Raia 10 wa Congo DRC wakisubiri kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wa Sumbawanga baada ya kukamatwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini bila kibali. wanane kati yao walipewa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela bada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi 30,000/- ambapo wawili waliolipa faini hiyo walipewa masaa 72 wawe wamekwisha ondoka nchini wenyewe kwa gharama yao. Picha na mdau Peti Siyame
Home
Unlabelled
wakongo kizimbani kwa kuishi nchini bila kibali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
upumbavu wa hali ya juu, mnafunga watu sababu ya 30,000, mwaka huo wakikaa jela watakula zaidi ya hizo, yani gharama za kuwatunza huko jela, nafikiri kuna haja ya kutowa takwimu za gharama za mfungwa mmoja kwa mwaka, si bora hata wangewarudisha kwao na kudai hizo 30,000 kwa serikali ya congo
ReplyDeleteTrue...I second U @ 11:41. Ni ujinga tu wa kutowaza na kutumia akili. Mwaka na dola 30 wapi na wapi...Kama ni kuwapa watu adhabu kali ili wasiishi nchini kinyume cha sheria basi waweke jela miaka 5 au walipishe hela nyingi. Hiyo 30 si watu watakuja kukaa tu halafu wakishikwa wanalipa mara moja wataondolewa kesho tena watarudi. Kwanza walioshindwa mngewaondoa tu au muwasaidie basi waishi kihalali. kam awameshindwa kutoa hiyo hela ujue hata pa kula walikua hawana.
ReplyDeletemichu nilidhani bado zile picha za sendoff zinaendelea tehe tehe tehe!!!
ReplyDeleteHiyo jela watakapofungwa si ipo Tanzania? Siwatakuwa bado wapo Tanzania? Swali ni kwamba wakiwawanatumikia vifungo vyao huko jela watapewa vibali vya kuishi Tanzania? Kwa sababu hata huko jela bado watakuwa wanaishi Tanzania.
ReplyDeletewanyonge mpaka kiama!!!
ReplyDeleteWatanzania kwa Pesa za Ziki na njaa tunajiaibisha Sasa pesa hiyo si rahisi kulipa? naona tumewapania wa Dr Congo. wekeni Sheria inayotakiwa na muifatilie.
ReplyDeletesasa kama si upumbau kitu gani? yaani faini elfu 30,uku ni kufuga maradhi,pia msako huu kwa nini usiende kwa wanamziki wanajichimbia ktk bendi za mziki,lazima watakuwepo wazaiaji
ReplyDeletewaachieni hao ni waafrika wenzetu wanatafuta riziki,timueni wachina wahindi wasomali na wazungu, kwani wao hawatawakaribisha kwao ni wabaguzi wakubwa.amkeni waafrika,.
ReplyDeleteKwa staili hii hapa USA jela ingepata wafungwa wapya milioni 12 maana hakuna ndege za kutosha kubeba idadi hiyo ya abiria kwa masaa 72 ambayo inachangia asilimia 6 ya uchumi wa nchi.Hata hivyo sijui hatma ya watoto karibu milioni moja waliozaliwa na kundi hilo ambao ni raia wema wa USA.Hayo yote yangefanyika wakati human right activists wamekwenda likizo mbuga za wanyama Arusha.
ReplyDeleteWakati Mh kikwete katika safari zake za kila mwezi USA,akifika hapa anatuambia kaeni vizuri na msisahau kusaidia nyumbani wakati anaelewa kundi kubwa linaishi kinyume cha sheria wakati wanasibiri(LPR)Lawful Permanent Residence.Kunatatizo gani Kabila akitembelea Sumbawanganga akawaambia wakongo kaeni vizuri,msisahau nyumbani?
mi nilkuwa nashauri serikali iwape kibali waishi tu hapo, kwani wanapunguza nini na wao si waafrica tuu?! ukienda ulaya unafukuzwa urudi kwenu huna kibali.. ukienda nchi za africa kama mwafrica mwenzao unafukuzwa, sasa sijui tukumbilie wapi.... jamani tuhurumiane hii yoote ni katika kutafuta maisha
ReplyDeleteFaini ya TShs 30,000/= au Kifungo cha Mwaka 1 jela...ni ujinga kabisa...hivi Tanzania hatuna adhabu za Public Service (Kutumikia Jamii)???
