Na Veronica Kazimoto - MAELEZO
Serikali imeamua kuwashirikisha watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kushiriki kikamilifu katika kuchangia na kuwekeza katika rasilimali zilizopo inchini ili kuleta maendeleo.
Akifungua mkutano wa watalaam mbalimbali wa ndani na nje ya nchi waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema ili kuinua uchumi wa nchi haina budi watanzania waishio nje ya nchi kushirikishwa kikamilifu katika nyanja zote za kimaendeleo.
“Baadhi ya watanzania wanaoishi nje ya nchi wana nafasi nzuri na kipato cha kutosha hivyo wana nafasi nzuri ya kuchangia na kuwekeza katika rasilimali zetu na hatimae kuleta maendeleo yetu.” Amesema waziri Membe.
Aidha waziri Membe amesisitiza kuwa kuna haja ya kubadili sheria ya uraia ya Tanzania ambayo haimruhusu mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili kwani sheria hii imepitwa na wakati na haimpi hamasa mtanzania huyo kuisaidia nchi yake kwakuwa amepoteza uraia.
“Ni ngumu sana mtu kuisaidia nchi yake wakati amepoteza uraia wa nchi hiyo, naamini sheria hii ikibadilishwa watanzania wengi watakuwa na moyo wa kuisaidia nchi yao kwani watakuwa ni sehemu ya nchi hiyo.” Ameongeza waziri Membe.
Nae mwakilishi wa watanzania waishio Uingereza na Mkurugenzi wa ujenzi wa nyumba mpya na ukarabati wa nyumba za kupanga Daniel Mwasandube amesema wako tayari kurudi nchini na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
Mwasandube amesema Tanzania inapotangaza nafasi za kazi itangaze pia na kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ili waweze kutuma maombi ya kazi hizo na hatimaye waajiliwe katika ngazi mbalimbali nchini.
Akifungua mkutano wa watalaam mbalimbali wa ndani na nje ya nchi waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema ili kuinua uchumi wa nchi haina budi watanzania waishio nje ya nchi kushirikishwa kikamilifu katika nyanja zote za kimaendeleo.
“Baadhi ya watanzania wanaoishi nje ya nchi wana nafasi nzuri na kipato cha kutosha hivyo wana nafasi nzuri ya kuchangia na kuwekeza katika rasilimali zetu na hatimae kuleta maendeleo yetu.” Amesema waziri Membe.
Aidha waziri Membe amesisitiza kuwa kuna haja ya kubadili sheria ya uraia ya Tanzania ambayo haimruhusu mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili kwani sheria hii imepitwa na wakati na haimpi hamasa mtanzania huyo kuisaidia nchi yake kwakuwa amepoteza uraia.
“Ni ngumu sana mtu kuisaidia nchi yake wakati amepoteza uraia wa nchi hiyo, naamini sheria hii ikibadilishwa watanzania wengi watakuwa na moyo wa kuisaidia nchi yao kwani watakuwa ni sehemu ya nchi hiyo.” Ameongeza waziri Membe.
Nae mwakilishi wa watanzania waishio Uingereza na Mkurugenzi wa ujenzi wa nyumba mpya na ukarabati wa nyumba za kupanga Daniel Mwasandube amesema wako tayari kurudi nchini na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
Mwasandube amesema Tanzania inapotangaza nafasi za kazi itangaze pia na kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ili waweze kutuma maombi ya kazi hizo na hatimaye waajiliwe katika ngazi mbalimbali nchini.


Serikali itangaze rushwa kama janga la kitaifa ili kuweka mazingira bora.watanzania wa nje wana mchango mkubwa sana wanaoweza kuuleta hapo nyumbani ila walishazoea mazingira yasiyokuwa na rushwa wanapata shida sana na kukabiliana na hali hiyo.nadhani inaeleweka.serikali ina mambo mengi sana ya kufanya kuweka amzingira supa.
ReplyDeleteMimi ni mtanzania anaeishi nje, sasa hivi najaribu kuanza business
ReplyDeleteDar, lakini nasubiri nijue naweza kurudi, naweza kufanya biashara bila kulipa rushwa, serikali ikitaka tujenge inchi yetu lazima
waturudishie citizenship, we are just waiting.
