Poems written by WIFE and HUSBAND.

WIFE:
I wrote your name on sand it got washed.
I wrote your name in air, it was blown away.
Then I wrote your name on my heart & I got Heart Attack.

HUSBAND:
God saw me hungry, he created pizza.
He saw me thirsty, he created Pepsi.
He saw me in dark, he created light.
He saw me without problems, he created YOU.

WIFE:
Twinkle twinkle little star
You should know what you are
And once you know what you are
Mental hospital is not so far.

HUSBAND:
The rain makes all things beautiful.
The grass and flowers too.
If rain makes all things beautiful
Why doesn't it rain on you?

WIFE:
Roses are red; Violets are blue
Monkeys like u should be kept in zoo.
Don't feel so angry you will find me there too
Not in cage but laughing at you

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mume amchinja mke kikatili Dar
    Na Richard Makore

    18th February 2010B-

    Kisa ugomvi wa kuuza nyumba


    Mwanaume mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Matiko Ng'eng'e (55), amemuua mkewe, Rehema Matiko (40), kwa kumchoma na visu katika sehemu kadhaa za mwili.

    Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:00 alfajiri jana katika eneo la Ukonga Machinjioni, jijini Dar es Salaam.

    Gazeti hili lilifika eneo la tukio na kushuhudia wanandugu hao wakiwa wanahangaika na kufuta damu zilizokuwa zimetapakaa chumbani hadi sebuleni.

    Nipashe lilifanikiwa kuzungumza na mtoto wa kwanza wa Matiko, Joyce Matiko (22), ambaye alisema kuwa baba yake ana wake wawili ambapo mke mkubwa amezaa naye watoto saba na marehemu mama yake alikuwa na watoto watano.

    Alisema kuwa baba yao wiki moja iliyopita alikuwa kwa mke mkubwa eneo la Ukonga Mombasa, ila alifika juzi usiku wa majira ya saa 4:00 na kuwaita watoto na mama yao na kuwaeleza kuwa hana mipango yoyote ya kuuza nyumba yao hata kama yeye atakufa kwani ni urithi wa watoto. Alisema kuwa alipomaliza kuzungumza hayo, watoto wote walinyanyuka na kwenda kulala ila wazazi wao walibaki sebuleni wakiongea. Joyce alisimulia kuwa awali wazazi wake walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara uliohusu uuzaji wa nyumba hiyo, baada ya marehemu mama yake kupata taarifa kuwa baba yao alikuwa akifanya mawasiliano na madalali kuiuza nyumba hiyo. Hata hivyo, alisema ukiachilia mbali mgogoro huo, baba yake alitaka kuchukua cheti cha mdogo wake ambaye anaitwa Vitus Matiko ambaye amemaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu ambaye alifaulu na kutaka kukipeleka kwa mtoto wa mke mkubwa ambaye alifeli masomo yake.

    Alisema kitendo hicho kilimkasirisha marehemu mama yake.

    Joyce alisema mama yake alimgusia baba suala la kutaka kuchukua cheti kwa kumweleza kuwa halitawezekana pamoja na kuuzwa kwa nyumba labda kama hatakuwepo duniani. Aliongeza kuwa baada ya mama yake kuongea maneno hayo, baba ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Polisi akiwa na cheo cha Sajenti, alikana kitendo cha kutaka kuuza nyumba hiyo na ndipo walipoondoka kwenda kulala. Kwa mujibu wa Joyce, ilipofika majira ya saa 9:25 usiku alisikia kelele kutoka kwa mama yake akiwa anaomba msaada na ndipo alipotoka haraka chumbani na kutaka kufungua mlango, lakini akakuta umefungwa. Alisema mama yake aliendelea kupiga kelele, lakini ilishindikana kumsaidia kwa kuwa baba alikataa kufungua mlango na kwamba madirisha yalizibwa kwa vitamba ili watu wasichungulie.

    Alisema mama yake alichomwa visu vitano na kwamba alianza kuchomwa sehemu ya moyo, shingoni na maeneo ya tumboni na kuwa damu nyingi zilitoka na hatimaye kukosa nguvu.

    Binti huyo alisimulia kuwa baada ya baba kukataa kufungua mlango, watoto walipiga makelele na ndipo majirani walipotoka nje na wengine kukimbilia polisi.

    Alisema polisi walifika katika eneo hilo na kumkuta baba yao akiwa chumbani kwake pamoja na maiti ya mama yao ikiwa imelala huku damu zikiwa zinaendelea kutoka.

