Wengine katika picha ni Balozi wa Haiti Leo Merores mwenye riboni ya njano, ambaye alisema licha ya majaribu yote hayo, Haiti haita kufa, Haiti itazaliwa upya. Mwingine katika picha ni Naibu Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Balozi wa Kazakastan Bibi Byrganyan Aitimova mwenye ua jekundu na Mke wa Katibu Mkuu, Bibi Yoo Ban.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki la Familia Takatifu lilipo karibu na Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York na kuongozwa na Mwakilishi wa Baba Mtakatifu katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Askofu Mkuu Celestino Migliore (hayuko pichani).
Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu Migliore alisema majanga kama hayo ya tetemeko la ardhi ambayo hayana maelezo yanapaswa kuchukuliwa na wanadamu kama sehemu ya kujikumbusha uhusiano kati yao na Muumba wao, na kusisitiza kuwa maswali ya kwa nini tetemeko hilo limetokea na kama Mwenyezi Mungu yupo au hayupo na kama yupo kwa nini anaacha watu wake wateseke. Amesema maswali hayo na mengine ambayo mwanadamu kwa hulka yake hujiuliza anapopatwa na majanga, kwa kweli hayana majibu.
Kwa upande wake Mh. Ban Ki Moon alisema licha ya mtikisiko na madhara makubwa yaliyowapata wananchi wa Haiti, wananchi hao wameonyesha uvumilivu wa hali ya juu huku wakiendelea kudumu katika imani jambo alilosema ni la kupongezwa na kushukuru na kwamba Umoja wa mataifa kwa kushirikiana na jumuia ya kimataifa itaisaidia Haiti kwa hali na mali ili iweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Umoja wa Mataifa ,wafanyakazi wa UN na vyombo vya habari .

Picha na Maelezo kwa Hisani ya
Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa
Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa
yasemekana kuwa baada ya wafaransa kuondoka walitega bom aina ya 34rtty ambaro lilikaa miaka 50 chini ya ardhi ili jamaa wafe wote ,kuna watu wanasema kuwa haiti ina mafuta mazuri kuliko ilaki na wanasema baada ya mambo yote wamalekani watapigania hiyo sehem na wafaransa
ReplyDelete