Nafikiri hiyo inaweza kusaidia kwa nchi yetu, kuna mamilioni ya watanzania ambao wana moyo wa kuijenga nchi yetu lakini wanashindwa kwa kuwa tayari ni raia wa nje wanaogopa kuwekeza kwao kutokana na sera mbovu za nchi yetu.
ReplyDeleteWajaribu kutazana nchi nyingine wanavyofanya na jinsi wazalendo wanavyowekeza tokana na kuwa na uraia wa nchi mbili
Watanzania wengi tunashindwa kuchangia maendeleo, si kwasababu tu ya Ruswha peke yake, bali kwavile serikali yenyewe inalifanya hilo jambo kuwa la kisiasa. Serikali inajua wazi kuwa hawawezi ku-implement hata kitu kimoja watakachoshauriwa na wataalamu...kwanini sasa wanajaribu kuwasumbua watu? Ninyi wenyewe mnajua kuwa mazingira mliyoyajenga haya-support input ya wazawa wanaokaa nje ya nchi. Kwamfano, biashara nyingi zinazofanikiwa za watu wa nje ni zile zenye mikono ya wakubwa. Wakubwa wengi ukiwapa idea wanakwambia tu andika proposal...tumeshajua watu wengi wameandika proposal..kisha mnawapa watu mnaowajua ninyi mnakula nao na kutwambia kuwa hizo proposal hazikufanikiwa...tunajua mnavyo-operate...kama huna ulaji huweki nguvu kwenye kitu. Tumieni huo muda kusafisha serikali na mtaona input ya Diaspora kwenye maendeleo. Nchi nyingi zimefaidika kama vile Ghana...ninyi bado mnakalia uchoyo, ubinafsi, wizi, tamaa ya kuiba vitu ambavyo hata kuvitumia hamtavitumia..ni kukusanya na kulundika tu mali...na pesa nyingine mfiche mufe hata watoto wenu na wake zenu hawajui zilipo. Yaani kweli Tanzania mnazidiwa Leadership na Rwanda? Mnatutia huzuni sana. Kweli hatuna leadership mpaka kanchi kama Rwanda kanakolingana na mkoa wa Tabora kanatuzidi kwa kufanya vitu vinavyoonekana? Mbona wengine mtaondoka madarakani hakuna historia mlioacha? Baba wa Taifa alituacha masikini lakini alituachia umoja. Ninyi mnatuachia nini mkimaliza terms zenu za uongozi? Visima vya maji? na giza? Mnatukatisha tamaa wenzenu...!! Kwani kama nchi inawashinda si mnapisha tu wenye uwezo..mbona mwalimu alitoa mfano mzuri sana...kaona ngoma imebana akajitoa mwenyewe...!! Hiyo ndo maturity....pesa hazina mwisho..ng'atukeni kwa heshima tu mamani tutawa-enzi kuliko mking'ang'ania halafu cha maana hakuna maneno mengi tu...tumechokaaaaaaaaa...!!! Mdau-USA
ReplyDeleteNapenda hiyo idea ya uraia wa nchi mbili.Nchi za kiafrica kibao wanafanya uraia wa nchi mbili na maemdeleo yao yako juu.Mie binafsi nilikuwa napanga Mungu akinijalia niwe nakuja nyumbani kufanya shughuli za maendeleo ila bila kulipia viza wakati narudi nchini mwangu na nakuja kwa lengo la shughuli za maemdeleo.So dual citizenship is the way to go, i agree with the pro 100%
ReplyDeleteSafi sana,
ReplyDeletekaka michuzi mimi nakubalian na uamuzi wa Serikali kuwashirikisha watanzania wishio nje katika maendeleo ila sioni ni misinghi ipi ambayo imeshawekwa kufanikisha hilo. Hii kauli ya mheshimiwa Membe naona kama ya kisiasa zaidi. ingekuwa vyema akatueleza mkakati gani ambao serikali imeshauweka.
