Wakazi wa eneo hilo inaonekana somo lililotokea kata ya Isongole mkoani Mbeya halikuwaingia ,wakaendelea na utaratibu wa kuchota mafuta bila kujhali kuwa wanahatarisha maisha yao. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
Wakazi wa eneo hilo inaonekana somo lililotokea kata ya Isongole mkoani Mbeya halikuwaingia ,wakaendelea na utaratibu wa kuchota mafuta bila kujhali kuwa wanahatarisha maisha yao. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
mmmm!mwe!mwe! kweli Bongo Tambarale,na mungu yupo pamoja nasi
ReplyDeletehivi haya mahilux ya kisasa yametengenezwa kwa maboksi au makaratasi duu
ReplyDeleteAKILI KWELI NI MALI, HAPO AKIPITA MVUTA FEGI TU NI MAAFA YASIYOSEMEKA. HATA KAMA NI UMASKINI, NDOO MOJA YA WESE ITAKUSAIDIA NINI MAISHANI?
ReplyDeleteHiyo sehemu ina kakona hivi na ka slope harafu mbele kuna daraja, hatari sana hapo kama unajidai wewe ni Michael Schumacher lazima ulambe tope. Poleni wahanga na hongereni kwa Israel kutowapitia maana ajali ni mbaya sana. Mkatoe shukrani ya pekee huko mnakoabudu.
ReplyDeleteDrive safe to rescue life.
Mr michuzi yule mama sijui ni mzambia huwa anakaa na watoto wake wanne pale ufukwe wa ocean road jirani na agha khani leo bado nusu nipate ajali nilipokuwa nashangaa baada ya kumwona ana mimba nyingine kubwa
ReplyDeletewanaume tuache tabia chafu nidhambi kama wanaompachika ni vichaaa basi wasamalia wema wamtoe kizazi ili asiwatese watoto wasio na hatia kwa jua na mvua nawakilisha
HIVYO TV KAMA TBC NA TVT ZINAFANYA NINI NCHINI TANZANIA? KATIKAK UELIMISHA JAMII KWENYE TV KUHUSU MAMBO KAMA HAYA? WANANCHI NA WAJUMBE WAO WANAWAFUNDISHA NINI WANA VIJIJI? KWANINI SIE BADO TUNARUDI NYUMA TU? TUNACHOKIJALI KWENYE MA TV YETU NI MISS TANZANIA SHOW NA FASHION SHOW BASI, ELIMU ZENGINE ZAK UJIKINGA NA MABALAA HATUONESHI. MASUDI.
ReplyDeletePoor Tanzanians. Hawa jamaa sio kwamba hawathamini maisha yao bali hali ya kimaisha ni mbaya sana, mtu bora afe kuliko kukosa dili la buku, kwani hujaona watu wanang'oana meno kisa wamedhurumiana sh 100. Inasikitisha sana, ila hiyo ndiyo inaonyesha hali halisi ya maisha ya Watanzania walio wengi. Bado maadui watatu aliowasema Baba wa Taifa wanatuandama kwa kasi kubwa na kwa kila hali inaonyesha tumeshindwa kuwakabili. Kwakweli Watanzania bado sana. Nadhani ktk kila Watanzania 100 watakaoona gari la mafuta limeanguka 85 watalikimbilia ili wachote mafuta yanayotiririka. Kwani hamjawaona watu Dar es Salaam wanaofungua matanki ya magari yanayobeba mafuta yanapokuwa kwenye foleni na inakuwa ni mchana na hakuna anayejali, na wakati mwingine matrafiki wanakuwa hapo hapo.
ReplyDeleteBado kazi kubwa sana ipo mbele yetu katika Taifa hili ambalo kila siku tunaliita changa wakati tuna miaka 49 sasa tangu uhuru.
TATIZO UMASKINI WATU WANAKOSA HATA AKILI KIDOGO ZA KUFIKIRIA HATARI
ReplyDeletebongo magaidi hawahitaji mabomu, hii ni njia mbadala, tena unaangusha malori matano kwa wakati mmoja
ReplyDeletemwenye kidumu ,mwenye kijiko akamimina.mwenye ndoo akachota ...
ReplyDeleteBWA SHEMEJI KWETU THITHI NI TAMBARARE TUMEENDELEA BWANA, EMBU HAPO BWA SHEMEJI KUNA TOFAUTI GANI NA MPITIMBI AU KIBAIGWA, NIKIMAANISHA UONEKANO WA WATU, TANZANIA NI MOJA SOTE TUKO SAWA KILA SEHEMU KUNA WA MATAWI YA JUU NA YA CHINI HATA LONDON WAPO WATU KAMA HAO
ReplyDeleteNJAAAAAAAA kweli mbaya !! Sasa awa wapuuuuzi wakiwaka moto je ?
