Watoto Mapacha walioungana wakiwa na uzito wa kilo3 waliozaliwa katika mkesha wa Mwaka Mpya katika hospitali ya Taifa Mnazi Mmoja Unguja wakipelekwa kuhifadhiwa katika chumba maalum. Bahati mbaya mapacha hawa walifariki dunia leo katika hospitali hiyo. Mama yao yu buheri wa afya. Picha na mdau Othman Maulid Mapara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ni mapenzi yake mola, Mwenyenzi mungu zilaze roho za malaika hawa pema peponi. wazazi jipeni moyo kila jambo laja kwa sababu. mwachieni mola atawafariji.

    ReplyDelete
  2. poleni mamamzazi na wafiwa wote. Mungu ni mkuu daima.

    Kaka michuzi Mungu akubariki kwa wema wako wa kutujuza yote ya nyumbani.

    ReplyDelete
  3. RIP poleni sana lakini mungu kaona watakuwa vizuri kwake sie wote tunapita njia tukielekea huko huko

    RIP Mzee Kawawa + Mwalim JK Nyerere

    Your names will live FOREVER

    ReplyDelete
  4. pole mama mzazi yote ni kazi ya mungu kaamua kuwachukua viumbe vyake mungu azilaze roho zao mahali pema peponi malaika zake!hawa wameungana vibaya ilikuwa tumbo kwa tumbo haki ya mungu,mungu mkubwa jamani!!!!inatia huruma sana!!pole dada yangu.

    ReplyDelete
  5. Innalillahi Wa Inna ilaihi Rajioun, Pole wazazi na hussan mama mzaziwa malaika hawa.Tatizo ni Umeme , kumekuwa na tatizo la Umeme Unguja na Hospitali kuu Umeme unawashwa kuanzia saa nne Usiku mpaka saa kumi na moja Alfajr na ni umemewa Jenereta.Pia mipango ya Mungu

    ReplyDelete
  6. RIP twins. Pole sana wazazi.

    ReplyDelete
  7. Sio mapenzi ya Mungu! mambo mengi Mungu huruhusu yatokee ili tujue kuwa Shetani (Ibilisi) yuko na anafanya maajabu na yeye hufurahi watu wakimsukumia Mungu lawama na kusema kuwa ni mapenzi yake ili watu wazidi kumchukia Mungu na kumuona ni mbaya sana. Hata mafuriko na maafa mengi (ajali n.k) yatokeayo ni shetani tu hujidhihirisha na kumsukumia lawama Mungu kupitia watu waishio duniani. Tunahitaji kumuomba sana Mungu ili daima atufunike na Damu ya Uzima na Malaika zake. Laiti Mungu angeamua kutufunulia kila kitu tunachopishana nacho katika maisha yetu ya kila siku hakika tusingeishi. Ni mengi mno ametupitishia mbali ila siku ya kiama yatafunuliwa mbele ya wote wanaomuamini na kumtegemea. Nawakilisha tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...