Timu ya Taifa Kilimanjaro Stars leo imeifunga Burundi goli 1-0 kwenye uwanja wa Mumias nchini Kenya katika mechi ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.
Alikuwa ni Mrisho Ngasa aliyewatungua Burundi katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi nzuri iliyounganishwa na Mussa Hassan Mgosi ambaye aliwekewa pasi murua na Juma Nyosso.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana na waliporudi uwanjani Kilimanjaro Stars ilipata nguvu zaidi na kujiweka sawa. Kilimanjaro Stars sasa imefikisha Pointi 4 baada ya kushinda michezo miwili na kufungwa mmoja ambapo ilifungwa na Uganda goli 2, kabla ya kuicharaza Zanzibar goli 1-0 alilofunga huyo huyo Ngassa.


Bro hii pub ni wanaume wa kawaida?Au wale wanao punga punga mikonos...
ReplyDeleteSorry but advert with those guys with no t-shirt might give wrong impression :D
Michuzi... hawa jamaa wa P-square mbona wako Cardiff Ijumaa hii sasa wataweza kweli kupanda ndege Heathrow na kuwa Dar by jioni? I doubt it unless wakache moja...!!!
ReplyDeletepoint 6 au?
ReplyDeleteyale yale hakuna chochote kile kipya kwanza hata tukabeba ubingwa hakuna rank yoyote tutakayoipata ya dunia tupo pale pale halafu hapa ikifungwa tz hatuoni kitu mpaka ifungwe znz ndio midomo juu znz tumeifunga znz tumeifunga hivi midudu nyie bongo wapi na wapi kwa mpira labda kunywa pombe na kucheza ngoma hapo duniani naona tutakuwa number one yakija mashindani. But mpira siku zote mtakuwa kichwa cha mwendawazimu na nidhamu zenu mbovu manake mnasifika kwa utovu wa adabu na ubabe mwengi ndio mkatufunga znz kwa kutembeza viatu. Nchi kama yemen ilikufungeni mlipoifunga znz hapo mlikuja na midomo mikubwa pumbav
ReplyDeletekwa hiyo wewe umekasirika kufungwa au michuzi kuweka hewani kuwa mmefungwa ?
ReplyDeletejazba , matusi , bado majini tu mtumalize .
Mi my concern yangu tu ni kuona bro Michuzi bado anahesabu pointi kizamani zamani yaani pointi 2 kwa kila winning!! Kaka tupo kwenye pointi 3 sasa hivi na pengine mwakani inaweza kuwa ni pointi 5 kwa kila winning...ha ha haaaaa. Tuna pointi 6 mzee wa nanihii.
ReplyDelete