Kulikoni Mitandao ya Vyuo vikuu vya Nyumbani?
Wikiendi hii nilikuwa natafuta some info. about our Universities, lakini nilichokikuta ni maajabu.
1 - Design za tovuti za vyuo vikuu vingi vyao ni duni, na ziko very slow. - (ninatumia Pentium4, with T1 connection).
2 - Tovuti hazina info za kutosha, nyingine hazin info at all (university of dodoma)
3 - page ziko linked na pdf files....why??
4 - Rangi za tovuti hizi haziendani kabisa na tovuti za vyuo vikuu.
5 - Kuna tovuti moja imeorozesha majina ya wanafunzi ambao hawalipa school fees zao (No Privacy).
6 - Some links are dead....no link at all.
7 - Some websites are down (It only costs $4.00 to host simple websites)
- Hivi kweli mko sirias?? how much does it cost to design a website, kwa nini msiwapatie wanafunzi wadesign (najua watafanya kazi nzuri tu).
- Hivi mkihitaji msaada, ma-sponsor wataona kweli mko serious?
- Jamani inabidi muende na teknolojia, otherwise, tutaendelea kupitwa na nchi ndogondogo tu kama Rwanda.
www.suanet.ac.tz/
www.udom.ac.tz/ - This is the worst of all.
www.tumaini.ac.tz/ - Not too bad, but very slow.
http://www.aru.ac.tz/ - outdated © 2007, pdf links, Not updates info,
http://www.hkmu.ac.tz/ - Website is offline
http://www.imtu.edu/cn.htm - Very Fast, but outdated info
http://www.muccobs.ac.tz/ - Very Fast - Okay
http://www.mmu.ac.tz/ - scanned pictures, Fast, Good info. but poor arrangement.
http://www.muhas.ac.tz - very Good and fast, you will find all the info. you need.
http://www.mzumbe.ac.tz - very fast, okay designed, you will find all the info.
http://www.openuniversity.ac.tz/ - not good, ugly colors.
http://www.ruco.ac.tz - Very fast, ugly colors, good info., not too bad design-just bad colors.
http://www.saut.ac.tz/ - very fast, too many colors, not enough info..
http://196.46.110.169/buchs/home.php (Bugando University) - they are not serious at all.
http://mwuce.co.tz/ (Mwenge University) site not setup
http://www.sjut.ac.tz - (St. Johns) - not serious
http://www.suza.ac.tz/ (State University of Zanzibar) - Website down
http://www.udsm.ac.tz/index.php - Nice site although the front page is not very attractive.
http://www.ucc.co.tz/index.php - Very Nice - I believe wanafunzi wa hapa wangewatengenezea website zenu for free.....)
Haya ndiyo maoni yangu, ninajaribu kuisaidia nchi yangu.
Wikiendi hii nilikuwa natafuta some info. about our Universities, lakini nilichokikuta ni maajabu.
1 - Design za tovuti za vyuo vikuu vingi vyao ni duni, na ziko very slow. - (ninatumia Pentium4, with T1 connection).
2 - Tovuti hazina info za kutosha, nyingine hazin info at all (university of dodoma)
3 - page ziko linked na pdf files....why??
4 - Rangi za tovuti hizi haziendani kabisa na tovuti za vyuo vikuu.
5 - Kuna tovuti moja imeorozesha majina ya wanafunzi ambao hawalipa school fees zao (No Privacy).
6 - Some links are dead....no link at all.
7 - Some websites are down (It only costs $4.00 to host simple websites)
- Hivi kweli mko sirias?? how much does it cost to design a website, kwa nini msiwapatie wanafunzi wadesign (najua watafanya kazi nzuri tu).
- Hivi mkihitaji msaada, ma-sponsor wataona kweli mko serious?
