and her students pose at Mkwawa University in Tanzania.
Han Shin-ha, 36, a volunteer worker dispatched by the Korea International Cooperation Agency (KOICA) to Tanzania, has landed a full-time professorship at Mkwawa University, Tanzania's national university.
According to KOICA, a state-run agency sending volunteers to developing countries, Han started teaching molecular and cellular biology as a professor at the beginning of the month.
Full story


Baada ya waChina wajifanyao wawekezaji sasa twatupiwa waKorea!!!Yaani nchi yetu imekuwa jalala...Maprofesa wetu watafanya kazi wapi kama hawa waKorea watazidi tupwa Tanzania??!!Haya ni mambo ya kuchafua roho.
ReplyDeleteMICHUZI UWE UNAWEKA MATANGAZO YA KAZI PIA, UTAONGEZA WATEMBELEAJI WA GLOBU YAKO.
ReplyDeleteSisi wamatumbi tukiwa huko kwao ni vigumu sana kupata kazi kama hiyo. Hata kama sifa tunazo.
ReplyDeleteLabda kama tumesomea nchini kwao. Hata hivyo inahitaji kusotea kwa miaka mingi. Sana sana utaambiwa ukafundishe somo la Kiswahili(part time).
Anyway, labda ndio kubadilishana maarifa. Hata hivyo, hii ikubalike pande zote si upande mmoja tu.
MDAU,
ASIA (Far East)
Mimi nashabikia hii, kwani kama hatutaki kusoma tunalalamika nini? mnataka vyuo vifungwe kwa sababu havina walimu, iwe changamoto kwetu ili tusome na kusomesha watoto si kupiga makelele ya bure ukiulizwa tuambie huyo mtaalamu wa molecular biology yupo wapi huna hoja yoyote. Waje wengi ili mradi watoto wetu wapate elimu tuone kama tunaweza badilika na kuacha longolongo vinywani mwetu.
ReplyDeleteWatanzania acheni roho ya chuki. Korea ya kusini inatoa fedha chungu mzima Tanzania na inaelimisha Watanzania bure. Hamjui huyu dada kaletwa vipi au analipwa na nani. Huenda mshahara wake unatoka kwao na yeye analeta faida ya elimu yake kuendeleza Tanzania. Kuna Watanzania wangapi wako tayari kufanya kazi Mtwara au kwa mshahara mdogo? Watu kama hawa dada wanaacha kuishi nchini kwao kwa raha na kuja Afrika kuishi na malaria na kiga ili watusaidie halafu mnakaa katika internet cafe na kukashifu watu bila ya kufikiria. Hii royo ya korosho ndio inayotufanya tusiendelee milele.
ReplyDeleteKwa taarifa ya mdau hapo juu, kama una elimu ya maana na lugha inapanda, unaweza kufanya kazi kokote, mbona wenzako tunafanya kazi za maana tu hapa Korea na Japani.
Ndugu zanguni, embu tuache kuwa na hisia zisizo na mantiki.
ReplyDeleteKwanza, she was a volunteer mwanzo. Kwahiyo inabidi tuwe na shukrani kwa kujitoa kwake kuja nchini mwetu na kusaidia ktk sekta ya elimu. Kupata watu wenye ujuzi kuja nchini mwako na kujituma kusaidia maendeleo ni jambo la kushukuru.
Pili, hiyo position sio kwamba kapewa tu. Ni kwamba ameonekana kuwa ana uwezo ndio maana akapewa hiyo nafasi. Niambie kuna waTanzania wangapi ndani na nje ya nchi wenye PhD ya Molecular and Cellular Biology? Kama wapo, wapo tayari kwenda Mkwawa kufundisha?
Hongera, asante Prof. Shin-Ha kwa juhudi zako.
mdau
PhD Candidate, molecular & cell biology, Mc Gill Univ
tunaposema tumejisahau na hatujui mda wingine tunakwenda wapi ndo matatizo hayo. ka volunteer hapo ndo tumeona tumepata, fika kwao uone, black tena africa hata heshima haupati hata kama unasifa kama mdau alivyosema, mi nishahidi na yamenitokea, sana sana wanaona tu matatizo yanayolipotiwa kwenye mitandao kwamba africa bwana wanamatatizo na hawawezi.
ReplyDeleteMdau south korea
MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU
hiyo misaada unayosema mdau unajua wanaitoa kwa dhati au wanakitu wanatafuta?
ReplyDeletetuwe watu wa kuchambua na si tu kuangalia ukipewa boga basi unakula na kulidhika. ua haukusikia mambo ya kununua nchi ardhi bongo nini. tuipende nchi yetu jamani hata kama ni masikini lakini tuone tunakwenda wapi. kwa hii molecular hakuna wabongo hapa wanaoweza?
