Emelda Mwamaga
Intavyuu na mkurugenzi wa jarida la Bang!
Emelda mwamanga.


SWALI: Tueleze kwa ufupi safari ya maisha yako?

EMELDA: Mimi nimezaliwa katika familia ya mabinti wawili mimi nikiwa mtoto wa kwanza na mdogo wangu anayenifuatia anaitwa Ritha.

Nimezaliwa miaka 31 iliyopita,nimesoma shule ya oysterbay primary school mama yangu alikuwa mwalimu hapo,baba yangu alikuwa marketing manager kwenye textile company,baadaye kukaja kuwa na ubinafsishaji baadaye akaja kukinunua hicho kiwanda kwa sasa kinajihusisha na magunia.

Nilivyomaliza primary school nikaenda jangwani secondary school nikafaulu vizuri nikiwa jngwani hapo ndipo nilipoanza kuwa na ndoto mbali mbali,ndoto ya kwanza nilikuwa natamani sana kuwa msichana lakini mjasiriamali kama baba yangu.

Pia nilikuwa natamani sana kuwa kama oprah winfrey kwa sababu oprah alikuwa ana magazeti yake pamoja na TV talk show ambayo ilikuwa inanivutia sana ila zote hizo zilikuwa ni ndoto sikufikiria jinsi ya kufika hapo lakini ni vitu ambavyo vilikuwa vinanifurahisha,nikatoka hapo nikaenda shabaan Robert nilichukwa masomo ya HGL baada ya kumaliza nikafaulu vizuri na baada ya hapo wazazi wangu wakanipeleka South Africa chuo cha UCT University of capetown ambapo nilihitimu mwaka 2002 december.

Mwaka 2003 nikarudi Tanzania, nilitafuta kazi sehemu mbali mbali ikiwemo na marekani lakini nikaona kwamba nikienda nje ya nchi je nitaweza kutimiza malengo yangu niliyo nayo,nikaamua kubaki nchini nikabahatika kupata kazi Coca cola baada ya kufanya kazi Coca cola miaka miwili nikafungua kampuni yangu nikiwa na wenzangu wawili waliokuwa wananisaidia upande wa graphics ilikuwa inaitwa Rell...

pata intavyuu nzima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hi Emelda

    Hatujapata Magazine since october what happening ??? hata x-mas hola au ndio ndoa

    ReplyDelete
  2. ni kumbukumbu zangu sio nzuri au yeye anatupiga changa la macho kuhusu shule alizo piata,


    mimi nilisoma jangwani miaka hiyo, sikumuona binti huyo hapo.
    pia nilisoma Tambaza, hapo tulisoma nae , tena kama sikosei alisoma masomo ya science. sasa mbona anasema vingine.

    ReplyDelete
  3. anony Mon Jan 18, 01:57:00 PM, unatia huruma kwa kuchoshwa na vijimambo. yaani wewe wanafunzi wote waliosoma jangwani ulikuwa unawafahamu? ungesema umepitia kitabu chenye majina ya wanafunzi waliopitia shule hiyo miaka aliyoitaja, ningekuelewa zaidi.

    ReplyDelete
  4. Mtu unatamani kuwa msichana wakati ni msichana tayari. Hii imekaa vibaya.

    ReplyDelete
  5. Wewe unayesema Emelda alisoma Tambaza umechanganya na Rita.Adanganye elimu yake ili iweje?

    ReplyDelete
  6. Kwa nini ana Kiswahili kibovu?

    ReplyDelete
  7. Aliyesoma Tambaza ni mdogo wake Rita
    sio yeye na wanafanana sijui siku hizi baada ya kukua watakua wanatofautiana
    Mdau bongo forever

    ReplyDelete
  8. Hata kama kaolewa potelea mbali, namtafuta huyu kimwana wa kinyakyusa.
    Smile lake limenisuuza moyo!!!!

    ReplyDelete
  9. we annony Mon Jan 18, 01:57:00 PM

    mimi nimesoma jangwani kuanzia mwaka 1992 form 1p na tuliingia na kina emelda wao walikua form 1r au s michepuo tofauti na cookery na nidowork,form 3 yeye alikua p na 4p na kina ruth mbwanji dr.sasa serikalini

    alipenda sana social tukifanya concert alikua akipeform nyimbo za kimarekani yeye na kina mirengenyi nyakilanganyi(aka mire yuko usa)yuko sahihi na huwa hajisikii hata kidogo mpaka kesho maana alikua na stutus sana jangwani na alikua anapenda kusoma novels.enzi za akina mama mkamati

    hongera sana emelda ,hope you will fullfill your careers


    mdau wa jasesco

    ReplyDelete
  10. NANI KAMUO EMELDA KIMYAKIMYA HIVYO?

    MDAU PATRIC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...