ReplyDeleteHawa watuhumiwa ni bora wangeepewa kazi ya kufagia barabara zetu kwa Wiki 3 kuliko kuwaweka Jela wale na kulala kwa gharama za walipa kodi kwa mwaka mzima.
nimewaonea huruma sana kwani najuwa maisha magumu sana ila hawa wamefikishwa mahakamani kwasababu hawakuwa na kitu kidogo cha kuwapa wazee wa nondo ila kosa hili si wapelekwe wakachunge ng'ombe bunju?
ReplyDeleteHivi mbona kuwanyanyasa ndugu zetu namna hiyo? Ndiyo wamevunja sheria lakini ni hali ya maisha imewafanya waje kuishi nchini. Hao ni binaadamu wanaotakiwa kuwa treated kwa heshima. Kwanza hao maofiza wa uhamiaji wanavyofanya hizo raids ni ukatili mkubwa...kanchi kenyewe Tanzania jamani!!!. Wakongo ni jirani zetu...tena ni kama ndugu kabisa, mpaka Lugha tuna-share. Leo kwao kesho kwetu. Please treat these people with respect and dignity, these are not criminals in the eyes of God. It's upon us the citizens to stand up for our fellow human beings,Africkans, neighbors....who just want a better life for themselves and their families.
ReplyDeleteUpumbavu mtupu. Kuna wa Kiongo wangapi Kigoma? Hawa wote ndugu zetu wangerudishwa kwao tu. Kiasi cha kuwakabidhi kwa balozi wao basi au kuwapa uraia wakae wajenge nchi. Inaonekana Tanzania ni poa kuliko Kongo la sivyo wasingekuja. Na watanzania kibao wako illegally nchi nyingi duniani si wanatafuta maisha? Anyway sheria ni sheria lakini na ubinadamu pia tusiusahau. Ni sawa na mwenye shmba la nazi kumuua mwizi wa nazi kwa mshale na anaanza kujisifia!
ReplyDeleteWaafrika tuwe na hi kitu 'Africanism'
ReplyDeletehebu waachieni wenzenu wacheni kuwaonea, kwani wameingia nchi gani ya mana
ReplyDeletetanzania tusiwe wavivu kufikiri,hao watu wako nchini wakitafuta maisha kutokana na hali ngumu ya maisha kwao,ikiwa wameshindwa kulipa faini ya shiling elfu thelathini watarudi vp kwao baada ya adhabu..tukiishi ulaya bila kibali hatufungwi jela wala hatupigwi faini tunarudishwa kwetu bure..mfungeni chenge aliyeua,mfungeni lowasa aliyeliibia taifa mamillion
ReplyDeleteFor the first time in a long time, I'M VERY PROUD TO BE TANZANIAN....All the comments are so positive. I hope wakuu wa nchi wanapitia hii blog na kusoma maoni haya. Treat these people kindly, tayari wanateseka rohoni kuwa mbali na nyumbani....they are here for a reason.!
ReplyDeleteI Love America!! they treat illegal immigrants so good, and guess what...they benefit from them too. There's a lesson.
Mbona wahamiaji haramu wapo wengi sana, haswa Dar,wewe njoo kampuni moja inaitwa SDVAMI opp na gazeti la mwananchi tabata,utashangaaa hata mpika chai,karani,dereva ni mhamihaji.
ReplyDeleteSidhani kama uhamihaji wanafanya kazi zoa sawasawa.
Mh.Masha vipi?huko kwenye kampeni?