Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Huyu Mzee Porojo tu!

    ReplyDelete
  2. Hasikiki vizuri. Wawekee wadau hii

    ====
    Kamanda kova akionyesha moja ya vitu alivyokutwa navyo Jerry Muro.


    Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Afande Suleiman Kova leo ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa juu ya sakata la mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC) juu ya madai ya kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Bw. Michael Carlos aliyekuwa mhasibu wa Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo kabla ya kutemeshwa mzigo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivi karibuni.
    Afande Kova akizungumzia sakata hilo amesema Bwana Michael Carlos alitoa taarifa polisi akidai kuna watu wanamsumbua sana na kumtisha wakidai awape shilingi milioni 10 kabla ya kuibua kashfa zake kwenye vyombo vya habari, hivyo Afande Kova aliwaamuru vijana wake kufuatilia tukio hilo katika mgahawa wa City Garden jijini Dar es Salaam na kuikuta gari ikiwa imeegeshwa , ilibidi Michael awasiliane na huyo mtu ili waingie hapo hotelini hata hivyo huyo mtu huyo alikataa na hivyo wakamfuata kwenye gari lake na kukuta Ni Bw. Jerry Muro mwandishi wa TBC.
    Anasema walimchukua mpaka kituo cha polisi na kuchukua maelezo ya bwana Michael ambaye alisema anamfahamu Jerry Muro kwani wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini, pia akadai kwamba kuna miwani yake aliisahau kwenye gari ya Jerry Murro na pia kuna pingu na Silaha yaani bastola ambvyo mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia kumtishia ili atoe hizo fedha.
    Hata hivyo afande Sulaiman Kova hakuthibitisha kwamba Jerry Murro amekamatwa na hizo shilingi milioni 10, lakini amesema kujipati fedha au kumdai fedha mtu yeyote kwa kumtishia ni kosa la jinai, hivyo kutokana na mazingira ya maelezo ya mlalamikaji na vielelezo vinatufanya kuamini kwamba tukio hilo lilikuwepo, ameongeza kuwa hawakuweza kuwashirikisha (PCCB) Kikosi cha kuzuia Rushwa katika mtego huo kwakuwa muda ulikuwa ni mdogo na mtuhumiwa angeweza kukimbia na kuwapotea
    Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro Afande Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Repumlic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria
    Ameongeza kwamba Kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali.

    ReplyDelete
  3. Jamani tuache ushabiki, Tanzania ni nchi ya rushwa na watu wanaona kula rushwa ni ujanja. Hakuna haja ya kumtetea Muro eti kwa sababu aliwaumbua polisi. Upo uwezekano kwamba ametenda kosa hivyo hivyo kama tunavyotaka kuhisi kwamba hakutenda. Hatuwezi kuamua kitu ambacho hatukukiona. Waandishi ni wala rushwa na mimi mwenye nimeshuhudia hii kitu mara kadhaa ila wahusika hawakuwa tayari kutoa ushirikiano ili mwandishi husika atiwe nguvuni. Waandishi wote walioko hapo wanajua fika kwamba rushwa inaliwa sana, wasijitie kinamna hapo, kuna tatizo kwa waandishi.

    ReplyDelete
  4. Bongo ki-mafia mafia,ukiingia anga za ulaji wa watu wanakupakazia kesi unafungwa or worse wanakuondoa kabisa.
    Kwa mtindo huu Maendeleo yoyote Bongo ni ndoto, YES NDOTO.

    ReplyDelete
  5. KINACHOONEKANA POLISI WANATUMIA NAFASI YAO KUMKOMOA MWANDISHI WA HABARI HILI NI JAMBO BAYA . NAOMBA POLISI WA TANZANIA MJIREKEBISHE

    ReplyDelete
  6. MI NAOMBA MNIWEKE SAWA..PESA KACHUKUA HAJACHUKUA,???MBONA KIZUNGULUMKUTI??ISHU YA KUWA ANAMILIKI KIDITOPILE CHENYE UWEZO WAKUBEBA RISASI KUMI.. JAMANI HII NAYO ILI IWEJE???AU NDIO MNAWAWEKA ATTENTION MAADUI SIKU YAKUMVAMIA WAANZIE WAPI,??KAMA KOSA LIPO KUWENI DIRECT...NA SHERIA ICHUKUWE MKONDOWAKE....
    mdau mitaa yakati

    ReplyDelete
  7. Hii yote ni spinning ya polisi lakini hii imethibitisha kuwa hawana elimu hata kama ni kumbambikia mtu kesi huwezi kufaya hivyo.