- Jamani inabidi muende na teknolojia, otherwise, tutaendelea kupitwa na nchi ndogondogo tu kama Rwanda.
www.suanet.ac.tz/
www.udom.ac.tz/ - This is the worst of all.
www.tumaini.ac.tz/ - Not too bad, but very slow.
http://www.aru.ac.tz/ - outdated © 2007, pdf links, Not updates info,
http://www.hkmu.ac.tz/ - Website is offline
http://www.imtu.edu/cn.htm - Very Fast, but outdated info
http://www.muccobs.ac.tz/ - Very Fast - Okay
http://www.mmu.ac.tz/ - scanned pictures, Fast, Good info. but poor arrangement.
http://www.muhas.ac.tz - very Good and fast, you will find all the info. you need.
http://www.mzumbe.ac.tz - very fast, okay designed, you will find all the info.
http://www.openuniversity.ac.tz/ - not good, ugly colors.
http://www.ruco.ac.tz - Very fast, ugly colors, good info., not too bad design-just bad colors.
http://www.saut.ac.tz/ - very fast, too many colors, not enough info..
http://196.46.110.169/buchs/home.php (Bugando University) - they are not serious at all.
http://mwuce.co.tz/ (Mwenge University) site not setup
http://www.sjut.ac.tz - (St. Johns) - not serious
http://www.suza.ac.tz/ (State University of Zanzibar) - Website down
http://www.udsm.ac.tz/index.php - Nice site although the front page is not very attractive.
http://www.ucc.co.tz/index.php - Very Nice - I believe wanafunzi wa hapa wangewatengenezea website zenu for free.....)
Haya ndiyo maoni yangu, ninajaribu kuisaidia nchi yangu.
Ankal, chonde chonde Ankal!
naomba usinitoe jina langu yasije yakanikuta ya Muro.
Mi ninadhani Tanzania umuhimu wa website bado haujajulikana. People think website ni kama tangazo la biashara tu. It should be more than just a simple page. Kama mtu ni researcher wa Bugando Univ au Tumaini ukimpa business card yako mfadhili akija akapib website ya chuo akaona huo utumbo nadhani atakimbia tu.
ReplyDeleteTanzania kila kitu ni feki feki tu, ilimradi watu wamepewa pesa for poor results.
ReplyDeleteEmbu tembelea tovuti ya baadhi ya vyuo vya majirani wetu muone walivyokuwa siriazz.
University of Botswana:
http://www.ub.bw/
University of Namibia:
http://www.unam.na/
Kenyatta University:
http://www.ku.ac.ke/
Makerere University:
http://mak.ac.ug/
University of Rwanda:
http://www.nur.ac.rw/
Mdau hongera sana, tena sanaaa! atayekubishia atembelee hizo zoote then atapata jibu!
ReplyDeleteNgojeni niwaambie wale wataalamu wetu wa IT ni ovyo ovyo ovyoooooo, kwanza hawapo updated na wanachojua ni kuiba vifaa vya computer na kwenda kuuza mtaani, hebu tujiulizeni hawa watu wa IT wanalipwa ili wafanye nn??? maana wanalipwa kutoka katika kodi zetu, wanatuangusha sanaaaaaa! Hawana uchungu na nchi yao, wapo wapo tuuu na wengi wao utajiuliza huyu mtu aliajiriwa kwa vigezo gani?? maana anajua kuistall na unstall antivirus, ukimpa komputer mbovu yeye ndio anaimalizia kuiua maana hawezi kukwambia hajui kitu! Shida sana na wanakera sana!! ni wababaishaji sanaaaa!
Ambacho huwa kinaniudhi kuhusu vyoote ni kuwa hakuna info kuhusu quality za walimu wao.
ReplyDeleteKuna watu wanasema kuna vyuo havina walimu kabisa wanafundishwa na ma-ta tuu na vingine vinajiendesha kama twisheni.
vipi mtu atachagua chuo bora kwa elimu ikiwa walimu hawajulikani uwezo wao?
Kwa wale waafrika wanaoipenda Afrika lakini wamechoshwa na utendaji wa serikali na wanasiasa wa afrika, Rwanda inatupa matumaini sana ya kurudi Afrika. Nikimaliza phD yangu tuu, nitaomba kazi ya kufundisha Rwanda.
ReplyDeleteHongera Kagame, kazi yako inaonekana.
NI kweli kabisa chuo kama hiki Zanzibar university kwa miezi kadhaaa website yao haifanyi kazi.
ReplyDeletetizama umakini wa vyuo vya Uganda.ISLAMIC UNIVERSITY IN UGANDA.WWW.iuiu.ac.ug
Ahsante kwa hilo yani umenikuna kweli ndugu yangu. Hapo ujiulize hao wa it wanamalizaje degree hapo bila kugundua udhaifu wa website zao na walimu wa it wako wapi?
ReplyDeleteAu ndo watu wa it wako hapo wameajiriwa mfano hawapewi nafasi ya kunyesha ujuzi wao kazi kapewa mzabuni anajifanyia anchotaka mean ha-qualify.
