Ankal pole na kazi za kulijenga Taifa letu

Kwanza napenda nikushukuru mwenyewe kwa kazi nzuri ya kutuletea habari za nyumbani na kwingineko.

Juzi nimeona kwenye blog yako clip moja au mbili zilizorushwa na TBS kutoka kwa Mr Jerry Muro kuhusuiana na askari wa barabarani ( traffic)
wa check point kua wanakula rushwa.

Ukiangalia vizuri zile clip hakuna rushwa ilitolewa pale ni fikra tu za huyo mwandishi na wengine . Lakini ukweli ni kwamba akiambiwa atoe vithibitisho nadhani hatakua na ushahidi na kama hana ushahidi unaothibitisha anapokea hela kazi yake HAPO INA KASORO / DOSARI.

Pili sina uhakika kama kazi za Police traffic anazijua sawa, maana ukimsimamisha dereva lazima uulize leseni ya udereva na uombe kadi ya gari, na ndicho kilifanyika pale kama utaangalia vema .
Walisimamishwa wakasimama na kutoa karatasi “Kadi ya gari” na wengine leseni ya udereva sikuona pesa pale. Sawa amehisi ni rushwa Je, kabla hajakimbilia kwenye luninga kutaka sifa alifanya upelelezi wa kutosha akajua chanzo cha hayo yote ni nini na kama kweli wale madereva walidaiwa hongo?

Ningefurahi saana kama angefanya hizo harakati zake uwanja wa ndege DIA, Bandari ya Dares-salaam, n.k . Mimi naona amezidi kuwaonea hawa police kila wakati wanakula rushwa, wanakula rushwa .
Ningefurahi kama angesema wanasababisha usumbufu wa geti mara kwa mara hapo ningeelewa lakini sio kuwalaumu hawa Askari wadogo kua wamekula rushwa na kukimbilia kwenye vyombo vya habari. Ninaomba uiwakilishe hii kwenye blog yako na watu wachangie Ili kutafuta dawa ya kudumu ili mambo kama haya yasitokee tena, Kwa kumalizia ninafikiri Bwana Muro anapaswa kuwaomba msamaha hao askari kwa kuwadhalilisha namna Ile.

Kwa leo naomba niishie hapa na ninatanguliza shukrani zangu za dhati ni mimi mdau wako mkuu.
Mdau Tokyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. I AGREE, NA KAMA KWELI JESHI LA POLISI LITAKUWA LIMEWACHUKULIA HATUA KWA PICHA TU BILA USHAHIDI WA PESA BASI WATAKUWA WAMEWAONEA HAO POLISI.

    SISI MADEREVA MARA NYINGI HUWA TUNAOMBWA KUTOKA LESENI ZETU. NI VITU VIDOGO SANA KWENYE CAMERA YAWEZA KUONEKANA KAMA PESA.

    HATUWATETEI POLISI LAKINI NCHI HII MLA RUSHWA NI POLISI PEKEE. VITU VIDOGO VIDOGO AMBAVYO HAVINA MAANA SANA TUNAVIPRESENT KWA MBWEMBWEEE!!

    BORING.

    ReplyDelete
  2. Napenda kumpongeza mdau wa Tokyo kuwa ameona kama nilivyoona mimi. Nilichokiona mimi ni askari ameomba hati anazostahili kuziomba na akapewa na baada ya kuzikagua akawaruhusu madereva kuendelea na safari. Kwanza tujiulize, dereva akisimamishwa tu na askari akiambiwa atoe kadi ya gari na leseni basi anatoa na pesa kumpa? Anampa za nini? Kabeba mali gani ambayo hataki askari aione? Au gari lake lina ubovu gani ambao yeye anaujua na kukimbilia kumpa askari pesa? Kabla hatujashikilia bango kwamba askari wanataka rushwa tuangalie wanapewa ili iweje? Kuna madhambi gani yanafanyika ambayo askari wanatakiwa wayafumbie macho? Dereva atatoa tu pesa bila ya sababu yoyote? Hapo nadhani ufanyike uchunguzi wa kina kuna siri gani kubwa ya kutoa fedha? Baadhi ya wafanya biashara walisema wakipakia viazi wanatozwa rushwa. Kweli inaingia akilini mwa mtu kuwa umepakia viazi ndani ya gari unasimamishwa na askari unaambiwa toa rushwa? Au umezidisha uzito? Au umepakia na vitu vingine?