    ReplyDelete
  8. Mmmh! Naona maelezo ya kamanda Kova na Carols yanajichanganya kiasi cha kunifanya nisiyakubali moja kwa moja.Taarifa za awali jerry anadai kupigiwa simu na watu kuwa kuna kazi, na alipofika eneo la kazi anakamatwa na kupelekwa kituoni. Haya wadau tazama maelezo haya ya kova "Afande Kova akizungumzia sakata hilo amesema Bwana Michael Carlos alitoa taarifa polisi akidai kuna watu wanamsumbua sana na kumtisha wakidai awape shilingi milioni 10 kabla ya kuibua kashfa zake kwenye vyombo vya habari" Picha inayojionyesha hapa inakuwa kama Bwana carols hakujua ni watu gani na alikuwa akiwasiliana nao kwenye simu tu.Angalia hii statement pia ilibidi Michael awasiliane na huyo mtu ili waingie hapo hotelini hata hivyo huyo mtu huyo alikataa na hivyo wakamfuata kwenye gari lake na kukuta Ni Bw. Jerry Muro mwandishi wa TBC." Yaani hapa inaonekani walipofika kwenye gari ndo wakajua ni jerry Muro. Utata unakuja pale bwana carlos kukili kumfahamu jerry Muro na isitoshe inaonekana alitumia pia hata pingu kumfunga ili asimtoreke kabla ya kukubaliana. Kwa bwana Carlos Jerry Muro si mgeni kwake kitendo cha yeye kumtolea pingu na siraha lilikuwa ni kosa tosha na kwa ujumla asingekubaliana naye. Iweje mtu unayemfahamu leo akusumbue? Kwa ujumla kama wenzetu wa kamuni za simu wana records nzuri naamini watasaidia kutoa ukweli hasa mawasiliano kati ya hawa wawili. kwa ujumla kila kitu huwa kinatunzwa wafuate utaratibu tu na wapate mawasiliano kati ya hawa wawili. kujilidhisha kutoka upande mmoja na kwa ushahidi huo Kamanda Kova hapo utakuwa unachemka fanya mambo kama mtaalamu wa taaluma hiyo na haki itendeke. Kwa kuwa ni rahisi sana kuhusisha tukio hili na kisasi cha tuhuma za rushwa. kitendo cha kutowashirikisha PCCB kwa wakati ni kosa, kisingizio cha muda hakitoshi PCCB wako tayari masaa 24.
    Fanyeni vitu kwa umakini msije mkaharibu sifa za serikali yetu, na ukizingatia wote nyie ni watumishi wa umma tene vyombo nyeti na muna maadili yenu ya kazi. Hebu fanyeni kazi kila mtu kwa nafasi yake na jamii iondoe mashaka.

    ReplyDelete
  9. WELL HII NI PAY BACK YA WAZI NI KUTAKA KUMNYAMAZISHA MURRO KWANI AMEGUSA ANGA ZA WATU NA HAYA YOTE NI KUTAKA KUMYAMAZISHA ILA AWE MAKINI SANA KWANI KESI HII NI YA KITOTO NA HAINA MISINGI ATASHINDA INAONEKANA WAZI NI YA KUPANDIKIZA HAIFIKI POPOTE KWANI HAKUNA USHAHIDI WOWOTE WA MSINGI. ILA UJEMBE KWAKE NI KWAMBA AWE MAKINI KWANI WAHENGA WALISEMA "NCHA YA MKUKI HAIPIGWI KONZI" RUSHWA KWA NCHI KAMA TANZANIA IMEKITA MIZIZI NA WANANCHI WANAONA KWAMBA NI KITU CHA KAWAIDA KWANI INAOKOA MUDA BADALA YA KUPELEKWA KITUONI (MAHAKAMANI)KULIPA FAINI YA SHILINGI ELFU ISHIRINI UNAONA BORA ULIPE SHILINGI ELFU KUMI HAPO UNAENDELEA NA SAFARI NA SHUGHULI ZAKO KAMA KAWAIDA. TATIZO LA RUSHWA NDIO HILO KAMA NCHI INATAKA KULIFANYIA KAZI SIO KWA MPOKEA RUSHWA TU BALI KUMWELIMISHA MTOA RUSHWA PIA AMBAYE NI MWANANCHI ANAYETAKA HUDUMA KWA NJIA YA MKATO.
    BWANA MURO HII KESI NI CHA MTOTO ILA JOTO YA JIWE ATAIONA KWA SIKU MBILI TATU HIZI NA MAMBO YATAPOA MUDA SIO MREFU. LAKINI HUO NDO KUKOMAA KIUME HII DUNIA BABU!
    MDAU WA DAMU USA.

