wachezaji wa ivory coast baada ya dina la mchana
kila mtu alikuwa anahamu na drogba
nyota wengine wa ivory coast
baadhi ya wachezaji wa taifa stars. toka shoto ni nizar khalfani, nsajiwa na mrisho ngasa
Kocha wa timu ya Ivory Coast, VahidHalihodzic akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa stars utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa leo




Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba akitoka kupata dina la mchana Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar ambako timu hiyo imefikia. Wacheaji wote isipokuwa mmoja tu, wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi yao. Leo wameanza tizi neshno na kesho watakipiga na Taifa Stars. Leo askari walikuwa na adabu na kila mtu kafanya kazi yake bila zogo linalosababishwa na kutaka sifa kusiko msingi kwa badhi ya hawa askari wetu ambao wanapenda kutumia nguvu nyiiiingi na maarifa kiduchu..
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na Arsenal Emmanuel Eboue akisaini katika fulanazzz ya mtoto aliyefika kwenye Hoteli ya kilimanjaro Kempiski kuwaona wachezaji hao
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast kushoto Yaya Toure na kulia Bajari Kone.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. VICTOR KILEOJanuary 04, 2010

    HAWA SIZANI KAMA WANAWEZA KUWAFUNGA TP MAZEMBE YA ZAIRE KWENYE FUNGUA DIMBA LA KIKOMBE CHA DUNIA, WANAONYEKANYA NI WADOGO WADOGO KIMAHUMBILE YAO. MAZAIRE YANAMISULI MIKUBWA KULIKO KINA DIDIER GLOBURA. LAKINI TUOMBE MUNGU BURUNDI WASISONGE MBELE WACHEZAJI WAO WAREFU SANA.

    ReplyDelete
  2. Kaka umekosea, huyo kando ya Yaya Toure ni Gervinho na sio Baky Toure!

    ReplyDelete
  3. bwana michuzi c vibaya tukakosoana labda mimi ndio mshamba,hivi dina ikiwa mchana na lunch itakuwa???

    ReplyDelete
  4. ALHAJ ABUBAKARYJanuary 04, 2010

    DUH YAANI WACHEZAJI WOTE WANACHEZA NJE YA NCHI YAO KASORO MMOJA TU HEE!!!!!!!!!!! LAKINI TUSIOGOPE MBONA CAMEROON WAKO HIVYO HIVYO NA TULITOKA NAO SARE? STAR MSIWAOGOPE HAO TUTAWAFUNGA TUU MSIOGOPE ULAYA HATA WABONGO KIBAO WAKO ULAYA JE WANGEKUWA WACHEZA SOKA? SI NA SISI TUNGEKUWA NA DROGBA WETU?

    ReplyDelete
  5. haya bwana watakaaa bongo for how long??

    ReplyDelete
  6. Aloo micuzi tumwagie linki basi ya kuangalia hilo game online. Na watahadharishe hao washabiki wa manu wasije kumpiga kipapai drogba wetu.


    Mdau True Blue
    helsinki

    ReplyDelete
  7. Michuzi Please sana Tunaomba utuwekee link ya kuona mpambano wa shoka ambao karibu Dunia nzima wanataka kuiona Tanzania inafanya nini katika ulimwengu wa soka!!! Pls MICHUZI Tunaomba kuiona hiyo mechi kati ya stars na Ivory cost!!!

    Mdau North america!

    ReplyDelete
  8. mbona autograph wanapewa watoto wa kihindi tu? au baba zao ndio wadhamini?

    ReplyDelete
  9. Anon wa hapo juu autograph wanapewa watoto wa kihindi kwa sababau wazazi wao ndio wenye uwezo wa kutia mguu Kempisk, hakuna mlalahoi anaweza kukanyaga pale

    ReplyDelete
  10. Dinner ya mchana is fun as it is-Contradiction ndio joke iliyokuwapo hapo.
    Ni kama poor english ama kutoelewa maana. So hakuna cha kusahihisha kwakuwa imekuwa fun and we like it
    Its like "barabara ya Morogoro Road"
    Some like that
    Just for fun

    ReplyDelete
  11. Aliyeko kulia mwa Yaya (mwenye rasta) sio Bakari Kone ni Gervinho

    ReplyDelete
  12. msijali wadau mlioomba kuona libeneke la ivory coast na taifa stars mtaliona tuu laivu bila zengwe mskonde nitamuhimiza husband wangu michuzi kipenzi chenu awawekee nikimwambia kitu huwa hapindui kamwe
    mrs michuzi orijino

    ReplyDelete
  13. We Professor hapo juu! hatukuja kukosoana na kuonyeshana ujuaji humu! Ile enzi ya wabongo kujifanya machinoo imeshaisha na kazi kubwa imefanywa na hii blog ya jamii!! KWA UFUPI tuna lugha zetu humu wenyewe watoto wa PAN. Kama umevamia mji haya bwana!! Hiyo ni misemo tu baba; kama
    barabara ya Morogoro Road,
    My Wifey wake,
    Dinner la mchana na vitu kama hivyo!!
    Hivi huji Michuzi anafanya gazeti gani?? Sio magazeti ya Sukununu, Jua kali, sijui machweo na vitu kama hivyo YUPO TANZANIA DAILY NEWS LTD! Yeye huwa nafurahisha watu na ndio maana blog imekuwa maarufu watu tukisha beba boksi tunataka tucheke walau stress zipungue kama wewe mtu wa kukunja ndita nenda kamtafute MJENGWAAAAAAA!!

