Benki ya NMB ilileta burudani ya aina yake
promo za wafadhili kwa kwenda mbele
vuvuzella ndani ya nyumba
Tajania oyeeee!

Kocha wa makipa Juma Pondamali akiwa kazini
Ivory coast wakipiga jalamba
Marcio Maximo na vijana wake
Nahodha wa Taifa Stars Nsajigwa akibadilishana bendera na nahodha mwenzie Didier Drogba wa Ivory Coast
Shilingi inarushwa kuchagua upande wa kuanzia
waamuzi na manahodha na wasimamizi katika taswira ya pamoja ya kumbukumbu
Ivory Coast
Taifa Stars
Juu na chini ni mlinzi wa Taifa Stars Nadir Haroub 'Canavaro' akimdhibiti Didier Drogba wa Ivory Coast wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita. Ivory Coast walishinda kwa bao lile lile moja lilofungwa na Drogba dakika ya 39. Hata hivyo Taifa Stars, iliyokuwa ikishangiliwa kwa nguvu na mamia ya washabiki wakiongozwa na JK aliyekuwapo uwanjani, wanastahili kila aina ya sifa kwa kuweza kuwamudu Ivory Coast. Canavaro alimzima kabisa Drogba sema walijipanga vibaya wakati Emerse Fae alipochoropoka na kuporomosha majalo
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Kila la heri Cannavaro naona sasa utaenda hata U.K maana kiwango chako si cha kucheza Canada....Hongera Stars.

    ReplyDelete
  2. si mbaya inatia moyo.Taratibu ndio mwendo.tutafika tu.
    Wadau kwa yeyote mwenye linki ya video ya gemu tunaomba atutupie hapa

    ReplyDelete
  3. ndo tatizo la soka ya bongo.tukifungwa kiduchu na timu zenye viwango bado tutajicfia.si mpaka tupigwe goli 30 ndo tujue sisi mdebwedo.

    ReplyDelete
  4. Kwa shida kivipi mbona sikuelewe Ankal michu?
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete
  5. Dah wabeba Box wametufunga. ila tumejitahidi mie msimamo wangu upo palepale Maximo njeeeeeeee. Si kwasababu tumefungwa sababu hafai. Kimaro. Huyu Canavaro na Ngassa na Tegete wanafaa kucheza nje Ubeligiji au wakadoee Ufaransa nafasi. Badae huwezi juwa.

    ReplyDelete
  6. dah huyu canavaro anacheza kilimanjaro stars au?AMKA MAXIMO VIPAJI VIPO ZENJI HUKOOOOO...

    ReplyDelete
  7. Hebu tumieni akili nyinyi,mnafikiri hao kina drogba watacheza kujiumiza na vitim venu?wenzenu wanahofia tim zao na game zao,hiyo wamecheza kupasha tu na ndio maana ukicheki game hata tulocheza na Cameroon Eto alikua anaogopa sana hata kushika mpira,we canavaro anaweza kumzuia Drogbaa?hakuna hata mmoja anaweza kufanya hilo si duniani wala ahera!!!!hata hivyo hongera canavaro si unakumbuka nilikusomesha chuo,pale jumba namba tatu?

    ReplyDelete
  8. Nilishawaambia Taifa Stars wasifungwe kwenye ardhi yetu...kwa nini hawanisikii vijana hawa !??

    ReplyDelete
  9. YOTE HAYA KWA AJILI YA MARXIMO. JK FUKUZA MARXIMO

    ReplyDelete
  10. Acha ushabiki Ankal kufungwa ni kufungwa maximo anapaswa aondoke! Ikumbukwe Ivory Coast, mechi hii haikuwa na umuhimu yaani frendly ndo maana hawakutukamia, lakini kama ingekuwa ACN tungekula goli si chini ya nne! Hawakutana ku-risk kuumia!

    ReplyDelete
  11. Duh, national limejaa kama Amirates vile. Che' Mkapa na kwikwi za hapa na pale lakini kwa hili uwanja tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  12. Enzi za mobutu Sese seko nzengekuku wa Zabanga hawa wote walikuwa ni kuchapwa viboko tu kwa kuanzia na kocha wao Mashimo !.....