"Mwisho mwandishi angalia yasijekukuta ya muro ukauziwa kesi umeiba nyaraka za chuo" just joke teh teh teh
ukistaajabu ya mussa, utaona ya firauni. Nyie mnashangaa vyuo vya tz, nani anaijua website ya IKULU? aibu ilioje ikulu ina kablog kachovu hata ka michuzi mukide.
ReplyDeleteMie simo
IKULU yenyewe haina hata website hivi unategemea hivyo vyuo viwe na website za maana? Watanzania hatuko serious kabisa na ndio maana siku zote tunaachwa nyuma. Uzembe, ugoigoi, ujinga, ufisadi na uzumbukuku umekithiri kupita kiasi nchini Tanzania. Makampuni kibao wana biashara lakini pia hawaoni umuhimu wa kujitangaza zaidi kupitia tovuti mbalimbali ili wajulikane zaidi. Kweli sisi ni BONGOLALA.
ReplyDeletecha kushangaza zaidi University of Dodoma,A) Hawajui maana ya INTERNET NA INTRANET,WAO WAMEWEKA MAJINA YA WANAFUNZI WASOLIPA HADHARANI,(wakati haya majina yanatakiwa wanafunzi tu wawe na access kama vyuo vya ulaya unakua Id yako ndio access ya kuingia INTRANET,(YAANI WEBSITE ZA NDANI TU NA SIO INTERNET AMBAZO NI WEBSITE ZA NJE.B)Kuna picha pale za viongozi kutembelea chuo,sasa viongozi walitembelea WANAFUNZI AU MAJENGO YA CHUO NA WALIMU?CHA KUSHANGAZA KUNA PICHA YA MWANAFUNZI MMOJA TU AMBAE KIKWETE ANAONGEA NAE,WALOBAKI NI MAWALIMU TU NA MASHEHA WA NYUMBA KUMI,SASA YALE MAELEZO KUWA ANAWAHUTUBIA WANAFUNZI YAFUTWE NA YAWEKWE ANAWAHUTUBIA WALIMU NA MAJENGO,(Inaonesha waliwafungia wanafunzi kwa kuwa wangetolewa aibu zao)MDAU ULOPITIA HII MADA UNAFANYA RESEARCH NINI,HONGERA SANA.NA NYIE WATU WA IT KASOMENI MAANA YAKE NA PRIVACY AS WELL.(Nuramo Umangaaniiii!!)
ReplyDeleteKilichoniacha hoi kwa mtoa mada ni kwamba amesifia tovuti ya UDSM ambayo ni moja kati ya tovuti chafu kiasi kwamba niliwahi kuwaandikia.
ReplyDeleteHata hivyo nakupongeza kwa kupoteza muda kuangalia haya madudu.
Tanzania kama taifa hatuna vision.
TAZARA website kaputi, TBC(Tanzania broadcasting Corp)?
ReplyDeleteBakhresa(Said Salim) company webusaiti ni mfano mzuri wa kampuni makini ya kuigwa.
Mdau hongera kwa research yako ya kina. Hili jambo linasikitisha kuona watu walivyokuwa na mawazo finyu.
ReplyDeleteKwa mtindo huu hivi inawekana vipi wanafunzi kusoma online, Je, tutafika kwenye karne ya ishirini na moja mwaka gani kwa mtindo huu?
Mimi napendekeza hii aibu iwekwe hadharani waziwazi kabisa kupitia kipindi cha televisheni. Wananchi ambao ni walipa kodi na ada katika vyuo hivi wajue nini kinaendelea. Yaani iwe kama kile kipindi alichokuwa anaendesha Salama EATV ambapo video za kijinga zilikuwa zinawekwa wazi kwamba ni za kijinga na za kipumbavu...same thing ila sasa iwe ni website...tena walinganishe na website nyingine tu za vyuo vya nchi jirani au ambazo ni za nchini, zimetengenezwa na wamatumbi na wapogolo lakini ziko juu!
ReplyDeleteTuseme ukweli usomaji wa kibongo umekaa kimadesadesa sana na kwa hiyo website zinakuwa hazina maana.
ReplyDeleteWengi ya hao wanaofundisha huko na wale wa serikalini walipita kwa mtindo huo huo ndiyo maana hawaoni umuhimu wake, kwao poa tu.
