Ankal na Wadau,
Mchekini Haruna Moshi 'Boban' akila tizi akiwa na vlub yake mpya ya GEFLE IF ya Sweden. picha hii nimeitoa kwenye web yao pamoja na haya maneno ambayo hata maana yale sijui. Nilijaribu kusoma sasa hv nina majeraha ya ulimi. Boban alianza tizi nusu saa tu baada ya kutua Stokholm. Jamaa hawataki mchezo ni kazi kwa kwenda mbele
" Haruna ”Boban” Moshi från Tanzania är tillbaka i Gävle. Han anlände vid tvåtiden i går eftermiddag och bara en halvtimme senare deltog han i GIF:s träning på Strömvallen."
Mdau Fred

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. TAFSIRI:
    Haruna ' Boban' Moshi kutoka Tanzania amerejea tena Gavle. Aliwasili majira ya saa nane jana alasiri. Nusu saa baadae alishiriki mazoezi ya GIF kwenye kiwanja cha Stromvallen. ( Stromvallen ni bonde la mkondo wa umeme).

    Haya wadau, miye Mtanzania mwenzenu, kama kuna kibarua cha kutafsiri Kiswidi, Kidenishi na Kinorway tupigiane debe kama wafanyavyo wenzetu!
    Maggid

    ReplyDelete
  2. Boban kama mdogo wetu na mtanzania mwenzetu tunakutakia kila laheri ktk safari yako ya kuing'arisha bendera ya taifa lako.Angalizo: NIDHAMU MDOGO WANGU...NIDHAMU MDOGO WANGU

    ReplyDelete
  3. Nimeitranslate kwenye google na inasema hivi "Haruna" Boban "Moshi wa Tanzania ni nyuma Gävle. Yeye waliowasili o'clock mbili jana mchana, na nusu saa tu baadaye, yeye walishiriki katika GIF's Workout saa Strömvallen."

    Haya Kilimanjaro, majeshi hayo yanazidi kuongezeka kutoka bongo, lakini mtakiona chenu summer hii, ile fluki ya mwaka jana mtaiota tu mwaka huu.

    Mdau FC Bongo
    Helsinki

    ReplyDelete
  4. Kwa mujibu wa Google Translator, maana ya hayo maneno ni:

    "Haruna" Boban "Moshi of Tanzania is back in Gävle. He arrived at two o'clock yesterday afternoon, and only half an hour later, he participated in the GIF's workout at Strömvallen."

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    www.scholarshipnetwork.ning.com

    San Diego, CA

    ReplyDelete
  5. Mbona yuko pekeyake?Imekaa kama ile picha ya Kajumulo miaka ya nyuma.

    ReplyDelete
  6. Ankal Michuxi tafsiri ya kile Kisweish ni hii: " Haruna ”Boban” Moshi from Tanzania is back in Gävle. He arrived the wide two time yesterday afternoon and only a half-hour latter participated he in GIF: s training on Strömvallen.
    Nimeipata toka http://www.stars21.com/translator/swedish_to_english.html
    Siku mambo yote mtandaoni hata ukitaka kupika ugali na choroko we nenda google tu... Mdau, IC Remmy, Maynooth, Dublin, Ireland.

    ReplyDelete
  7. KWA KIINGEEREZA ANAMAANISHA Haruna "Boban" Moshi of Tanzania is back in Gävle. He arrived at two o'clock yesterday afternoon, and only half an hour later, he participated in the GIF's workout at Strömvallen.

    ReplyDelete
  8. Tafsiri yake:
    "Haruna" Boban "Moshi of Tanzania is back in Gävle. He arrived at two o'clock yesterday afternoon, and only half an hour later, he participated in the GIF's workout at Strömvallen."

    ReplyDelete
  9. Tafsiri yake ni

    despite wenye roho mbaya na wasiopenda maendeleo wengi wao wakiwepo Tanzania kutaka kumbania Boban asifike sweden lakini alifika jana mchana na baada ya nusu saa alijiunga mazoezini.

    mdau

    ReplyDelete
  10. Hili Changa ,mbona yuko peke yake?picha za Nizar Halfani zilikuwa za mechi kabisa,ndo tunataka hizo.

    ReplyDelete
  11. sawa sawa wana kijiji naona mnajitaidi kutasfiri kisvenskaaa.ookiiii senkyu

    mdau boxi 4 laifu

    ReplyDelete
  12. Kaza buti kijana, MAXIMO alie tu eti anasema we si mchezaji, MAXIMO arudi kwao akafundishe Mamiss wa Brazil hatumtaki kabisa hakufanya lolote, zaidi ya blabla tu kila siku hakosi sababu, tumemstukia

    ReplyDelete
  13. aachane na jina Boban!!

    ReplyDelete
  14. Mimi sielewi kwanini kapachikwa jina Boban,si atumie jina lake ili afagiliwe kihivyo?Wenzetu wanajivunia majina yao,huyakuza na kuyaimarisha halafu sisi twajibandikia kama vile kuonea haya majina tuliyopewa na wazazi wetu!!Wewe kaka jitangaze kwa jina lako halisi sisi tutakusifia kwa kipaji chako si cha Boban mslavo!!

    ReplyDelete
  15. Annete Cristiano Ronaldo mbona anatumia "Ronaldo" akiwa amepewa aka na dingi yake kwa ushabiki wa mcheza filamu Ronald Reagan na yeye analitumia tu bila shida?Kuna mchezaji wa Ghana alikua anaitwa Abedi Ayew maarufu kama Abedi Pele aliitwa Pele na ikawa shwari tu?A Ivory Coast wana mchezaji wao anaitwa Gervais Yao Kouassi lakini anatambulika kama "Gervinho" na kila mtu? So Haruna Moshi Boban kama kawa, au vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...