    ReplyDelete
  3. hoja yako nimeifeel mdau, nakuunga mkono, zote ni sifa tu hamna lolote, unaambiwa ukitaka kukata mti usiote tena ondoa mzizi wake, ukiukatia juu utaota tena....

    ReplyDelete
  4. Wewe uliyetuma huu waraka hauna hoja ya msingi, au na wewe ni mmoja wao kati ya watu walioshutumiwa kula rushwa??? Acha kuwatetea polisi wamezidi kutunyanyasa wananchi. Inaonekana hauishi nchini ndiyo maana haujakumbana na haya machungu, juzi tu ndugu yangu kakamatwa anaambiwa gari inamakosa 4 polisi anadai 80,000/= baadae anasema ahaa tuelewane leta 30,000/= uende zako. Jamani kwa hali hii tutafika.

    Tusitetee ujinga bwana.

    Asanteni.

    Kanyomozi hapa.

    ReplyDelete
  5. ASKARI WA USALAMA BARABARANI = TRAFFIC? SI KWELI TRAFFIC NI AUTOMOBILE = GARI= CAR MAYBE YOU COULD SAY TRAFFIC POLICE!!1

    ReplyDelete
  6. stop doubting the obvious. kwani unadhani rushwa dereva atatoa wazi wazi akiipeperusha noti ya elfu kumi wakati anampatia askari? rushwa haitolewi kama ilivyo wakati ukienda kumtunza msheza dansi au mwimbaji wa taarabu. pesa inafichwa katika upande wa pili wa kadi ya gari, ili ku'obstruct any observer's view. mara nyingine askari anatoa faili akishikilia kuzuia view ya watazamaji, wakati huo huo dereva anapitisha noti upande wa pili.... stop critisizing just for the sake of

    ReplyDelete
  7. mdau pole sana nafikiri una matatizo ya kisaikolojia na nafikiri aujawahi kutumia usafiri wa anga kuanzai 2001 na aujafika bandarini siku nyingi sana naomba nikuambie kwamba pale JKNIA airport, km zilivyo airport zingine duniani kuogopa ugaidi kuna kamera kila kona kiasi kwamba kila kitu kinachofanyika kinaonekana sema atujui ni namna gani tunaibiwa mizigo yetu hila pale kamera zipo na bandarini kwa muandishi wa habari kwenda ni lazima ukaguliwe na ni kwa shughuli maalumu ndio unaweza kwenda pale sio km swala alilolifanya jerry kwa traffic, kwa level yake ya uandishi amejitaidi na sio traffic tu ameweza kufichua mzungu aliyekuwa ana kibali cha kuishi bagamoyo na uhamiaji wamemrudisha kwao mzungu huyo so rushwa za wakubwa siku hizi kukamata ni ngumu sana maana wako makini sana
    pia mi nakuomba umpongeze tu hata jamaa yako ni traffic mla rushwa amekamatwa khari tanzania inatisha sas kwa rushwa njoo uone km autarudi huko tokyo

    ReplyDelete
  8. Mdau upo sahihi upande mmoja na wakosea upande mwingine. Ila nikifanya majumuisho ya habari yako ni kwamba kama hawa askari wakiadhidiwa basi kwao ni kama uonevu maana wakubwa zao wanafanya hivyohivyo. Na kama hawajawahi kuhusika kupokea rushwa ya hela basi wamefanikisha ajira wa watu fulani kiupendeleo na hiyo ni aina ya rushwa pia. Huko kwenye bandari na uwanja wa ndege sisemei maana kunaeleweka.
    Kumalizia naomba ujiendeleze kwenye fani ya uwakili maana unajitahidi sana katika kipengele cha kutengeneza defensi!