Website za vyuo na serikali zote hazifai and they don't think about it.
Hii nchi watu inabidi wawe washituliwa na shock za umeme to know what they supposed to do otherwise safari itakuwa ndefu sana.
Ni mtazamo tu.
Hivi kuna rangi maalumu za vyuo vikuu? Tuelimisheni maana naona hii ni mpya.
ReplyDeletefor ur info, UCC is NOT a university BUT a company...which side of the earth did u drop from, mmh?
ReplyDeletefor tazara visit www.tazarasite.com,
ReplyDeletemimi ni mdau niliyegraduate chuo kimoja IT mwaka jana, ukweli ni kwamba msione watu wanajivunia kusoma IT/Computer science kwenye hivi vyuo vyetu ila ukweli tunaujua wenyewe, walimu wenyewe wako kinadharia,ukiwapeleka kwenye utekelezaji soo 2.
ReplyDeleteBaadhi ya wanafunzi kwa jitihada zao wenyewe wanakua fit,tena pengine fit katika utekelezaji kuliko hata walimu wao, lakini nani atawaona mfumo ushaharibika.
Utakuta mtu anamaliza shahada ya kwanza,anarudishwa kuwa mwalimu, baada ya miezi kadhaa anapelekwa masters na kuunganisha phd,hivi kweli mnategemea huyu mtu asiye hata na experience ya kazi zinafanyikaje mtaani ataweza kutatua matatizo kiutekelezaji????halafu eti huyo huyo aliyejazwa nadharia anakuja kuwa mwalimu,atawafundisha nini wanafunzi zaidi ya kuwamezesha hizo hizo nadharia????
ukweli mfumo wa kuchukua walimu wa vyuo ni mbovu nisahihisheni kama nakosea,angalau hawa walimu wahasle kidogo kazini ili kupata experience na kuwafundiya wanafunzi real things.
La mwisho huwa nakumbuka kuna wakati tulipokuwa chuo tuliletewa ticha mmoja,assistant proffesor kufundisha programming, ilikuwa balaa maana alikuwa anatema sumu zakufa mtu sio siri alikuwa anafundisha uongo,alikuwa hajui ni nini anacho fundisha.naongea kwani kitu hiki kiliniuma, lakini nilipofuatilia nikajua kwamba ni wale wale waliounganisha from undergraduate to phd without experience.
ni hayo tu.
ndio watu wanaweza kuwa bado wanachanganya, zamani ucc ilikuwa ni part ya udsm, hivi karibuni imebadilishwa kuwa kampuni inayojitegemea,siwalaumu watu kwa kuchanganya.
ReplyDeleteUpatikanaji wa taarifa za Tanzania katika internet limekua ni tatizo ambalo hatujalitia maanani. Mwaka jana nilikua nje ya nchi, cha kushangaza sana taarifa muhimu za nchi yetu unazipata kutoka CIA.
ReplyDeleteVyuo vyetu viendeshwe kibiashara, kwa mfano, unaweza kuomba Prospectus toka Uingereza na ukaipata kwa haraka na bure. Prospectus za vyuo vya bongo zinapatikana kwa nadra sana tena hadi uwapigie magoti na kuwalipa pesa.
Wananchi inabidi tuelewe vitu husika nahakika web-designer huwa anakurupuka bila kufikiria nini kinatakiwa angalieni vizuri templates na color code, logos, fonts yaani hakuna mpangilia buttons zipo tofauti inabidi tuwe tunagawana mipangilio huwezi kuniambia website itakuwa mzuri kama atatengeza raia mmoja tuu never, lazima kuwe na script designer , graphics designer n animation designer ambaye atakuwa kila mtu anaweka mambo kwenye mstari ila lecture akurupuka huko na kuanza kutengeza web ni sawa na muuza barafu mtaaani yaani web iko kama nini cjuwi na unaambiwa ni web ya university alafu mbaya kuna course ya IT/CS, tanzania kweli bado tupo nyuma sana bora kwenda kwenye private companies wakawasaidie kuliko wananchi nyie mnamwaga sumu kwa dent, mnaharibu jamani
ReplyDeleteBinafsi nilishawahi kumwandikia mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma juu ya ubovu wa website yao na kupropose changes ili kuifanya iwe makini. Lakini waapi! Si hizo tu bali na nyingi nyinginezo. Tembelea WWW.VARSITYCOLLEGETZ.NING.COM ujaribu tovuti kadhaa na ujionee. Hatupo serious kwa kweli.