ReplyDeletedaaah,kweli Mungu Mkubwa.sasa hao jamaa walivyotapakaa mafuta,hapo kama gari lingelipuka si wote wangeangamia?Mungu tu kaamua kuwanusuru lkn hali wala haikuwa shwari kivile.
ReplyDeleteUmaskini wetu huu ................
bongo njaa kweli kweli,watu wamekuwa hawajali roho zao tena.
ReplyDeletemaisha magumu!!! wanasema unapotafuta maisha usiogope kufa, kufa ni ajali kazini!!!
ReplyDeleteKaka hapa nasikiliza kwanja rudeboy la rihana dah hili kwanja si mchezo!!!
bwana dickson busagaga mambo vipi mkuu. vipi huko moshi mambo yakoje hapo?? mambo ya enh enh enh yakoje hapo wakichaga hao?? lete vitu bwana tutoke watu
mdau wapajazzzz+titizzzz
yote hayo ni umasikni..mtu anawaz nyumbani mpaka giza linaingia hakijaeleweka anaona bora ajitoe muhanga akijua likitokea lolote atakimbia..jaman umasikin huu sijui watanzania tutaendelea lin
ReplyDeleteKIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.SIDUMU ITIKADI SAHIHI ZA CCM.CCM OYEEE!!
ReplyDeletehivi watanzania wataelimika lini wanajigawia tu wese hivi ni kweli maisha magumu au kutokujijali maisha ni zaidi ya mnavyofikiri na ukikosa leo kesho utapata
ReplyDeleteHata hifo derefa wa hako kahailux amechitahiti.
ReplyDeleteapa sina mbavu adi nimepaliwa na chai,,,hahahahahhaaa ndo mana naipenda hii blogu ata nikiamka vibaya nikisoma tu umu basi cheko
ReplyDeleteebu msomeni annon Feb 18,06:51:00pm
kwi kwi
Wazungu wanasema "Unless you risk you can't harvest". Hawa jamaa wana-apply hiyo hapa.
ReplyDeletendugu zangu wabeba mafuta:ninaelewa sana hii hali ya maisha ndo ivo ilmradi kipatikane cha kula na kuendesha maisha kwa sasa!!poleni sana na iyo hatari
ReplyDeletewatu hawaelewi hali ngumu ya watu bongo,nyie mshukuruni mungu wenu mna hali zuri unajua wala nini baadae,,,MSITUKANE WATU
Hizi hilux za sasa ni mabox.....acha hiyo. Angalia wachota mafuta hao. Lakini tutafika, baada ya kizazi hiki kuisha. Binadamu wa sasa na maisha ni vitu tofauti.
ReplyDeleteDunia itaumbwa upya na nchi itabadirika.
Mungu wasamehe hawa ndugu zangu wachaga kwa kuwa hawajui watendalo. Najua kwenu nyie hela haifananishwi na kitu chochote ndio maana hiyo ajali haikufananisha na ile iliyotokea Mbeya au Chalinze. Kilichokuwa kikiwazwa hapo ni hela tu.
ReplyDeleteIla mlianza kwa tahadhari kubwa!!! naona kama mlianza kusali kwanza wote kabla hamjaingia kuchota.
Serikali inapiga kelele tu ajali ajali ajali..Nae Rais anaagiza tu ajali zipunguzwe. Lakini hakuna hatua mahsusi zinazochukuliwa kushughulikia hilo.
ReplyDeleteTatizo kubwa ninaloliona Tanzania ni kutokuwepo kwa utaratibu wa kuhakikisha kosa linamilikiwa. "Own a Mistake". Mara hili litakapokuwepo basi inakuwa rahisi kuweka gharama ya umiliki huo.
Hii ndio wenzetu wamefanya na ndio maana hapa UK ukimuazima mtu ghari atakuuliza unayo insurance? Na kichwani atajiuliza je huyu jamaa rekodi yake ya udereva ikoje? Na zaidi ya hapo ataweka rekodi ya muda alipokupa gari na muda umerudisha. Hivyo Ukifanya mafyongo yako huko yeye anatoa tu data zako kwa watu wa bima na Polisi. Kwa misingi hiyo utakuwa Zoba kumpa mtu usiyemjua na wala hujui address yake tena ni vizuri ukachukua kabisa namba ya leseni yake ya Gari. Sasa lile kosa ni lako na Bima wataliweka kwenye hesabu zako na utalilipia kwenye bima.
Sasa hapo akili itakujia na Polisi pia wanakunyonga Leseni yako sasa adabu inaingia. Na kama kazi yako inabidi gari basi wewe adabu kweli kweli!!
Hivyo hii si sayansi ya maroketi Serikali inabidi ikae na watu wa bima ili utaratibu huu uweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa maana kadiri watakavyokubana mfukoni akili kichwani itafanya kazi maana upande wa Polisi kwetu bado maana kaufisadi.
Sasa tusilie tu ajali tuchukue hatua ambazo wala hazihitaji kutumia nguvu ni akili tu kidogo.