    ReplyDelete
  13. Kwa walioangalia mechi ya leo tofauti iliyoonekana ni kuwa wenzetu wana Drogba na sisi hatuna. Nafasi tulitengeneza na mpira uliochezwa ulikuwa unafaa kuangaliwa kwenye luninga.
    Sio kazi ya kocha wa taifa kutengeneza kina Drogba ingawa Maximo kajitahidi kumtengeneza Tegete. Alipokuwa anamtengeneza wabongo ninyi ninyi mlikuwa mnasema dogo ni mtalii, mkawa mnataka Maximo ampange Mwaikimba au Emmanuel Gabriel. Siku hizi asipompanga Tegete inakuwa lawama.
    Mafanikio hayaji kwa muda mfupi. Kama mnataka mabadiliko baada ya mkataba wa Maximo kuisha fanyeni mabadiliko lakini msibeze mafanikio. Kuna wakati ilikuwa mkisikia tu kuna mechi na Ivory Coast hata uwanjani hamtaki kwenda. Siku hizi watu wanaenda uwanjani kwa kujiamini wakijua kwamba hatuendi kutia aibu na tunaweza kushuhudia kigogo akiangushwa.
    Safi sana Taifa Stars, keep it up.

    ReplyDelete
  14. HUYO DRGBA AMAESHINDWA NA VAMAELEN ATAWEZWA NA CAVANARO SIJUI NANI TENA KUTOKA TANZANIA SISI BADO KUJUA LABDA MPYA AKIACHA JK NAYEKUJA THEN ANAYEFATIA KDG ATAKUA NAJUA DUNIA YA SASA NA MAANA YA FUTBAL

    ReplyDelete
  15. Taifa Stars leo imecheza na vikosi viwili tofauti. Ivory Coast walibadilisha timu yote kabisa kipindi cha pili. Kikosi cha kwanza na kikosi cha pili kilikuwa tofauti.

    Kwa hiyo tuwapongeze kwa kuweza kucheza na timu mbili tofauti na kupoteza mechi ya kwanza kwa 1-0 huku wakitoa droo mechi ya pili bila bila.

    ReplyDelete
  16. hiyo inaitwa sportsmanship.. hawakutaka kutuvua nguo kabisa kwetu. Mngerudisha hilo moja, wangeongeza matatu.. hawakutaka kuwafanya Taifa wajione wachumba!!
    Mdau, Boston, US.

    ReplyDelete
  17. mi nafikiri huyu mwalimu mzuri ila papara zetu tutakujaletewa mwalimu ambaye hajali kukuza sako la vijana atawachukua hao mastaa wenu akimbizane nao akishindwa tunatafuta mwingine tena, mfano mzuri ni kwenye mahojiano aliyoyafanya humu, ameliona tatizo sasa anataka kutengeneza mfumo wa kudumu wa uchezaji kuanzia mashuleni mpaka ligi kuu, kwao brazili wanaweza kutengeneza timu nne za taifa na zikacheza zenyewe nusu fainali ya kombe la dunia, kwa sababu wana mfumo bora wa uchezaji, sasa mtu akitaka kuutengeneza kwetu mnaleta majungu, makocha waganga njaa wako wengi sana duniani watakuja na kuenda tu

    ReplyDelete
  18. Taiga Wuds ex girlfrendJanuary 05, 2010

    yani supa staa ni supa staa tu yani kila picha ukiangalia macho yako yanavutwa kwa Drogba, cheki picha ya grupu ya timu yani unaona hata chuchumaa yake inashaut super star. Da namfagilia na ai wili bii rutingi fo zem in sauzi afrika.

    ReplyDelete
  19. Yaani kwenye makabiziano ya hiyo bendera taratibu unaanza kuona tofauti za hao manahodha,unaanza na urefu,nguvu za misuli na uchangamfu.Na pia unaweza kujua yupi amefanya mazoezi mazuri ya muda mrefu.Anyway ndugu zangu kama alivyosema mhishmiwa mzee wetu kifimbo,tutafika tu siku moja.By the way did u know Ivory coast walikuwa wanachinjana kama kuku na kupigana risasi za vichwa,na ndio maana wengi wao wapo wanaishi nje.But they do know something about taking someone's life.

    mdau
    kalumanzila

    duniayetukubwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  20. maximo akimaliza mkataba atenda kwao hiyo haina shaka auatakwenda nchinyengine, lakini tuwe na shukrani na tukumbuke fadhila. tumefika tulipofika sio mbaya Maximo amefanya kazi na JK pia amefany akazi kazi, wabongo ndio kazi yenu , watu wazuri kwenu ni vijicent mnajulikana ,

    Tunakuthamini Maximo na tunathamini maamuzi ya JK kumleta maximo. Naonga mkono tu jitihada za kuongezwa wachezaji kutoka Zanzibar .
    mpeni mzirai hiyo timu akimaliz a maximo halafu wekeni mechi ya kirafiki na Zanzibar katka huo uwanja mpya na iwe usiku.

    tuone uwezo wa maximo na huyo mtz na roho mbaya zeu..............

