Mtandao mpya umefunguliwa kwa ajili ya kuleta habari tofauti (muziki, matukio, mitindo, utamaduni, burudani na kadhalika) kutoka Zanzibar na Pemba. Nao ni:
www.zenjiflava.com

Kwa wale ambao wanataka kutuma habari zao zinazohusu Zanzibar na Pemba ili ziwekwe kwenye mtandao, naomba mtumie barua pepe hizi: info@zenjiflava.com au zenjiflava@hotmail.com

Kwa wale ambao wanataka kupiga soga (online chat) huku mkicheki habari mbalimbali kwenye tovuti basi mnabidi mjiunge kwanza. Mkiangalia kwenye mtandao, hapo juu kulia mtaona majina ya watu mbalimbali waliojiunga ambao wako LIVE wanapiga soga, ukigonga katika jina basi utaweza kuongea nao.

Kwa wale ambao wako Facebook, mnaweza mkajiunga nasi vilevile: facebook.com/zenjiflava

Ahsante Sana
www.zenjiflava.com
-----------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi za dhati na hongera kwa waandaaji wa libeneke la Zenjiflava ambalo sio tu litaleta mabadiliko na kutupasha mengi yahusuyo visiwa vya karafuu bali pia hii hatua imechelewa sana. Hivyo kazeni buti, acheni kutambaa simameni na muanze kukimbia ili tufaidi mambo ya Zenji.
HAPPY NEW YEAR
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kitu cha akili au bao la kisigino.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...