gari aina ya Suzuki Vitara lilikiwa limepinduka ndani ya mtaro mkubwa uliopo pembezoni mwa barabara ya Morogoro Road, katika eneo la Kimara bucha.
gari hii ilijikuta ikiingia mtaroni humo mara baada ya kuchomekewa na daladala kuingia upande wa pili wa barabara bila ya ishara yoyoye na kusababisa dereva wa gari hii aina ya vitara kutaka kujaribu kumkwepa na kujikuta katika hali hii.
daladala lenyewe ni hilo hapo ambalo liko chini ya usimamizi wa Askari Polisi ambao kwa bahati nzuri walikuwepo jirani kabisa na eneo lilipotokea tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Keland Nursery & Primary SchoolDecember 04, 2009

    TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA

    ReplyDelete
  2. Dereva wa daladala ana makosa.
    Lakini wa kwanza kukosea ni mmiliki wa hio barabara kwani haikusanifiwa na kujengwa kwa viwango vinavyojali usalama wa watumiaji. Niliishawaeleza wamiliki wa hio barabara kwamba ilikosewa toka mapema miaka ya 2000.
    Hiyo si ajali ya kwanza na ya mwisho.

    ReplyDelete
  3. jamani barabara kama hizo zinatakiwa ziwe na nguzo za pembeni kuzuiya magari kuingia kene mitaro kama hiyo.lazima serikari za mitaa zipitie hapa na kurekebisha hayo,mitaro iko uchi namna hiyo no hatari hata kwa wapita pemebeni jamani au wanaopaki kwa ajali.they need to put some sorts of guards to protect this kind of accident.kuspin out of control aina maaan uingie mtaroni kama hivyo.

    ReplyDelete
  4. michu,
    mimi kaaa yangu yote ulaya sasa zaidi ya miaka 10 sijaona 'high-way' yoyote ktk nchi za ulaya zenye 'mitaro mikubwa ya maji iliyo wazi' pembeni ya barabara.

    labda wadau wa sehemu nyingine za dunia watufahamishe.

    aina hii ya ujenzi huongeza uwezekano ya kupata majeruhi zaidi bila sababu za msingi.

    mdau
    ulayaulaya

    ReplyDelete
  5. Hiyo barabara inajulikana sana kwa ajali si kwa kuchomekewa tu hata full light usiku ni maarufu kwa kusababisha ajali eneo hilo.JAMANI INATISHA

    ReplyDelete
  6. HUYO MKANDARASI LAZIMA ALISOMEA INDIA,HUWEZI KUWEKA MTARO MKUBWA KIASI HICHO PEMBEZONI MWA BARABARA THATS DANGEROUS NOT ONLY FOR DRIVERS BUH ALSO FOR PEDISTRIANS.SUPPOSE SOMEONE IS REALLY DRUNK AND IS WALKING ALONGSIDE THAT DITCH AND HAPPENS THAT HE/SHE FALLS WOULD LIKELY DIE OR SUFFER SOME SEVERE INJURIES.AS FOR THE FORE CONTRIBUTORS HAVE SAID THESE KINDA DITCHES SHOULD HAVE SOME BARRIERS ALL ALONGSIDE TO AVOID THESE UNNECESSARY CASUALITIES.WAPI KODI ZA WANANCHI ZINAENDA??????KUJENGEA NYUMBA ZA MAFEDHULI SIO?OK

    ReplyDelete
  7. Siyo siri attitude na mwenendo wa madereva wa daladala hinifanya nitamani nitembee na kiboko ili kila wakikosea niwacharaze. Wahuni wakubwa hawa!!!AAgh

    ReplyDelete
  8. hii ya leo kali!!mtaru huu ni kabuli tosha kwa madeleva na abiria inatisha hata kuendesha gari

    ReplyDelete
  9. Hapo hao maofisa watapewa mshiko halafu huyo iliyeingia mtaroni ataachwa hapo ajijue.Mmmh aibu tupu!!

    ReplyDelete
  10. Nimeona hiyo picha ya gari abalo limetumbukia kwenye mtaro mkubwa wa kimara na hiyo ndio nilikuwa nasema hawa maijinia wetu ni wa style ipi, kuwa na mitaro mikubwa?
    please Tanzania yetu ni ya sayasi na technology sasa where are we going? na hao wakakuzi wa barabara wanafanya nini? labda wameamua kupunguza watu wa jiji la dar tumekuwa wengi>>..

    ReplyDelete
  11. Madereva wa daladala wanahitaji adhabu kali kwa sababu sioni haraka ya nini na roho mbaya ya kumzuia dereva mwingine ambaye hayuko kwenye ushindani wa biashara huyo dereva anatakiwa kunyang'anywa leseni na adhabu kali.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa Fri Dec 04, 04:05:00 PM na wenzio mnaomlaumu mkandarasi wa barabara hiyo ya Morogoro hasa kuanzia kimara bucha hadi ubungo maji,binafsi namshukuru sana kama kweli alikosea,maana kosa lake limekua faida kwetu.Wengi wanaosema kakosea humjali dereva na abiria wake tu, na sio watembea kwa miguu na wenye makazi jirani na barabara hiyo. Na hawa ni kina sie ambao hata gari gani ipinduke wewe ukiwa service road hudhuriki kabisa, pia hata gari iliyotumbukia hua haiharibiki vibaya ukilinganisha na kama zingeweza kupata fulsa ya kuchagua shamba!Ilishawahi kutokea ajali pale katikati ya Safari Resort na kituo cha mafuta cha Oryx miaka ya tisini yaani Coaster dungu ilining'inia juu ya mwembe na abiria watu walifanya kuwakusanya viungo maana hakuna kilichotoka hai! Kama kuna mtu angebahatika kuishuhudia asingemlaumu mkandarasi wa sasa(Skanpil Colas)ambaye pia katengeneza barabara ya Chalinze Morogoro kipande kilichokua kikitisha kwa ajali. Ni yeye aliyeanzisha njia tatu sehemu yenye mlima na kona kali ili kupunguza ajali eneo hilo.So tuachieni mkandari wetu,kwani kwa sasa kuna matuta ya kutosha na ajali zimepungua sasa kipande cha kimara mwisho hadi ubungo. Ukitaka kujua ni kiasi gani kulikua na ajali sana eneo hilo kahesabu idadi ya taa za barabarani na vizio vyake utapata jibu

    ReplyDelete
  13. Sidhani barabara ilivyo wazi ndivyo design ilivyoelekeza.

    Hela nyingi imeliwa hapo. Bampa za chuma zilihitajika ukingoni mwa barabara kama ilivyo sehemu zenye bonde refu kando ya barabara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...