ReplyDeletekazi nzuri but tuzungumzie hata blog zingine, haina maana ni vituko tu watu wanadesa mambo toka nje nk. hivi nini hasa tunafanya watz ktk hizi blog wengine tubaki mashabiki sabu blog zinafanana matukio blog moja na ingine hamtofauti afu IKULU naeza washauri watafute mtu awe anafanza mambo ya maana wala haitakua aibu
ReplyDeletewww.tazara.co.tz/ THIS SITE IS UNDER CONSTRUCTION
ReplyDeletehalafu mdau hapo juu asante umetufahamisha kuwa kuna www.tazarasite.com(sounds like parasite.com)
sasa which is which? hata hivyo www.tazarasite.com ina info nyingi ila wawe makini jina gani linafaa kwa kampuni kubwa:
www.tazara.co.tz au www.tazarasite.com
umakini unatakiwa ktk jambo la webusaiti, maana uki-google TAZARA, www.tazara.co.tz ndio inaibuka mwanzo.
Hao wataalamu wetu wa IT hata mimi niko fit (mtumiaji wa kawaida tu) embu tembelea tovuti kama hii www.duce.ac.tz (chuo kikuu kishiriki cha ualimu chan'gombe)...jaribu tu ulizia bajeti yake utachoka!
ReplyDeleteNampongeza sana mdau aliyeibua mada hii. Mimi si mtaalam kabisa wa mambo haya ila huwa nakerwa ninpotaka jambo katika website ya wizara fulani unakuta haiko update; taarifa nyingi ambazo ni za kuhabarisha umma hakuna. Sometime simlaumu IT, yeye atajuaje mambo gani wizara ingependa yaende public na yapi siyo kwani yeye pia si mtaalamu wa taaluma za wizara fulani. Utakuta wizara kubwa ina idara kibao. Nilitegema kila idara ingekuwa na ukurasa ambao mtu ataingia humo kutafuta taarifa husika. IT anasubiri umpe habari anajua ataziweka kwenye ukurasa gani n.k. Hivyo si vyuo tu hata ma wizara. Sijui kama huwa waingia kusoma hizi comment. Tafadhali tuwe serious.
ReplyDeleteHello.Mdau kaongea mada nzuri,lakini angeomba maelezo kabla ya kulaumu tu! wanaomsifia kwa kufanya research sijui niwaitaje! sijawahi kuona research ya namna hiyo! sijawahi!
ReplyDeleteTechnology ina vitu vingi sana,na kuendelea si mchezo! huw serious the goverment is in Technology innovation? mbona hamshangai madaraja.barabara na masoko kujengwa na wachina wakati tuna Maaengineer miaka nenda miaka Rudi? kuhusu information,chuo ndio kinatakiwa kujuwa info za kuweka kwenye website na sie mtu mwingine! Hakuna la privacy hapo,hamtaki wazazi wenu wajuwekama mmekula Ada? angalia body ya mokiopo matangazo kwa wadaiwa hata kwenye TV,tunaijenga Tanzania tupewe muda! kama kuna udhaifu utashughulikiwa! lakini si porojo za intranet na internet! watu wala hawajui maana ya vitu hivi! Ulizeni muambie Rwanda wamewekeza kwenye nn hasa? tatizo la Bongo mwawekeza kwenye siasa! itakula kwenu!
Hizi ni changamoto hasa kwa watu wa IT na watawala wa hivi vyuo. kuna mdau katoa sample za vyuo vya kuigwa mf.http://www.ub.bw/ cha botswana mbona copyright ni ya 2008? Vyuo vikuu karibu vyote vinamthamini Academician na si suporting staff(wanapenda kuwaita hivyo) kwahiyo ni changamoto. pia jamani mambo ya customize nayo yasizid sana maana yanaua utalaamu wetu ebu check website yetu ya bodi ya mikopo http://www.heslb.go.tz (Loans board) jamaa customize Joomla na amesahau ku-edit Newsflash kwenye Latest Events. kwahiyo hii ni changamoto na wana-IT wakipewa nafasi wanaweza maana Tender nazo ndo zinatufikisha huku na wasimamizi wenyewe si wana-IT maana nawe ukiingizwa chain itakuwa ndefu na mshiko utapungua wakati wa kugawana.