    ReplyDelete
  21. Uncle Michuzi vipi mbona unakuwa mnazi? hatujafungwa kwa tabu, tumefungwa kirahisi tu ila goli ni moja. Tukumbuke walikuwa wanafanya mazoezi na sisi tulikuwa kiushindani zaidi.

    Tuache kujiongopea jamani Ngassa na Tegete waliruka ruka tu. Tumewashuhudia uwanjani, Ngassa anapata nafasi ya kwenda kufunga anasimama anamsubiri Uncle Michuzi ampige picha kwanza. Huwezi kuwa professional kwa style ile.

    Cannavaro ameshindwa kucheza Canada, msifikirie hata kidogo kucheza UK. Akapige jalamba Arabuni labda. Jana yeye na Nsajigwa wanacheza undava undava. Yule mtoto wa kiarabu Humud sijui mmemtoa wapi? Anapewa mkono wa fair play na Drogba anakataa mara 2. Mpira unaisha anaanza kuwazonga zonga wachezaji wa Ivory Cooast. Yaani full uswahili tena anajisahau Rais yupo jukwaani.

    Nadhani ni jambo la busara sana wachezaji wetu kujenga urafiki na wachezaji superstars wa Duniani kama Didier Drogba, siyo kujaribu kuwaonyesha kuwa sisi ni wababe kuliko wao.

    Bongo bado sanaa. Maximo anapenda nidhamu sijui anaisimamiaje. Mchezaji kama Humud hastahili kuwepo. Sidhani kama yule ananidhamu kuliko Chuji.

    ReplyDelete
  22. Ninachosema siku zote...hata kama tungeishinda Ivory Coast..bado tatizo kubwa ni kuwa na maendeleo endelevu ya soka.....hakuna long term plan ya kuendeleza soka..hivyo tutaendelea kusua sua na kujipa matumaini ya kubahatisha kila mara...na kubaki kuwakamia masupa staa kama akina drogba..ukimkaba basi soka imepanda!!!!ujinga mtupu....tujiulize katika miaka mitano hado kumi ijayo tutakuwa wapi tokea hapa tulipo??..kalaghabaho
    Manara Jnr

    ReplyDelete
  23. Timu imejitahidi lazima tuwape sifa yao tuache majungu,ila mimi kama kocha ningebadilisha na mfumo wa kuteua wachezaji.Mfano watu wengi wenye kazi ya kulinda haswa kwenye mikusanyiko mikubwa ni mabaunsa,hiyo yote ni kumpa mtu hofu ya kuleta fujo...thatha haka kamchesaji ketu kama Nsajigwa ukilinganisha urefu wake na Drogba kwakweli si shangai imekuwaje kafunga kwa kichwa......ni andunje!!!

    ReplyDelete
  24. mimi nimependa hizo vuvuzela tuu.

    ReplyDelete
  25. "THERE IS A HOPE WE NEED TO FOCUS FOR THE FUTURE NATIONAL TEAM STRUCTURE"

    Taifa Stars wamecheza vizuri katika mchezo wa jana na kutupa moyo wa maendeleo ya baadaye ingawaje matokeo hayatowaridhisha wote,tukubali kama tumecheza na timu yenye maelewano ya utaalamu wa kucheza pamoja kama timu moja,inahitaji muda mrefu kuwapa nafasi ya wachezaji wetu kuwa kama timu moja katika kiwango cha juu,wana vipaji vya kuzaliwa lakini kwa sasa ni wachache wenye utaalamu wa michezo ya kimataifa,juhudi za mchezo wa jana zinastahiri sifa zote.

    "MAXIMO IS AND WILL REMAIN THE ONLY SOLUTION FOR OUR NATIONAL TEAM HE SHOULD BE GIVEN MORE TIME & FREE SPACE FOR OUR FUTURE NATIONAL TEAM STUCTURE"

    Mickey Jones Amos
    Denmark

    ReplyDelete
  26. NYIE WOTE MNAOMKANDIA MAXIMO HAMJUI SOKA!!!

    MKUBALI,MKATAE MAXIMO KAFANYA KAZI YA KIHISTORIA KTK SOKA LA BONGO.

    HONGERA SANA MAXIMO !!!!

    WE APRECIATE UR JOB MAXIMO!!! BIG UP !!!

    Mdau # 22.

    ReplyDelete
  27. hao Ivory Coast wamebadili kikosi sababu wamekuja kupiga tizi na sio kukamia.hata kama wangefungwa wala isingewastua sana kwani nina imani kuna wachezaji wao wengi tu wanahofia kukosa namba kama wakiumia.
    tuache tabia ya kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa.tutaendelea kuota ndoto zisizo na ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...