Pili. Mimi binafsi sidhani kama ni kweli kubadilisha sheria ya Uraia ndo kigezo cha watu kuchangia maendeleo ya nchi yao. Kwanza Mhe. Membe hana mamlaka ya kusema kuwa sheria hiyo ibadilishwe au inafaa au haifai. Kama anaamini hivyo apeleke hoja hiyo Bungeni ili Waheshimiwa waaanze mchakato wake. Suala la kubadili sheria yeyote ile lina taratibu zake. Haiwezekani waziri mmoja au mbunge aksema hii ni sheria nzuri au mbaya, ibadilishwe au isibadilishwe. hapa Mhe. ameshaihukumu hiyo sheria.
Mimi naona tarfiti zifanywe tujue kwa nini vijana wanakimbilia nje na hawarudi nchini, wanafanya nini huko wanakipato gani na watachangia vipi. kuna mambo mengi yanahitaji kufanyiwa kazi na si rahisi kama Mhe. alivyoongea. hii ni politix....
Mtz anayeipenda nchi yake atachangia tu hata kama ana uraia wa nchi nyengine, wengi waTz walioko nje ni wanafunzi au watu ambao ndio kwanza wanaanza kutafuta maisha huko nje na hali yao huko nje ni ya kawaida tu, sio kama wana mipeeesa na hawataki kuileta Tanzania ati kwa sababu wamenyimwa kuwa na dual citizenship. nisiieleweke vibaya pia kwani nasapoti dual citizenship ili kuwarahisishia wabongo maisha! maisha ya kuishi unapotaka bila kujificha ficha.
ReplyDeleteI am posting my comments to congratulate our governmnet for this bold step.
ReplyDeleteIn my view hesitating to act in a timely fashion to do what's right and advantageous to our people constitutes lack of discretion and vision.
Time has come to show some leadership in the region. To heck with being last in everything.
TRIO Wewe ni wale wale tu umepitwa na wakati. Thanks Membe kwa kuwa na hoja ya maana mna kuangalia maendeleo na sio wivu usio na kichwa wala miguu. Ndio maana hatuendelei watanzania.
ReplyDeleteIt sounds very familiar - have I not heard it all before?
ReplyDeleteNashukuru sana kaka michuzi kutuwekea hii mada.Kwanza ileweke kwamba kuna watanzania wengi wamejificha tu huku,na walilelewa na Tanzania hiyo.Sasa Mheshimiwa Rais tumia busara yako ,kuwatumia kuleta maendelea.kwa mfano ili kuboresha kila sekta ,tunakuomba uwatumie pia wataalam na watanzania wa nje.mfano sekta ya umeme,ni nini kifanyike pata mawazo na fikira na utaalam kutoka kwa watanzania wanaofanya kazi katika sector hiyo nje,sekta ya maji fanya vivle vile,sekta ya madini vile vile na zinginezo.sio mnakaa na kusaini mikataba mibovu na baadaye mnasema tulikosea ?hiyo si nzuri.mnakuwa wachoyo na mnajifanya kama smart kumbe sio smart wala nini,shame on you mnaokula pesa za nchi na mnanga'nga'nia madarakani.mwisho wenu umefika sasa.
ReplyDeleteMdau USA
Ankal, mtu anapochukua uraia wa Marekani, anakula kiapo kuukana uraia wa kule anakotoka, na hatambui mamlaka ya mkuu au serikali ya nchi ile anakotoka. Kiapo chenyewe ni hiki hapa:
ReplyDelete"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; that I will perform noncombatant service in the armed forces of the United States when required by the law; that I will perform work of national importance under civilian direction when required by the law; and that I take this obligation freely without any mental reservation or purpose of evasion; so help me God."