    ReplyDelete
  10. Eti "KIDITOPILE" hahahahhha we jamaa noma!!

    ReplyDelete
  11. KWELI MIPOLISI YA TANZANIA HAINA HATA ELIMU,A)INAONEKANANI MPANGO TOSHA KWA NINI TENA KOVA AANDAE PRESS CONFRESS KWA AJILI YA RUSHWA YA MWANDISHI WA KAWAIDA?WAKATI RUSHWA NA UFISADI KIBAO UPO BUNGENI HUKO HAKUNA PRESS CONFRESS,B) HUYO MZEE ALODAI JERRY ANAMDAI RUSHWA NA KUMUONESHA PINGU JE HAJUI YEYE KAMA JERRY NI MUANDISHI NA SIO TAASISI YA RUSHWA WALA POLISI HUU SI UONGO HUU? C)HUYU KOVA ANAJICHANGANYA MWENYEWE NA KOSA LA RUSHWA LISHAKUA LA JINAI LEO WAKATI KUNA CIVILIAN CASE NA CRIMINAL CASE SASA HAPO LIMEINGIA VIPI KATIKA CRIMINAL WAKATI HAKUNA NGUVU ILIYOTUMIKIA AU SHERIA YA TZ INASEMA HIVYO.AIBU YA NANI ..APO VIPI?

    ReplyDelete
  12. AFANDE KOVE HII ITAKUTOKEA PUANI!!!!!!!! KUVALIA NJUNGA MAMBO MADOGO SUBURI UONE ULIVYOCHEMSHA.

    ReplyDelete
  13. Kwa maelezo ya Afande na mlalamikaji, hii ni wazi hakuna kesi hapo.

    Pengine hata picha zilizotegeshwa siku za nyuma zitaonyesha wakiwa katika mazungumzo n.k na pengine kupeana mikono na nyaraka n.k lakini haitakuwa clear kuonyesha mtu akitishia mwenzake kwa bastola wala kupokea rushwa.

    Wanaweza kumng'ang'ania juu ya pingu ambazo nadhani alitupiwa humo ndani ya gari na tusiyemjua.

    Vinginevyo watamwachia Jerry Muro kwa FUNZO LA MWAKA kuwa:
    Taarifa zake alizozitoa juu ya wale Maaskari wa Trafiki nazo zilikuwa kama hivyo tu za kimazingira (not clear beyond reasonable doubt) kuwa walikuwa wanapokea rushwa na siyo nakala ya kadi ya gari au leseni n.k

    Unajua binadamu huweza kutumia njia nyingi kukufunza na si lazima uwekwe darasani.

    All in all, kama tasnifu yangu ni sahihi; bado nasikitika sana kuwa vita dhidi ya rushwa ni ngumu kuliko tunavyofikiri maana bado hatujakubali kuwa ipo na watu wetu au sisi tunahusika kuomba au kutoa rushwa.

    Yaani kama kampeni ya kupima HIV ilivyokuwa pengine inabidi Rais (akiwa na ulinzi wake) angie katika gari lenye mizigo kimya kimya saa za jioni na kushuhudia mwenyewe askari trafiki akiomba au kupewa rushwa kisha baadaye atangaze mwenyewe adharani.


    Waziri Mkuu aungane na mfanya biashara fulani mwenye skandali kuweka mtego kwa mwanahabari kudilute habari kwa mshiko wa nguvu na ndipo na yeye mwenyewe atangaze hadharani aliyoyaona.


    Kisha Rais wa Zanzibar ajibanze kwenye baa jioni wakati wa kampeni za uchaguzi aone wagombea wanavyotoa hongo ya kilaji kwa wananchi na Mawaziri wote waweke mitego kama hiyo wenyewe kutafuta ardhi, kutibiwa mahospitalini, kulipa kodi kubwa TRA, kutafuta ajira, kuomba nafasi za scholarship, harakati za kujinasua katika kesi kwa Mahakimu n.k

    Halafu kila mmoja aripoti katika kipindi maalumu mwenyewe live kupitia TV alichoona na kusikia na wahusika wachukuliwe hatua kali mahakamani pengine ndio tutajua mtapakao na kiwango cha uambukizo wa mlipuko huu wa rushwa nchini mwetu!

    ReplyDelete
  14. Mazungumzo kati ya Muro na huyo Mtoa Rushwa yanaweza kuwekwa wazi katika vyombo vya habari kwa kushirikiana na mtandao wa simu anaoutumia Muro! Ni rahisi sana, kama mnataka msaada nioneni! Then ushahidi unaweza kuwekwa wazi kama alikuwa na nia ya kuchukua Rushwa ama la?

