Kampuni ya Bia T anzani (TBL), hivi karibuni iliendesha semina kwa wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, kuhusu mafanikio ya kampuni hiyo tangu ilipobinafsishwa 1994 hadi sasa. Semina hiyo ilifanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo waandishi
walibahatika pia kutembela sehemu mbalimbali za kihistoria, kama picha hizi zinavyoonesha. Msafara huo uliongozwa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Maneno Mbegu.
wakiwa ngome kongwe
wakiwa katika spice tour
Maneno Mbegu akifurahi na wanahabari ndani ya basi.
Mwandishi mkongwe Bw. Salim Salim alipata nafasi ya kutoa lekcha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. BROTHER MITHUPU ACHA UCHIZI TUNATAKA MATOKEO YA SIMBA NA YANGA,MDAU NIPO CANADA

    ReplyDelete
  2. Bunge linatarajiwa kupiga marufuku takrima (khanga, pilau, vitnge, sukari, pesa n.k) kwenye uchaguzi. Bunge liko kimya akini kwenye maeneo mengine kwenye takrima. Uandishi na enezaji wa habari husemekana kuwa muhimili wa nne wa dola. Na hapa tunaona ndugu zetu wa TBL na waandishi wa habari wakitoa na kupokea takrima na kusheherekea kabisa. Utendaji kazi wa waandishi hauathiriki hapa.Hapatakuwa na upendeleo katika kuripoti mambo ya TBL na kuficha mabaya na madhambi(kama yapo)ya TBL? Takrima kama haitakiwi kwa wagombea wa siasa inafaa kwa wengine k.m. waandishi wa habari, vyombo vya dola kama polisi, vyombo vya usimamizi kama TCRA au EWURA n.k? Na tabia ya takrima kwa wafanyakazi ipo sana na kwa muda mrefu. Tunasemaje wanablogu ya jamii?

    ReplyDelete
  3. mbaya zaidi wamegeuzwa matangazo kwa kuvikwa fulana za tbl.

    ReplyDelete
  4. Je pamoja na tripu ya Zenji, naona ktk picha ya kwanza ka vile na makubazi ya wanaocheza twaarabu yamefanana, je mlipewa pia makubazi buree?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...