MHESHIMIWA BERNAD MEMBE, NAKUPONGEZA KWA JITIHADA ZAKO KUHUSU HILI SUALA LA URAIA WA NCHI MBILI CHINI YA UONGOZI WA MHE RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, MMEONA MBALI, TATIZO NI KULIPITISHA KATIKA BUNGE ILI IWE SHERIA, WABUNGE WETU WENGI NI "MYOPIA" HAWAONI MBALI, WAPELEKENI UGHAIBUNI WAKAFANYE UTAFITI ZAIDI KATIKA NCHI ZINGINE ILI WAJUE UMUHIMU WA DUO CITIZESHIP & NATIONALITY, MHE MEMBE WEWE UMETEMBEA UGHAIBUNI NA UNALIJUA HILO NA KUTAMBUA MCHANGO WA "DIASPORA" WELL DONE MHE MEMBE KWA KUENDELEZA LIBENEKE LA "DUO CITIZENSHIP" BUT WE NEED CLEAR ANSWER " EITHER "YES" OR "NO" FOR DUO CITIZESHIP, THEN TANZANIAN IN DIASPORA WILL KNOW WHICH SIDE THEY ARE IN. MDAU READING BERKSHIRE - UK
ReplyDeleteSi lazima mchango uwe wa kipesa jamani,hata mawazo na nguvu kazi katika ujenzi wa taifa,Rwanda walifanya kuwaita wasomi mbali mbali waliokuwa nje ili waje kushika nafasi katika serikali na taasisi zake hapo si mchango wa pesa watu waliotoa mchango wa nguvu kazi ambao ni uzalendo mkubwa,Tz ina wasomi wengi tu madaktari,maprofesa na hata wataalam wa nyanja mbali mbali ambao waliondoka kwa kukereka na mambo yanavyokwenda au hata kwa changamoto za kimaisha kwa kushawishiwa na mishahara minono isiyo na mazinguzi kwenye nchi za nje kama Botswana,Namibia na nchi nyingine nyingi ambazo zina madaktari wengi tu na wasomi wengi wa kibongo ambao wanahitaji motisha tu warudi huku si hizi siasa zisizo lenga "Mutual benefits" katika jamii yetu.
ReplyDeleteSerikali inabidi idhamirie kuleta maendeleo ya kweli na si porojo hao wataalam wa kitz wengine ni very good policy makers waje huku waokoe jahazi.Hilo suala la rushwa ni moja tu ya vitu ambavyo kiuhalisia serikali inabidi itafute kikomo chake,hata kama itabidi kutangaza adhabu ya kifo kama China basi ifanye hivyo maana si kweli kuwa maendeleo yote yanayopatikana lazima yatimize haki zote za binadam maana kwa kumpa mmoja haki unamkandamiza mwingine ko ni bora kifo cha mla rushwa mmoja kuliko wananchi wote kupata hasara ya kunyang'anywa haki yao.
Jamani ndio mnastuka leo
ReplyDeleteTanzania yetu ina matatizo mengi nasi tunayavumilia; kama mtu ana pesa zake nyingi huko nje na hataki kuja kuwekeza hapa nchini na akae nazo huko nje. Tafsiri rahisi ya Dual citizenship ni UKIMBIZI.
ReplyDeleteMimi nasema zaidi ya mambo ya uraia ambayo naunga mkono pia, kuanzia uchaguzi huu Watanzania tulioko nje lazima tupige kura.
ReplyDeleteNi haki yetu, hivyo mabalozi na makonsuli wafanye taratibu zinazopaswa, kutuwezesha kupiga kura uchaguzi mkuu ujao mwaka huu. Bunge liseme sasa suala hili na kuweka msimamo vinginevyo tunakuja huko huko na kuwapinga KABISA WABUNGE WALIOPO BUNGENI SASA wasipate kura majimboni maana hii ni haki yetu ambao bado ni Watanzania wenye akili timamu na umri wetu wengi ni zaidi ya miaka 18, hii ni haki na si bhakhishishi!
Kwanza: Tuache kusema serikali imejaa rushwa na tuanze kusema rais kikwete na serikali yake wamejaa rushwa.
ReplyDeletePili: Kama alivyosema bwana Mbele hapo juu kuhusu uraia wa marekani unavyokulazimisha kuukataa uraia wako "orijino"; pia tunatakiwa tufahamu kwamba uraia wa marekani haumkatazi mmarekani yoyote kusherehekea au kujihusisha na maendeleo ya nchi anayotoka, na ndiyo maana hapa marekani kuna sikukuu kama za "saint patrick's day" ambayo ni sikukuu ya watu waliotoka Ireland; na pia kuna "tartan day" ambayo ni ya wa-scotland.
