POLE SANA. RIPOTI YAKO KWA MWAKA
2009 IMETOKA! NA NI KAMA IFUATAVYO:-
KUOGA - D
WIVU - B
UVUMILIVU - F
ULEVI -A
UTU WEMA - C
KUKUBALIKA KATIKA JAMII - F
UCHONGANISHI - A
KUBISHA KILA JAMBO- A
UPOLE - D
KUZURURA - A
KUJITUMA - F
MAPENZI - A+
KUROPOKA - A
KUSALI - F
KUTUSI WENZIO KWENYE MABLOG - A++
UNACHEKA UNAFIKIRI MAZURI?
JIREKEBISHE 2010 HII.
UMEKUWA MTOTO WA 2 KATI YA WATOTO 81 KATIKA SKULI HII YA NIDHAMU. HUNA HAJA YA KUONGEZA BIDII. WEWE NI NGULI.
SHULE IKIFUNGULIWA NJOO NA UNIFORM MPYA,
KALAMU NA MADAFTARI MAPYA. USISAHAU UFAGIO WA CHELEWA...
Mdau A.KP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. mama mbavu zangu wee

    ReplyDelete
  2. hii special kwa wakaanga sumu kazi kwenu matokeo mabaya jirekebisheni acheni pumba fateni ya msingi ilikujenga jamii penye haki na ukweli kubalini sio kuona kil akitu kibaya nyie mmekamilika? Michuzi mola akupe maisha marefu unatustiri kweli na news mzee big up mwaka mpya mwema masupu original

    ReplyDelete
  3. Labda ungeongezea na walete madawati yao wenyewe. Bilioni moja ina shughuli nyingine.

    ReplyDelete
  4. Sio vizuri kuwasema vibaya viongozi wakuu wa nchi. Safari za kikazi sio uzururaji.

    ReplyDelete
  5. Dah aisee nimecheka mpaka nimepaliwa

    ReplyDelete
  6. Excellent report. Strong CV. Perfect candidate wa umasikini.

    ReplyDelete
  7. Hi ni funga mwaka....
    Tnx Mithupuuu
    happy New year

    ReplyDelete
  8. no. Huyu mtoto amekuwa wa 78 kati ya watoto 79 na huyo wa 79 alikuwa si mhudhuriaji mzuri katika hayo masomo..Happy New everybody..

    ReplyDelete
  9. Mh! huyo mtu noma, but kitu kimoja, how com'z ana mi-A mingi hivo afu awe wa pili toka mwisho???? nafikiri wewe mwalimu unahitaji kutandikwa mifimbo kwa kutokuwa makini na kazi yako

    ReplyDelete
  10. Tafadhali weka ufafanuzi kama A ni ushindi wa juu eg 10 out of 10 na labda F ni ushindi wa chini eg 1out of 10.Kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  11. umesahau kipengele cha ngono isiyo salama kaka michuzi,ni somo la lazima kama hisabati.

    ReplyDelete
  12. Jamani hii ni kweli kabisa nimefurahi kuona kama watu wanauwezo wa kufikiria vitu kama hizi.Happy New Year wadau.

    ReplyDelete
  13. Mwanafunzi huyu ni nani?:)

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  14. Hii ni ripoti ya ankal mwenyewe!!! teh teh teh

    ReplyDelete
  15. wadau naomba kueleweshwa nini maana ya ngono salama!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...