    ReplyDelete
  9. HIVI MNAFIKIRI KWANINI TAKUKURU WAKITEGA MTU WANATOA HELA ZAO WALIZOREKODI NAMBA??SABABU NI USHAHIDI,MAANA YAKE HATA UKIMSHIKA MTU NA HELA UWEZE KUTHIBITISHA NI ZA RUSHWA,HUYU MWANDISHI AMEFANYAKAZI NZURI,LAKINI KAMA WALE ASKARI WAKIJITETEA ANAWEZA KUTHIBITISHA KUWA WALIZOPOKEA NI HELA?TENA HELA ZA RUSHWA??KESI NYINGI TZ WATUHUMIWA WANASHINDA KWA SABABU YA KUKURUPUKA BILA GATHERING EXTENSIVE EVIDENCE,HUYU MWANDISHI ANA KAZI KUBWA YA KUTHIBITISHA,NACHUKIA RUSHWA NA NAWACHUKIA POLISI WALA RUSHWA...NA KUHUSU BAHASHA HATA MIMI POLISI AKINISIMAMISHA NAMPA BAHASHA YENYE CERTIFIED(BY LAWYER)COPY OF ALL DOCUMENTS ZA GARI(je utasema nimempa hela kwenye bahasha) AKASOME KWENYE GARI YAKE AKIRIDHIKA ANARUDISHA NA HAPATI KITU SABABU NI FULL COVERED LEGALLY TO BE ON THE ROAD,MALORI NA MAGARI MENGI TZ NI DODGY NDIO MAANA UKIPEWA MAKOSA YAKO FAINI ZINAFIKA HATA 120,000 NDIO MAANA UNAAMUA KUTOA 30,000 BILA KUOMBWA,KAMA HUNA KOSA HUNA CONFIDENCE YA KU PLEAD INNOCENCE YAKO??UNAKUBALI KUTOA 20-30000 BILA KOSA???POLISI WANAKULA RUSHWA NA WANANCHI NDIO WATOA RUSHWA,TWO WAY PROCESS,WOTE MNA MAKOSA

    ReplyDelete
  10. Askari wa Bongo wanapokea rushwa kama maji,Ila si askari tuu,kila sehemu watu nwanajaribu kukinga tuu, hivi ujiulize mtu anapokea shillingi laki tano kwa mwezi na ana nyumba gari na anakunywa bia kila siku na hana biashara ya aina yoyote,wanatoa wapi hizo hela,Kima cha chini bongo i think ni laki mbili, kila kitu expensive ni rushwa tuu.

    ReplyDelete
  11. Ni kweli picha zile azitoi uthibitisho wa moja kwa moja kuwa ni rushwa. hivyo ni lazima vyombo husika viwe na tahadhali sana kabla ya kufikilia kuchukua hatua!!

    ReplyDelete
  12. mimi ninamawazo tofauti kidogo,nimeangalia picha na pia kusoma maeleo ya wenzangu,naona karibu wote mpo sawa.ila wewe unaejiita mdau wa tokyo(sehemu gani,nina wasiwasi na wewe,kwani kwa japan,hakuna staili ya kuombwa leseni na trafiki kuchukua hadi kwenye gari yao),nahisi unaonyesha ujiko tu.kwa japan trafiki ni wakali kuliko maelezo.pengine ungeunga mkono wa bongo nao wawe wakali namna hiyo,je ni wabongo wangapi wameshakamatwa huko kwa makosa ya barabarani,asilimia kubwa wana au mnaendesha bila kuwa na leseni,polisi akisimamisha mnatoka mbio),kuhusu hao matrafiki,inawezekana pia kuwa ni kweli walikuwa wanachukua vitu vinavyowahusu,yaani leseni na kadi ya gari.je hawawezi kupokea na kusoma na kuhakikisha bila kuleta mafinyango finyango ? nani asiejua huwa wanaweka hata kwenye kofia zao.ninapatwa na wasiwasi kuwa wewe ni mmoja kati ya matrafiki au polisi unajaribu kutetea.je unajua kuwa wamekithiri kwa RUSHWA hapa bongo?je umeshawahi kupanda basi likasimamishwa na trafiki likiwa na makosa halafu halikuendelea na safari hadi likalipiwa faini kamili? kuna trafiki yeyote unayemjua asiye na kitambi,au mjengo(hususani hao wa kwenye so called highways)? embu lete habari,wapi kwa tokyo unaweza kuendesha gari ukakosa kuona kama sio alama za kuonyesha uende kwa spidi gani,au trafiki lights na mambo kama hayo!? je unajua kuwa camera za barabarani huko tokyo zinasaidia kuondosha mambo mengi ya barabarani? la mwisho, kweli hujui kuwa trafiki wanakula rushwa wewe shenzi taipu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...