Home
Unlabelled
nani wa kulaumiwa?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
huku kijijini hakuna norma kama dar,amri mahakamani
ReplyDeletenachelea kuamini mawili, AIDHA kiwango cha elimu kimeshuka sana na watu wasiojua kusoma au/na kuandika ni wengi na huyo akawa mmoja wao AMA maisha magumu, mwananchi alishaona tutajuana mbele kwa mbele, najifanya hamnazo, au bahati askari asistukie hiki kibao na biashara yangu.
ReplyDeleteMaisha yenyewe haya? ah, liwalo na liwe.
mafisadi ndio wakulaumiwa kwa kuifikisha nchi hapo ilipo kwa wananchi kuuza ndizi, alishe familia watoto waende shule, hospitali etc, sasa unadhani anapenda kuuza ndizi hapo??
ReplyDeletejamani dhuluma ni kudhulumiwa siku ya hesabu. huyu mama amepumzika na biashara yake iko safarini iko katika shehena hata kupakuliwa haija guswa na usafi unang'ara . sasa nasema ukimwona mwana usalama anamsumbua si utalalamika na kufanya makundi hapo. hiyo ni rai binafsi yarabi salama.
ReplyDeleteAskari hawajaliona hilo bango, huyo dada hajui kusoma na wewe Mmbeya! period!
ReplyDeletesamaani mithupu kama ni wewe, sababu nakuheshimu!
Sehemu nyingi za kazi au mahospitalini Tanzania unakuta kuna bango hatupokee rushwa.Lakini rushwa inatpokelewa kama kawaida.Doktori au nurse Tanzania unaweza kumuonga hata shillingi elfu tatu elfu moja na akakuandikia vyeti feki au akakuondolea ugonjwa.Huyo Dada aidha anajua akija Askari kumkamata atampa shillingi mia mbili au mia tatu na akamwachia afanye biashara yake.Labda huyo Askari amechukua rushwa huko alipotoka na ameshiba kwa hiyo anajipitia zake na kutojali.
ReplyDeleteJambo lingine la kufikirika labda huyo Dada hajui kusoma kwa hiyo hajui kama kunakatazwa kufanya biashara hapo au hajui kwa nini asifanye biashara hapo;labda wangeandika kwa nini wananchi wasifanye biashara hapo.
Kuna mchangia maoni ameandika 'Mafisadi ndio wa kulaumiwa kwa kuifikisha nchi ilipo,hii nchi imetafunwa na Baba zetu,mama zetu,ndugu zetu,makaka na madada.Tulikuwa na viwanda vingi tu miaka ya 80 na mwanzoni wa 90 lakini vingi vilikufa achia sababu zingine mojawapo ilikuwa ni uzembe,uvivu,wizi wa wafanyakazi ngazi za chini hadi juu.Nakumbuka miaka ile mji kama Morogoro kulikuwa na kiwanda cha viatu MoroShoe na cha mafuta Moproco.Uwizi ulishamiri wa viatu na mafuta kupita kiasi kuna wafanyakazi walikuwa wanauza viatu vya wizi mitaani kama walikuwa/ kiwanda kilikuwa chao.Viwanda vote vikafa na kuuzwa kwa wageni baada ya kushindwa kuviendesha sasa karibia kila kitu tunaagiza nje hadi Asali tuyokuwa tunazalisha Tabora unabidi kuagiza'China'
Nachojaribu kusema wananchi wa matabaka yote wameshiriki au wanashiriki kuibomoa nchi.
Siajabu hao askari wenyewe wemetoroka kazini..au wamevaa uniform wakati hawako zamu wanaenda kuzitumia kinyume cha sheria..nani ajuae? Mdau-USA
ReplyDeletekwanza hata askari mwenyewe hana sare rasmi za jeshi juu kavaa koti la kiraia
ReplyDeleteLabda hiyo ni sehemu yake tu huyo mdada ya kufanyia biashara na yeye ndiye aliyeliweka hilo bango. Kwahiyo hilo bango linawahusu watu wengine na si yeye na askari wanajuwa hivyo.
ReplyDeleteNani kasema anafanya biashara mbona hakuna bei za ndizi.Hata kupumzika jamani ni kero acheni unafiki wenu dada katoka kuzinunua na anavuta pumzi ili asonge mbele na safari yake.
ReplyDeleteMama hajavunja sheria hata kidogo. Hapo alipokaa na biashara yake hapajakatazwa. Ila pale chini ya kibao ndipo palipokatazwa ndiyo maana yeye kakaa pembeni.
ReplyDeleteMdau amenena, mama amepumzika kidogo kabla hajaendelea na safari yake.
ReplyDeleteHata kama anafanya biashara hapo, tatizo ni kukosekana kwa miundombinu. Mnataka akauzie wapi ndizi zake? Si zitaozea njiani. Ukizingatia anatakiwa 'kuchangia' gharama za matibabu, elimu ya watoto wake, kodi kulipia gharama za mikataba mibovu nk hatupaswi kusema lolote juu ya uwepo wake hapo.
dada anajali afya za wagonjwa ndo maana hajataka kujali hilo tangazo,anajua wabongo wengi kula matunda mpaka waugue..dada endelea mwayego kwani huyo polisi aliruhusiwa na nani kula rushwa?mbn ndo zao! ukifuata hvyo vibao vyao utalala njaa ewe mlala hoi,wanakataza biashara hapo nje sababu za kwao zipo ndani tana kwa bei ya juu
ReplyDeletesababu askari hajui kusoma.
ReplyDeleteUKWELI NI KWAMBA KUUZA NDIZI SIO JINAI. HIVYO ASKARI HANA LA KUFANYA HAPO. HAO WALIOWEKA KIBAO NDIO WAJEKUMUONDOA HUYO MAMA
ReplyDelete