Tatu: Kwenye hili suala la uraia wa nchi mbili, mimi binafsi ni diaspora ninayepingana na suala hili. Kinachonotisha ni kwamba, wazungu (matajiri) watautumia mwanya huu watachukua uraia wa Tanzania na watanunua ardhi kubwa sana nchini kwetu, na vizazi na vizazi vyao wataanza kuleta zao zile zile za kizungu na watoto wetu watalazimika kupigana vita vile vile vya "umkhoto we sizwe" walivyopigana akina Nelson Mandela.
Kama lengo ni kurejesha diaspora kusaidia maendeleo ya nchi, hili linawezekana kufanyika bila ya sheria ya uraia wa nchi mbili. Kwa mfano, serikali inaweza kuanzisha kitu kama "diaspora visa" ambayo ili uipate inabidi uwe umezaliwa Tanzania au uwe na mzazi aliyezaliwa Tanzania; na visa hii itakuwezesha kukupa haki zote anazopewa mtanzania ndani ya Tanzania.
Kenya, mzungu mmoja tu ambaye ameamua kujiita mkenya anamiliki ekari 48,000. Wakati huohuo wakikuyu 1000,000 wanaishi kibera katika eneo lisilozidi km 3 za eneo. Na mkikuyu akiingia kwenye ekari za mzungu anapigwa risasi.
Sasa kwa wale tuliokuwa na uraia wa nje, tuzingatie maslahi ya nchi kwanza, au vinginevyo tunakuwa hatuna tofauti yoyote na hawa mafisadi wanaoitafuna nchi nyumbani.
DUAL CITIZENSHIP:
ReplyDeletekwa faida ya nani?
asilimia ngapi ya watanzania wanaishi nje?
na wakenya wakichukua uraia wa Tanzania ili wapate ardhi yetu je? maana sio kuangalia upande mmoja, maana hii itaruhusu pia wasio watanzania kuomba uraia wa tanzania kwa faida yao...
TAFAKARI...CHUKUA TAHADHARI!
ruhusuni urai wa nchi mbili kama kweli mnataka mchango mkubwa wa wanaoishi nje ya nchi. well kwa tanzania hilo ni mwiko au vipi?
ReplyDeleteMdau Mbele hapo juu, Kuwa na uraia wa nchi mbili kwa Marekani sio kweli lazima ukaane uraia wa nchi nyingine ukichukua uraia wa Marekani ila wanataka utumie uraia wao unaporudi marekani au ukiwa nje. Ubalozi wa marekani hauwezi kukusaidia endapo utakwama tanzania kwa matatizo yoyote huku umeingia na pasi ya Bongo. Lakini si kweli kuwa lazina ukaane uraia wako wa ulikozaliwa kama wanavyofanya nchi kama Norway au Japan.
ReplyDeleteHii inatoka State Department ya marekani:
"A U.S. citizen may acquire foreign citizenship by marriage, or a person naturalized as a U.S. citizen may not lose the citizenship of the country of birth.U.S. law does not mention dual nationality or require a person to choose one citizenship or another. Also, a person who is automatically granted another citizenship does not risk losing U.S. citizenship. However, a person who acquires a foreign citizenship by applying for it may lose U.S. citizenship. In order to lose U.S. citizenship, the law requires that the person must apply for the foreign citizenship voluntarily, by free choice, and with the intention to give up U.S. citizenship.
Intent can be shown by the person's statements or conduct.The U.S. Government recognizes that dual nationality exists but does not encourage it as a matter of policy because of the problems it may cause. Claims of other countries on dual national U.S. citizens may conflict with U.S. law, and dual nationality may limit U.S. Government efforts to assist citizens abroad. The country where a dual national is located generally has a stronger claim to that person's allegiance.
However, dual nationals owe allegiance to both the United States and the foreign country. They are required to obey the laws of both countries. Either country has the right to enforce its laws, particularly if the person later travels there.Most U.S. citizens, including dual nationals, must use a U.S. passport to enter and leave the United States. Dual nationals may also be required by the foreign country to use its passport to enter and leave that country. Use of the foreign passport does not endanger U.S. citizenship.Most countries permit a person to renounce or otherwise lose citizenship".
Kwa kifupi, serikali hawana sheria za kuwa na pasi mbili ila hawatakupokonya uraia wako wa kuzaliwa wa Marekani ila una haki ya kuukana.
