gari aina ya Suzuki Vitara lilikiwa limepinduka ndani ya mtaro mkubwa uliopo pembezoni mwa barabara ya Morogoro Road, katika eneo la Kimara bucha.
gari hii ilijikuta ikiingia mtaroni humo mara baada ya kuchomekewa na daladala kuingia upande wa pili wa barabara bila ya ishara yoyoye na kusababisa dereva wa gari hii aina ya vitara kutaka kujaribu kumkwepa na kujikuta katika hali hii.
daladala lenyewe ni hilo hapo ambalo liko chini ya usimamizi wa Askari Polisi ambao kwa bahati nzuri walikuwepo jirani kabisa na eneo lilipotokea tukio hilo.


TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA
ReplyDeleteDereva wa daladala ana makosa.
ReplyDeleteLakini wa kwanza kukosea ni mmiliki wa hio barabara kwani haikusanifiwa na kujengwa kwa viwango vinavyojali usalama wa watumiaji. Niliishawaeleza wamiliki wa hio barabara kwamba ilikosewa toka mapema miaka ya 2000.
Hiyo si ajali ya kwanza na ya mwisho.
jamani barabara kama hizo zinatakiwa ziwe na nguzo za pembeni kuzuiya magari kuingia kene mitaro kama hiyo.lazima serikari za mitaa zipitie hapa na kurekebisha hayo,mitaro iko uchi namna hiyo no hatari hata kwa wapita pemebeni jamani au wanaopaki kwa ajali.they need to put some sorts of guards to protect this kind of accident.kuspin out of control aina maaan uingie mtaroni kama hivyo.
ReplyDeletemichu,
ReplyDeletemimi kaaa yangu yote ulaya sasa zaidi ya miaka 10 sijaona 'high-way' yoyote ktk nchi za ulaya zenye 'mitaro mikubwa ya maji iliyo wazi' pembeni ya barabara.
labda wadau wa sehemu nyingine za dunia watufahamishe.
aina hii ya ujenzi huongeza uwezekano ya kupata majeruhi zaidi bila sababu za msingi.
mdau
ulayaulaya
Hiyo barabara inajulikana sana kwa ajali si kwa kuchomekewa tu hata full light usiku ni maarufu kwa kusababisha ajali eneo hilo.JAMANI INATISHA
ReplyDeleteHUYO MKANDARASI LAZIMA ALISOMEA INDIA,HUWEZI KUWEKA MTARO MKUBWA KIASI HICHO PEMBEZONI MWA BARABARA THATS DANGEROUS NOT ONLY FOR DRIVERS BUH ALSO FOR PEDISTRIANS.SUPPOSE SOMEONE IS REALLY DRUNK AND IS WALKING ALONGSIDE THAT DITCH AND HAPPENS THAT HE/SHE FALLS WOULD LIKELY DIE OR SUFFER SOME SEVERE INJURIES.AS FOR THE FORE CONTRIBUTORS HAVE SAID THESE KINDA DITCHES SHOULD HAVE SOME BARRIERS ALL ALONGSIDE TO AVOID THESE UNNECESSARY CASUALITIES.WAPI KODI ZA WANANCHI ZINAENDA??????KUJENGEA NYUMBA ZA MAFEDHULI SIO?OK
ReplyDeleteSiyo siri attitude na mwenendo wa madereva wa daladala hinifanya nitamani nitembee na kiboko ili kila wakikosea niwacharaze. Wahuni wakubwa hawa!!!AAgh
ReplyDeletehii ya leo kali!!mtaru huu ni kabuli tosha kwa madeleva na abiria inatisha hata kuendesha gari
ReplyDeleteHapo hao maofisa watapewa mshiko halafu huyo iliyeingia mtaroni ataachwa hapo ajijue.Mmmh aibu tupu!!
ReplyDeleteNimeona hiyo picha ya gari abalo limetumbukia kwenye mtaro mkubwa wa kimara na hiyo ndio nilikuwa nasema hawa maijinia wetu ni wa style ipi, kuwa na mitaro mikubwa?
ReplyDeleteplease Tanzania yetu ni ya sayasi na technology sasa where are we going? na hao wakakuzi wa barabara wanafanya nini? labda wameamua kupunguza watu wa jiji la dar tumekuwa wengi>>..
Madereva wa daladala wanahitaji adhabu kali kwa sababu sioni haraka ya nini na roho mbaya ya kumzuia dereva mwingine ambaye hayuko kwenye ushindani wa biashara huyo dereva anatakiwa kunyang'anywa leseni na adhabu kali.
ReplyDeleteMdau wa Fri Dec 04, 04:05:00 PM na wenzio mnaomlaumu mkandarasi wa barabara hiyo ya Morogoro hasa kuanzia kimara bucha hadi ubungo maji,binafsi namshukuru sana kama kweli alikosea,maana kosa lake limekua faida kwetu.Wengi wanaosema kakosea humjali dereva na abiria wake tu, na sio watembea kwa miguu na wenye makazi jirani na barabara hiyo. Na hawa ni kina sie ambao hata gari gani ipinduke wewe ukiwa service road hudhuriki kabisa, pia hata gari iliyotumbukia hua haiharibiki vibaya ukilinganisha na kama zingeweza kupata fulsa ya kuchagua shamba!Ilishawahi kutokea ajali pale katikati ya Safari Resort na kituo cha mafuta cha Oryx miaka ya tisini yaani Coaster dungu ilining'inia juu ya mwembe na abiria watu walifanya kuwakusanya viungo maana hakuna kilichotoka hai! Kama kuna mtu angebahatika kuishuhudia asingemlaumu mkandarasi wa sasa(Skanpil Colas)ambaye pia katengeneza barabara ya Chalinze Morogoro kipande kilichokua kikitisha kwa ajali. Ni yeye aliyeanzisha njia tatu sehemu yenye mlima na kona kali ili kupunguza ajali eneo hilo.So tuachieni mkandari wetu,kwani kwa sasa kuna matuta ya kutosha na ajali zimepungua sasa kipande cha kimara mwisho hadi ubungo. Ukitaka kujua ni kiasi gani kulikua na ajali sana eneo hilo kahesabu idadi ya taa za barabarani na vizio vyake utapata jibu
ReplyDeleteSidhani barabara ilivyo wazi ndivyo design ilivyoelekeza.
ReplyDeleteHela nyingi imeliwa hapo. Bampa za chuma zilihitajika ukingoni mwa barabara kama ilivyo sehemu zenye bonde refu kando ya barabara.