Sasa sisi Tanzania bado tunawekea bima gari badala ya dereva au Mmiliki. Sababu gari haligongi bali Dereva. Mfano ukipaki gari hapo nyumbani litamgonga nani?!! Na hata gari likiibiwa halipati hasara bali mmiliki ndio anaepata hasara. Ndio maana katika sheria ya bima husema kwa kimombo..."Insured Interest".
Kwa kufanya hivi hata wamiliki wa magari watakuwa waangalifu katika kuajiri madereva maana akiajiri dereva ambaye rekodi yake mbovu bima yake itakuwa juu na kwa misingi hiyo madereva nao watakuwa waangalifu zaidi maana bima kwao itakuwa juu na kazi kupata itakuwa ngumu. Na pia hatathubutu kumpa dayworker!!!
Vichwa ngumu watakuwepo kama ilivyo huku lakini watakuwa wachache na 40 yao huwa haiko mbali.
Mimi hata sielewi kwa nini tunashindwa kufanya mambo ambayo ni madogo sana badala yake tunaanza kufikiria Maflyover wakati kadaraja tu tunaomba misaada...ajabu kabisa.
Mzawa
mnawashangaa hao! wanamavazi bomba kabisa, nyie kweli mmekulia mbogo saba. Kuna vijiji huko sehemu hata kaputura hawana. Hawa wako fit kabisa basi tu njaa zao tu. Tz acha bwana
ReplyDeleteBetter die trying than dying poor that i think is the mentor right there.but what a stupid decision is that watu kweli hawawezi kuona mifano mengine ya watu wengi walioteketea kwa kufanya issues za namna hio its a shame aibu kinoma kudadadadadeki
ReplyDeleteNIMEANGALIA MAONI KARIBU YOOTE YANAPONDA KITENDO CHA WATU KUCHOTA MAFUTA, LAKINI HII BLOG INGEKUWA INAFIKIWA NA MAJIDA WA MITAANI UNGEPATA PICHA HARISI KAMA KILE KITENDO NI CHA KISHENZI AU LAH. MIMI NIMEONANA NA KACHALA WANGU MAENEO YA KIBORORONI ANALIA NILIPOMUULIZA ANALIA NINI AKADAI YEYE AMEZALIWA NA MKOSI KWASABABU NEEMA IMETOKEA AKIWA YUPO MBALI ENEO LA TUKIO NA NI JANA YAKE TUU ALIKUWA MAENEYO YA AJARI NA WASHIKAJI ZAKE WANAMPIGIA WAKIWA WAMECHOTA MAFUTA NA KUYASUKUMA FAASTA SASA WANAZIGIDA BIA NA KITIMOTO KUTOKANA NA NEEMA ILE, MIMI MWENYEWE KULIKOSA LILE ZALI IMENIUMA NINA UHAKIKA NISINGEKOSA JAPO LITA25 KWA BEI YA FASTA NISINGEKOSA EF20. ALAFU MTU MWINGINE UMEKAA OFISINI UNAPIGWA NA KIPUPWE HUKU UKICHEKI NETI NA KUPONDA WATU WAKIFANYA KAZI ZAO AU KWASABABU WEWE KAZI ZAKO ZIPO KWENYE JOBUDISKRIPSHENI? SISI WENGINE TUKIAMKA ASUBUHI NA JOBUDISKRIPSHEN YETU INAANZA WAKATI WOWOTE KUTEGEMEA NA MATUKIO NA INABADILIKA KILA SAA, HIVYO SISI WENGINE HIYO NI KAZI KAMA KAZI ZINGINE NA TUNAIHESHIMU. MICHUZI ANGALIA NAMNA UNAVYOWEZA KUTUSAIDIA MAJIDA WA MTAANI NAMNA TUNAVYOWEZA KUTOA MAONI KWENYE MADA ZINAZOTUGUSA SISI MAJIDA.
ReplyDeleteusipoweka hii komenti nitamaindi mbaya maana nimeingia intaneti cafe kwa buku langu la fegi ili kutafuta marafiki huko mamtoni ili kama vp ipo siko mzee huuuyo ma-Jobegi au ma Newyork tukapigane vikumbo na akina Jay zee
Jamani,ukiwa na njaa ,hauwezi kufikiri .....msifanye mchezo...kama mfukoni huna hata buku then unategemea nini ktk ishu kama hii?
ReplyDeletehapo issue sio tu kiberiti au fegi..hapo nyanya za battery zikisuguana tu..stori inakuwa mpya..
ReplyDeletekweli its not easy ila tutafika tu
Wabongo wanafikiria moto kulipuka kapo ni mpaka kiberiti kiwashwe..mto hapa unaweza kulipuka from no where..
ReplyDeleteUmaskini au uchu jamani!!! Hivi hao wazoa mafuta hawaogopi kifo? Kibiriti, sigara, cheche inawasha hayo mafuta na tungesikia vilio kibao!
ReplyDelete