Nawakilisha.
Reference US state Dept. URL:
http://travel.state.gov/travel/cis_pa_tw/cis/cis_1753.html
Na wewe mdau wa Jan 20, 01:25:00 Unayeogopa wakenya.
ReplyDeleteWakenya ni ndugu zetu na wala si maadui zetu, na usiogope kwamba eti wakenya watachukua ardhi yako. Mkenya hata akinunua ardhi bongo, hiyo haina madhara yoyote kwako wewe. Mkenya, M-nigeria, M-malawi akinunua ardhi Tanzania, basi kizazi chake kitakuwa watanzania na kamwe hawataihujumu Tanzania kwa manufaa ya nchi nyingine. Mzungu hata akiwa kizazi cha mia mbili hapa kwetu, bado atakuwa mgeni tuu na ajenda yake itakuwa ni kuihujumu nchi hii. Angalia wazungu wa south africa, zimbabwe na kenya.
Kama alivyosema agano la kale huko juu, waogope wazungu, siyo waafrika wenzako.
Ankal,
ReplyDeleteNingeomba Serikali ifanye tafakari ya kina kuhusu sheria ya uraia wa Marekani, hasa kipengele hiki kinachohusu mtu anayeomba uraia wa Marekani wakati ni raia wa nchi nyingine.
Nawashukuru wadau wanaotahadharisha kuwa tukifanya papara na suala hili, tutaweza kuja kulia mbele ya safari.
Nimevutiwa na wazo la "diaspora visa." Huku Marekani, kama wewe si raia wa Marekani, una fursa ya kuomba visa inayokuwezesha kuishi na kufanya kazi hata kwa maisha yako yote, bila kuwa raia. Hii ndio inayoitwa "green card." Nimevutiwa na wazo la "diaspora visa," kwa wale ambao watakuchukua uraia wa nchi kama Marekani.
Nimeleta hiki kiapo cha uraia wa Marekani ili wa-Tanzania wapate muda wa kukitafakari, na wabunge wetu nao wakiangalie.
Mimi sijasomea sheria, na kwa hivi sina ubavu wa kuitafsiri hii sheria ya Marekani. Ndio maana naiomba serikali yetu ifanye hii kazi na kutuletea ufafanuzi.
Mbona watu mmepitwa na wakati hili swala la dual citizenship limeshajadiriwa na serikali ya Kikwete 2008 na wamepinga kubadirisha sheria. Sasa MEMBE ULIKUWA WAPI KULIPIGIA DEBE THEN??!!! LABDA USEME LIRUDISHWE KWENYE MJADALA TENA AU UNATAFUTA KURA ZA MA-DIASPORA ASSOCIATES???
ReplyDeleteRISHWA KILA MAHALI HATA KWENYE MATAIFA MAKUBWA.....NA KUSMEA UKWELI NI VIGUMU KWA HILO KUOPOTEA KWENYE NCHI YETU.
ReplyDeleteKUHUSU URAIA WA NCHI MBILI NI MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI...LITAPIGWA DANA DANA HADI KUPOTEA NA HAKUNA KITAKACHOFANYIKA....NI USANIII KAMA MAMBO MENGINE..KAMA VILE DARAJA LA KIVUKONI NA EPA....NA UNYANYASAJI WA KIPAWA NA KIGAMBONI...
mimi ni mtanzania na nipo nje ni kweli tunahitaji kuendeleza nchi yetu kwani hata huku tax zetu ndio zinafanya kazi ila sasa kama hata tukiamua kusaidia nchi yetu si mafisadi tu ndio watafaidi na si wananchi na lengo ni kuinua kipato kusaidia hata wale ambao wanaishi chin ya $1?
ReplyDeleteHongera Membe! wafungue macho hao,mawazo yako ni mazuri, ukiendelea hivyo hivyo Urais wa TZ utaupata bila matatizo!!!!
ReplyDeleteHalafu na wewe TRIO kweli u,epitwa na wakati,wewe ni akina wale wale ndiyo hao hao, amka pumbavu wewe.
kwenye hii forum kuna mawazo mazuri kuliko kwenye bunge la waheshimiwa wasiojiheshimu dodoma huko. Huu ni ushahidi kwamba diaspora input in necessary.
