MPITANJIA AKIANGALIA MABAKI YA MWILI WA KIJANA MMOJA ASIYEJULIKANA AMBAYE WAKAZI WA MBEZI RUBOKO JIJINI DAR WENYE HASIRA KALI ALFAJIRI YA LEO WAMEMCHOMA MOTO HADI KUFA BAADA YA KUKUTWA AKIIBA VITU VYA NDANI KWENYE NYUMBA YA KARIBU NA ENEO LA TUKIO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. mgosi wa kayaDecember 30, 2009

    wabongo mna roho mbaya sana nyinyi watu ,mnajifanya mna hasira,hasira kitu gani wewe utakatiza vipi maisha ya mwenzako kwa kumchoma moto kisa kaiba kuku nani kakupa haki hiyo ya kumuhukumu mwenzio?Mbona mafisadi hamuwachomi moto kama mna hasira sana eti mnasubiria rais atoe tamko mbona hawa waiba kuku hamsubiri tamko likatolewa?Wewe unayemchoma mwenzio una mazuri gani ulioifanyia jamii?

    ReplyDelete
  2. NDUGU ZANGU WATANZANIA,KITENDO HICHI NI CHA KUSIKITISHA HAS UKIANGALIA KUNWA WEZI WENGI TU KATIKA SERIKALI YETU AMBAO WANAWAIBIA MAMILIONI YA WATU.NASIO HATA MTU MMOJA.JE HAWA VIONGOZI SIO WA KUCHOMWA AU KUTEMEWA MATE.HUYU KIJANA MLIYEMCHOMA SIO NDO JAWABU LA VIONGOZI AMBAO SIO WAADILI NA WENYE KUPENDA MADARAKA,WEZI NA WALA RUSHWA?
    MUNGU AMEWALAANI!
    WALLAH,KIAMA KINAKUJA.

    ReplyDelete
  3. Jamani, mtaenda toa hesabu huko tuendako. Si angeambiwa avirudishe tu jamani?

    Mi naona watu wangetafuta njia sahihi za kupunguza hasira zao zitokanazo na ugumu wa maisha, kama Yoga n.k.

    Yaani alikuwa amebakiza siku mbili tu kuuona mwaka mpya.

    Hatua zianze kuchukuliwa dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivi.

    ReplyDelete
  4. Yeah!! Tanzania kuna amani na utulivu!!

    ReplyDelete
  5. ila itasaidia kupunguza vibaka maana wamezidi unajua wewe hujaibiwa ndio uone uchungu wa kuibiwa.safi sana

    ReplyDelete
  6. Jamani inasikitisha sana kukatisha maisha ya mwenzio, si angeambiwa avirudishe kuliko kumchoma. Tuwe na huruma, mafisadi wanaendelea kufisadika lakini hawachomi moto ila kaka wa watu usikute kaiba vitu vya hela kidogo lakin anachomwa moto.
    Muogopeni mungu, nimesikitishwa sana.
    Rest in peace.

    ReplyDelete
  7. Sasa huyo anayemchoma mwenzie kisa kaiba mali tu anatofauti gani na mchuna ngozi au anayeua albino??????

    ReplyDelete
  8. Watanzania tunajifanya wabaaaabe wakati kuku tu.. waoga balaa..

    ReplyDelete
  9. Pamoja ya kwamba kaiba na kunahasira lakini what right do we have to decide who dies? Mtoto wa mwenzetu huyo?...

    ReplyDelete
  10. ...unajua kila siku tunajivunia amani,lakini matukio ya miaka ya karibuni yanafanya kwa kwelituanze kuangalia upya swala zima la kuwa na amani Tanazania.hivi unafikiri wenzetu wa Burundi,Rwanda walianzaje?kama unakuwa na mkono mwepesi kiasi hiki cha kutoa uhai wakati wowote unapoona inakufaa,je ni nini kitakuzuia kufanya kitu kama hiki pale kundi lako fulani sema la kikabila au la kidini au hata la kiitikadi litakapokwenda kinyume na kundi lingine?tunakokwenda siko jamani,najua wengine watasema..oooh!we hujawahi kuibiwa ndo maana unasema hivyo,lakini kuibi3wa au kutoibiwa TUNAKOKWENDA SIKO JAMaNI kwani inatisha ukatili tunaoonyesha..........

