Mfanyabiashara ndogondogo akiuza ndizi katika eneo linalokatazwa kandokando ya barabara ya kuelekea hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma. Lakini kwa nyuma askari nao wakipita na hamsini zao, ingawa bango linalokataza biashara limeandikwa kuwa na amri halali..... Hapo sasa....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. huku kijijini hakuna norma kama dar,amri mahakamani

    ReplyDelete
  2. nachelea kuamini mawili, AIDHA kiwango cha elimu kimeshuka sana na watu wasiojua kusoma au/na kuandika ni wengi na huyo akawa mmoja wao AMA maisha magumu, mwananchi alishaona tutajuana mbele kwa mbele, najifanya hamnazo, au bahati askari asistukie hiki kibao na biashara yangu.
    Maisha yenyewe haya? ah, liwalo na liwe.

    ReplyDelete
  3. mafisadi ndio wakulaumiwa kwa kuifikisha nchi hapo ilipo kwa wananchi kuuza ndizi, alishe familia watoto waende shule, hospitali etc, sasa unadhani anapenda kuuza ndizi hapo??

    ReplyDelete
  4. jamani dhuluma ni kudhulumiwa siku ya hesabu. huyu mama amepumzika na biashara yake iko safarini iko katika shehena hata kupakuliwa haija guswa na usafi unang'ara . sasa nasema ukimwona mwana usalama anamsumbua si utalalamika na kufanya makundi hapo. hiyo ni rai binafsi yarabi salama.

    ReplyDelete
  5. Askari hawajaliona hilo bango, huyo dada hajui kusoma na wewe Mmbeya! period!

    samaani mithupu kama ni wewe, sababu nakuheshimu!

    ReplyDelete
  6. Ndoto ya mchana,Sweden.January 03, 2010

    Sehemu nyingi za kazi au mahospitalini Tanzania unakuta kuna bango hatupokee rushwa.Lakini rushwa inatpokelewa kama kawaida.Doktori au nurse Tanzania unaweza kumuonga hata shillingi elfu tatu elfu moja na akakuandikia vyeti feki au akakuondolea ugonjwa.Huyo Dada aidha anajua akija Askari kumkamata atampa shillingi mia mbili au mia tatu na akamwachia afanye biashara yake.Labda huyo Askari amechukua rushwa huko alipotoka na ameshiba kwa hiyo anajipitia zake na kutojali.
    Jambo lingine la kufikirika labda huyo Dada hajui kusoma kwa hiyo hajui kama kunakatazwa kufanya biashara hapo au hajui kwa nini asifanye biashara hapo;labda wangeandika kwa nini wananchi wasifanye biashara hapo.
    Kuna mchangia maoni ameandika 'Mafisadi ndio wa kulaumiwa kwa kuifikisha nchi ilipo,hii nchi imetafunwa na Baba zetu,mama zetu,ndugu zetu,makaka na madada.Tulikuwa na viwanda vingi tu miaka ya 80 na mwanzoni wa 90 lakini vingi vilikufa achia sababu zingine mojawapo ilikuwa ni uzembe,uvivu,wizi wa wafanyakazi ngazi za chini hadi juu.Nakumbuka miaka ile mji kama Morogoro kulikuwa na kiwanda cha viatu MoroShoe na cha mafuta Moproco.Uwizi ulishamiri wa viatu na mafuta kupita kiasi kuna wafanyakazi walikuwa wanauza viatu vya wizi mitaani kama walikuwa/ kiwanda kilikuwa chao.Viwanda vote vikafa na kuuzwa kwa wageni baada ya kushindwa kuviendesha sasa karibia kila kitu tunaagiza nje hadi Asali tuyokuwa tunazalisha Tabora unabidi kuagiza'China'
    Nachojaribu kusema wananchi wa matabaka yote wameshiriki au wanashiriki kuibomoa nchi.

    ReplyDelete
  7. Siajabu hao askari wenyewe wemetoroka kazini..au wamevaa uniform wakati hawako zamu wanaenda kuzitumia kinyume cha sheria..nani ajuae? Mdau-USA

    ReplyDelete
  8. kwanza hata askari mwenyewe hana sare rasmi za jeshi juu kavaa koti la kiraia

    ReplyDelete
  9. Labda hiyo ni sehemu yake tu huyo mdada ya kufanyia biashara na yeye ndiye aliyeliweka hilo bango. Kwahiyo hilo bango linawahusu watu wengine na si yeye na askari wanajuwa hivyo.

    ReplyDelete
  10. Nani kasema anafanya biashara mbona hakuna bei za ndizi.Hata kupumzika jamani ni kero acheni unafiki wenu dada katoka kuzinunua na anavuta pumzi ili asonge mbele na safari yake.

    ReplyDelete
  11. Mama hajavunja sheria hata kidogo. Hapo alipokaa na biashara yake hapajakatazwa. Ila pale chini ya kibao ndipo palipokatazwa ndiyo maana yeye kakaa pembeni.

    ReplyDelete
  12. Mdau amenena, mama amepumzika kidogo kabla hajaendelea na safari yake.
    Hata kama anafanya biashara hapo, tatizo ni kukosekana kwa miundombinu. Mnataka akauzie wapi ndizi zake? Si zitaozea njiani. Ukizingatia anatakiwa 'kuchangia' gharama za matibabu, elimu ya watoto wake, kodi kulipia gharama za mikataba mibovu nk hatupaswi kusema lolote juu ya uwepo wake hapo.

    ReplyDelete
  13. dada anajali afya za wagonjwa ndo maana hajataka kujali hilo tangazo,anajua wabongo wengi kula matunda mpaka waugue..dada endelea mwayego kwani huyo polisi aliruhusiwa na nani kula rushwa?mbn ndo zao! ukifuata hvyo vibao vyao utalala njaa ewe mlala hoi,wanakataza biashara hapo nje sababu za kwao zipo ndani tana kwa bei ya juu

    ReplyDelete
  14. sababu askari hajui kusoma.

    ReplyDelete
  15. UKWELI NI KWAMBA KUUZA NDIZI SIO JINAI. HIVYO ASKARI HANA LA KUFANYA HAPO. HAO WALIOWEKA KIBAO NDIO WAJEKUMUONDOA HUYO MAMA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...