ReplyDeleteProfesa Mbele generation yako imekwisha mda wake. Mda wa kung'ang'ania uraia wa nchi uliozaliwa hata kama haikunufaishi kitu chochote umepitwa na wakati. Nakubali kwamba enzi zenu ukimaliza chuo nje baada ya kusomeshwa na serikali ,ukirudi nyumbani unakuta kazi inakusubiri na unapata ajira na kuendeleza nchi bila tatizo kabisa.
ReplyDeleteHali sio hivyo kabisa sasa hivi katika hii generation. Vijana wa sasa wanakwenda wenyewe kusoma huko nje na wanajisomesha kwa fedha zao na kwa kufanya kazi ngumu. Sasa hivi hakuna matumaini ya kupata kazi wanazozitaka wakirudi nyumbani na hivyo wao kuwa na uraia wa nchi mbili ni muhimu sana sasa kuliko wakati wowote.
Wewe ndio unaweza nchi marekani kwa kibali chako cha kazi au green card na huna haja ya kuukana uraia wa TZ kwa kuwa unavuna kote kote.
Unataka fedha za marekani kama mwalimu unayefundisha huko pia unataka ugombanie ubunge wa upinzani TZ. Hivyo kwako wewe uraia wa TZ ni muhimu sana kuliko hawa vijana wa sasa.
Vijana wa sasa hawataki ubunge TZ, wanataka kuja kufanya kazi na kuwekeza na kutoka na kurudi muda wowote wanaotaka.Hivyo uraia wa nchi mbili ni muhimu kuliko wakati wowote kwao.
Nakuomba profesa Mbele kama hujui sheria ya marekani kuhusu citizenship usiwanyimie vijana walioko huko kuupata. Nionavyo mimi na huu ni mtizamo wangu pekee -ni kwamba unataka wawe vijana wa sasa wawe kama wewe, ambaye umesoma nje na ukafanya kazi TZ na ukaona maisha hayakai vizuri kwako ukajaa nje kufundisha. Hivyo hupendi kuona hawa vijana wa sasa wakifaidi kupata uraia wa nchi mbili. Nilitegemea wewe ndio utakuwa wa kwanza kuku-bali wapate uraia wa nchi mbili haraka kwani umekuwa huko na unajua umuhimu wake.
Mimi niko TZ na ninafanya biashara na inabidi nikae TZ miezi sita halafu nirudi Marekani kwa wiki mbili ili green card yangu iendelee kuwa halali na sioni wengine kwa nini wasiweze kupata uraia wa marekani au hata green card na kunufaisha nchi.
Nimesoma juzi WATZ walio nje walichangia milioni $100 tu mwaka 2005 , kulinganisha na wakenya katika muda huo walituma zaidi ya $ Billion 1.
Angalia hiyo tofauti na elewa umuhimu wa kufanya TZ kuwa na uraia wa nchi mbili. Wenzetu wakenya walishajizoelea kwamba kwao hakuna kazi hata kama wakirudi, na wala hawagombei ubunge ila ni kutuma fedha tu za kusaidia nyumbani kwao hata kama wao pia hawana uraia wa nchi mbili.
Profesa mbele nakushauri uache mambo ya generation hii yaende kama wanavyotaka, au kama wewe huitaji huu uraia wa nchi mbili basi na wewe rudi nyumbani TZ, ukalime mihogo, na sio kuwakatalia vijana wa sasa.
Hiyo paragraph ulioiandika ni sawa katika nchi zote unapotaka uraia wao ikiwemo Tanzania pia. Hivyo isikustushe sana kwa kuwa wewe umeshakuwa mzee sasa.
Mwisho usinielewe vibaya mchango wako ninauheshimu wakati wa ujana wako ila tupe mda sisi pia kutoa mchango wetu.
Linganisha hizi oath of Allegiance za USA na TZ halafu ona profesa Mbele alivyokuwa hajui mambo, maana zote zinafanana:
ReplyDeleteOath of Allegiance U.S.A
To become a citizen, one must take the oath of allegiance. By doing so, an applicant swears to:
• support the Constitution and obey the laws of the United States;
• renounce any foreign allegiance and/or foreign title;
• bear arms for the Armed Forces of the United States or perform services for the government of the United States when required.