    ReplyDelete
  15. Anony wa Tarehe Mon Feb 01, 05:04:00 PM,
    You must be genius
    Waandishi woote wanatetea rushwa
    Nchi inanuka na friends wanateteana
    Hata mawaziri wanateteana
    So kamata hao wooooooooote
    Weka mitego kibaaaaaaaaoo
    Funga vibaka hao

    ReplyDelete
  16. Hivi kweli Jerry ni mjanja kuliko jeshi zima la polisi, ikiwa jeshi la polisi lilipokea malalamiko toka kwamlalamikaji, je limeshidwa kutumia njia za kumnasa na vidhibitisho au kwa kumtumia mlalamikaji ili kurahisisha njia za upatikanaji wa vithibitisho?vya kesi hiyo,je ni muda gani mlalamikaji alitoa taarifa polisi ?ni vipi polisi walishindwa kumtia mkononi mtuhumiwa?, inaelekea jeshi letu la polisi kanda husika imeshindwa kuonyesha ukomavu wa mafunzo ya medani za kipolisi ya jinsi ya kuwanasa watuhumiwa wa aina hiyo na kama hiyo sio kazi ya polisi iweje polisi kulishughulikia na suala hilo badala ya kulipeleka kwa wahusika?Tunaomba haki itendeke kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuingilia kati suala hilo na kumfikisha mtuhumiwa haraka mahakamani, na pindi ikibainika kuwa mtuhumiwa ana makosa tunaomba ADHABU KALI ZICHUKULIWE ZIDI YAKE ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
    "SHERIA NI HAKI NA HAKI NI SHERIA"

    ReplyDelete
  17. 1.POLISI
    2.JESHI
    3.VIONGOZI

    WEZI,MATAPELI,WAUWAJI,WABINAFSI,MAFISADI, NCHI IMEOZA, INANUKA RUSHA, UTAPELI, WIZI, UJAMBAZI, MAGONJWA, NGONO, KILA AINA YA BALAA LINAPATIKANA HUKO

    FEZEHA,AIBU,MACHUNGU,BALAA,SIMANZI,

    KAENI MKIJUWA KILA GOTI LITAPIGWA SIKU HIYO IKIFIKA UNYANYASAJI KWA WALIO WANYONGE KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI


    KUNYIMWA HAKI KWA WALIO NA HAKI NA KUWAPA HAKI WASIO NA HAKI

    KAENI MKIJUWA HAKUNA LISILO NA MWANZO LIKAKOSA MWISHO WAKE

    SIKU MOJA YOTE HAYO YATAISHA WANANCHI WATAKAPOCHOKA NA KUAMUA KUINGIA POLINI

    TUTAUWANA KAMA KUKU KUSHINDA HATA HUKO BURUNDI NA RWANDA NCHI TUTAIWACHA TUPU

    WATAKUJA WENGINE KUJA KUISHI TUTAHAKIKISHA TUNAMALIZANA ALAFU WATAKAOKUJA WATAISHI KWA FURAHA NA UPENDO


    MUNGU TUNAKUOMBA PITISHA MIUJIZA YAKO ANGUSHA MTIKISIKO WA ARDHI UWAKUMBE HAWA MAFISADI

    PITISHA MYIKISIKO KWENYE NYUMBA ZA MAFISADI MAJAMBAZI WANAJESHI NA HAWA MAPOLIS WOTE WALIO NA UNYANYASAJI NA UONEVU KWA RAIA.......AMEEN AMEEN AMEEN.

    TUMUOMBE MUNGU KWA PAMOJA ILI TUFANIKIWE KWANI NJIA ILIYOBAKI NI HIYO TU

    HAWA JAMAA WAMESHIKA KWENYE MPINI WAMETUACHIA KWENYE MAKALI ILIYOBAKI KUWAOMBEA GOD AWAANGAMIZE.......

    ankal fikisha machungu yangu.

    ReplyDelete
  18. jamani hv kweli tutafika kama kamanda wa kova anaongea kishabiki jambo ambalao bado halijathibitishwa anaonekana kabisa ana side na upande mmoja kabisa, hii ni ishu inamhusu jerry muro ambaye ni mtu maarufu kimsingi sasa je fikiria ikitokea kwa mtu ambaye hana umaarufu wowote na hana access na vyombo vya habari si atafungwa mapema kabla hata ya upelelezi. jeshi kimsingi limechemsha sana tena sana na hiyo ndio tabia yao, muro mungu yupo nawe bro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...