Fundi rangi Bakari Yusufu akimalizia jana kupaka rangi jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya Viziwi Buguruni jijini Dar leo linalokarabatiwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa. Mhandisi Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kulia) akimwelekeza fundi Umeme Imma Maembe jinsi ya kuweka taa katika moja ya vyumba vya madarasa vya Shule ya Viziwi ya Buguruni jijini Dar ldo inayokarabatiwa kwa msaada wa TBL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kinyasi NicholausJanuary 28, 2010

    duh! hiyo picha imenikumbusha mbali. nilisoma hapo kati ta mwaka 94 na 2001. ilikuwa shule bomba enzi zile za miaka ya 90 kurudi nyuma. ilikuwa na mahusiano mazuri na shule za uk, ikiwepo exchange program ya kial mwaka. kabla ya kuja kuvurugwa na ufiadi Headmaster Mnyakusa mwenye Kipara. jamaa aliuza school buses mbili, pick up moja pamoja na kuifisidi misaada ya iliyokuwa inaletwa na wafadhili hasa Waingereza. hadi kupelekea kuwaudhi na kusababisha wakatye misaada yote ikiwemo ilie program kutembeleana shule za uingereza. enzi hizo ilikuwa mojan kati ya shule za kisasa jijini Dar kuanzia majengo hadi mazingira ikiwemo football ground ya kiwango cha juu.
    thanks TBL kwa kuikumbuka shule yangu ya zamani. nami now nipo California, USA naangalia uwezekano wa kufanya something kama shukrani kwa hiyo shule kwa kunifikisha hadi hapa nilipo.

    Mdau Kinyasi

    ReplyDelete
  2. neno kiziwi linakubalika kweli?? watu wa kiswahili watusaidie

    ReplyDelete
  3. Nadhani linaweza kukubalika, na nadhani ukisema shule ya wenye mtindio wa kusikia sijui kama ni kiswahili sahihi.
    Mdau wa US ni kweli taasisi nyingi zinapata wafadhili lakini sababu yaa uroho wa Tanzania wenzetu wanatumia mwanya kujisaidia wao na familia zao

    ReplyDelete
  4. Hongera TBL, Huu ni mfano mzuri sana. Kama kila kampuni ingefanya hivyo tunge kuwa mbali sana. Na dhani gharama haikufikia hata million 10. Asante TBL. Hii ni changamoto kwa kampuni zingine.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza nakubaliana na wewe shule ilikuwa inapata sana misaada na wanafunzi wote walikuwa wakipata opportunities za kwenda majuu nmikumi trip na beach. Kuna mama mmoja alikuwa anairan vizuri sana huko nyuma kama mwenyekiti. Gone are the days!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...