Source: U.S. Citizenship and Immigration Services, Department of Homeland Security
Oath of Allegiance TZ
. I, .................................... do swear that, I will be faithful and bear true allegiance to the United Republic and that I will preserve, protect and defend the Constitution of the United Republic, as by law established. So help me God
. Where under any provision of this Act a person is required to renounce the nationality or citizenship of any country other than the United Republic and the law of that other country makes no provision for the renunciation of nationality or citizenship.
. Any naturalized citizen will be deprived of citizenship if during any war in which the United Republic was engaged, unlawfully traded or communicated with any enemy or been engaged in or associated with any business that was to his known ledge carried on in such a manner as to assist an enemy in that war.
Souce: Tanzania Citizenship Act, 1995
Profesa mbele fanya research kwanza katika mambo usiyoyajua kabla hujayarukia.
wewe unayejiita Msemakweli watu hawasomi ili waje kuajiriwa tuu, vijana tunatakiwa tusome ili kuja kutengeneza ajira. Hizo akili "zezeta" za kutegemewa kuajiriwa peke hazitatupeleka mahali popote na bwana Mbele alichokisema ni kutahadhalisha tuu kwamba tusifanye mambo kwa kuangalia faida utakazozipata ukiwa na uraia wa nchi mbili, pasipo kuangalia athali zinazoweza kusababishwa kwa taifa na vizazi vijavyo.
ReplyDeletewewe Msemakweli; jifunze kukosoa hoja na wala siyo "personality". Umeongea "ubwabwa" mrefu bila ya kukosoa hoja yoyote ya bwana Mbele na wala hujapendekeza "solution" yoyote ya hoja ungependa kuikosoa.
ReplyDeleteDONT KID US!!!! WATANZANIA IN THE DIASPORA... TRUST ME..YOU WILL BE DISAPPOINTED OUR COUNTRY IS NOT READY FOR US. THERE ARE NO MECHANISMS OR SYSTEMS IN PLACE TO ASSIST OR ENSURE OUR SUCCESS...ESPECIALLY THE MINDSET YA WATZ IT STINKS...THEY ARE CRAB MINDED THEY DO NOT WALK THE TALK...IMEKUWA WIMBO SASA KUWA WATU WA DIASPORA TWENDE NYUMBANI KU-INVEST UKIFIKA UNAJUTA KUZALIWA BONGO...WANATUDANGANYA NI SIASA WANATAFUTA KUCHAGULIWA TENA HII 2010. TUPO WENGI HADI SASA TUNAYUMBISHWA HUKO KUWEKA INVESTMENT ...WANAKARIBISHA VIZURI WAGENI (WEUPE) KULIKO SIE.... KAMA MTZ ULIE KWENYE DIASPORA UNAWEZA INVEST ULIPO SIYO BONGO....TANZANIA NCHI YA WENYEWE SIYO WAZAWA! AJE APINGE ANAYEJIFANYA KASAIDIWA NA SERIKALI, FAMILIA, UKOO, MTANZANIA MWEUSI KAMA MIE...HAKUNA. WACHENI POROJO WAHESHIMIWA. NEFERTITI.
ReplyDeleteNimesoma mada zote na utaona jinsi gani watu wanavyoandika pumba.
ReplyDeleteKuwa na urai wa nchi mbili sio jambo baya na wala watu wasiogope wazungu kuchukua urai wa Tanzania kwani serikali ikiweka sheria za maana kutakuwa hakuna mwanya hata kidogo wa watu wengine kupata urai wa Tanzania.
naomba watu wachunguze Japan na Germany wanafanya nini mpaka uwe raia.Sio raisi kama watu wanavyofikiria kuna vitu vingi unatakiwa upitie mpaka upate urai kamili wa nchi hizo na pili kama sio mzaliwa wa pale uwezi kuwa na haki sawa na mzawa.
Fanyeni uchunguzi wa kutosha na angalieni ni nini faida na nini hasara zake.Kwani mpaka sasa nchi karibu zote Afrka zinakubali Dual Citizenship imebakia Tanzania na nchi chache sana (may be 15%).
Mjusi