    ReplyDelete
  14. BWANA MICHUZI SANTE KWA HABARI ZA KILA KONA YA DUNIA, ILA MCHANGO NI MUHIMU BWANA MICHUZI DINNER NI CHAKULA CHA MCHANA TU NA HAKUNA DINNER LA ASUBUHI WALA USIKU.

    ReplyDelete
  15. HE MBONA WANAONEKANA WAKUBWA KULIKO SISI EMBU WATAZAME WACHEZAJI WA BONGO NA HAWA HAWALINGANI,INGEKUWA MECHI YA KUWANIA KOMBE KWA KWELI TUNGEOMBA KUGOMA MAANA SIO HAKI AKUUUU

    ReplyDelete
  16. sipendi kuandika kuhusu lugha ya kiingereza lakini samtaim inabidi.

    Chakula cha wakati wowote waingereza wenyewe wanakiita dinner, na wala siyo cha usiku peke yake. (Najua kama mwalimu asumani alikufundisha darasa la nne kwamba mchana-lunch; usiku dinner)

    Dinning table ni meza ya chakula na wala siyo meza ya chakula cha usiku.

    Dinner ladies ni wanawake wanaopika na kugawa chakula kwenye canteens; ingawa siyo chakula cha usiku.

    mdau, Amigo

    ReplyDelete
  17. Jamani wadau nmaofikiri kuwa Michuzi kakosea, hajakosea, bali hii ni STYLE yake ya kuandika kwenye hii blog ya jamii katika kutia chachu na kuweka utofauti kidogo. Na si kama kakosea, so msijisumbue kumsahihisha maana hii ndo style yake.

    ReplyDelete
  18. VICTOR KILEOJanuary 04, 2010

    MICHUZI NI BINADAMU KAMA SISI KAKOSEA KUANDIKA DINNER LA MUCHANA ANGEHANDIKA DINNER LA USIKU. DINNER SIKU ZOTE HUWAGA NI MAUSIKU USIKU HAKUNA MA DINNER MUCHANA TANZANIA LABUDA KAMA ANAHONGELEA DINNER YA FUTALI SAA KUMI NA UNUSU SAA ZA JIONI JIONI. MIMI NIMEUZULIA MA DINNER MENGI YA BABA YANGU YOTE YANAKUWA MAUSIKU TU SIYO MUCHANA WALA JIONI.IM REMEMBERED THEN EVERY MUCH

    ReplyDelete
  19. Kwa wasiofahamu Dinner.
    Michuzi hajakosea

    By defn:
    Dinner is the name of the main meal of the day. Depending upon region and/or social class, it may be the second or third meal of the day.Originally, it referred to the first meal of the day, eaten about noon, and is still occasionally used in this fashion if it refers to a large or main meal.
    -In some usages, the term dinner has continued to refer to the largest meal of the day, even when this meal is eaten at the end of the day

    By Master deeky
    http://masterdeeky.blogspot.com

    ReplyDelete
  20. Nikugaambilege Iwe Bagambaakabo bwana...! utawajua tuu...., yaani katika vitu vyote vya msingi, mtu anakuja na argument ya dinner la mchana, eti michuzi kakosea.

    Michuzi hajakosea wala nini, sana sana umeonyesha udhaifu wako wa kutokujua mambo lakini kuyjifanya unayajua.

    Nipo hapa napata dinner langu la imitondo.

    San francisco, bay area.

    ReplyDelete
  21. Mbona hiyo "dinner ya mchana" imekaa sawa tu. Ule msosi wa usiku unaitwa "Lunch ya jioni".

    Mdau Nederlands!

    ReplyDelete
  22. Of course ni wakubwa kuliko wachezaji wetu! Wachezaji etu wako 30yrs old labda jamaa wanagonga 40 ila ukiwaona katika timu zetu za Ulaya unaona miaka yao eti 22 mara 25. Wapiiii Vijeba tu vimechomekea!

    ReplyDelete
  23. Hi kumbe hawa wachezaji wanavyokuja Africa wanakua kama watu wachezaji wetu tu,wachafuuu hata hawang'ari lakini wanapokua kwenye luninga-AAAAMA KWELI-ULAYA,ULAYA TU,Hebu angalia hiyo miguu ya Toure kama ndio kwanza anacheza mtibwa,Kweli mipopo mipopo tu hata iwe vipi.Nuramo

    ReplyDelete
  24. huyo pembeni ya yaya na g siyo JOTI kweli!?

    ReplyDelete
  25. wewe anoy 05:11:00 wa hapo juu, unaonekana hujakuwa kifikra, hao wachezaji niwatu kama watu wengine, kung`ara au wasing`are hiyo sio point, point niuwezo wa mchezaji anapokuwa uwanjani tu. kwani hakuna wazungu waliopauka? acha ubwege wewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...