    Joyce alisema kuwa chanzo kikuu cha mgogoro huo ni taasisi moja kumshawishi baba yao kuwauzia eneo hilo na nyumba ili iendeleze shughuli zake. Alisema taarifa walizozipata ni kwamba taasisi hiyo ilitaka kutoa kiasi cha Sh. milioni 30 ili baba yao aiondoe familia yake.

    Mtoto huyo alieleza kuwa baba yake amekuwa akishawishiwa mara kwa mara ili auze eneo hilo na kwamba kuna wakati aliilazimisha familia kuondoka kwenda kijijini ili apate nafasi ya kuliuza, lakini waligoma baada ya kubaini mipango hiyo. Baadhi ya majirani waliofika katika eneo la tukio walionekana kujawa na huzuni kutokana na tukio hilo la kinyama na kumsikitikia marehemu ambaye anaelezwa kuwa alikuwa akiishi vizuri na watu.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.

    Alisema kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo amepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya kuchunguzwa.

    ReplyDelete
  2. The effort is appreciated there, however...keep working on your craft. Poems don't always have to rhyme, but there has to be a flow somehow or some sort of rythm (if you will) The message should also make sense.

    The best way to improve is by reading others' art and keep on writing your own. Let others read and critique your work, and re-edit.

    Keep it up....just a friendly criticism.

    ReplyDelete
  3. duh hii poem imetulia ila inaonekana jamaa wamechokana maana la sivyo hamuwezi tumiana msg za namna nii. Lakini pia kama mmepata muda

    ReplyDelete
  4. wewe Abdlhaqq hiyo poem mtu kaitoa internet kaituma kwa michuzi au unafikiri michuzi ndo kaandika.. by the way it's a collection of some seriously daaamn good poems I laughed like crazy when I was reading..

    ReplyDelete
  5. ukisikia vijembe vya kizungu ndo hivyo. Hapo hakuna tena malavi davi kinachofuata ni talaka tatu.

    ReplyDelete
  6. Wanagombana mchana usiku wanapatana! Tena ugomvi wa maneno ya hivyo wala usiingilie utakuja kupata lawama bure, kumbukeni wimbo huu

    "Wanapogombana ooh ooh mtu na mke wake ndani ya nyumba usiingilie kati kabisa ugomvi wao.
    Utakuja pata baa wee kijana
    lakusingiziwa mengi na isitoshe,
    .............mwisho wake utapata lawam"

    Labda kama ugomvi wenyewe ni wa kuterana mapanga kama wa kina Matiku. Ila huyo mwanaume naye mjinga sasa mke amekosa na 100m amekosa. Faida yake nini?

    Kula pesa za mwanamke ni rahisi sana lakini sio kwa kutumia maguvu/mabavu, tumieni nyama za ulimi mtafaidi. Hivi hapo angemwambia katika milioni 100 nitakayopata kwa kumuuzia Mchina hili shamba, wewe nitakupa 50m, mimi nitachukua 50m angepata hasara gani? Maana hata kama mke angeenda kununua shamba lingine akajenga nyumba nyingine bado ingekuwa ni matrimonial property. Ila Mura tamaa ilimponza vyote kakosa!

    Bi Mkora

    ReplyDelete
  7. what! mume kaua mke kikatili namna hiyo?!!! akafie jela shetani mkubwa! mungu aipokee roho ya marehemu na awape faraja watoto, jamani duniani hapa kuna watu wakatili kuzidi hata shetani! kha!

    ReplyDelete
  8. Japo najua kuwa ni dhihaka, sikulipenda shairi hili limeifanya ndoa kuwa ni kitu kibaya wakati si haki kufikiri kuwa ndoa ni kitu kibaya. Inafurahiusha moyo kujua kuwa una muenzi na sisemi kama mtu aliyeingia ndoani leo au jana hasha ni mtu wa siku nyingi, kuna machungu na matamu katika ndoa, lakini mkivumilia matamu yanazidi machungu.

    Kazaneni ( jitahidini) ndigu zangu.

    ReplyDelete
  9. Nimemaanisha quality kwenye komenti yangu. Na mkusudiwa ni mwandishi wa hilo shairi. Inaonekana alikuwa anajitahidi kuweka balance kati ya rhyme na kuchekesha, lakini bahati mbaya ukilazimisha sana maneno ku-rhyme, inakuwa ngumu kufanya sentenso kubeba maana unayotaka (if your vocabulary is limited).

    Nia yangu sio kumshusha au kumtia aibu mwandishi, ila kutoa ushauri. Tafuta English Thesaurus...inasaidia.

    By the way: Najua sio Michuzi aliyeandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...