Mkuu wa Wilaya ya Same Ibrahim Marwa (wa pili kushoto) akiangalia sehemu ya msaada wa mabati na cementi yenye thamani ya shillingi millioni kumi uliotolewa na benki ya NMB kama msaada kufuatia maafa ya maporomoko ya udongo yaliyotokea Wilayani Same hivi karibuni na kusababisha baadhi ya nyumba za wakati wa maeneo hayo kuharibika vibaya. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano benki ya NMB Shy-Rose Bhanji na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Viciky Bishubo


Mkuu wa Wilaya ya Karatu Methew Sedoyeka akishuhudia makabidhano ya mashine ya kusaga iliyokabidhiwa na benki ya NMB kwa kikundi cha akina mama wilayani karatu kama msaada wa kuendeleza biashara ndogo ndogo wanazofanya kina mama hao. Kikundi hicho kimekuwa vile vile mfano mzuri unaorejesha mikopo kwa wakati kutoka benki ya NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. benki ya nmb iko mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya jamii. kila siku tunaona benki hii inatoa misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mashule, wanatoa madawati, vifaa hospitalini na vile vile kwenye michezo wamo. hii benki inastahili pongezi. kinachotia moyo kuhusu hii benki kila panapotokea maafa wapo mbele kusaidia..nakumbuka mbagala disaster pia walikuwepo mstari wa mbele

    ReplyDelete
  2. safi sana nmb

    ReplyDelete
  3. akinamama ni walipaji wazuri wa mikopo

    ReplyDelete
  4. utaratibu wa kupatiwa misaada nmb ukoje shyrose?

    ReplyDelete
  5. safi sana hivi juzi tumeona wametoa msaada wa shillingi millioni kumi kule kilosa, na sasa wametoa millioni kumi zingine maafa ya same. NMB kweli inajali sana jamii inayowazunguka kwani hapa tunaona kabisa kwamba pamoja na kwamba benki inafanya biashara lakini tunaona pia japo kuna pesa ingine inawarudia jamii.

    ReplyDelete
  6. jamani kusema ukweli NMB wapo juuu tena juuu sana,maana wao kila siku wanatoa misaada kwa jamii.Inabidi mashirika mengine yaige mfano wa NMB.
    NMB OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  7. hii benki ni kiboko sijaona benki ingine inayofanya mambo ya kijamii kama nmb...ni kweli benki zingine zinatoa ila hawa nmb ni kiboko...kweli wako juuuuu muendelee hivo hivo ili wengine waige mfano wenu

    ReplyDelete
  8. MHE IBRAHIM MARWA, NAKUMBUKA HUYU ALIKUWA MMOJA KATI YA WABUNGE MACHACHARI SANA BUNGE LILILOPITA. VIPI KAKA UNARUDI ULIONGONI?

    ReplyDelete
  9. benki ya watu....

    ReplyDelete
  10. kaka mithupu..BLOG YAKO IKO JUU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...