mdau unayefanya kazi ya maana korea tuwasiliane bwana unaweza kuwa msaada nipo korea 01058323289
ReplyDeleteMimi si mtoaji wa maoni katika ukumbi huu.lakini napenda kuchangia katika hili.Ni ni taabu sana kupata kazi katika nchi za wenzetu hasa hizi za kusomesha, mpaka mtu anaetaka kukujiri atoe ushahidi wa kuwa hakuna mzalendo mwenye uwezo kama wako.Je sasa na tujiulize kuna Pro wangapi wa molecular biology TZ? jibu hakuna. mimi nilikuwepo Muhimbili pale maprofesor karibu ya asilimia 70 hawakufanya Phd na kwa ujumla chuo kizima hata 20 hawafiki.na hivi mmejiuliza kwa nini Muhimbili hawatoi Phd kozi? kwanza tafuteni sababu ndiyo mulalamike. kwa kifupi sisi Tz tuko nyuma sana kielimu yaani mtu anamliza degree mwezi wa tatu wa tisa anaajiriwa na kuwa msadizi lecture? sasa je akitokea mtu mwnye sifa na yuko tayari kuwapa elimu wa tz tusimuajiri?mimi ni dr na degree zangu zote nimesoma nje na sijaona mwalimu fresh Phd hapewi lecture kusomesha lakini TZ tuna phd holder hawafiki 400 na vyuo kibao vinaanzishwa.jee tutawatoa wapi walimu?mimi naomba tusiporoje kaa kitu hatukijui.
ReplyDeleteTanzania haina walimu wa kutosha wa sekondari, iwe vyuo vikuu? Waleteni tu hao wageni waje watupe darasa, kwani hatupotezi kitu, PhD ya mtu mmoja inaweza ikazaa hata 5 kati ya hao wanafunzi wa Mkwawa. So in the end we benefit in the long run. WaTZ wenye PhD ya Molecular Biology wapo, ila tatizo ni kwamba idadi haitoshi. Ninauhakika hatufiki 50 dunia nzima. Tunahitaji msaada.
ReplyDeletePia, vijana wajitume kusoma masomo kama haya, na sio kukimbilia MD pale Muhimbili. Kwani kasumba ya kuwa ukisoma PCB na kuchana pepa lazima uwe daktari nadhani inabidi tuitupe. Kwani nchi inahitaji research base, na masomo kama biophysics, molecular biology, biochemistry, systems biology, computational chemistry, nk ndio yenye manufaa hasa ktk kuinua nchi na kusaidia ktk matazizo yetu kwenye afya, viwanda, na mazingira.
Mi majuzi tu nimepata PhD ktk masuala hayo hayo, in fact kuhusu Transmission dynamics of heritable silencing induced by dsRNA. Kiufupi kwa kiswahili ni ......... anyway, translation yake ni mada nyingine.
Kazi kweli kweli. Mtu mwenye PhD anapewa kazi as a professor??? Only in Tz. Ningependa kuona publications zake zinazompa sifa ya uprofessor!!
ReplyDeleteMdau unaolalamika sijui unataka kuona sifa za huyu dada. kwani wewe ni nani? Kwa nini kila akija mgeni akipewa kazi mnanalika kama vile tuna elimu ya kutosha wenyewe. Tuna wasomi wa chuo kikuu wangapi wenye Ph.D (sio ya internet) Tanzania unafikiri katika fani ya huyu dada?
ReplyDeleteKama tuna madaktari wa kutosha kwa nini hatuwezi kujitibu mpaka tukimbilie India au Afrika Kusini?
Ilikuwa tumshukuru huyu dada kaja katika nchi ambayo ni ya kimasikini kutusaidia kwa kutumia elimu yake. Hata kama kuna wasomi kama yeye, sidhani watakuwa tayari kwenda Mtwara, utakuta wanakimbilia ulaya kutafuta maisha kwa kuwa mshahara nyumbani ni mdogo na hatuna nafasi ya kujiendeleza katika masomo yetu. Utakuta daktari anatibu miaka chungu mzima pengine akitumia madawa ya kizamani au mitindo ya kizamani. Kama wadau hawafahamu maswala ya elimu na sayansi, bora wanyamaze tu.
Pia, Sisi wenyeze lakini ndio wazembe kwa kuwa tunakubali kufundishwa na walimu tangu shule ya vidudu mpaka sekondari ambao wengi wao hawana elimu ya ualimu ya chuo kikuu. Serikali mpaka leo imesinzia kuhusu hili swala la kuruhusu walimu wafundishe bila ya elimu ya ualimu kama wanavyofanya nchi nyingine.
Mmmnh yaani tunachekesha kweli yaani tunapoteza na muda kabisaaa kumtetea huyu mdada,sijui kama mjadala huu ungekuwepo huko kwao kama kungekekua na yeyeote kati yao anayemtetea mBongo afundishe wakati watu wao hawana kazi?!!Hizi scholarship zitolewe kwa manufaa na maendeleo ya nchi yetu sio kutuletea wazamiaji hapa!!
ReplyDeleteLeo BBC imetangaza kuwa Korea ya Kusini itajenga nyumba 200,000 Ghana. 90,000 itapewa serikali na nyinginezo zitauzwa. Pia wanakodishiwa ardhi ili walime kwa teknolojia ya kisasa kama za kujenga nyumba.
ReplyDeleteHapa Waghana watapata nyumba za bei nafuu, watu wao watapewa elimu ya kisasa ya kilimo na kila nchi itafaidika.
Sisi tumekaa bado na ardhi yetu, hatutaki itumiwe na wageni.