ReplyDeleteIts true kabisa hawa wasomi wanatuyeyusha...Ankali hetu mdau atufanyie pia sensa ya website zifuatazo one after another,
ReplyDelete(1) Taasisi za Serikali (Wazara na taasisis zinazojitegemea)
(2) kampuni za Sekta Binafsi
Huko nako ni sooo
Baadhi ya hivi vyuo na colleges wan partnership ma Microsoft, Je, hii partnership inahusu nini, my assumption ni kuwa Microsoft wana programs za kusaidia kutengeneza web sites, au hamjaomba tu?
ReplyDeleteHaya ndio matatizo ya kuacha kuajiri watu na sifa zao...matatizo haya hayatakwisha mpaka vizee viachie ngazi katika kila sekta na kuawaachia vijana wenye elimu kufanya kazi.
ReplyDeleteMdau hapo juu...nchi yetu haiwezi kuendelea kwa kutegemea kusaidiwa kila kitu mpaka kitu kama kuapdate website...
Haya ya website ni mfano wa ubaya wa kutegemea misaada na tunategeme kufanyiwa kila kitu...maafa ya kilosa yasingetokea iwapo nchi yetu ingekuwa imeyakarabati mabwawa aliyo yajenga mjerumani enzi za ukoloni...haya ndio yaliyopelekea reli kufaaaa...TAZARA kufaaa...Sunguratex kufaaa...Elimu kufaa...chuo kikuu kufaaa...na mpaka leo tunatumia vitabu vya 1967.
Ukiwa nje ni rahisi kuona matatizo na kuwatupia lawama watu fulani lets say watu wa IT. Kuna matatizo mengi sana kwenye vyuo vyetu. Tatizo moja kubwa idara za IT zina bajeti ndogo sana ambayo huwa karibu yote inatumika kulipia mtandao( hakuna pesa kwa ajili ya acqusition ya hardware na software). Pili department nyingi zipo under staff. Tatu, website hazijapewa priority kubwa inaonekana tu ni kitu cha kawaida kwa menejimenti ya vyuo. Halafu kazi ya kutengeneza website sio ya lecturer. Anatakiwa mtu maalumu kwa ajili ya website. Lecturer aki design anafanya kwa kujitolea. Lakini kama amaebanwa na teaching, research, na consultancy hiyo kazi atafanya saa ngapi? Website inahitaji mtu awe dedicated
ReplyDeletehahahaaaa hii kiboko
ReplyDeletesina mbavu apa,anyway tupe rangi za website za vyuo vikuu ili niwahsauri bugando na saut
napita tu
kama maprofesa wapo kwenye majukwaa ya kisiasa wengine wanapiga kelele bungeni unategemea Tutorior atamfundisha nini IT wa Tz zaidi ya sumu
ReplyDeleteNONDO
ahsante mdau kwa topic ambayo nilikuwa naisubiria kwa muda mrefu. natumaini hii italeta changamoto ama kufungua macho na masikio ya wanataaluma. kama ulivyosema ni kweli kama tutawatumia wanafunzi kudesign website zetu kwa kutumia utengenezaji website nzuri kwa design na coding kama mazoezi ya kila siku na kuahidi mshindi japo tuzo kwa kila chuo , chuo kinaweza pata team inayoweza kudesign site nzuri na kwenda na wakati kwa kua update mara kwa mara.
ReplyDeleteMichuzi ahsante kwa kuweka hewani topic hii. Kuna katatizo ka morali hapa pia unapenda kuiga na sio kujifunza ndio maana tunapata tatizo kama hii, tuende kwa undani kuona wenzetu wanafanyaje. siku hizi kila info ni bure kama utatumia mda wako ku google.
kwa kweli inatia aibu tovoti za vyuo veytu huwezi kupata information zote ambazo mtu unahitaji katika ulimwengu wa habari.hata ukitaka kujaribu kutafauta form online application huwezi kufanya, muda wakuhangaika na makaratasi umepita nawakati. hiyo tovoti ya udsm juzi tu nilishindwa kufungua kwa sababu server yao ina virus, so unashindwa kupata mawasiliano.Jamani ni lini tutakuwa angalau seriuos? sidahani kama kwlei hatuna watu wakutengeneza website nzuri zenye hbari zote muda wate wadau tuakazipata nakufanyaia kazi.
ReplyDeletemzalendo