindano haya. Nani ajuaye? Tanzania itajikuta iko juu zaidi kuliko Kilimaniaro. Nakukaribisha Norway nikupeleke wakuhoji katika utangazaji wao. Nitafurahi ukipata fursa ya kimpikia Mfalme wao na ma vikining wengine. Hongera mno. Ninajivunia kuwa nimetoka nchi moja na wewe. Unanifanya nitembee bimenyoosha mgongo na shingo hapa baridini.
ReplyDeleteMimi ni dada wa nchi moja na wewe,
Chiku Ali
Bergen, Norway