    ReplyDelete
  11. Umasikini ni kitu kibaya

    ReplyDelete
  12. SIJAIPENDA.

    PEOPLE BE SERIOUS, KUKU?? IT DOESN'T MAKE SENSE, REALLY.

    SOMEONE'S LIFE IS MORE THAN KUKU. TUWE WASTAARABU KWA MAISHA YA WENZETU. THIS IS NOT A LAWLESS COUNTRY.

    RIP, THE POOR SOUL!!

    ReplyDelete
  13. Tungeichoma moto nyumba ya Billion moja tungeonekana wamahana Hata katika sura za KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  14. Kwa kweli lawama kubwa ziende kwa polisi wetu. Laiti wangefanya kazi yao sawa sawa basi haya matokeo yasingekuwepo.

    Leo kibaka anapelekwa polisi halafu baada ya masaa machache ameachiwa anakwenda tena mtaani kuiba kwa kujisifu. Ndio maana raia wameamua kuchukua sheria mikononi mwao.

    Mukumbuke kwamba hawa vibaka wanawaibia walalahoi ambao wametumia jasho lao jingi kujitafutia hivo vitu vichache, halafu wao wanaamua kuiba. Ndio maana wakimpata wanaamua kumchoma.

    Sio kwamba natetea vibaka wachomwe moto lakini polisi wajaribu kuzuia matokeo hayo kwa kuwaadhibu ipasavyo hao vibaka.

    ReplyDelete
  15. unapomwibia maskini elewa kwamba piga ua shingo itagawanyika, hapo mastress na machungu yote ya maisha ndio stendi yake

    ReplyDelete
  16. Nami niungane na wadau waliotangulia hapo juu - sawa kijana kaiba na ni tendo la kulaaniwa na kukomeshwa lakini hii kumtoa mwezio roho (rip) kwa kuiba kuku ni unyama wa aina yake kuliko huo wizi wa kuku. KAMA KWELI WABONGO TUNA HASIRA NA TUNACHUKIA WEZI MBONO TUKO TUNAWACHEKEA NA KUWASHANGILIA MAFISADI ambao ndio wanasababisha umaskini unaowatumbukiza vijana katika vitendo vya ukwapuzi. Mbona kesho tutawapa kura ili wandelee kufisadi. Kama tuna akili sawa na hasira basi tuionyeshe angaa kwa kuwanyima kura mafisadi!! bongo bwana inahitaji hadi yesu au mtume arejee tena duniani!!!!
    mlalahoi

    ReplyDelete
  17. bwana eeh wamezidi poa tuu asiefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu hata mbinguni adhabu ni fire

    ReplyDelete
  18. Halafu mwuwaji matamfanya nini?

    NYIE NCHI YENU INA AMANI YA KUIGWA.

    HAYA MZEE WA POLISI JAMII (MWEMA), UNALIONA HILO?

    ReplyDelete
  19. This is not even funny. Mambo ya kuchukulia sheria mkononi kama hivi sio poa kabisa. Piga lakini usiue kihivyo jamani. Tuwe na utu na roho duuh.

    ReplyDelete
  20. kuchukua sheria mkononi mwako ni kosa hata ikiwa umeibiwa mkeo. i hope waliotenda kosa hili watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

    hang on!! nasema nini hapa? haya yametokea tanzania, mnonge myongeni, kijana keshabandikwa title ya kibaka nani atafatilia kesi hii? askari wote wako wanawalinda wezi wa kweli, vigogo wanaoteka mamilioni ya umma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...